Ufadhili Ndogo ya Uandishi Kuhusu Uhalifu  Dhidi ya Wanyapori Afrika Mashariki

Grant Call Poster Wildlife Crime

InfoNile pamoja na Oxpeckers Investigative Environmental Journalism inawaalika waandishi wa habari kutoka Uganda, Kenya, Tanzania and Rwanda kuwasilisha wazo la undani kuhusu uhalifu kwa wanyamapori na juhudi za kisheria za  Afrika Mashariki.

Muungano wa kimataifa ya kupambana na uhalifu wa Wanyamapori (The International Consortium on Combating Wildlife Crime) unaelezea uhalifu wa wanyamapori kama kuwanasa, kufanyia biashara (kuwasambaza, kuuza ama usafirishaji haramu), kuagiza, kusafirisha nje, kuhusika kwa usindikaji, kumiliki, kupokezwa kwa matumizi ya mimea na wanyama mwitu, halikadhalika mbao na bidhaa zinginezo za msitu, kinyume cha sheria za kitaifa na kimataifa.

Biashara haramu ya wanyamapori ndiyo ya nne kubwa zaidi baada ya  biashara inayohusisha madawa ya kulevya, magendo ya binadamu na bidhaa ghushi. Kwa saa hii imekuwa kiwanda kubwa sana haramu kwa wanyamapori inayotishia kuangamiza na kutowekwa kwa baadhi ya aina mbalimbali za wanyamapori bila kujua hatima yao wala idadi waliotoweka.

Sheria mbovu zenye lengo mbaya za wanyamapori na zinazoeleekezwa vibaya zinachangia kukatisha juhudi za jumuiya za mitaa, mashirika na idara zakutilia sheria mkazo kwa kupambana na  uhalifu wa wanyamapori. Vyombo vya habari ni muhimu sana kwa kuangazia mambo muhimu yenye kuzingatia vitendo vya kupambana na uhalifu wa wanyamapori.

Idara ya Oxpeckers inayoshughulikia Uandishi Habari za Upekuzi kuhusu Mazingira (Oxpeckers Investigative Environmental Journalism) imeanzisha #WildEye  ambayo ni jukwa kidijitali ya habari yenye inahusika na takwimu (GeoJournalism) kwa kusanya na kushiriki usambazaji wa takwimu pamoja na kuzingatia sheria dhidi ya usafirishaji haramu wa wanyamapori. #WildEye  huonyesha takwimu kwa ramani kuhusu kukamatwa, kesi zenye ziko mahakamani na mahukumu. InfoNile inashirikiana na Oxpeckers kwa kuzindua #WildEye mpya ambayo ni ya Afrika Mashariki, uzinduzi wake ni mwaka huu 2022.

Tunataka wewe ufanye:

1.Kupekua na kuchunguza changamoto/mianya/ufanisi/ubunifu au fursa zilizoko za kuingilia kati sheria dhidi ya usafirishaji  wanyamapori.

2.Tumia #WildEye ambayo ni ramani ya Afrika Mashariki kwa kujumuisha data  kwa taarifa za habari  zenye upekuzi. 

3.Jitahidi kuchapisha taarifa hii ya habari-pekuzi kwa chumba chako cha habari mnamo 31st March, 2022  baada ya uhariri na kutengewa takwimu za taswira kwa wajibu wa InfoNile.

Matarajio 

Kazi yako inastahili kuwa habari pekuzi ya undani inayozingatia uhalifu wa wanyamapori Afrika Mashariki. Tunahitaji habari pekuzi yenye lengo aina yake ya kipekee, kibinadamu na inayolenga data.

Tafadhali zingatia ya kwamba ukifanikiwa kupata msaada huu wa uwezeshaji wa kufanya habari pekuzi, utasaidiwa kwa michoro ya grafu, taswira ya data na mchoro wa ramani. Habari pekuzi yaweza kuchapishwa kwa lugha zinginezo lakini itatafsiriwa kwa Kizungu.

Siku ya mwisho ya kutuma wazo la habari pekuzi yenye undani ni 25 Februari, 2022

Ukifanikiwa kwa msaada, habari pekuzi yako itakuwa miongoni mwa habari pekuzi zitakazo hushishwa kwa mradi huu wa uhalifu wa wanyamapori Afrika Mashariki. Utafundishwa jinsi ya kutumia #WildEye, pia kutumia data ziliziomo kama msaada kuongeza sifa kwa kazi yako. Habari pekuzi yako pia itachapishwa papo hapo kwa hilo jukwaa.

Sisi ni akina nani?

InfoNile ni shirika la kundi la waandishi wa habari kutoka baina ya mipaka wajulikanalo kama Kijiografia yaani “Geo” journalists wenye maono ya uandishi habari kuhusiana na maji kwa maaneo ya Bonde la Mto Nile pande la Afrika kupitia msingi wa data na hadithi kwa vyombo vya habari za kisasa. Kazi zetu zinahusika na uandishi habari pekuzi na data  kama miradi muhimu ya maji na mazingira katika Bonde la Nile. Habari pekuzi za miaka iliyopita  zilizingatia  unyakuzi wa ardhi eneo Bonde la Nile, suluhu za jamii wenyewe kuhusu uharibifu wa ardhi oevu  jimbo la Afrika Mashariki, na  athari za viwanda vya mafuta na gesi nchini Sudan kwa mazingira na afya.

Oxpeckers Investigative Environmental Journalism ni kitengo cha kwanza ya wanahabari barani Afrika inayozingatia maswala ya mazingira. Kitengo hiki kinachanganya jinsi ya kuripoti habari za uchunguzi tangu jadi na uchambuzi wa data na zana za ramani za kijiografia ili ifichue makosa ya mazingira na kufichua makosa ya mazingira na wahusika eneo la Afrika Kusini, na wandani wao duniani.

 Kitengo hiki #WildEye tools kinawezesha wanaotumia kufuatilia uhalifu wa mazingira kote duniani.

Jinsi ya kutuma maombi ya Ufadhili: 

Tuma kwa barua pepe: info@infonile.org

  • Andika wazo la pendekezo lako ukielezea kwa uwazi kisa cha hadithi ( si zaidi ya

 ukurasa moja). Pendekezo lako lazima liwe lenye muundo wa kueleweka kwa uwazi, likianza kwa kuelezea kwa ufupi juu ya hadithi, ikifuatwa na jinsi na mahali hadithi itafanyiwa upekuzi, jambo linatarajia kupekua au kuvumbua na vile itachangia, penye utachapishia,(chumba kamili ya habari), na athari inayokusudiwa kusababisha. Pendekezo lako ni lazima liwe na mpango wa kujumuisha matumizi ya data. Tafadhali tiliamaanani jinsi utatumia habari mtindo wa kisasa(video, picha, sauti, michoro  pamoja na makala ). Pia unastahili kuweka yafuatayo :

  • Pendekezo la bajeti isiozidi  $300.
  • Wasifu kazi.Tafadhali kumbuka ujuzi wa kuchambua data ni nguzo muhimu wa mwaradi huu;
  • Sampuli mbili za kazi zako ulizozifanya hapo awali;
  • Barua ya mhariri wako inayodhibitisha ya kuwa kazi hii itachapishwa / tangazwa kwa redio au kupeperushwa kwa runinga.
Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp