Kulikuwa na kesi 44 zinazohusisha kukamatwa kwa viuongo vya pangolini kwa muda wa miaka 3, pamoja na ongezeko ya usafirishaji wa magamba ya pangolini 

Na Benjamin Jumbe

Uganda ni nchi moja iliyojaliwa sana na wanyamapori, mimea, na viumbe vya  majini, ingaweje baadhi ya wanyamapori wake wanatishiwa na uwindaji haramu na biashara ya wanyamapori.

Haswa waliohatarini sana sana kati yao ni pangonili kwa sababu ya magamba walionao.

Pangolini ni wanyama wenye umbo uliofunikwa uliofunikwa kwa magamba yanayopishana na hutegemea wadudu kama chakula chao. Jina lao limetoka na neno ‘penggulung,’ la Kimalalay kumaanisha viringo.

Kulingana na mwenendo, Shirika Lisilo la Kiserikali linayofuatilia biashara ya wanyamapori, wanasema pangolini ndio wanaolengwa  zaidi kwa uwindaji haramu na usafirishaji usiohalali nchini Uganda.

Takwimu za Shirika hilo zinaonyesha kati ya 2012 na 2016, zaidi ya 1,400 ya pangolini walipokonywa kwa wawindaji haramu.

Rebecca Sandoval, mwanamazingira and mwanzilishi mwenza wa shirika lisiliokuwa ya faida lijulikanalo kama Biodiversity Alliance, limethibitisha ukweli kwamba pangolini ndio wanaosafirishwa zaidi duniani, na wameorodheshwa kwa orodha nyekundu ya umoja wa kimataifa wa kuhifadhi asili kuhusu wanyamapori waliohatarini. ( IUCN’s red list of threatened species)

“Ukweli mchungu; wanyama hao ndio wangali wanaosafirishwa zaidi duniani. Hivi karibuni kumetokea kukamatwa kwa  wanyamapori kote duniani na ukilinganisha, kumekuwa na mabadiliko ya magamba  na viungo vingine vya pangolini kusafirishwa kushinda pembe za ndovu,” Sandoval asema. 

Rebecca Sandoval, mwanzilishi mwenza wa shirika la Biodiversity Alliance
C:\Users\ben\Desktop\pangolin project\videos and pix\207CDPFQ\S2070004.JPG
                          Rebecca Sandoval, mwanzilishi mwenza wa Biodiversity Alliance 

Mwaka wa 2019, Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) walifanya opareshi ya lazima kisheria wakilenga Vietnamese ambayo ni kundi kubwa ya biashara haramu ya wanyamapori na kukamata tani 3.2 za pembe za ndovu na kilo 423 za magamba ya pangolini yenye thamani takriban USD $2.3 milioni na $1.2 milioni mtawalia. Maafisa wa forodha pale kuvuka mpaka kati ya Elegu Uganda- Sudan Kusini waligundua na kuzuia shehena ndani yake vyombo vitatu iliyofichwa kwenye magogo ya mbao na nta yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwelekea Asia.

Kesi zilizofunguliwa mashtaka kuhusiana na kukamatwa kwa magamba ya pangolini zimeongezeka kutoka 7 Mwaka wa Fedha 2018-2019 hadi kesi 8 Mwaka wa Fedha 2019-2020 mpaka kesi 10 Mwaka wa Fedha 2020-2021, hii ni kulingana na ripoti ya Mashtaka ya Mamlaka ya Wanyamapori Uganda kufuatilia #WildEye map.

Kuna sababu nyingi zimesemwa kuhusu ongezeko kwa hamu ya usafirishaji haramu wa kiumbe huyu maalum wa kipekee na viungo vyake, pamoja na faida zake mara tu inapowasili soko la Waasia na dhana kuwa magamba yake yanaumuhimu za kimatibabu zakutibu maradhi mbalimbali.

“Kama unamatatizo za kunyonyesha kama wewe ni mwanamke, inaminika itakusaidia. Wahusika wa usafirishaji haramu wa pangolini wanaamini kuna nguvu za kimatibabu na magonjwa mengine mengi, na sehemu zingine za pangolini zinatumika kwa mapambo ya vito,” asema Sandoval.

Kulingana na #WildEye East Africa data map na InfoNile pamoja Oxpeckers Investigative Environmental Journalism, wanaume wawili kwa jina Bosco Musaka (34) na Simon Kyakwahuwre walishikwa kule Kibaale, magharibi ya Uganda mnamo tarehe 6 Julai, 2020 wakiwa na pangolini mmoja hai baada ya kudokezewa na wakazi wa eneo hilo kwamba  wanajiushisha na pangolini.

Wawili hao walihukumiwa kwa kosa la kumiliki aina ya viumbe waliolindwa kinyume cha sheria ya sehemu 36(1) na 71(1) (b) kulingana na Sheria kuhusu Wanyamapori 2019, nchini Uganda.

Kwa kesi nyingine ya tarehe 28 Mei 202, Mamlaka ya Wanyamapori Uganda (UWA) waliwashika watu wanne kwa tuhuma za kusafirisha usiohalali na uwindaji haramu pamoja kupatikana pangolini watatu hai eneo la Wilaya ndogo ya Kachumbala, Wilayani Bukedea mashariki.

Fred Kiiza, Mlinzi Mkuu wa Mbuga ya Kitaifa ya Wanyamapori Mlima Elgon, alisema washukiwa walishikwa kwenye soko la Kachumbala lilioko Bukedea wakimpelekea pangolini mwanabiashara ambaye kufikia wakati huo alistahili kukamatwa.

“Kufikia sasa tumekamata washukiwa wanne, na pangolini watatu kuokolewa,” asema Kiiza.

“Ninawahimiza jumuiya za mitaa hasa Kanda ndogo ya Teso waachane  na biashara ya pangolini,” aliongezea kusema.

Mojawapo kati ya kesi za hivi karibuni mwezi Machi 2022, polisi Wilayani Amuru, Uganda kaskazini waliokowa pangolini wawili na kukamata mtu mmoja aneyehusishwa na biashari hiyo pahali pajulikanapo kama Pabo.

Hata hivyo pangolini mmoja, alijeruhiwa wakati wa kunaswa kwake, na kupelekwa kwa hospitali ya kitaifa ya wanyamapori na karantini katika Kituo cha Elimu ya Uhifadhi wa Wanyamapori (UWEC), Entebbe, Uganda mahali anayeendelea kupokea matibabu.

C:\Users\ben\Desktop\pangolin project\videos and pix\wildlife hospital\S2090056.JPG
Dk. Victor Musiime (C) , afisa wa mifugo wa UWEC na wafanyakazi wengine wanaohudumia Pangolini aliyejeruhiwa katika hospitali ya wanyamapori. Picha na Benjamin Jumbe

“Baada ya kuangaliwa, tulipata majeraha ya mitego kwa kiungo cha nyuma cha kulia na majeraha hayo yamekwishatibiwa,” asema Dk. Victor Musiime, afisa wa mifugo wa UWEC, “Tunawezaona ubashiri mzuri sana ya kesi, na hivi karibuni baada ya matibabu na ukarabati, tunatafikiria kumwaachilia huyo pangolini arudi mwituni,” asema Dk. Musiime.

Dk. Mbabazi Racheal, mkurungenzi mkuu wa Idara ya Wanyama na Kilimo cha Bustani wa UWEC, asema pangolini ni sehemu ya wanyamapori wa nchi, kwa hivyo lazima wahifadhiwe na kulindwa.

“Kila mnyamapori anasehemu na jukumu yake muhimu kwa mfumo wa mazingira/ikolojia; hawako tu hapo. Pangolini wanatusaidia kwa kukula wadudu, hivyo basi wanadhibiti idadi, na pia watu wanatoka kote duniani kuja kuwaona hawa wanyama ambao nchi hupokea pesa kutokana nao, kwa hivyo tunapaswa kuhifadhi wanyamapori,” asema Dk. Mbabazi.

https://soundcloud.com/user-963336216/fighting_poaching_and_illegal_trafficking_of_pangolins?utm_source=clipboard&utm_medium=text&utm_campaign=social_sharing

Uhalifu wa kihusiano wa kimataifa yatishia viumbe vilivyo hatarini kutoweka

Vincent Opyene, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uhifadhi wa Maliasili, ambayo ni Shirika Lisilo la Kiserikali linaloshirikiana na Mamlaka ya Wanyamapori Uganda kupambambana na uhalifu, asema shida ya biashara haramu ya pangolini yanazidi kuongezeka duniani kote, pamoja na Uganda.

“Shida ya biashara haramu ya pangolini na magamba yake ni kuongezeka kila kuchao na kama haitadhitiwa na kusimamishwa, basi kutasababisha kutoweka kwa aina maalum ya viumbe waliolengwa kwa biashara,” Opyene atahadharisha.

Kunao aina nane za pangolini kote duniani, nne wanapatikana Asia na wengine aina nne Afrika.

Uganda kuna aina tatu kati ya nne ya pangolini wanaopatikana Afrika, wao ni Ground Pangolin, Giant Pangolin na the White Bellied Pangolin,ambaye pia hujulikana kama the Tree Climbing Pangolin.

C:\Users\ben\Desktop\pangolin project\videos and pix\204CDPFQ\Opyene 1.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Vikundi vya Kuhifadhi Maliasili (NRCN), Vincent Opyene. Picha na Benjamin Jumbe

Opyne husema aina wote ya viumbe wamelengwa nchini Uganda, huku wafanyabiashara pamoja na wawindaji haramu wa ndani wanahusika pakubwa kwa biashara hii wakiwa na matumaini ya kupata pesa.

 “Wanaua aina hii ya viumbe na kuchukuwa magamba yao wakiwa na matumaini ya kupata soko na hakika wafanye biashara na kuuza,” 

“Wakati wote tunapowakamata majangili wenye wanahusika kwa uwindaji haramu wao hutuambia wanauza takriban $150 kwa kilo, na sijawahi pata mtu yeyote aliye tayari kununua magamba ya pangolini kwa bei hiyo; kwa hivyo ni dhana tu wanaendelea kuamini ya kwamba soko lipo,” aliongezea kusema.

Kwa sasa duniani kote, hakuna soko halali kimataifa ya biashara ya magamba ya pangolini na nyama kwa sababu ya marufuku iliyopo kwa biashara ya kibiashara na mambo kama hayo.

Vyama vya Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Viumbe vilivyo Hatarini Kutoweka (CITIES), kwa walipokutana Johannesburg, Afrika kusini kwa mkutano wa kumi na saba ya Kongamano wa Vyama (CoP 17) mwaka wa 2016 walipiga kura kwa kauli moja walipiga marufuku biashara ya kimataifa ya kibiashara ya aina nane wote wa pangolini. (ban the international commercial trade of all eight species of pangolin).

Kauli hio ilisaidia pangolini kurodheshwa kwa orodha kwanza ya CITIES (CITIES Appendix I),maanake inawakilisha kiwango cha juu ya ulinzi kwa sheria ya kimataifa.

Mnano Desemba 2021, idara ya NRCN pamoja na UWA ilifanya operesheni ambapo kilo 900 za magomba ya pangolini, kilo 200 za pembe za ndovu na aina zingine za bidhaa zilipatikana kwa kituo cha mtaa wa Nakirama Wilayani Nsangi, Wakiso.

Washukiwa wawili walikamatwa na kulepekwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi pamoja na Gasama Sikhou, mwenye umri wa miaka 59 raia wa Senegali, na na msaidizi wake, Suleiman Katende, mlinzi.

“Mkuu wa Sheria nchini ametupatia maelekezo yakufuatilia faili ili kuidhinishwa, kwa hivyo tunajaza pengo zilizoko kwa faili kisha turudishe iidhinishwe,” Opyene aongeza kusema.

Tangu 2013, Kundi la Uhifadhi wa Maliasili (Natural Resources Conservation Network)  limesaidiwa kushtaki wahalifu zaidi ya 5000, na kuchunguzwa kwao kumesaidia kukamatwa kwa zaidi ya wahalifu 8000,

Matokeo na hitimisho kutoka kwa Tume ya Haki kwa Wanyamapori (WJC)’s Kitengo cha Maendeleo ya Ujasusi inaelekeza lawama kwa kundi la uhalifu linayofanya kazi kwa kiwango cha kiwanda na inayotishia aina maalum ya wanyamapori nzima hatarini.

Kulingana na tume hiyo, kati ya 2016 na 2019, takriban tani 206.4 za magamba ya pangolini zilizuiliwa mahali tofauti 52 kote duniani zikachomwa (intercepted and confiscated).

Wadadisi wa WJC wanaamini kuwa hiyo ni sehemu tu ya idadi inayosafirishwa kiharamu, kwa sababu sehemu kubwa  muhimu ya magendo hazijatambuliwa.

Uchambuzi wa shirika hiyo kuhusu takwimu za uzuizi kwa muda wa miaka nne yaonyesha ongezeko la usafirishaji haramu wa hali ya juu zaidi karibu thuluthi mbili ya tani 132.1 zilizozuiliwa na zikagunduliwa kati ya mwaka 2018 na 2019.

Ilibainika zaidi ya kuwa mwaka wa 2019, kusafirisha shehena moja yenye magamba ya pangolini  ulikuwa na uzito wa wastani tani 6.2 ikilinganishwa tani 2.2 miaka mitatu hapo awali.

Uwindaji haramu wa pangolini hasa hutekelezwa kwa maeneo yaliyolindwa na kuhifadhiwa kama Hifadhi ya Kitaifa ya Murchison Falls.

Wawindaji haramu wa zamani watoa tahadhari

Wilayani Nwoya, inayopakana na Hifadhi ya Kitaifa ya Murchison Falls, gazeti ya Daily Monitor na InfoNile iliwahushisha wawili wa wawindaji haramu kupata ukweli wa mambo kiliyowachochea kuingia kwenye biashara hiyo.

https://soundcloud.com/user-963336216/tales_of_a_former_poacher?utm_source=clipboard&utm_medium=text&utm_campaign=social_sharing

Mmoja aliyekubali lakini kupendelea kutojulikana kwa manufaa ya usalama wake alisema alianza uwindaji haramu mwaka wa 2009 kwa sababu ya kutafuta karo ya shule.

“Miaka hii yote nikiwanawinda, nimekamatwa karibu mara 5 na kupelekwa hata Masindi; nilihukumiwa kwa miezi mitatu kwa gereza la Isima, wengine kule magereza ya Gulu, Logore,” akasema.

Alisema wakati alipokirudi nyumbani mwaka 2019 baada ya kumaliza hukumu yake, alimua kuachana na uwindaji haramu, hii ni kutokana na hasara ya pesa alizozitumia kurejesha uhuru wake. 

“Niliacha uwindaji haramu mwaka wa 2019 kwa sababu nilipoteza ardhi nyingi, kwa sababu kila nilipokamatwa, wangeuza kipande cha ardhi kunitoa nje, na pili, watu wengine waliuawa,”

Aliyekuwa Mwindaji haramu

Alisema hakuwahi kukutana na watu ambao hutoka ng’ambo kununua pangolini lakini huwanashirikiana na washirika wao ambao wangewaelekeza nini kupata.

