Curity Adhiambo na Alis Okonji

Mto Kisian hupitia milima ya Kisian hadi kijijini. Mashamba madogo yanaonekana kwa umbali, huku  kilimo cha unyunyizi usio rasmi ukistawi ukingoni mwa mto.

Mary Akinyi Ouko, aliyeolewa akiwa na miaka 13 tu, alijiunga na jamii ya Kisian Mashariki ya Kisumu, Kenya, angali mwanamke mdogo; mchanga zaidi. Kwa miongo sita iliopita Ouko na familia yake wameishi kijiji hiki, huku wakipata riziki yao kutoka kwa mto Kisian, pamoja na mamilioni ya Wakenya. Walakini, yeye hajui chanzo chake.

“Kwa kusema kweli, sijui chanzo cha mto huu,” asema Ouko, mzaliwa mtunga hadithi asili, hapo anasisitiza kwamba “Najua unatoka mbali sana, labda Kajomwa- maneo ya Magharibi ya Kenya”, huku akikumbuka tu kumbukumbu zinazofifia.

CSBxXFLUdfGAFpljL Ui6pcxzk5hCfPtFaP0283bO4
Mary Akinyi, mkazi wa Kisian

Hata hivyo, ana uhakika na jambo moja: mto huu ni wa maana sana kwake na jamii ya hapa. Umehudumia bibi zao wakuu, ambao walipitisha manufaa ya mto huo kwao, na sasa wanawapitishia wajukuu wao. Umekuwa kama chemichemi kinachoendelea kutoa maji bila kulegea yanapohitajika. Ni chanzo cha maji ya kunywa kwa jamii na mifugo wao; wanayatumia kupikia, kwa kilimo na ujenzi, miongoni mwa mambo mengine. Mto Kisian unashikilia jamii hii pamoja; ukiteremka kwa siri, kumbukumbu, kifo, furaha, uovu, na mengi zaidi.

Ni kiini cha jamii hii.

Mto na Chanzo chake

Chanzo cha Mto Kisian unaanza kwa Msitu wa Maragoli na kuzungukwa na vyanzo vya maji ya Riat na milima Kodiaga. Unateremka kupitia Wilaya ya Kisumu.

MH3p7o 3S8K92IipDX93cE8vDnrfaeb pf6Zi77uIJKXXACPpFLqa9GZIcENXfRmfyVRWG68syzz6UZeNSnD 1 SybYpEMsNzmayfT4Nq tULNMLdTbUZQQpZYt2sYMaqfivGt2FmHmjErWNKMg7W8TqRTIMwOeIP 8gM6q1qKheTQhUYX
Milima ya kuvutia ya Kisian, kwenye Mto Kisian unapitia kabla ya kuingia kwa jamii ya Kisian.

Eneo hilo hupokea mvua mara mbili kwa msimu, mmoja mfupi kutoka Oktoba hadi Disemba na msimu wa mvua mrefu kuanzia Machi hadi Julai. Mvua hutofautiana kwa viwango kutoka 258.0mm hadi 816.0mm kila mwaka. Wakati wa mvua kubwa, sehemu za juu za mto hupata mvua nyingi sana, na husababisha Mto kufurika zaidi, kuvunja kingo zake na kuosha mashamba ya nyanda za chini.

Tabia na Harakati za Mto Kisian

Tabia inaweza maanisha utulivu na amani, pamoja na harakati kidogo au shughuli. Katika fani hii, ninarejelea mwendo wa Mto Kisian kama safari ya amani kabla tu kuingia kijijini.

Milima yenye mawe ya Kisian, kwenye mto unapitia, ni ya kuvutia sana kana kwamba ni ajabu usioaminika. Unapokuwa hapa, unajihisi kama unasafirishwa kwa ulimwengu mwingine ambao mambo yake ni tulivu tupu.

Nimekulia hapa. Safari hii ya kuandika masaibu ya Mto Kisian unanikumbusha utoto wangu wakati rafiki zangu na mimi tungethubutu kuogelea ndani yake. Bila shaka, nilikatazwa kuogelea kwa Mto huu kwa sababu mama alifahamu ningezama, na ni sawa kwa sababu singeweza kuogelea.

Hapo awali, nakumbuka  mto huu ulikuwa wenye kina kirefu, na kingo zenye afya pamoja na  mimea maji. Nakumbuka nyoka walikuwa wanazaana kando ya mto huu. Tungefua nguo zetu kwa kingo zake, kuoga na kuwaleta mifugo wetu kunywa maji. Kulikuwa na waogeleaji kila wakati wakipiga mbizi kutoka kwa ukingo moja hadi mwingine wenye kina kirefu, huku wapiga kelele, kucheka, na kucheza michezo mingi ndani ya maji. Hizo ndizo kumbukumbu za utoto ambazo ninathamini sana hadi sasa. Mto Kisian ulikuwa pahali pa furaha pwangu wakati wote.

Bow1CLqiNGTEf5jLsV LnUUv4o kFw3Vnr2PGlyEe KIYs9fGeyM 4Ki2JmLflm0ChDxb6ZOtiRu4dET199NdTiVNVsc7LHkXlRujE6hDRj0jWoeRtAZCHgfxn4oRPlkHtujQ707upslwaBgEKTcOaKTOMNnqUukVZ HWGG 8vwMKqTSjy1 mU6ekdY7nu2vUBWajcO9Xg
Wanawake wanafua nguo na kuteka maji Mto Kisian.

Mto Kisian kwa Usalama wa Chakula

Kijijini Kisian wakulima wanakuza mboga, mahindi, mitama, maharagwe, gramu za kijani, na kunde. Wanatumia maji ya mto Kisian kwa unyunyizi. Mamia ya mashamba yako kwenye kingo za Mto.

Chiro (soko la jamii) limejaa mazao kutoka kwa mashamba na bustani jirani ambazo wakulima, wafanyabiashara, na wanawake huweka bidha zao kila jioni kwa minajili ya kuuza.

Hd8ABz m9yRTwtc3A5E8nD4Kpmi8cN o07uj1WruPlb7Ynxk5b5Y76imPiVUyp6KeyaeNEMKX9ACYv7frZy2PkqbVHi l1iSEa8E yhwUVfPeRakBUOytEcmg1YqtONBWJByEvStrfKrSi2L4 HeMjzpZ6gnZML TYKSzylb4LedRE kLtGfoYY1BIl9 0Zn4Gihkc9EAQ
Sukuma wiki hustawi chini ya unyunyizi usio rasmi kando ya mto.
6HmlGhBLumDtrjrCe9bwlVQEJKfF09Wl kknn4onXhDdRccJeA
Jamii hii pia hupanda mtama, hasa kwa milima yenye rutuba zaidi na vilevile kando ya Mto.
njoFavGgby5qhM1LAjzyycgsPB4MofYHFHW sMsDmMZyb5 lwLdYtQHHdgw7WUx KxxmhMqKwkKu7D3qaDz77HYmDJSRn2ZFBgokHiLDKy0R2gwZCHVSVhAmMHoQphkGR9d3NWBOJgZBh8aX Qtogpihcx
Aina mbalimbali za ndizi hustawi kando ya Mto Kisian.
u SLLU7DcRE1nBFpNytanwK96v0JFTE2n TRQi6bMBj4UVqbTt 7yC2G01WLtXw4O7OlTMWiSvaPAq6xz6e56c5918ZbL0LrFhX 4sNAHp8ZAq0Z8yEXTNUtZRLTOpWq4VQgbcKm4ThCZbsKsLJhPvnZLSdV3pmS2fD8sOT0nTa0OQX7aclfDMOws
Shamba la mpunga ambalo linategemea sana unyunyizi usio rasmi kutoka Mto Kisian. Jamii hii haijulikani kwa kilimo cha mpunga, lakini mto Kisian umewawezesha  kuwa.

“Niliwahi kuwekeza kwenye kilimo wakati ulikuwa wazi nisingeweza kupata kazi haraka baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu. Nilihitaji kutunza familia yangu; kilimo kando ya Mto kilinisaidia kwa kupata maji kwa urahisi kumwagilia matunda na mboga zangu, ambayo ningewauzia wanawake sokoni kwa faida,” Francis Oduor, mkulima wa zamani na mhitimu wa Chuo Kikuu cha Egerton.

Licha ya usalama wa chakula unaoonekana wa faida za kiuchumi wa Mto Kisian kwa jamii hii, manufaa ya unyunyizi endelevu kwa ardhi na kilimo ni suala linalojitokeza.

Mwaka wa 2015, Sekretarieti (Nile-sec) wa Nile Basin Initiative (NBI) ilifanya Uchambuzi Mkakati wa Rasilimali za Maji kwa nia ya kuendeleza endelevu ya kukidhi mahitaji ya maji yanayozidi kuhitajika kwenye nchi maneo ya mto Nile, ikiwemo Kenya, na kupunguza shida za maji ya sasa na baadaye.

Utafiti huo uligundua kuwa upanuzi na kuimarisha kilimo ni muhimu kwa kuhakikisha usalama wa chakula, uboreshaji maisha, na kupunguza umaskini katika bonde. Uboreshaji wa vifaa vya unyunyizi unazingatiwa kuwa mkakati muhimu kwa kuongeza tija katika kilimo.

Kulingana na ripoti hii, nchi za Uhabeshi, Kenya, Sudan, na Tanzania, eneo chini ya  unyunyizi kwa mimea ni ndogo sana likilinganishwa na eneo lililopangiwa unyunyizi kutokana na utofauti kati ya maji yanopatikana na mahitaji yake.

Mto Kisian uko katika eneo lililorodheshwa kati ya Entebbe Nile Basin Initiative (NBI)) kwa msingi wa Juhudi za Pamoja ya Bonde la Nile kwa ripoti yao ya kiufundi  kama Pembezoni hadi Wastani inafaa kwa unyunyizi. Ripoti hiyo ilikadiria ufaafu wa ardhi kwa kutathmini udongo na ardhi, mteremko wa topografia, na mali ya udongo kikamilifu na kikemikali.

Shughuli za kibinadamu, zikiwemo ukataji miti na ukulima kando ya Mto Kisian, husababisha kuongezeka kwa joto la maji, umeme majimaji, jumla ya vigae vinavyoelea na kuchanganyika  kwa maji na tope, hii ni kulingana na Kituo cha Utafiti wa Uvuvi  na Baharini ya Kenya (yaani, Kenya Marine and Fisheries Research Institute -KMFRI).

Mifugo wametumia vibaya  maeneo ya kando ya mto na kuongeza amonia na nitriti kutokana na kuongezeka kwa chafu za mifugo kwenye vijito. Shughuli za binadamu  kando ya mto kama uchimbaji mchanga, kuoga, kufua nguo na kilimo cha mimea yanayopandwa kwa mistari imeathiri  pakubwa makazi na mkondo wa kijito na sifa za kibayolojia. 

Kwa miaka mingi, ukingo wa Mto Kisian umekuwa ukikabiliwa na uvunaji mkubwa wa mchanga, na kusababisha mmomonyoko mkubwa wa udongo wakati wa mvua kubwa au mafuriko. Mto Kisian unafahamika kwa kuvunja kingo zake wakati wa msimu kama huo, lakini maporomoko ya ardhi yanaelekea kusababisha kingo zake kupanuka kwa sababu ya mchanga kuvunwa.

Juhudi za pamoja ya Bonde la Nile inafahamu ya kuwa kutekeleza vipimo vya mwenendo wa mazingira kwa mahitaji yako kwa hatua ya mapema. Sera za kitaifa zinazoshughulikia mwenendo wa mazingira ni za Tanzania na Kenya pekee. Tathmini na ufuatiliaji zaidi kwa hali ya kihaidrolojia na za maji masafi na mifumo ya ikolojia inahitaji mpango endelevu na usimamizi wa kuhifadhi maji . Mwenendo wa mazingira kwa ufupi ni ubora na wingi wa maji masafi kwa kijito au mto kwa muda mrefu.

Nchini Kenya kanuni ya matumizi endelevu husema kwamba, rasilimali za mazingira zitatumika kwa namna ambayo haziathiri ubora na thamani ya rasilimali, au kupunguza uwezo wa kushikilia mifumo ya ikolojia.

Hali Mbaya

oyRuC qmfPRWg7IekvI9aYda1lZ5uN5nKbgj5fhEfTE7iBn3a8 ujl6pufB2HQUbnvOS1 5JqkIYqHVQlG37WdNKOh57Ln7sWRj7iF0B qDYco5bbXKgaq8F8a9osK CZuRLW NZ6dq3QpqF0mpNjSygskoULy0d 8tNx FIol8NAw8ShGe2eTF uhFDjJJtT8qOeS9BfQ China ya daraja la makutano ya Mto Kisian, mita michache kutoka kwa soko la Kisian ni mahali wakazi wengi huja kuteka maji ya kunywa or kupikia. Msichana wa shule pia anaviosha viatu vyake kando ya ukingo. 

DKBMYFKm xhYoeDH1YKBQHEvQo bx4EPTjSisunxj1Ry0od0C yIsGmeUBmaFcHZfjtQne6vKa C5fJjkjoT0w9W5OO0V0X7ZSQOdJ xDfFi6bqAYs1PvnZC1Lte6IsJQc3gPT hULAnbiryzQKb
Miamba iliyokusanywa kando ya kingo za Mto Kisian inasuburi kuchukuliwa. Sehemu hii ya Mto kiasili imejaliwa mawe mengi kwa sababu inakaribia milima. Mawe na mchanga  hayajasazwa hapa. Kuna uvunaji mkubwa wa miamba pia ambayo inaendelea katika mto huu.
AkCPG2IZHithVcCt1S9L dwdkXPlD30rHY0IDJ6bGOBJAwjFfrgzuI5wUu3I25xRAdTOetOlTqDU9F3mr6HWYARfNvnROK37ILxAmPIJEhNp4D88RuGaN1Cl tRsM7S8VD2P3hAtwWuzXu5AOefetzAPBk40YdkMbXnYQsfvlN9LD HU2Rvj2GHMijgxBXAtlfH rJ9RRg
Nyumba ilioko hatarini kusombwa na maji, labda wakati mvua kubwa ijayo itakaponyesha. Mvulana anatazama.

Mbali na mchanga na miamba, kuvunwa kwa mchanga aina ya klei ni shughuli nyingine ya uharibifu wa uchumi wa mazingira zinazofanyika kwa Mto Kisian. Vyungu vya ajabu na vilivyochongwa vya kupendeza ni baadhi ya vifaa vya ufinyanzi kutoka kwa udongo uliovunwa kwa kingo za Mto Kisian.

“Wanawake wengi wanategemea ufinyanzi kwa kulisha familia zao. Uvunaji wa udongo umekuwa katika jamii zetu kwa miaka mingi! Miaka michache iliyopita, baadhi ya wafinyanzi walizikwa ndani ya machimbo hayo huku wakichonga udongo,” asema Mourine, mkazi hapa.

Wavunaji wa udongo mara nyingi hushawishiwa kuchimba zaidi kwenye kingo za Mto kwani wanaamini  huko ndani wanaweza pata udongo uliosafishwa zaidi, laini na bora zaidi. Vichuguu na machimbo waachao  nyuma huathiriwa kwa kusombwa na maji na mara nyingi kuanguka.

Erza3SS0WyrZDEhHexVOldz12ayx2dfirx2kO K82ZgoDKLNheJzxdf0OZ2Bq8AzzvizsA5PmjhEImLTZW kH0LcxU3O6AyFufjMcQKKLDF2k0KS46DDvykQUjUy3hfbMYeBrrRj6SRG0zwCc2RJVReNjfOSLLUp
Mourine Awuor, mkazi wa Kisian.

Watoto wanaotumia barabara hii wanalazimika kuvuka Mto kila siku ili kwenda shule pia wako hatarini kwa sababu  daraja iko karibu kuporomoka na barabara za kutembelea zimemomonyoka. Hivi karibuni harakati katika sehemu hizi za Mto Kisian zitakuwa haziwezekani. Licha ya uharibifu unaoonekana, uvunaji wa udongo unaendelea kutokana na ukosefu wa ajira na umaskini.

