Taasisi ya InfoNile inawatangazia wapiga picha na wapiga picha za kihabari, kutoka katika nchi za Burundi, DR Congo, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania na Uganda kuwasilisha maombi ya kampeni ya uandishi wa picha za kihabari yatakayofanyika kwa njia ya mtandao. Kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuripoti habari za Mto Nile na taarifa nyingine za kisayansi kwa njia ya picha.
Ruzuku kwa ajili ya kutengeneza hadithi za picha ni USD 1000/=
Lengo la mradi huu ni kuchapisha picha zitakazoibua maisha ya kila siku katika mazingira yanayozunguka Mto Nile, ikiwamo changamoto na utatuzi.
Habari zitakazozalishwa kutokana na picha hizo zitaonyesha mifumo na taratibu za maisha ya wakazi waishio kuzunguka nchi zilizo katika ukanda wa Mto Nile, uhusiano wa watu na mto Nile na maji, changamoto wanazopitia na suluhisho.
Wapiga picha za kihabari pia watapewa nafasi ya kushiriki mafunzo na warsha kwa njia ya mtandao.
Historia
Kufungwa kwa shughuli kulikosababishwa na mlipuko wa Covid-19 kulichangia kuibuka kwa mijadala ya kitaifa kuhusu masuala ya mto Nile, hasa katika ukanda wa Egypt na katika bwawa kuu la Ethiopia (Grand Ethiopian Renaissance Dam).
Hali hii, imekuwa mbaya zaidi kwa wanahabari, wanadiplomasia na watafiti ambao walishindwa kusafiri na kuripoti wakiwa katika maeneo yao kama inavyotakiwa. Mitazamo ya kimataifa, mawazo ya kibaguzi, yaliendelea kuenea katika mitandano ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida.
Kuna haja ya kuwa na mawazo mbadala na ushirikiano kati ya wakazi wa nchi zinazozunguka mto Nile. Kwa kuhamasisha habari kwa njia ya picha, mradi huu utakuza simulizi, muundo na uelewa wa masuala ya mto Nile, kama rasilimali shirikishi, inayohusisha mipaka tofauti ya kitaifa.
Kutokana na mwonekano mzuri wa picha hizo, habari zinazolenga maisha ya binadamu na taarifa za kisayansi kuhusu mto Nile, zitasambazwa katika mitandao ya kijamii ili kuwafikia wasomi, wasio wasomi na hadhira iliyo katika mipaka ya nchi.
Wapiga picha za kihabari watakaopata ruzuku hii, watapata fursa ya kupewa mafunzo na warsha kuhusu upigaji picha za kihabari, ujuzi wa uandishi wa habari za kisayansi na watapigwa msasa na wapiga picha wakubwa katika programu hiyo kuanzia Desemba 2020.
Unachotakiwa kufanya;
- Kuwasilisha andiko litakalotokana na utafiti wa masuala ya maji na sayansi.
- Kutumia mrengo wa masuala ya kibinaadamu na masimulizi kueleza hadithi iliyo katika picha.
- Kuunganisha sayansi, tafiti, takwimu katika habari zenye mrengo wa masuala ya kibinadamu kwa kutumia maelezo katika picha yenye taarifa na masimulizi.
- Uwe mchangiaji hai katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii inayoendesha kampeni za #EverydaNile. (Pia pitia katika kurasa zetu za instagram: @everydayafrica, @everyday.nile, @everydayegyt, @ihedelt na katika mitandao ya Twitter, InfoNile.
Usiwe na shaka, kama unaweza kufanya chochote kati ya hivyo hapo juu, hicho ndicho tutakachofanya pamoja katika warsha na mafunzo.
Hizi ni baadhi ya mbinu na mifano ya mawazo ya habari ambazo zitakusaidia kuelewa kile tunachotafuta katika mradi huu.
Mawazo ya habari yanaweza kutofautiana kulingana na mada unayotaka kulenga katika habari yako. Ifuatayo ni mifano lakini si yote inayoweza kukusaidia kupata wazo sahihi la habari:
- Usimamizi sahihi wa maji hasa katika sekta ya kilimo
- Uboreshaji wa usimamizi wa maeneo ya makorongo na delta salama
- Upatikanaji wa maji safi ya kunywa na usafi wa mazingira
- Jinsia na ushirikishwaji unaohusisha masuala ya maji na maendeleo
- Diplomasia ya maji yenye malengo ya kushirikisha mto Nile na masuala ya kibinadamu na kwa usawa kati ya nchi na jamii zilizo katika mipaka ya mto Nile.
- Uchafuzi wa maji
- Mikakati yenye mafanikio na mawazo bunifu kuhusu mto Nile na maji katika Mto Nile.
Matokeo ya Mradi
- Simulizi fupi ya video ya hadithi picha, inayoonyesha habari za maji ndani ya Mto Nile ikionyesha watu na uhusiano wao na maji.
- Kuchapisha habari picha katika akaunti ya EverydayNile, Infonile na WJA na kushirikiana na wengine katika mradi wa Everyday Egypt na Everyday Africa na wengine ili kufikia hadhira kubwa zaidi na kushirikishana ujuzi kuhusu Mto Nile.
- Kuonyesha kazi zilizozalishwa katika matukio mbalimbali ya maji katika nchi za Netherlands na Africa kukiwa na uwezekano wa mpiga picha kuwepo.
- Kuchapisha habari katika vyombo vya habari vilivyo katika nchi za ukanda wa Mto Nile, InfoNile na Water Journalists Afrika. Katika warsha hiyo, tutawasaidia kuandaa andiko la habari zenu kwa ajili ya kuchapishwa katika vyombo vya habari vya kimataifa.
Habari zinaweza kuchapishwa katika lugha tofauti lakini ni lazima kutafsiriwa katika lugha ya Kiingereza.
Ruzuku hii ya kimataifa ya upigaji picha, ni sehemu ya mradi wa Everyday Nile unaohusisha picha, hadithi na sayansi ya Mto Nile.
Mradi huu umefadhiliwa na IHE-Delft Global Partnership for Water and Development na kuratibiwa na Taasisi ya InfoNile/Water Journalists Africa na EverydayNile.
Namna ya kuwasilisha maombi ya Ruzuku
Tafadhali wasilisha vifuatavyo kwa kutumia baruapepe ya: infonile2017@gmail.com tarehe ya mwisho ya maombi ni Novemba 20, 2020 ikiwa na kichwa cha habari katika barua pepe kisemacho: EverydayNile-Jina lako la kwanza-nchi unayotoka.
Kwa mfano; EverydayNile-John-Kenya.
Ambatanisha vifuatavyo:
- Kurasa moja ya andiko la pendekezo ikielezea wazo lako la picha. Andiko lazima liwe limeandikwa vizuri na mwanzoni mwa andiko, eleza kwa kina kuhusu wazo lako la habari, likifuatiwa na kwa jinsi gani litafanyika, wapi habari itazalishwa, dhumuni lako na mchango wa habari hiyo kwa jamii, rasilimali ulizonazo katika habari hiyo na matokeo tarajiwa ya habari.
- Wasilisha kabrasha la kazi zako ulizowahi kufanya. Unaweza kuzituma kwa kutumia kiambatanisho(link) kwa njia ya mtandao au faili la PDF na kisha tuma kwa njia ya barua pepe.
- Akaunti ya Instagram kama ipo
- Camera na vifaa vingine ulivyonavyo
- Bajeti isiyozidi USD 1000
- Wasifu wa kazi(CV)
Waombaji watakaochaguliwa watapewa taarifa kuanzia Novemba 22, 2020-11-02.
Tafadhali zingatia kuwa wapiga picha watakaochaguliwa watatakiwa kuhudhuria angalau mikutano miwili na warsha tatu kwa njia ya mtandao ili kupata ujuzi wa kuandaa habari zao wakati wa kipindi cha mradi.
ANGALIZO KUHUSU COVID-19: Tafadhali zingatia kuwa, wakati tunaendelea kutoa ruzuku hii, tutafanya kazi na mwanahabari mmoja mmoja kwa wale watakaochaguliwa ili kumsaidia kuripoti kwa njia salama katika kipindi hiki cha mlipuko wa Covid-19.
InfoNile ni kikundi cha waandishi wa habari za mazingira katika maeneo ya mipaka, wenye dhamira ya kuchapisha habari muhimu kwa njia ya takwimu na simulizi kuhusu masuala ya maji hasa katika Bonde la Mto Nile Afrika. Tunafanya habari za uchunguzi, mfumo wa takwimu na mitandao ya kijamii katika maeneo nyeti ya maji na mazingira yaliyo katika ukanda wa Mto Nile.
Habari za uchunguzi zilizowahi kutayarishwa ni pamoja na uporwaji wa ardhi katika ukanda huo, utatuzi wa masuala ya kijamii na uharibifu wa mabwawa Afrika Mashariki na madhara ya kimazingira na kiafya yaliyosababishwa na viwanda vya mafuta na gesi, Sudan.