Mary Akinyi does not filter or treat the water scaled

Kwa Nini Mto Nile?

Mto Nile, mto mrefu zaidi duniani, unapita katika nchi 11 barani Afrika na ni muhimu katika uchumi, diplomasia na ustawi wa mataifa haya. Mto huo pia ni sehemu kuu ya bayoanuai ya ulimwengu na uti wa mgongo wa mifumo mingi ya ikolojia dhaifu ya Afrika. 

Leo, upo katika vitisho vipya na vinavyoendelea: mabadiliko ya tabia nchi, ukuaji wa idadi ya watu na uchumi, siasa za maji baina ya nchi hizi, na ujenzi wa mabwawa makubwa ambayo yanatishia kupunguza upatikanaji wa maji kwa nchi zinazotegemea sana maji ya Mto Nile – kutaja machache tu. 

InfoNile inalenga kuziba pengo kati ya wanasayansi na watafiti, waandishi wa habari, na umma ili kujenga uelewa wa pamoja  wa masuala mbalimbali ya maji katika mto huu muhimu na wa kale.

Tunatoa ruzuku za habari, mafunzo na ushauri kwa waandishi wa habari katika Bonde lote la Mto Nile ili kuwasaidia kutengeneza habari za kina kuhusu maji, mazingira, bayoanuwai na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Tunaangazia taarifa zinazoleta suluhu ambazo zinafanya kazi ya kutatua changamoto za masuala  kama vile mabadiliko ya tabia nchi na usafirishaji haramu wa wanyamapori katika jamii za wazawa. Kwa kushirikina na Code for Africa, tunawafundisha na kuwanasihi wanahabari katika uandishi wa habari za data, michoro na uandishi wa habari wa kijiografia.

Tunazalisha habari mbalilmbali za uchunguzi nje ya mipaka, ikiwa ni pamoja na habari za ardhi kwa wageni kutoka je ya nchi, usafirishaji na uhifadhi wa wanyamapori, mabadiliko ya tabia nchi, na athari za mabwawa makubwa; kwa njia hiyo, tunakuza ushirikiano katika nchi zote na kukuza mbinu mpya za kuandika habari  za kijiografia kama vile ramani zinazotegemea data, video zisizo na rubani na picha za setilaiti.

Tunatengeneza ramani shirikishi, kuhusu masuala ya maji na mazingira, na “tunachora” habari  zetu kwenye ramani hizi ili kuongeza safu ya ubinadamu katika data. InfoNile ni sehemu ya Waandishi wa Habari za Maji Afrika (Water Journalists Africa), mtandao mkubwa zaidi wa waandishi wa habari wanaoripoti masuala ya maji barani Afrika.

Tumepokea ufadhili kutoka kwa mashirika mbalimbali ya maendeleo ya vyombo vya habari, taasisi za utafiti wa maji, na wafadhili wengine wanaopenda uhifadhi wa mazingira. Je, ungependa kuunga mkono ripoti za mazingira ambazo hazijaripotiwa? Tafadhali wasiliana nasi kwa [email protected].Unaweza kusambaza ramani zetu shirikishi au kupachika moja katika tovuti yako. Data zote ni chanzo huria na zinapatikana kwa kupakua.

Athari za Umma

martelo

Mnamo Agosti 2023, baada ya hadithi ya Jonas Kiriko kuhusu ufisadi katika taasisi za kuhifadhi wanyamapori, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliwaidhinisha maafisa kadhaa wa DRC, wakiwemo wakurugenzi wa zamani wa Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira ya Kongo na CITES, kuwazuia kuingia Marekani.

pavao

Kutoka kwa hadithi ya Aimable Twahirwa, Wizara ya  Mazingira ya Rwanda iliunda maeneo zaidi ya hifadhi za kreni ili kukuza  juhudi za uhifadhi Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) imeanza kushirikiana na Chama cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Rwanda  (RWCA) na washikadau wengine ili kukomesha biashara haramu na ufugaji wa ndani wa Gray Crown Cranes.

ondas

Hadithi ya Prosper Kwigize iliangazia ukiukwaji katika mradi wa maporomoko ya maji ya Rusumo, ambapo mafuriko yaliathiri jamii, na kusababisha onyo na faini ya Tsh 10m kwa mkandarasi kutoka Baraza la Mazingira la Tanzania.

Mafunzo na ushauri

Slide

Usaidizi wa InfoNile umebadilisha taaluma yangu ya uandishi wa habari, na kuniweka kama mwanahabari wa kuigwa na mwenye ujuzi wa kuripoti kuhusu maji na uhifadhi wa wanyamapori katika mkoa wa Mara. Hili limenitia moyo kuzindua Mara Online News, jukwaa la kidijitali linalojihusisha na masuala ya maji, uhifadhi wa wanyamapori na masuala ya maendeleo ya ndani.

Mugini Jacob(Tanzania) Daily News/ Mara Online News blog

avatar2

previous arrow
next arrow
image 23
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384
Rectangle 384

Ushuhuda

Slide
avatar test

Kufanya kazi kwenye mradi wa Infonile kumeongeza uelewa wangu wa jamii zilizotengwa, kuonyesha jinsi uandishi wa habari unavyoweza kukuza sauti na kuleta mabadiliko ya kijamii. Ilithibitisha imani yangu katika uwezo wa kusimulia hadithi ili kuhamasisha mabadiliko.

Kwame Niaje, Mwandishi wa Habari wa Mradi wa Infonile