Migogoro ya binadamu na wanyamapori inaongezeka katika mwambao wa Ziwa Victoria nchini Kenya, huku sampuli za maji zikiwa chini ya viwango vya maji ya kunywa

Harold Odhiambo na Robert Amalemba

Wanaume wawili wakipakia magunia ya mkaa kwenye Lori lililo umbali wa mita chache karibu na mdomo wa Mto Wigwa uliochafuliwa vibaya, kando ya ziwa Kisumu.

Kiboko anainuka taratibu juu ya maji na kukoroma kwa hasira, pengine ili kuwatia hofu vidume waliovamia eneo lao. Muda mfupi baadaye, vichwa vingine viwili vya viboko vinainuka juu ya maji na kuungana kuanza kukoroma.

Katika siku mbaya, matokeo yangeweza kuwa majanga, lakini siku hii, viboko wamechagua kutoondoka nyumbani kwao kukabiliana na wavamizi.

Mita chache kutoka mahali ambapo wanaume huuza mkaa, kuna barabara ya lami inayopitia katika ukingo wa ziwa,  imejengwa na imewazuia vilivyo viboko hao kupata malisho upande wa pili wa ardhi oevu.

Karibu na eneo hilo, karibu malisho yote ambayo wanyama wa majini hutegemea kwa chakula chao yamekuwa yakiharibiwa huku wenyeji wakiyavamia maeneo ya ardhi oevu.

Lakini hiyo ni ncha tu ya barafu: uharibifu unaofanywa kwenye mfumo wa ikolojia unaonekana na kila hatua iliyochukuliwa.

Young boys kiboko bay 1
Vijana wadogo wanajitayarisha kufurahia safari ya mashua karibu na Ghuba ya Kiboko huko Kisumu. Kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kando ya fukwe zinatishia bayoanuwai.

Mto Wigwa ni mfano dhahiri wa uozo huo. Maji ni ya kijani kibichi, yamechafuliwa na plastiki zinazoonekana na hutoa harufu kali ambayo wageni hawawezi kuihimili bila ya kuwa naVifaa kinga (Barakoa).

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Standard kando ya ufukwe wa ziwa huko Kisumu, Siaya na Busia uligundua jinsi gani maendeleo ya wasiwasi yanatishia uwepo wa viumbe vya majini, kuongezeka kwa uchafuzi wa maji, kuharibu mazalia ya samaki na kuongezeka kwa matukio ya migogoro ya wanyamapori na binadamu. 

Sehemu za ardhi ambazo hapo awali zilikuwa malisho ya viboko zimechukuliwa na hoteli na nyumba za kifahari, huku zingine zikiwa zimezungushiwa uzio.

Hoteli hizo ni pamoja na Hoteli ya Sh 100M Crystal Charlotte Beach Resort iliyojengwa mwaka wa 2018 ambayo kwa sehemu ilisombwa na mafuriko, na Dunga Melon Beachfront na Milimani Resort iliyojengwa mnamo mwaka 2013 kufuatia serikali ya ugatuzi nchini Kenya.

Kando ya barabara ya Kisumu-Dunga kwa mfano, ukanda wa ziwa umegeuka kuwa mgodi wa dhahabu wa kitalii miaka miwili iliyopita huku hoteli mpya zikihamia kujengwa kando ya ufukwe wa ziwa. Ukaguzi wa Gazeti la The Standard uligundua kuwa takriban hoteli saba mpya zimeanzishwa kando ya eneo hilo na ndani ya maeneo oevu yaliyo karibu, katika miaka miwili iliyopita.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) Kaunti ya Kisumu Tom Togo alisema wengi wa watengenezaji walitumia mapungufu katika utekelezaji wa sheria za kuendeleza sehemu za mito. Adhabu kali zaidi na taratibu za utekelezaji zinahitajika, alisema.

“Ni changamoto kuhifadhi maeneo haya kwani maeneo oevu mengi hayajatangazwa na serikali. Hiyo inafanya mafundi kuyapata kwa majina yao,” alisema. “Ili kuwahamisha au kuwatoa hapo na kuhifadhi eneo hilo, lazima sheria ibadilishwe.”

Togo anatetea kuanzishwa kwa miongozo iliyo wazi zaidi juu ya utekelezaji na adhabu. 

