Mataifa yatakosa kutimiza malengo yaliyokubalika ulimwenguni ya kupunguza athari za kemikali na uchafu kufikia mwaka wa 2020, hivyo kuhitajika kwa hatua za dharura ili kupunguza athari dhidi ya afya na chumi, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo.