Kilimo ni tegemeo kubwa la uchumi wa bara la Afrika na kati ya asilimia 20 hadi 35 ya Pato jumla la Mataifa mengi ya Afrika hutegemea kilimo.
Janga la Korona ni kadhia inayoendelea kuleta athari kubwa kwenye uchumi wa nchi nyingi barani Afrika.
Hatua zinazochukuliwa kwenye baadhi ya nchi katika kujaribu kuzuia kuenea kwa janga hili kumeathiri mnyororo wa thamani kwenye sekta kilimo. Kwa upande mwingine nchi nyingi zimeitenga sekta ya kilimo na chakula na kuiondolea makatazo kama kufungwa kwa biashara na kusafiri.
Usalama wa chakula, maji na lishe bora vina uhusiano wa moja kwa moja na janga hili, na maji yakiwa ni muhimu katika uzalishaji chakula na miundombinu bora ya maji taka. Maji yanasaidia katika uzalishaji wa mifugo, uzalishaji wa chakula, utayarishaji na matumizi chakula hicho.
Hata hivyo, mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la mahitaji ya maji na kuongezeka kwa uhaba wa maji, uchafuzi na janga la Korona vinahatarisha mfumo wa kiekolojia na usalama na upatikanaji wa maji endelevu.
Janga la korona linaaangazia mahitaji ya maji safi na usafi wa mazingira kwani zaidi ya watu bilioni 2.2 ulimwenguni bado wanakosa maji ya kunywa, wakati bilioni 4.2 hawana huduma za usafi wa mazingira. Wakati huo, usafi kwa ujumla wake pia na maji kwa ajili ya uzalishaji chakula ni muhimu sio tu katika kuukabili ugonjwa wa Korona bali ni muhimu katika kujenga uthabiti kwenye jamii.
Bila kuwepo kwa maji safi zoezi la unawaji mikono halitawezekana, bila ya kuwa na maji safi, usalama wa chakula nao hautakuwa na mafanikio.
Kwenye nchi zinazoendelea zilizopo kwenye bonde la mto Nile virusi vya korona ni tishio kubwa kwa usalama wa chakula na maisha kwa ujumla kwa sababu mifumo ya uzalishaji kwenye kilimo ni nguvu kazi kubwa ya watu zaidi na kuna uwezo mdogo wa kuhimili mtikisiko wa mkubwa wa uchumi .
Wito wa Kuomba Ruzuku
INFONILE inawaalika waandishi wa habari waliopo kwenye nchi zilizopo kwenye bonde la mto Nile kuandika mchanganuo wa kina ili waweze kupewa ruzuku itakayowawezesha kuandika habari zinazuhusu athari ya Korona kwenye kilimo cha umwagiliaji, upatikanaji wa maji na matumizi yake kwa wakulima.
Tunawaalika muwasilishe mapendekezo katika vikundi vya watu wawili au watatu. Mnaweza kuomba kama kikundi cha waandishi wa habari kutoka nchi tofauti mkiandika habari moja – au kikundi cha waandishi wa habari kutoka nchi hiyo hiyo ambao huripoti kwa majukwaa au kwa lugha tofauti; kwa mfano, mwandishi wa redio na mwandishi wa habari wa Runinga au wa gazeti.
Ni kwa namna gani korona imewaathiri wakulima katika upatikanaji maji kwenye umwagiliaji?
Je wakulima wamekumbana na changamoto yoyote kwenye upatikanaji wa zana za kilimo, pembejeo na ukarabati kwenye teknolojia ya umwagiliaji kutokana na vikwazo kwenye na janga hili na ongezeko la matatizo ya kifedha kwa ajili ya ushuru, upungufu wa masoko na upatikanaji wake, ukosefu wa nguvu kazi na sababu nyingine za kiuchumi? Ni fursa zipi zimejitokeza ikiwamo uvumbuzi mpya?
Tunakaribisha mapendekezo ya kihabari ili kuchunguza upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo, usafi wa mazingira na usafi. Je ni kwa namna gani, usafi wa mazingira na usafi kwa ujumla na kwa mtu mmoja mmoja vimechangia kuathiri afya za watu wakati wa janga hili?
Kwenye kilimo wanaohusika na usafi ni wakulima na wafanyakazi wa shambani na wafanyabiashara wengine wa vyakula ambao wanahitaji kuwapo na upatikanaji maji safi na salama na ukusanyaji wa taka wenye ufanis.
InfoNile inawaalika waandishi kuwasilisha maombi ya kufanya habari za uchunguzi zinazohusu kilimo cha umwagiliaji, usafi na usafi wa mazingira. (AgriWash).
Usafi wa Mazingira na usafi kwa ujumla ni mambo ya mtu binafsi yanayochangia afya njema. Katika kilimo, na katika kitovu cha kilimo kuna wakulima, wafanyakazi wa mashambani na wafanyabiashara wa mazao ya chakula ambao wanahitaji upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na ukusanyaji na taratibu za utunzaji salama wa taka za shambani.
Ingawa kemikali za mazao ya kilimo na dawa za kuua vijidudu vya shambani, zinatumika zaidi katika mfumo wa uzalishaji wa chakula, lakini pia wanyama, usimamizi wa taka zinazotokana na ufugaji wa samaki, vyote hivi vinatakiwa kuangaziwa kwa jicho la kina ili kuzuia viini vya magonjwa na usugu wa vijidudu katika mifumo ya maji taka kama sehemu muhimu ya ufugaji wa samaki au kilimo cha majini.
Hivyo basi, InfoNile inawaalika wanahabari kutengeneza habari za kina za uchunguzi zinazolenga namna Covid-19 ilivyoathiri usimamizi wa kilimo cha umwagiliaji katika nchi za bonde la Mto Nile.
Mambo ya kuzingatia
Tafadhali zingatia kuwa, kama utapata ruzuku ya kuandika habari hizi, InfoNile, itakupa fursa ya kupata mafunzo katika program maalum ya mafunzo ya uandishi wa habari za takwimu. Pia utapata usaidizi wa kina wa namna ya kutengeneza habari kwa kutumia picha, takwimu na ramani.
Habari zitakazochapishwa kwa lugha nyingine, zitatafsiriwa kwa lugha ya kiingereza.
Hakuna kiwango cha fedha kilichowekwa katika maombi ya ruzuku hii, lakini tunatarajia maombi ya ruzuku kwa habari hizi yawe kati ya USD 1,000.
Kwa wale wanaofanya habari za uchunguzi za kina au ambao wana kikundi chenye watu wengi, wanaweza kuomba ruzuku inayozidi kwa kiasi kidogo k USD 1000. Tafadhali omba ruzuku unayohitaji tuu.
Tafadhali tuma yafuatayo kwa kutumia barua pepe hii ya @infonile.org. Mwisho wa maombi haya ni Julai 31, 2021
- Pendekezo lako linaloonyesha wazo lako la habari(lisizidi kurasa moja) .
- Pendekezo hilo liweke wazi, likieleza mapema wazo la habari, likifuatiwa na namna na wapi habari hiyo itafanyiwa utafiti.
- Habari hiyo inatarajia kuibua nini au kuchangia nini katika jamii.
- Wapi habari hiyo utachapishwa(Taja chombo cha habari kitakachochapisha habari hiyo)
- Matokeo tarajiwa ya habari yako.
- Pendekezo lako halina budi kuonyesha mpango kazi wa namna utakavyotumia takwimu. Pia namna utakavyotumia chaneli mbalimbali za habari (video, picha, sauti, na maandishi).
- Bajeti
- Wasifu wa kazi(CV)
- Sampuli mbili za kazi zako zilizowahi kuchapishwa au kurushwa. (Ni linki pekee za habari yako ndizo zinazopokelewa)
- Barua ya udhibitisho kutoka kwa mhariri wako, itakayokuthibitisha na kukubali kuwa chombo chako cha habari kitachapisha au kurusha habari yako.