Kando kando ya Kisumu na Dunga, visa vya viboko vinavyotokea ni karibu kila siku, hutokea hata mchana kweupe kwenda kutafuta chakula, wakati mashambulizi ya mamba pia yamekuwa yakiendelea kuongezeka, kulingana na mahojiano na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Katika kilele cha mashambulio mnamo 2020, Kamanda wa Polisi wa Nyakach Jonathan Koech alisema watu 10 waliuawa na wanyama hao kati ya Januari na Mei mwaka huo huo. Kulingana na wakazi hao, viboko hao wamekuwa wakivamia mashamba yao kutafuta chakula.

KWS pia imelazimika kutenga kiasi kikubwa cha fidia kutokana na migogoro ya binadamu na wanyamapori.

Afisa wa KWS Bi Millicent Ondudo pia anasema visa vya mashambulizi ya viboko vimeripotiwa haswa kando ya fukwe za Rachuonyo Kaskazini, Suba na Mbita huku binadamu na wanyama wakigombea rasilimali.

Wakazi na wanasayansi wote wanakiri kwamba uvamizi katika maeneo ya ardhi oevu na maeneo ambayo yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya wanyama pori ni lawama kwa hali hiyo.

Mwathiriwa wa shambulio hilo aliambia The Standard kwamba walishambuliwa usiku na wanyama hao wa porini. Phillip Owino, mvuvi huko Dunga, ana bahati kuwa hai. Kwa ajili yake, nyufa na majeraha katika mikono yake  ni ukumbusho mkali wa jinsi alivyokuwa karibu na kifo baada ya kushambuliwa na mamba.

Huko Dunga anakofanyia kazi, makumi ya migahawa ya muda imejengwa hata kwenye maji. Matete ambayo zamani yalikuwa maficho na mawindo ya mamba na viboko yameharibiwa, kuweka njia kwa ajili ya ujenzi wa hoteli mpya.

Siku ya maafa mnamo Oktoba 1, 2022, Owino alikuwa ameenda kuangalia mashua yake ufukweni, kwa mbali alijua kuwa kiboko alikuwa akimvizia kimya kimya.

“Pamoja na hapo, nilisikia kitu kikinijia na kunishika mkono kwa meno yake makali,” alisema Owino. Alipoteza fahamu na kujikuta tu hospitalini akiwa na bandeji mwili mzima.

“Sijui hata jinsi wavuvi wengine walivyoniokoa kutoka kwenye taya za mamba. Nisingefanikiwa,” anaeleza.

Lakini si peke yake. Katika eneo lote la ziwa ikiwa ni pamoja na kaunti ya Siaya na Homa Bay, visa vya mashambulizi vimekithiri katika maeneo ambayo watu wamevamia fukwe za ziwa, kama Kamanda wa Polisi wa Nyakach Bw Koech anavyothibitisha.

Afisa huyo anasema kuwa katika Kaunti ya Yimbo Siaya, haiwezi kupita mwezi mzima bila kupata taarifa ya shambulio la kiboko. Visa vya mashambulizi ya mamba pia vimeongezeka, kulingana na utawala wa eneo hilo.

Mnamo Agosti mwaka jana, wakaazi walimnasa na kumuua mamba wa futi 17 huko Asembo Mashariki. Mamba huyo alishukiwa kumkatakata mtoto wa miaka mitatu hadi kufa na mtu mwingine wa miaka 21 mwezi Februari. Inasemekana kupotea katika kitongoji hicho cha Ralayo kilichopo pwani ya ya Ziwa Victoria.

Mnamo Agosti 2020, mwanamke mwenye umri wa miaka 32 aliuawa na mamba katika ufukwe wa Ralayo. Katika tukio la mwaka 2021, mchuuzi wa samaki aliyekuwa mjamzito pia aliuawa na mamba katika ufukwe wa Kowang’. Baadhi ya fukwe zinazojulikana kwa mashambulizi ya kiboko na mamba ni pamoja na Anyanga, Nyenye-Misori, Ralayo, Kamito na Rabolo.

Ardhi oevu chini ya tishio la Binadamu

Dunga beach 1
Pwani ya Dunga huko Kisumu. Hoteli kadhaa zimejengwa kando ya fukwe, na kutishia viumbe hai

Katika ukanda huo, ukosefu wa ardhi ya kilimo na maisha umesukuma familia kwenye mwambao wa ziwa na katika makazi ya asili ya aina mbalimbali za wanyama, ikiwa ni pamoja na maeneo ya ardhi oevu ambayo taratibu yanapotea.

