Mwito wa kutuma maombi: Ushirika wa Hadithi za Uchambuzi wa Rasilimali za Maji za Kimkakati  

InfoNile  na MiCT/ The Nile inaalika wanahabari walioko nchi za Uhabeshi, Eritrea, Misri, Sudan, Sudan Kusini, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na DRC wanaombwa kuwasilisha maombi ya habari upekuzi aina ya mseto(multimedia) inayohusika na /au malengo ya Nile Basin Initiative (NBI) Strategic Water Resources Analysis na kuzilinganisha na seti ya data na makadirio mitindo katika bonde la Nile.

WATER GRANT SWAHILI

Usuli na Muktadha 

Mojawepo ya mambo yanayostahili kuyatatuliwa  kwa Nile Basin, na chanzo kikuu cha kutoelewana  kati za nchi zinazotumia kwa pamoja rasilimali za maji, usawa kati ya mahitaji ya maji na upatikanaji kwa muda wa wastani hadi muda mrefu.

Ongezeko la ukosefu wa maji yatarajiwa kwa Nile Basin hasa idadi ya watu ikiongezeka na maneo yanayo tumia unyunyuzi yakizidi kupanuka.

Kwa hali ya kutatua changamoto hizi, Nile Basin Initiative pamoja na washiriki wake, kwa sasa wako harakati za mwishomwisho za kutekeleza Strategic Water Resources Analysis (SWRA), yakiwepo yafuatayo:

  • Kadirio ya mahitaji ya maji na upatikanaji wa rasilimali kwa maji ya basin 
  • Maendeleo tekelezi kulingana na mipango ya taifa  
  • Uundaji wa matukio kushughulikia matarajio ya kutokuwa na usawa siku zijazo.
  • Utafiti maalumu wa ndani kuhusu “nguzo muhimu” kuelezea vipengele vya makadirio ya mahitaji na kuchagua kuhifadhi maji na mfumo wa uboreshaji, kutolewa kupitia njia iliyothibitishwa, uchambuzi na matukio.

Mifano ya hadithi ambazo yanaweza kuandikwa huku kuzingatia data na habari kutokana na uchambuzi ni kama: Wakulima wanaozingatia kuboresha ufanisi wa unyunyuzaji, Miradi yakuondoa chumvi, Kuongeza kilimo kinachotegemea mvua, Kutumia Nile vizuri kwa urambazaji/ madhumuni ya biashara, Uboreshaji wa kiuchumi wa kikanda, Kuhifadhi mtiririko wa mazingira kwa mifumo ikolojia na mengineyo.

Stakabadhi zakungeza makali juu ya wazo la ombi lako:

Hadithi zote zitachapishwa na InfoNile (watazamaji na mtindo), na hadithi zingine zitakazoteuliwa kwa minajili ya kuchapisha kwa The Nile, baada ya kuchapishwa kwa vyombo vya habari ya mwandishi wa hadithi.

Jinsi ya kutuma maombi

 Unaweweza tuma maombi kama mtu binafsi, lakini ushirikiano (kati ya waandashi wa habari kutoka vituo tofauti kutoka nchi moja, na/au kati ya waandashi wa habari kutoka nchi mbili tau zaidi tofauti) waalikwa. Mkiwa mnatuma kwa kushirikiana, tuma maombi kwa kutumia barua pepe moja na stakabadhi zote za wenye wanaomba nafasi.

Tafadhali tuma maombi kwa info@infonile.org kabla ya tarehe 15th Aprili, 2022.

Tuma ukurasa moja inayoeleza wazo la hadithi yako. Mapendekezo yako lazima yakuwe na muundo iloyofafanuliwe kwa uwazi, kwa mukhtasari eleza malengo yake au mchango, pahali pakuchapishia( chumba maalum cha habari), na matarajio ya hadithi hii kwa uma. Pendekezo hili ni lazima liwe na mpango wa kuhusisha matumizi ya data. Tafadhali tathmini jinsi utakavyo tumia mseto wa vyombo vya habari yaani ‘multimedia’ (video, picha, sauti, and data ya michoro pamoja maandishi). Pia kadiria bajeti usiozidi USD 800.

– Wasifu kazi

-Sampuli mbili ya kazi yako ya awali. Viunganishi (links) kwa hadithi zilizochapishwa .

-Barua kutoka kwa mhariri au wahariri wako, ikithibitisha kupeperusha au chapisha hadithi yako pamoja na hadithi nyinginezo zitakazofuata kuchapishwa kwa pamoja mwisho wa mradi huu kama tulivyofanya hivi majuzi na  mradi wetu uliyokamilika ya Pandemic Poachers story.

Wazo la hadithi yako lazima lizingatie mpango wa kuunganisha uchambuzi wa data na taswira ya data kutoka kwa ripoti zilizotolewa na vyanzo vingine vya data.

Ukamilifu wa hadithi hii lazima izingatie undani wa mseto wa vyomvo vya habari(multimedia) kama maandishi, video, picha, sauti,na taswira ya data/ramani. Inaweza ikachapishwa kwa redio,runinga, na jarida mbalimbali.

Machapisho haya yametolewa na InfoNile na Media in Cooperation Collaboration and Transition (MiCT) kwa ushirikiano na Nile Basin Initiative (NBI) na usaidizi  kutoka kwa Deutsche Gesellschaft fuer Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH, kwa kudhibitishwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp