COVID 19 inasababisha hofu ya vifo vya wanyama na kupungua kwa watalii

Prosper Kwigize- Kigoma, Tanzania

Skiza habari hii kwenye SoundCloud

Wakati biashara ya maliasili na mazingira inazidi kushamiri duniani, mazingira hatari na ulinzi mdogo wa wanyamapori zinatajwa kuwa ni vitisho vikubwa kwa uchumi wa Eneo la Maziwa Makuu hasa Tanzania ambako utalii ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya serikali. Tanzania iko katika orodha ya nchi ambazo zina vivutio vingi vya asili zikiwemo mbuga za wanyama ambazo ni vivutio vya kidunia kutokana na wanyama wake waliomo kama vile twiga, simba wanakaa mitini, vifaru, viboko, ndege, vipepeo na sokwe ambao wanafanana sana na binaadamu. 

Mbuga za wanyama za Gombe na Mahale zilizopo kandokando ya ziwa Tanganyika ni makaazi ya sokwe ambao wamekula maarufu sana, baada ya serikali ya Tanzania pamoja na taasisi za kimataifa kuanzisha mpango mkakati wa utafiti na ulinzi wa sokwe hao. 

Hifadhi ya wanyamapori ya Gombe iko umbali wa kilometa 25 kutoka bandari ya mji wa Kigoma. Hifadhi hiyo ndimo wanamopatikana sokwe hao wanaofanana na binaadamu kwa kiasi kikubwa na ambao wamekuwa kivutio maarufu cha watalii duniani. Watalii hufika katika hifadhi hiyo kwa boti kupitia kwenye ziwa lenye kina kirefu kuliko yote barani Afrika, ziwa Tanganyika. 

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa maliasili lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, vitendo vya watu ukiwemo uwindaji haramu, kilimo na ufugaji Hifadhi za Wanyama za Gombe ziko hatarini kutoweka kabisa duniani. 

Afisa Hifadhi Mwandamizi wa Gombe Bwana Pellagy Marando ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utalii  aliiambia InfoNile pamoja na Radio ya Sauti ya Ujerumani (DW) kuwa sokwe hao wanakabiliwa na kitisho hicho cha kutoweka kabisa duniani kutokana na ongeseko la vifo na sababu myingimezo kama vile kuharibiwa kwa makaazi yao ya asili (misitu), ukataji wa miti kwenye hifadhi, ukosefu wa chakula pamoja na magonjwa. 

Hifadhi ya Wanyama ya Gombe ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 56,000. Mbali na sokwe, kuna jamii zingine za nyani, swala, mijusi na nyoka. 

Takwimu kutoka Mamlaka ya Uhifadhi ya Gombe zinaonyesha kuwa idadi ya sokwe hao imepungua kutoka 150 iliyokuwepo mwaka 1980 hadi kufikia 90 katika mwaka 2020. Takwimu hizo zinainyesha kuwa kuna hatari ya kutoweka kabisa wanyama hawa kwenye uso wa dunia kama inayoonyeshwa katika jedwali lifuatalo.

Mtafiti katika Taasisi ya Jane Goodall Dk. Anthony Colin kutoka Scotland ambaye ameishi Tanzania kwa miaka 30 akitafiti kuhusu sokwe hao amesema sababu kubwa inayosababisha vifo vya wanyama hao ni magonjwa ya kuambikiza hasa mafua ambayo yanatokana na muingiliano wa wanyama na binaadamu wanaoingia katika hifadhi kwa ajili ya masuala kama vile utalii, uwindaji haramu, kilimo, utunzaji misitu na wanyama. 

Dk. Collins alisema kuwa takribani kila mwaka sokwe mmoja hufa na mwaka 1987 sokwe tisa walipoteza walikuwa na miaka 10 baadae wengine tisa walipoteza walikufa kutokana na mafua ya binaadamu. Baadhi yao vifo vyao vilisababishwa na magonjwa mengine pamoja na mabadiliko ya haki ya hewa. Njaa iliyosababishwa na uharibifu wa mazingira pia ni sababu nyingine ya vifo vya sokwe hao katika kipindi hicho.  

https://lh3.googleusercontent.com/iixcjSuYVDUDRozZkOez6kkGloT_dOs1fFAjI9LD555dT4IiAyGWMLCW8vbO2LTdA5LjTuLMFgMDJq0FB8eyZUBC9Q4byLX8FoLIBRJwVQKRqf4XrlWTeloyYWY8oDMYs8SZtGM

Uharibifu wa vyanzo vya chakula cha sokwe hao pamoja na maeneo yao ya kuzaliana ndiyo sababu kubwa inayowalazimisha baadhi ya sokwe hao kuyahama makaazi yao ya asili na kwenda katika maeneo mengine ambako wanahangaika kupata chakula na malazi. Wakiwa huko katika maeneo ambayo hayana ulinzi, mara nyingi hukutana na wawindaji haramu ambao huwauwa kwa sababu mbalimbali. 

Inakadiriwa kuwa kama wananchi hawataelimishwa juu ya umuhimu wa misitu na hifadhi za wanyamapori sokwe waliomo katika hifadhi ya Gombe pamoja na nyinginezo watakabiliwa na kitisho kikubwa zaidi cha kutoweka kabisa katika uso wa dunia kufikia mwaka 2030.

Hii inatokana na uvamizi wa maeneo ya hifadhi na uharibifu wa ardhi asilia unaofanywa kwa kasi kubwa sana na jamii wakiamini kuwa wanyamapori wako hatari misituni. 

C:\Users\Buha Fm\Pictures\2020-07\20200723_160414.jpg

Kijiji cha Mkatanga katika Wilaya ya Kigoma ni moja ya maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Gombe katika kingo za ziwa Tanganyika ambako huharibifu wa mazingira unaonekana wazi kabisa. 

Sababu nyingine ni ongezeko la kasi la idadi ya watu nchini Tanzania ambapo watu wamekuwa wakiongezeka kwa asilimia moja kila mwaka tangu mwaka 1960. Wakati wa uhuru wa Tanganyika kulikuwa na watu 10,346,697 sawa na ukuaji wa asilimia 2.93. Lakini takwimu za mwaka 2020 zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao 59,734,218 ambao ni sawa na ongezeko la ukuaji wa asilimia 2.93 hadi 3. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Takwimu nchini humo, NBS pamoja na makadirio ya Umoja wa Mataifa. 

Ongezeko hilo lina athari za moja kwa moja katika hifadhi za misitu na wanyamapori kwani zenyewe haziongezeki na badala yake ardhi yake hupunguzwa na binaadam na kutumiwa kwa kilimo makaazi ya watu. Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania kutoka mwaka 1960 hadi 2020. Takwimu hizi zinajumuisha na makadirio ya Umoja wa Mataifa hadi kufikia mwaka 2100.

https://lh3.googleusercontent.com/I1ax2_9k090mms6MKozpfTtB0aA3rBQiRBZsHDVPqEp2VD0Rm7etq844uZG1FIQ9aj_CgMIWLBQKCvzB_c5WhKSyFuGNRUqg_d_G-9Puws2WTtUKOB3u-idV7-p6Fq5W9hgpQlQ
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=_dMb_kHCBXg[/embedyt]

Uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi unatokana na jamii hizo kutokuelewa umuhimu wa kuwepo kwa misitu na wanyamapori. Mbali na hilo, wananchi pia wanaamini kuwa wanyama hawawezi kupotea kabisa duniani hali ambayo inafanya vitendo vya uwindaji haramu na ukataji misitu vizidi kushamiri katika hifadhi za taifa. 

Deus Makungwa ni mkazi wa Mpanda katika mkoa wa Katavi ambako ndiko iliko Mbuga ya Wanyama ya Katavi yenye viboko wengi, twiga, Ng’ombe mwitu pamoja na simba. Wakati wa mahojiano Deus alisema kuwa Watanzania wanapaswa kunufaika moja kwa moja na wanyama pamoja na maliasili zilizomo katika hifadhi na si kuwanufaisha watalii pekee, maofisa wakubwa wa serikali pamoja na makampuni ya uwindaji. 

“Rais wetu Dk. John Magufuli alikuja Katavi na kuahidi kuwa mfumo wa kuwinda wanyamapori hasa Ng’ombe pori utawekwa pamoja na mabucha ya kuuzia nyama ili wananchi nao wanufaike. Lakini hadi leo hakuna kikichofanyika”, alisisitiza Bwana Makungwa. 

Licha ya kiu ya Makungwa ya kutaka serikali iweke Mfumo huo, Noelia wa hoteli ya Mpanda yeye anakubaliana na faida za kutunza hifadhi za wanyamapori.

Alisema kuwa utunzaji huo u a faida nyingi ikiwemo fursa ya kuwavutia watalii kuja kuona wanyama jambo linaloweza kuchangia ukuaji wa uchumi, kufungua fursa za ajira kwa vijana na wanafunzi wa ngazi mbalimbali za msingi, sekondari na vyuo kupata sehemu ya kwenda kufanyia mafunzo kwa vitendo. 

“Utunzaji wa misitu na wanyamapori ni muhimu sana kwetu. Siungi mkono kabisa uwindaji haramu. Natoa wito kwa serikali kuanzisha mfumo wa utoaji elimu juu ya umuhimu wa wanyamapori na misitu katika hifadhi za taifa. Hali ilivyo sasa si sawa kabisa kwa ustawi wa mazingira na wanyamapori”, aliongeza Bi. Noelia. 