“Hawa wavuna mchanga sio watu waovu; ni watu tunaowajua; hawana ajira; jinsi gani nyingine wanatakiwa kutunza familia zao,” alihoji mwanamke mmoja ambaye jina lake halikufahamika akiyachota maji karibu na miteremko ya kingo zilizomomonyoka. Maji aliyokuwa anayochota hayakuonekana kuwa safi hata kidogo.

mwanmke kisian
Mwanamke akiyateka maji kwa ajili ya familia yake kwa Mto Kisian.

Nashangaa alifikaje pale na atapandaje akirudi.

“Nimezoea,” asema, “lakini inakuwa ngumu zaidi na zaidi kuyapata maji kutoka upande huu wa mto kutokana na miteremko. Wakati wa mvua, hatuwezi hata kukaribia kingo hizi; ni mtego wa kifo” anaeleza.

Vile ninavyofahamu, shughuli kama uvunaji mchanga zinaweza kusababisha matatizo yao; jamii hawajui cha kufanya, wakiwaona wavunaji  mchanga wamezidi ujanja wenye mamlaka.

Wakati Mamlaka ya Kitaifa ya Mazingira (NEMA) wanashika doria, lori zinazosomba mchanga wakati wa mchana hubadilisha wakati na kufanya kazi hiyo usiku.

Mteremko mkali karibu na mto ambao madonge ya mchanga zimevunwa.

“Tumepoteza mifugo wetu wengi sana kupitia mto huu. Ikiwa ng'ombe atateleza ndani haswa wakati wa mafuriko, haiwezekani kumtoa.Tunaangalia ng'ombe wakifa. Watoto wetu pia wako katika hatari kubwa,” alieleza kabla sijamtazama akirudi akipanda mlima unaoonekana kuwa hatari akielekea nyumbani kwake akiwa ameekeza mtungi wake wa maji kichwani. 

Uvunaji wa mchanga unaathiri ubora wa maji aje? Sayansi

Hapo zamani za kale, Mto Kisian ulikuwa chanzo maarufu kwa samaki, anayefahamika sana kwa eneo hilo ni kambare almarufu kama mumi, lakini hii sio hali kwa sasa. Hakuna shughuli za uvuvi tena kwenye Mto huu; wanyama wa majini walikwenda wapi?

“Uvunaji mwingi wa mchanga kwa Mto Kisian umechafua maji na kusababisha hasara kwa mimea na wanyama wa majini waliokuwa wakinawiri ndani ya mto” aeleza Linet Andiego, Mwanasayansi wa Ubora wa Maji na aliyekuwa katika Mamlaka ya Kitaifa ya Mazingira chini ya sehemu ya Ubora wa Maji.

Wakulima kando ya ukingo wa Mto Kisian wanatumia mbolea za kemikali na dawa za kuua wadudu kwenye mimea yao. Kupitia unyunyizi na wakati wa mvua, kemikali hizi hupata njia ya kuingia mtoni kupitia mkondo wa hayo maji, na hivyo kubadilisha hali ya kawaida ya maji (pH). Kupanda au kushuka kwa pH ya mto pia una jukumu kubwa katika maisha ya wanyama na mimea ya majini, ambayo imekuwa sababu ya upotevu wa maji, anaeleza Andiego.

Kiwango cha pH pia huathiri familia wanaotumia maji haya bila kutibiwa, mifugo wanaokunywa, na mimea iliyonyunyiziwa maji yake. Kubadilisha pH ya maji ni hali nzuri kwa magonjwa ya bakteria kwa watu na mifugo. Kemikali na uchafu kwa maji inaweza pia kusababisha kukauka kwa mimea na kusababisha uhaba wa chakula.

Rangi ya maji ya Mto Kisian ni kahawia kwa sababu ya shughuli za kuchimbwa kwa mchanga kutoka mtoni ambayo husababisha uchafuzi wa matope (kipimo cha uwazi wa angalau kioevu) cha maji.

Mchanga una jukumu muhimu katika kudumisha na kusafisha maji. Wakati mchanga unavunwa, hasa kwa kiasi kikubwa kama Mto Kisian, hakuna mchanga wa kutosha kwenye mto ili maji yasafishwe yakawa safi zaidi.