Kwa kuwa ardhi oevu haijalindwa, inakabiliwa na vitisho visivyo na kifani kutokana na maendeleo ya kiuchumi, uchafuzi wa mazingira, mabadiliko ya mkondo wake wa maji na ubadilishaji wa matumizi mengine ya ardhi.

Ardhi oevu ni muhimu kwa mazingira yenye afya. Inachuja maji, hutoa makazi kwa wanyamapori na kutoa fursa za burudani. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, sehemu ya Ziwa Victoria nchini Kenya ilipoteza zaidi ya nusu ya ardhi oevu, kulingana na maafisa wa NEMA. Hii inaakisi picha ya ulimwengu kulingana na UNEP, ambayo inasema kati ya 1970 na 2015, ardhi oevu ya bara na pwani zote mbili zilipungua kwa takriban asilimia 35 duniani kote.

Hata hivyo, hali imefanywa kuwa mbaya zaidi kutokana na ukweli kwamba hakuna ardhi oevu hata moja iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali katika Kaunti ya Kisumu, hivyo kufanya iwe vigumu kwa mamlaka zilizoidhinishwa kulinda mfumo wa ikolojia dhaifu.

Kulingana na ripoti ya mwaka 2011 ya Kamisheni ya Bonde la Ziwa Viktoria, ghuba na ufukwe ni maeneo muhimu ya viota kwa aina kadhaa za ndege. Ripoti hiyo inaiorodhesha ardhi oevu ya Dunga kati ya nyingi zaidi maeneo oevu hatarishi pamoja na Rota na Kogony.

Eneo oevu la Dunga, ambalo linachukua kilomita 10 kwenye mwambao wa Ziwa Victoria kusini mashariki mwa Kisumu, ni nyumbani kwa aina 60 za ndege, kulingana na Tom Togo, mkurugenzi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) kaunti ya Kisumu.

Lakini ardhi oevu inasongwa na mfereji wa maji machafu na taka ngumu, hata kama baadhi ya wananchi wachache wanapigania kuihifadhi.

Victor Didi, mwanamazingira na mwanachama wa kikundi cha watu wa kujitolea ambao wamekuwa wakifanya usafi mto Wigwa unaotiririsha maji yake karibu na Dunga, wanasema eneo hilo limechafuka sana.

“Tumekuwa tukikusanya plastiki na kuziondoa katika mwambao wa ziwa na Mto Wigwa, lakini hakuna tunachoweza kufanya kuhusu mfereji wa maji huo wa maji machafu,” anasema.

Mnamo Januari 2, 2022, hali ilizidi kuwa mbaya wakati moja ya mifereji ya maji taka ya Kampuni ya Usafi wa Mazingira ya Kisumu ilipopasuka na kutiririka moja kwa moja ziwani, na hivyo kuzidisha hali kuwa mbaya ya ubora wa maji. 

Didi anaamini kwamba uvamizi wa makazi umezidisha uchafuzi wa ziwa na upotevu wa bioanuai.

Maji ya ziwa chini ya viwango vya maji ya kunywa

Fishermen in Dunga beach 1
Wavuvi wanapita kwenye hoteli iliyojengwa katika ardhioevu ya Dunga huko Kisumu.

Pamoja na uvamizi pia huja uchafuzi mkubwa wa mazingira. Uchunguzi huru wa sampuli za maji wa 2022 ulionyesha kuwa maji katika ziwa hilo yapo chini ya viwango vya maji ya kunywa.

Vipimo vya 2022 vya kubaini ubora wa maji ya Ziwa Viktoria katika Ghuba ya Kisumu ulibaini kuwa Maji yana viambata vya kemikali za hydro-kemikali ambazo viwango vyake katika maji vinaongezeka hatua kwa hatua, pamoja na viwango vya baadhi ya kemikali na vichafuzi vya vijidudu kuvuka Viwango vya Utiririshaji wa Majitaka vya Afrika Mashariki, Sheria ya Usimamizi na Uratibu wa Mazingira (2006) na kanuni na Usimamizi wa Rasilimali za Maji Kanuni (2007).

Ripoti hiyo iliyofanywa na Mamlaka ya Rasilimali za Maji (WRA), iliyoratibiwa na InfoNile, ilikagua kemia ya maji katika mifereji ya maji taka inayotiririka katika Ziwa Victoria katika ghuba ya Kisumu kati ya Julai 4 na 8, 2022. Sampuli zilichukuliwa kando ya Mto Auji na Kisat na ndani ya Ghuba ya Kisumu.