Anasema aliwanasa takriban pangolini watano lakini hakufaidika kutoka kwao kama alivyotarajia. Badala yake karibu apoteze maisha kutokana na hatari, na hiyo ndiyo maana hatimaye aliacha biashara na kwa sasa anawahimiza wenzake wangali kwa biashara hiyo waachane nayo kwa usalama wao na manufaa ya wanyamapori.

Jangili mwingine wa zamani, Chrales Oryem mwenye umri wa miaka 57, mkazi wa Olwiyo kituo cha biashara, mtaa wa Patira mashariki, kata ndogo ya Parungo, aliyeanza uwindaji haramu mwaka wa 2012, alisema yeye pia alilazimika kuachana na mazoea mwaka 2016 baada ya kukamatwa mara kadha na upotezaji pesa. 

C:\Users\ben\Desktop\pangolin project\videos and pix\205CDPFQ\Oryem.jpg
Charles Oryem, mwindaji wanyamapori wa kitambo wilayani  Nwoya. Picha na Benjamin Jumbe

Oryem hatua ya kugeuka ilikuwa wakati alipigwa risasi na walinzi wa UWA alipopatikana katika bustani mwaka wa 2016 na kujeruhiwa vibaya sana.

Alisema alisaidika na Shirika Lisilo la Kiserikali waliokuwa wanawasaidia waathirika wa vita kutoka kwa Jeshi la Upinzani wa Bwana (LRA) baada ya kujisajilisha kama mmoja wao.

“Walitumia shilingi milioni 25 kwa matibabu yangu,” alisema.

Oryem awahimiza Mamlaka ya Wanyamapori Uganda walenge vikundi vya jamii waliokaribu na bustani na manjangili waliobadilika wapate njia bora ya kuishi.

“Hii itasaidia kuokoa wanyama wengi kwa kufa,” alisema.

Vile husemwa mtu humweka mwivi ashike mwivi, anasema Mamalaka ya Wanyamapori Uganda wanastahili kuhusisha manjangili wa kitambo wasaidie kumaliza uasi na kufikia wenzao wa kitambo wangali biasharini. 

“UWA wanastahili kuja kwetu hapa chini na wazungumuze nasi wawindaji haramu na tuwape ushauri juu ya kufanya kukomesha uwindaji haramu,”

Charles Oryem, mwindaji wanyamapori wa kitambo wilayani  Nwoya.

“Hata kama UWA wakuje kwa jamii na waongee na wawindaji, hatuwezi sikia; hata hivyo mwindaji akiongea na mwenzake ni rahisi sana wasikizane na kuwashawishi wengine waache kuwinda,” alisema.

Oryem asema ni muhimu sana kwa UWA wapate habari kutoka kwa wawindaji wao wenyewe kwa sababu viongozi wengine wakijaribu kuwaongelesha, hawatakuwa na mamlaka na uadilifu kisa na maana baadhi wao wanahushishwa kwa ulaji wa nyama ya porini.

Kwa mfano nilipokamatwa, nyama yenye tulipatikana nayo; ilichukuliwa na LC3. Sasa kama viongozi wanaohusika kwa nyama ya porini, kisha baadaye wanakuja kwetu kutuongelesha tuwaachane na uwindaji, hatuzingatia kama watu wa kutegemewa, lakini tutaamini wenzetu ya kwamba wanatuambia ukweli; na hivyo ndivyo tutakomesha uwindaji haramu,” alishauri.

Hatua za kisheria zinaongezeka, ingawa rushwa bado ni changamoto

Rebecca Sandoval, kiongozi wa mradi wa uhifadhi wa pangolini, alisema bado kunaohaja ya kuhamasisha umma kuhusu sheria mpya ya wanyamapori, alisema wengi bado hawathamini umuhimu wa kuhifadhi wanyamapori na adhabu kubwa katika sheria.  Adhabu kubwa  zaidi kwa sheria mpya 2019 ya wanyamapori ni faini isiyozidi shilingi bilioni 20 au kifungo cha maisha au zote mbili kwa kosa nilinalohusiana na aina ya viumbe vya wanyamapori walioainishwa hatarini sana kutoweka porini.

“Nafikiria tunahitaji elimu zaidi;kufahamishwa zaidi manufaa ya wanyama kwa jamii, watalii, uhifadhi, na nafikiria tunahitaji kufahamishwa zaidi kuhusu sheria ya wanyamapori. Watu wanastahili kuelewa ya kwamba kuna sharia ya wanyamapori na madhara makubwa ukikamatwa,” alisema Sandoval.

Aliongeza kusema juu biashara usiohalali wa wanyamapori ni ya kimataifa, kuna kazi nyingi ya kufanya kuvuruga biashara hiyo na waandani wake.

“Tunahitaji waandani wenye wanaweza kupambambana na waandani wahalifu. Ushirikiano zaidi na kutoa habari kwa umma inahitajika na umuhimu wa pangolini na haja ya kuwalinda,” alisema.

Walakini, adhabu katika kesi za mashtaka inayohusisha pangolini na Mamlaka ya Wanyamapori Uganda kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019 hadi 2020/2021 kwa ujumla ni wapole zaidi.

Adhabu katika kesi 44 zinazohusisha pangolini kwa ujumla ilitofautiana kutoka kwa faini kati ya shilingi za Uganda 200,000 hadi shilingi za Uganda 3,000, 000 (USD $56-$838), na kati ya miezi 3 hadi 24 gerezani. Kulikuwa na kesi mbili tu zilizohusisha kifungo cha jela zaidi ya mwaka mmoja, mojawapo ya vifungo hivi vya lazima ikiwa tu aliyehukumiwa hawezi kulipa faini. 

Kwa mfano, kesi moja inayohusisha mzoga wa pangolini mwaka wa fedha 2019/2020 alihukumiwa faini ya shilingi za Uganda 300,000(USD $84) pekee. Kesi nyingine inayohusisha pangolini mmoja hai mwaka wa fedha 2020/2021 alihukumiwa faini ya shilingi za Uganda 1,000,000 (USD $279). Kesi katika mwaka huo huo inayohusika na kilo 3.62 za magamba ya pangolini ilipigwa faini ya shilingi za Uganda 2,000,000 ($559). Kesi nyingine inayohusisha pangolini mmoja hai alihukumiwa miezi 3 tu gerezani.

Data hii imefuatiliwa na kuchapishwa kwenye ramani ya the #WildEye East Africa map na InfoNile pamoja na Oxpeckers.

Alipoulizwa kuhusu hali ilivyo, John Makombo, Mkurugenzi wa Kuhifadhi katika Mamlaka wa Wanyamapori Uganda alisema Mahakama ni taasisi huru “inayoweza kufanya maamuzi kuzingatia maoni yao laikini pia kuongozwa na sheria.”

Hata hivyo alisema moja kati ya mikakati ya kuboresha hayo, mamlaka yanafanya uhamasishaji mwingi juu ya mahakama.

 “Kwa kweli hiyo ndiyo mojawepo ya mikakati tunayotumia kuhakikisha wahalifu wanahukumiwa kulingana uhalifu waliotekeleza,” alisema Makombo.

Biashara haramu ya wanyamapori na usafirishaji wa wanyama hurahisishwa na kushindwa kwa baadhi ya watu ndani ya duru za utekelezaji wa sheria kufanya kazi kitaaluma. Moja kati ya changamoto hizo ni rushwa.

Wakati huo huo, Opyene kutoka kwa Waandani wa Uhifadhi wa Maliasili (NRCN) alisema rushwa inaweza kudhihirika katika hatua yoyote ile, katika uchunguzi, polisi, mahakama, au mkurugenzi wa mashtaka ya umma, na  kwa hivyo inabidi ichunguzwe, kutambuliwa na kusimamishwa kabla halijatokea.

 “Jambo moja tumeona ni kwamba suala kwa nini uchunguzi umeshindwa ni kwa sababu ya rushwa. Wakati watu wanaopaswa kuunga mkono kugeuka na kuanza kufanya kazi kwa wasafirishaji, watu wasio sahihi, basi uchunguzi hauwezi kufanikiwa,”

Opyene kutoka kwa Waandani wa Uhifadhi wa Maliasili (NRCN)

Anaongeza kuwa wana watoa taarifa wanaowasaidia kubaini ufisadi na mapungufu ndani ya mashirika ya utekelezaji na kuhakikisha kwamba haya yanaripotiwa na haki inatendeka.

Ili kuboresha mashtaka, Opyene alisema walisema wamewasiliana na waendesha mashtaka na kujadili namna bora ya kuboresha. “Njia pekee ya kufanya hivyo kwa ufanisi ni kuwa na uchunguzi unaoongozwa na mashtaka ambapo mwendesha mashitaka huletwa kwenye bodi tangu mwanzo wa upelelezi ili ikihitimishwa, mtuhumiwa afikishwe mahakamani,” alisema.

Hii ni kuzuia suala la washukiwa kutoka kwenye ndoano kutokana na kukosekana kwa ushahidi,huku upande wa mashtaka ukiomba muda zaidi wa kuchunguza kesi hiyo.

George Owoyesigire, kaimu mkurugenzi wa uhifadhi wa wanyamapori katika Wizara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale, alisema wizara ina wasiwasi kuhusu uwindaji haramu kwa jumla na hasa uvunaji haramu wa pangolini.

“Tuliona ujangili mkubwa karibu mwaka wa 2015 tulipokamata takriban kilo 2,000 ya magamba ya pangolini. Lakini kwa sababu ya juhudi za pamoja kuwekwa ili kushughulikia suala hilo,ujangili umepunguzwa,” alisema Owoyesigire.

Asema baadhi ya kesi za kukamata na kunyang’anywa leo kuakisi kiwango cha juhudi za serikali ya Uganda imejipanga kupambana na tabia hiyo mbaya na sio ongezeko katika ujangili kwa kusema.

 “Tumesambaza taratibu na uingiliaji kati tofauti kuwanasa na kuwakamata wahalifu hawa, hivyo utaona ongezeko la kutaifishwa kwa pembe za ndovu,magamba ya pangolini na meno ya kiboko, lakini hii ni kama matokeo ya ufuatiliaji mkali, vyombo vya sheria na ujasusi pia,” aliongeza.

C:\Users\ben\Desktop\pangolin project\videos and pix\206CDPFQ\Mr O.G.jpg
Bw. George Owoyesigire, kaimu mkurugenzi wa uhifadhi wa wanyamapori katika Wizara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale. Picha na Benjamin Jumbe

Owoyesigire alisema kuwa wakati awali kulikuwa changamoto katika kushughulikia kesi za wanyamapori, uanzishwaji ya Huduma, Mahakama ya Kawaida na Wanyamapori tangu Mei 2017 imesaidia kuleta mbele wasifu wa uhalifu wa wanyamapori, ambao pia umeonekana kuongezeka kwa mashtaka na kushughulikia kwa ufanisi kesi hizi.

Owoyesigire asema katika ngazi ya bara, kikanda na kitaifa kuna mikakati ya kupambana biashara haramu ya wanyamapori, akionyesha matumaini hayo kwa kuongezeka kwa ushirikiano kati ya nchi washirika, zoezi hili litaondolewa kwa ufanisi.

“Masharti chini ya mkataba huu yanatulazimisha kama nchi wanachama kufanya kazi pamoja ili kuhifadhi maliasili na wanyamapori pia kupigana kinyume cha sheria na biashara ya mipakani. Kwa hivyo, tunayo njia kadhaa za kuhakikisha tunapunguza tishio hili linaloongezeka,” Owoyesigire aongeza.

Chini ya ibara ya 116 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka wa 1999, Nchi Wanachama ziliazimia kuunda umoja na sera iliyoratibiwa kwa uhifadhi na endelevu matumizi ya wanyamapori na maeneo mengine ya utalii.

Inaeleza kuwa hasa, Nchi Wanachama;

 (a) kuoanisha sera zao za uhifadhi ya wanyamapori, ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa;

 (b) kubadilishana habari na kupitisha sera za pamoja, juu ya usimamizi na maendeleo ya wanyamapori;

(c) kuratibu juhudi katika kudhibiti na ufuatiliaji uvamizi na shughuli za ujangili;

(d) kuhimiza matumizi ya pamoja wa vifaa vya mafunzo na utafiti na kuendeleza mipango ya pamoja ya usimamizi ya ulinzi wa maeneo ya mpaka; na

(e) kuchukua hatua za kuidhinisha au kukubaliana na, kutekeleza mikataba ya kimataifa

Mnamo Machi, waendesha mashtaka wa serikali kutoka nchi 11 za Afrika mashariki iliahidi rasmi(pledged)  kuratibu juhudi za kupambana na mipaka usafirishaji wa wanyamapori na ubadhirivu wa fedha 

Ili kuimarisha zaidi juhudi za kupambana na haramu na uhalifu wa wanyamapori, Mamlaka ya Wanyamapori Uganda (UWA) imeanza uundaji wa mtaala kwa uhalifu wa wanyamapori,maarifa, uchunguzi na utekelezaji wa sheria. 

Mtaala huo utasaidia UWA kuwa na kiwango chake cha kutoa mafunzo kwa nguvu yake ya kuanzia hatua za awali za kuingia katika shirika. Sehemu nyingine ya mafunzo inazingatiwa ni pembe ya taaluma, itakoangazia jinsi mlinzi wa kawaida anakuwa mwafanyakazi/afisa mwerevu na mchunguzi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa UWA, Sam Mwandha alionyesha matumaini kwamba katika miaka ijayo, Mamlaka itakuwa na watendakazi bora zaidi wa kulinda wanyamapori na kupambambana na uhalifu kwa wanyamapori katika kanda.

 “Hatua hii matokeo yake kwetu ni kutuletea ujuzi wa hali ya juu ya wanakazi eneo la Afrika mashariki, ambayo itasaidia taifa kwa kupambambana na uhalifu wa wanyamapori. Mara tu tuna nguvu yenye ujuzi, wahalifu watachukia biashara yao na idadi ya wanyamapori itaongezeka,” alisema Bw. Mwandha. 

Kulingana na Meneja wa Uchunguzi- UWA Major Joshua Karamagi, hii ni mwanzo wa safari ndefu ya kuhakikisha uwezo wa kutosha kwa maarifa, uchunguzi na utekelezaji wa sheria kwa watumishi katika taasisi hiyo.

“Tunasonga mbele kuhakikisha tunawataalam wenye nguvu na uwezo wa kusanya  habari za ujasusi kuhusu uhalifu wa wanyamapori; hii itaendeleza kazi yetu ya kupambambana uhalifu wa wanyamapori,” alisema.

Hi ilikuwa zoezi la mafunzo mwezi Machi iliyowaleta washiriki kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Uganda, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda na polisi ya Uganda. Wengine walikuwa wawezeshaji wa ndani na kimataifa kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu.

Msaada ya maendeleo na uzalishaji wa hadithi hii imetoka kwa InfoNile, kwa kushirikiana na Oxpeckers, kwa ufadhili wa Earth Journalism Network. Ripoti ya ziada na uhariri ni pamoja na Ruth Mwizeere  na Annika McGinnis wa InfoNile.Vielelezo vya data kwa taswira na Ruth Mwizeere.