Serikali imeamuru jamii 600 ambao waliingilia Msitu wa Maasai Mau, kuondoka. Naibu wa rais William Ruto, ambaye alizungumza wikendi iliyopita katika shule ya upili ya Sogoo, Narok Kusini, ambapo ipo sehemu ya msitu, aliwataka maskwota hao kuondoka, akinena kuwa uhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa nchi. Hatua hii imechukuliwa ili kuhifadhi hektari 46,000 ya msitu, ambao ndio chanzo kikuu cha maji ndani ya Afrika ya Mashariki na Kati