Kwa msaada kutoka JRS Biodiversity Foundation, sampuli 24 za maji zilichukuliwa ili kupima mfululizo wa vigezo vya ubora wa maji.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mto Auji na Kisat ndio njia kuu za uchafuzi wa mazingira katika ghuba hiyo.

Mito yote miwili inapita katikati ya makazi ya Kisumu, ikiingiliana na shughuli za kibinadamu ambazo huchangia uchafuzi wake.

Kulingana na ripoti hiyo, baadhi ya shughuli zinazochafua mto huo ni pamoja na dampo zilizo na eneo duni, utupaji wa taka za maji kutoka majumbani, vyoo duni, maji yatokanayo na kuoshea na  safishia  magari, uchafu unaotoka kwenye dampo la Kachok, utupaji hovyo wa mafuta yaliyotumika kutoka kwenye Karakana na Gereji ya Jua Kali, kutupa mizinga ya maji taka ndani ya mto, na kufunga njia za maji taka.

Kati ya viashirio vilivyopimwa, ripoti ilionyesha kuwa Mahitaji ya Kemikali ya Oksijeni (COD), Jumla ya Coliforms na E-coli, Risasi,Mafuta na viwango vya Grease vilikuwa juu ya viwango vilivyopendekezwa. Jumla ya Nitrojeni, Total Suspended Solids,, Mahitaji ya Oksijeni ya Kibiokemikali, na Thamani za Oksijeni Iliyoyeyushwa pia zilikuwa nje ya viwango vinavyopendekezwa, hasa katika Mto Kisat.

Mahitaji ya Oksijeni ya Kemikali (COD) ni kiasi cha oksijeni kinachohitajika ili kuongeza oksidi ya viumbe hai vilivyomo ndani ya maji. Kadri thamani ya COD inavyoongezeka, ndivyo uchafuzi wa maji unavyozidi kuwa mbaya.

Ripoti hiyo ilibainisha kuwa sehemu zote za sampuli kando ya Mto Kisat, Mto Auji, Eneo la kutibu maji taka la Kisat na Nyalenda zilisajili majaribio chanya kwa coliforms na e-coli colonies kwa kila 100ml ya Too Numerous to Count (TNTC).

Maji ya kina kirefu katika ghuba hiyo pia yalisajili idadi kubwa ya E-coli na jumla ya colonies ya coliform, ambayo ni pamoja na bakteria kutoka kwenye uchafu wa binadamu au wanyama.

“Viwango hivyo ni dalili ya kutofuata viwango vya maji ya kunywa vya Afrika Mashariki,” ilisoma ripoti hiyo.

Kulingana na Mamlaka ya Rasilimali za Maji, uchafuzi huu unaweza kuwa unatokana na mitambo ya sasa ya kutibu maji machafu kutokuwa na uwezo wa kuua vijidudu vya maji machafu.

 “Mitambo ya kutibu maji machafu haijajumuishwa na mfumo wa matibabu wa hali ya juu wa kuua vijidudu kabla ya kutiririka kwenye mazingira. Zaidi ya hayo, maji machafu ya majumbani ambayo hayajatibiwa yanayotoka katika makazi yasiyo rasmi ya Obunga na Nyalenda na pia maji yanayotiririka na dhoruba yanayotiririka moja kwa moja kwenye mito na ziwa yanaweza pia kuwa chanzo cha uchafuzi wa coliform,” ripoti hiyo ilibainisha.

falling house 1
Nyumba zilizoharibiwa kutokana na kufurika kwa ziwa katika kijiji cha Nduru huko Kisumu.

Dk Onyango alibainisha kuwa kuwepo kwa bakteria hao kwenye maji ni dalili ya kuwepo kwa bakteria wengine wa pathogenic kama wale wanaosababisha typhoid na kipindupindu.

Kulingana na ripoti ya Kenya Health Information Systems (KHIS), matukio ya magonjwa yanayoenezwa na maji yakiwemo kipindupindu na salmonella katika kaunti ya Kisumu kwa ujumla yamepungua kutoka 2017-2021, lakini homa ya ini iliongezeka tena 2020.

Cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya sehemu za sampuli pia ziligundua metali nzito ya risasi katika kiwango cha juu ya viwango vinazopendekezwa.