Uvunaji wa mchanga husababisha kupotea kwa mimea kando ya kingo za mto, kulegeza udongo katika eneo hilo, kuifanya ikabiliwe na mmomonyoko wa udongo ambao husababisha maporomoko ya ardhi. Hii inachochea kwa kupungua kwa wingi wa maji na mwelekeo wa maji kwa mto, na kusababisha ugavi wa maji yasiotosha kwa jamii wanaoishi maeneo  ya juu ya mto ambao hutegemea sana maji hayo.

Z0dqmfpxOqR8LuSDEiiTmw9gnmrqx 84qI7lg5jAb6Qyi6EPm9wmYucW2lyIzNggJ8wvmzYgYe1Hiu5p9hv 86s3IGnT6AJ YiVGyHGKRRW2xc8 cuAA2NZx7AfKSY ggakAXr
Rangi na ubora wa maji ya Mto Kisian yaendelea kuzorota baada ya miaka mingi ya kupuuza

Uvunaji wa udongo, zikiwa pamoja na klei na mchanga, husababisha uharibifu mkubwa wa kingo za mto na mfumo wa ikolojia na huzuia ukuaji wa bioanuwai katika eneo hilo. Hivi ndivyo tunavyopoteza aina tofauti za wanyama, samaki, na mimea ambayo hapo awali ilistawi katika ukanda wa mto huo.

Je, Jamii/viongozi wamejaribu kutatua suala hilo?

Mbunge aliyemaliza muda wake wakudumu, Olago Aluoch, alijenga daraja mwaka 2013/2014 ili kusaidia jamii kuvuka mto huo kuhudhuria shughuli zao za kila siku kwa upande mwingine na vilvile watoto wa shule huvukia daraja hiyo wafike shuleni. 

XuyK VZyPCejfL 3HGPdXMren2GJ9K3K0 r9Qe3xfEipF08sqEzn5 DQOSxgjoqRFcvB1imQd CjEK8eIpUyQHK8uoWh77bgbMNESZYwIK5xqp
Daraja hili linakaribia  kuanguka kutokana na kuendelea kwa uvunaji wa mchanga na mmomonyoko wa udongo inayosababishwa na mvua kubwa.

Kando ya daraja, shirika la KEMRI(Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya), lilijaribu kusaidia kwa kujenga mfumo mpya wa mifereji ya maji na kuweka mitaro mipya ya maji badala ya iliyojaa mchanga kusaidia kukabiliana na ongezeko la kuporomoka kwa mto, bila mafanikio.

Chini ya Sheria ya Madini, mchanga ni mali ya serikali licha ya eneo la ardhi na umiliki wake. Hii ni kulingana na Katiba ya Kenya kwenye Ibara ya 62(3) inayowezesha serikali ya kitaifa kumiliki madini pahali popote.

Licha ya serikali kumiliki mchanga chini ya Sheria ya Madini, uvunaji wa mchanga nchini Kenya unaonekana kutawaliwa na watapele ambao kila mchimba mchanga wanaendesha shughuli hizo kama wao ndiyo wenyeji.

Katika utafiti wake wa 2021 kuhusu uvunaji wa mchanga nchini Kenya na maendeleo endelevu, Caroline Njoroge anasema kwamba ufikiaji kwa ardhi ya umma kwa urahisi (miti na mwambao wa pwani) umepunguza hali ya hatari na gharama ya chini kwa bidhaa zinazohitajika hivyo kuunda ushindani kwa maeneo yaliyo chini. Hakuna kinachotia motisha kwa wavunaji mchanga au wafanyabiashara au wanaosimamia ili wahifadhi rasilimali. Hatua zozote za kuhifadhi zinakabiliwa na hali tata ya upinzani . Kwa sasa hakuna njia sahihi yakufuatilia asili ya rasilimali za mchanga, hivyo kuacha mwanya wa uchimbaji haramu wa mchanga.

Kuna haja ya kuoanisha muundo wa utawala uliogawanyika ili kuweka msingi dhabiti ambazo zinaweza kusaidia kuokoa mito iliyoko Bonde la Nile inayopitia hatima kama hiyo.

Je, kuwahamasisha wachimbaji mchanga kujiunga na shughuli mbadala ya kujiongezea kipato ni motisha ya kusitisha uchimbaji mchanga kikamilifu?

A4HFas4jwohH431CMW2UHHdKqHOebv NjvzX goPMyJoMFLRDMztsXhK2zX1JDhnXVmPbforUzM6av0H9Td4r7guAnZTaFAsRB4WhI7a YR 8Yb6S0qhXLjTHFkucVOBsUXEp n5GgwN5HVjZkKTNi4JAmiCyjEs8Q1WT3MqZx
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kisian wakivuka daraja wakati Mto unaendelea kupanua kingo zake huku njia zilizotumika kwa miaka mingi zinapotea.
JEQGQ0zECy7laNT39p8KKvfl18pcWM TciZkKfThpXktELXg3bsxJwRaaOfLiOAziVSkhCsZ6thIFQjsraGt50ogqMfBQdty9rp7ZT86tGxANifpyey 0o5Z9vjhZEsGrnBM1OJQMAKxUvN BsQd1fSZ5Ex6BvX3hJQe2iI8W CbqpmmqUURDetA1rXaLeo4SqKvfb72Rg
Mchanga uliovunwa, tayari kwa uchukuzi.

Mtazamo wenye Matumaini

Kabla Mto Kisian kumwagilia maji Ziwa Victoria, hupitia jamii ndogo iitwayo Rota. Hapa, maji yanapokaribia Ziwa, kuna daraja kuu ambalo limesimama imara kwa miaka mingi.


Kwa wakati huu, kingo za Mto Kisian zimejengwa upya kutumia kuta za mawe na mitaro ya maji ambayo mara nyingi huisaidia kuhimili mafuriko wakati wa mvua kubwa.

Hakuna uvunaji wa mchanga unaoshuhudiwa katika sehemu hizi za Mto. Kuta za mawe zimejengwa chini yake, na daraja imesimama kwa msingi imara inayohakikisha huduma yake inaendelea kwa jamii kwa miaka mingi.

fjrP4xT4zAv047NBPNZMN2JE5cM SpVdwPqcURq5HhMPVHgmBDloV9y8OuunJla1jRjRkEyvrHuG 4VSzYNLBL6Dxm03xVMcQ8IjmvMvHHGl72JaMWrRIsOqK 4PWPXu7y8niIvWHuurMRaiQyoElqQyftSNEhCGw7IyGf4XnhVrjxJIVkrlk5 6jEs7 URJgrjkjL 3mg
Daraja la Mto Kisian eneo la Rota

Rota ni jamii ya mfano bora kwa kuongoza katika uhifadhi na urejesho wa Mto Kisian.

James Alai, mwenye umri wa miaka 85, mmoja wa wazee wa jamii ya Kisian, anataka hatua za haraka za kurejesha Mto Kisian.

Anawataka jamii ya Kisian wachukuwe mfano kutoka kwa mikakati ya Jamii ya Rota ili nao pia wahifadhi sehemu yao ya Mto.

BB43 uOAY8DvOAeyIAHL2QouyT8jeV6Q8odEpNcdE1ZbuRXd3eT4P8gBGinM3ClZrupIDQhodeZKr2wGDcBjsuSgzb eI88kHQgut 9fS mJQ1pLCnVVlSfQccTBicVAZ3SnIp2eHCDwqC8
James Alai, mzee wa jamii ya Kisian mwenye umri wa miaka 85.

Baadhi ya wakazi  wa Kisian pia wamewekeza kwa kupanda mianzi kwenye kingo zilizomomonyoka kwa mto. Mianzi husaidia kwa kufufua hali nzuri ya udongo. Matumizi ya mianzi husaidia kwa kudhibiti mmomonyoko wa udongo mbinu ambayo imeonekana ikifanikiwa kote duniani. Mbinu hii ya kutumia sifa za mianzi na uwezo wa kimakanika ni gharama nafuu kwa uimarishaji wa sehemu za mteremko. Mianzi ni rahisi  kwa kuzaliana na ukuaji wake wakufunika udongo pia ni wa haraka. Jamii hii ina busara ya kutosha kutambua vile wanaweza punguza mabaya yaliyofanywa kwenye mto huu, upanzi wa mianzi ni njia ambayo ikitekelezwa na wote inaweza saidia kurejesha mfumo wa ikolojia na kustawisha viumbe vyenye uhai kwenye Mto Kisian.