C:\Users\Buha Fm\Pictures\2020-07\20200723_120636.jpg

Sokwe katika Hifadhi ya Wanyama ya Gombe akiranda mitini jambo ambalo ni utaratibu wa kawaida wa maisha yake ya kila siku. Wanahitaji kulindwa. 

Athari za COVID 19 katika utunzaji wa wanyamapori

Wakati idadi ya wanyamapori inazidi kupungua nchini Tanzania, mripuko wa virusi vya Corona nao umeleta kizaazaa katika sekta ya uhifadhi wa wanyamapori.

Watalii wamepungua sana na kuna hofu kuwa sokwe wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizo ya Corona. 

Afisa Uhifadhi, Ikolojia na Utalii Bwana Pellagy Mara do amegundua kuwa watalii kutoka Ulaya, Asia na Amerika hawakuja kuona wanyamapori nchini Tanzania kwa kipindi cha miezi 3 jambo ambalo limedhoofisha kiwango cha mapato katika sekta ya utalii kwa asilimia 80.

Ingawa Marando alikataa kutaja kiwango cha mapato yanayopatikana kwa mwaka katika sekta ya utalii, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangalla alinikuliwa akisema kuwa sekta hiyo inachangia asilimia 17 ya pato la taifa kwa mwaka hivyo kupungua kwa asilimia 80 kunamaamisha anguko kubwa la sekta ya utalii nchini humo baada ya kugundulika kwa virusi vya Corona.

Je, nini kifanyike kuzuia virusi vya Corona visiingie katika hifadhi za wanyamapori na kuzuia kupungua kwa sokwe kunakoendelea sasa nchini Tanzania? 

Dk. Anthony Collins kutoka Scotland ambaye anafanya kazi na taasisi ya Jane Goodall amesisitiza kuwa njia pekee ya kuwalinda sokwe hao ni kuzuia watalii kuingia katika hifadhi kwa wingi na kwa wakati mmoja. Kuwekwe utaratibu wa kupima afya za watalii na wafanyakazi wa hifadhi kabla hawajaingia mbugani na kuzuia watalii wasiingie katika makaazi ya sokwe. Pia mamlaka zihakikishe kuwa kila mtalii, mfanyakazi wa hifadhi na watafiti wanafuata kanuni za afya kwa kuvaa barakoa na kutumia dawa za kuuwa vijidudu mikononi wakati wote wanapokuwa katika hifadhi. 

Hata hivyo Mhifadhi Msaidizi na Kiongozi wa Kitengo cha Usalama wa Wanyamapori katika hifadhi ya Gombe ambaye pia ni mkuu wa mizunguko ya watalii Bwana Isaya Mkude ameelezea ugumu wa utekelezaji wa masuala ya ulinzi kutokana na mipaka ya wazi ya hifadhi hizo pamoja na uwepo wa watu wanaoingia misituni kuvuna mazao ya misitu, kuwinda, pamoja na kufanya shughuli za kilimoltura

Mkude, ambaye mara zote huvaa barakoa anapokuwa katika shughuli zake ndani ya hifadhi, amesema kuwa ni rahisi kudhibiti maingiliano ya wanyama na watu lakini ukosefu wa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wanaozunguka mbuga hizo kunachangia uvunjifu wa makusudi wa sheria ambao unaweza pia kuchangia maambukizo ya virusi vya Corona. Sababu ni kuwa watu wanaingia katika maeneo ya hifadhi bila kufuata taratibu.

Serikali ya Tanzania ilianzisha Mpango mkakati wa Kuwalinda Sokwe mwezi Juni mwaka 2018 baada ya kugundua hatari inayowakabili sokwe katika nchi hiyo pamoja na kuimarisha mpango wa muda mrefu wa kuwinda wanyama na viumbe hai walio hatarini kutoweka kabisa duniani. 

Katika mpango mkakati huo, Waziri wa Maliasili na Utalii alikubali kuwa sokwe hao wanahitaji kulindwa kama wanavyostahiki. 

Waziri Kigwangalla alitoa wito kwa washikadau wote kuungana pamoja na kuwalinda sokwe wa Tanzania popote pale walipo ikiwemo katika hifadhi maalum za wanyamapori na katika maeneo ya vijiji. 

Dira ya mpango kazi huu ni kuhakikisha kwamba kufikia mwaka 2023 maisha ya kiikolojia na baioanuwai waliyonayo Kima nchini Tanzania yanahifadhiwa ili waongezeke, kusimamia mafungamano baina yao ili kuhakikisha muendelezo wa vinasaba vyao mchanganyiko.