“Vituo hivi viko karibu na bandari ya reli ya Kisumu ambayo iko karibu na mji na makazi yasiyo rasmi ya Obunga na Nyalenda,” ripoti hiyo ilisema. “Shughuli mbalimbali za “juakali” na taka kutoka maeneo haya, mafuta ya risasi yanayotumiwa na magari, rangi na utupaji wa taka za viwandani na manispaa ni vyanzo vinavyowezekana kuchocha ongezeko la risasi katika maeneo haya.

isasi ni sumu kali katika mwili wa binadamu. Inaweza kusababisha madhara makubwa kiafya, kama vile kupoteza uwezo wa kusikia, shinikizo la damu, kuharibika kwa figo, kutofanya kazi kwa mfumo wa kinga, na kuwa sumu katika viungo vya uzazi. Hasa ni hatari kwa kichanga kilichopo tumboni, watoto wachanga na watoto wadogo, ambao viungo vyao vinaendelea kukua.

Mabwawa ya oksidi ya Kisat na Nyalenda hayana uwezo wa kudhibiti viwango vya ziada vya metali nzito, ripoti ilihitimisha.

Hakuna zebaki iliyogunduliwa katika sampuli ya 2022 huko Kisumu, ingawa viwango vya zebaki viligunduliwa hapo awali kwenye maji na samaki katika Ghuba ya Winam, Kenya.

Pamoja na afya ya binadamu, uchafuzi wa mazingira pia huathiri viumbe hai vya majini. Katika tathmini, Mafuta na Grease pia yalikutwa juu ya viwango vilivyopendekezwa, ambayo inaweza kuingilia kati maisha ya kibaolojia katika uso wa maji na kuunda filamu zisizovutia.

[Dataviz: Oil and Grease]

Link to view: https://public.flourish.studio/visualisation/11505495/

Embed code: <div class=”flourish-embed flourish-chart” data-src=”visualisation/11505495″><script src=”https://public.flourish.studio/resources/embed.js“></script></div>

Dk. Paul S. Orina, Mkurugenzi Msaidizi wa Ufugaji wa viumbe Maji katika Taasisi ya Utafiti wa Bahari na Uvuvi ya Kenya, alisema “Viwanda vingi, viwanda na karakana za sekta isiyo rasmi ndio vyanzo vikuu vya utiririshaji wa mafuta na grisi kwenye mfumo ikolojia wa ziwa”. 

Pia alibainisha kuwa uchafuzi wa mazingira unaogunduliwa una athari kubwa kwa viumbe wanaoishi ndani ya maji.

Uhai wa majini hutegemea kiwango cha kutosha cha oksijeni iliyoyeyushwa ndani ya maji. Katika sehemu kadhaa za sampuli kando ya Mto Kisat, thamani zilikuwa chini ya viwango vya chini, kumaanisha kuwa viwango vya oksijeni vilikuwa chini sana.

Naitrojeni, ambayo huchochea ukuaji wa mwani (algae) ambao hupunguza oksijeni, pia ilikuwa juu sana katika sehemu mbili za sampuli za Mto Kisat. Naitrojeni inaweza kutoka kwenye mbolea za kilimo, maji machafu, na taka za wanyama.

Ubora wa maji katika Ziwa Victoria umekuwa ni tatizo kwa miaka mingi. Utafiti wa 2020 na sampuli zilizokusanywa mwaka wa 2015 kutoka fukwe mbalimbali za uvuvi katika Ziwa Victoria upande wa Kenya ulihitimisha kuwa vigezo vya ubora wa maji vinatofautiana kwa kiasi kikubwa katika maeneo tofauti ya sampuli katika eneo lililofanyiwa utafiti.

Hata hivyo, sampuli zilizofanywa mwaka 2022 zilionyesha kiwango cha kemikali ambacho kimekuwa kikiongezeka hatua kwa hatua, kulingana na ripoti ya Mamlaka ya Rasilimali za Maji (Water Resources Authority report ) iliyoombwa na InfoNile.

Wastani wa thamani za mahitaji ya oksijeni ya kibiokemikali (BoD), jumla ya yabisi iliyoyeyushwa na jumla ya yabisi iliyosimamishwa ilikuwa juu zaidi katika sehemu nyingi za sampuli mwaka wa 2022 kuliko katika maeneo ya karibu ya Kichinjio na Seka mwaka wa 2015, ingawa maeneo yalikuwa tofauti kidogo. Hii inaonyesha uwezekano wa kuzorota kwa uchafuzi wa maji.

Ripoti ya Mamlaka ya Rasilimali za Maji iliyoidhinishwa na InfoNile inapendekeza kutekelezwa na kuchukuliwa kwa hatua za makusudi zinazolenga kupunguza mizigo ya uchafuzi wa mazingira ili kuhakikisha utiririshaji wa maji taka yanayokidhi mahitaji kwenye rasilimali ya maji.

Pia inatoa wito wa kuimarishwa kwa kanuni za kitaifa na mashirika husika ili kuhakikisha uzingatiaji wa usimamizi wa taka.

Serikali inachukua hatua dhidi ya uchafuzi wa mazingira na uvamizi

plastic fish model 1
Wakazi wa ufukwe wa Dunga wamekusanya plastiki ambazo zimechafua ziwa kutokana na ongezeko la watu kuvamia ziwa hilo na kujenga kizimba cha samaki. Sananu hiyo inalenga kutuma ujumbe kuhusu hitaji la kulinda ziwa dhidi ya plastiki.

Kulingana na Tom Togo wa NEMA, mamlaka hiyo ina kazi nyingi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuangalia uchafuzi wa mazingira katika maeneo oevu na mfumo ikolojia wa ziwa.

“Tuna fosforasi nyingi zinazoingia ziwani kupitia sababu za asili na kiasi cha nitrojeni pia,” anasema.

Kufuatia maandamano, Togo alisema kuwa mamlaka hiyo kwa miaka miwili iliyopita imechukua hatua kali dhidi ya viwanda vinavyomwaga taka ziwani, na baadhi yao vilifungwa kwa muda hadi vitakapofikia matakwa. Miongoni mwa makampuni ambayo yalitajwa na mamlaka hiyo katika eneo hilo ni pamoja na Gereza la Kisumu Maximum na Agrochemicals and Food Company sambamba na vibanda kadhaa.

Hata hivyo, pia alibainisha kuwa hakuna ardhi oevu hata moja ambayo imetangazwa katika gazeti la serikali katika eneo la Kisumu na hivyo kufanya iwe vigumu kulinda ardhi oevu.

“Tuna eneo la kijani kibichi ndani ya jiji lakini kwa bahati mbaya maeneo oevu ni ya watu kwa sababu wana hati miliki ya maeneo oevu yalipo, na hivyo ni changamoto kubwa katika uhifadhi wa ardhi oevu tulionao katika jiji hili,” alisema.

Dunga beach eatery 1
Mkahawa uliojengwa katika ufukwe wa Dunga huko Kisumu. Mkahawa huo ni miongoni mwa zile ambazo zimejengwa kando ya ufukwe.

Michael Nyanguti, mwanaharakati wa mazingira, anasema kwamba uvamizi katika maeneo ya ardhioevu ya ziwa ni “mwelekeo hatari sana ambao lazima ukomeshwe.”

“Tunawaomba wadau wote kujitokeza ili kuhakikisha tunahifadhi uvuvi wetu, ambao ndio chanzo cha maisha ya wengi wanaoishi karibu na ziwa,” alisema.

Alisema moja ya tishio kubwa kwa bayoanuwai ya Ziwa Victoria na sekta ya uvuvi leo ni uvamizi wa maeneo oevu ya Ziwa Victoria.

Hivi sasa, anasema, kuna watu ambao hununua ardhi karibu na ziwa na kumiliki eneo lote hadi majini.

Kanuni za Usimamizi na Uratibu wa Mazingira za 2006 (ubora wa maji) zinakataza watu kulima au kufanya shughuli yoyote ya maendeleo ndani ya angalau mita sita na upeo wa mita 30 kutoka kiwango cha juu kabisa cha mafuriko kilichorekodiwa.

“Wengi wa watu hawa wanaovamia maeneo oevu wanaharibu uoto wa ardhi oevu na hata kumwaga maji taka na vitu vingine ndani ya ziwa, hivyo kupuuza athari za uhifadhi. Juhudi hizi zimesababisha uharibifu wa uoto wa ardhi oevu, huku nyingine zikienda kwa uzuri,” alisema. 

Tarifa hii imezalishwa Kwa ushirikiano na InfoNile kwa ufadhili wa JRS Biodiversity Foundation; ripoti ya ziada na Annika McGinnis, Ruth Mwizeere na Primrose Natukunda.