“Mianzi hukua haraka sana na hufunika sehemu pana kwa sababu ya asili yao ya ukuaji, husaidia kulinda na kwa kufunika udongo. Pia husaidia katika kupunguza mmomonyoko wa udongo na kudumisha uwiano wa vijidudu. Halikadhalika husaidia katika usawa wa virutubisho vya udongo na kupunguza kukatika kwa maji,” anasema Andiego.

Mkazi wa Kisian, anapanda miti kadhaa ya mianzi kwenye miteremko mikali ya mto, juhudi inayolengwa kwa kudhibiti mmomonyoko wa udongo.

Safari ya Mto Kisian katika Ziwa Victoria; Mzunguko wa nyumbani

Wakati maji ya Mto Kisian yanasafiri chini ya milima na miamba viungani vya Kisumu, yanajitokeza tena, baada ya kuhimili shughuli za uharibifu wa mazingira zinazoelekezwa ndani yake.

Kwa mkondo wake wa mwisho kuelekea Ziwa Victoria, Mto Kisian unashika kasi tena kama mtoto anayekimbia kwa mama yake, huku akililia msaada. Umeimarika kwa kina na nguvu. Eneo linalolizunguka ni kijani. Shughuli za uvuvi zipo tena. Kando za mto zina afya na pembeni mwa mto zimejazwa maisha; jambo nzuri la kutia moyo, na viumbe vyenye uhai ndio msingi wake.

“Ndiyo, hapa ni kina sana; kama unavyoona, hata tunavua samaki kwa kutumia mashua za mwendo wa kasi; ukizama hapa, hatutakupata kamwe. Inaweza kumeza mtu mzima,” mvuvi kutoka jamii ya Rota anasimulia kwa uchangamfu, huku yeye na wavuvi wengine wakipita kwa kasi baada ya usiku kucha wenye mafanikio wa kuvua samaki.

XTIpkB2tqAXqo5PO5pnTmmGuOheyWhNp74qZ1IxNq9cOnxcdmnZWagU SIW wQL5LA0SDz6vxol3zwN6uCJMbHK3glFaEqTxTI2WZXLBKjgrPeB6ElITTkfTbvmhS4DsXSqN3rJxMChP Z7BAYZzx1wOSMFYu4F0uhDG9vP65EvThvSBd 7t3Xw7mAn
Mita michache kabla ya Mto kuingia kwa Ziwa Victoria, Wavuvi wanaandaa nyavu zao za uvuvi tayari kwelekea  Ziwani wakitumia mashua za mwendo wa kasi.
VH8Fha7RD ao2HDv3yhWTC6j0s Q0W A1 rWNzi rTLMjToaaDoJd1aZcN8W9kOeErzwCgRZbL37g7UT0AWlWucictdPAOZWPZF5Rnz23THqY03tIcjl9 m2qFhOIpiGyfrY9gV6rCosYgeocqOVU9z8bVz GqP a5mApN2vfXAPg

Ni mtazamo wa kuvutia Mto Kisian hatimaye unapojiunga na Ziwa Victoria, huku kukiwa na pumzi ya raha hewani si kwa jamii pekee wanaoutegemea na watoto ambao wanaishi kuvuka kila siku, lakini pia kwa Mto wenyewe ambao umetoka mbali katika safari iliyojaa changamoto ya mapambano, maumivu, kupuuzwa, furaha, na maisha.

Hatimaye, Mto Kisian umefika nyumbani na kuunganishwa na Ziwa Victoria kwa kumbatio la daima. Mto Kisian unalilia usaidizi wa dharura. Dhidi ya shughuli za kibinadamu. Dhidi ya viongozi fisadi Mto Kisian unaungana na mito mingi katika Bonde la Nile, kulilia urejesho.

Hadithi hii ilitolewa Juni 2022, ilidhaminiwa na InfoNile na Media in Cooperation na Transition (MiCT) kwa ushirikiana na Nile Basin Initiative (NBI) na kwa msaada kutoka kwa Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH, iliyoagizwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.