Vyama vya Ushirika vya Mazingira vyaanzisha njia mbadala za kujikimu katika maeneo ya hifadhi.

Vyama vya Ushirika vya Mazingira vyaanzisha njia mbadala za kujikimu katika maeneo ya hifadhi.

Na Christopher Bendana

Laban Zaribugire, kwa ufahari, alionyesha sehemu ya ardhioevu ya mfumo ikolojia wa ardhioevu ya Igona katika wilaya ya Kabale iliyorejeshwa.

“Tazama ule ujiuji katika kila upande unaofunga mto,” alisema akionyesha kidole chake katika bonde ambapo maji ya mabwawa yalikuwa yakitoka katika pande zote za mto huko Nyamigamba, wilaya ya Kabale. “Unaona hiyo bustani ya viazi ulaya; kabla ya sisi kuliingilia kati eneo hilo, mimea hii ingekuwa inanyonya maji.”

Uingiliaji kati anaouzungumzia ni ule mpango mkakati wa ukarabati wa bwawa, ambao ni ushirikiano kati ya Wizara ya Maji na Mazingira (MWE) na chama cha ushirika cha mazingira SACCO yaani Upper Maziba Farmers Water and Environment Cooperative.

Hii ni mojawapo ya programu kadhaa zinazoendeshwa na wizara ya maji, chini ya mkakati wake wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Jamii katika Kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi Kupitia Ushirikishwaji wa Mikoa, Usimamizi wa Maji na Rasilimali Husika nchini Uganda (EURECCCA). Mradi huo ulianza 2017-2023 na unafadhiliwa na Mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Adaption Fund) chini ya uangalizi wa Sahara na Sahel Observatory. 

Laban Zaribugire area cleared of encalptus. He is the chairman of UMEEC 1
Laban Zaribugire, mwenyekiti wa kuta za UMEEC akipitia eneo lililokatwa miti ya mikaratusi

Mradi huu ulikusudiwa kusaidia jamii kukabiliana na mafuriko na maporomoko ya ardhi kupitia vyanzo vilivyounganishwa, usimamizi endelevu wa maji na rasilimali zinazohusiana na hizo. Programu ya Maziba ilitekelezwa, moja ikiwa huko Aswa kaskazini na nyingine huko Awoja mashariki.  

Kiukweli, yuko sahihi. Sehemu ya bwawa hapa Nyamigamba, sehemu ya mfumo wa ikolojia wa ardhioevu ya Igona imerejeshwa. Bustani pia hazinyonyi maji tena. Yanaishia kwenye ukingo uliowekwa na MWE. Hata watu pia wanafahamu sana jukumu la madimbwi katika mfumo wa ikolojia.

Lakini maji bado yana matope, na baadhi ya madimbwi yamejaa ng’ombe wa Friesian, na hii ina maanisha kwamba bado kuna kazi kubwa inahitajika ili bwawa hilo lirudishe eneo lake lote na liendelee kusafisha maji.

Kulingana na taarifa ya wizara ya mazingira, inasema, Uganda imepoteza takriban asilimia 40 ya ardhi oevu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, mengi yakiwa yamejaa maji huku idadi kubwa ya watu nchini Uganda ikitafuta mashamba mapya au kutengeneza maeneo mapya ya viwanda.

Area not recovered 1
Maeneo ambayo hayajarejeshwa yenye maji ya matope

Ripoti hii iliyopewa jina la “Hali ya Ardhi Oevu nchini Uganda 2019” ya Wizara ya Maji na Mazingira inaonyesha kupungua kwa eneo la ardhi oevu kutoka asilimia 16 mwaka 1994 hadi asilimia 13 mwaka 2015 ya eneo lote la ardhi nchini. Kati ya hizi asilimia 13, asilimia tisa iko salama, wakati asilimia nne ya ardhi imeharibiwa. 

Utafiti huo, wa kwanza na wa aina yake nchini Uganda, ulijikita kuangalia takwimu za 1994 na 2015. Unaorodhesha vichochezi vikuu vya uharibifu wa ardhioevu: ukuaji wa miji, ukuaji wa idadi ya watu, uratibu mbovu wa mipangomiji, na mahitaji ya ardhi ya kilimo. Utafiti huo ulionya kuwa hali ya uharibifu ilivyosasa, ifikapo mwaka 2040, nchi haitakuwa na ardhioevu.

Hivi karibuni, ardhi oevu ilianza kujirejesha yenyewe. Wakazi wa Kabale walisema kuwa hali ya hewa imebadilika, na kuna mafuriko zaidi sasa kuliko hapo awali. 

“Mafuriko yanasababisha viazi ulaya kuoza bustanini kabla hata havijavunwa,” Hope Busingye, mfugaji wa kuku kutoka kijiji cha Karugashe, Parokia ya Butobere, Manispaa ya Kabale, ambaye pia ni mwanachama wa kikundi cha SACCO, aliiambia ScienceNowMag. 

“Tayari tulikuwa na hamu ya kutafuta njia mbadala za kujikimu kwasababu bustani zetu katika maeneo oevu muda mwingi zinajaa maji. Ujenzi wa barabara na ujenzi wa masoko katika mji wa Kabale umesababisha mafuriko na dhoruba”.

“Mfumo wa hali ya hewa pia umebadilika. Mvua ilikuwa inanyesha baada ya mavuno, sivyo tena, lakini ndiyo hivyo hatusikii. Baadhi ya watu bado wanapanda kwenye ardhi oevu.”

Busingye aliyekuwa akilima katika eneo oevu kwenye ardhi iliyokodi kutoka kwa mwenye leseni ya NFA na kufanikiwa kwa kiasi fulani cha mapato, yeye na wengine wameamua kuondoka kwenye mabwawa na kujitosa katika vitega uchumi mbadala.

MWE kupitia Excel Hot Consult iliwapatia mafunzo ya ujuzi wa kimsingi kama vile mafunzo katika njia mbadala kama vile kuhifadhi vitabu, kuunda vikundi na utambuzi wa mradi.

Mwaka jana, Wizara ilitoa pia mtaji (Ruzuku) ya UGX 206Mil katika kikundi cha wanachama 335 katika wilaya za Kabale na Rubanda. Mfuko huo umepanda hadi kufikia UGX 260Mil kupitia mauzo ya hisa na ada za uanachama.

Mwanachama yeyote anayekopa zaidi ya UGX 1Million anapata hisa na anayejiunga kwa mara ya kwanza analipa UGX 20,000 ili kuwa mwanachama. Kando na banda la mifugo, Wengine wapo katika ufugaji wa ng’ombe na ulimaji wa uyoga.

Wanachama huunda vikundi na kukopa kutoka kwenye ushirika ingawa kila mmoja ana uhuru wa kuchagua biashara yake mwenyewe. Kiasi cha juu ni 3m kwa kila mwanachama anayelipwa baada ya miezi 18 kwa 1% kwa mwezi kwa msingi wa kupunguza. Pia kuna kipindi cha ufadhili cha miezi 3.  

Busingye, mkulima wa mjini Butobere, katika manispaa ya Kabale amewekeza katika ufugaji wa kuku tangu Juni mwaka jana. Ananunua vifaranga 300 vya kuroiler kwa siku kila mwezi na huuza baada ya siku 30.

“Kipato changu kinakaribia kile kiwango nilichokua nikikipata wakati nalima kwenye mabwawa, lakini, unajua kuna kawasiwasi Fulani hivi kwenye ufugaji wa kuku kuliko katika kilimo cha viazi ulaya,” alisema.  Kwa viazi ulaya, msimu mmoja ukifanya vizuri, basi msimu unaofuata kunakuwa na mafuriko. Lakini kwenye kuku, unachohitaji ni kumtunza tu vizuri huyo ndege.”

Deogratias Kabebasiza, mkulima wa kawaida wa Kigoji, katika tarafa ya Kabale ni mwanachama mwingine anayefanya kazi zake katika bustani ya nyuki, ingawa anasema bado hajapata faida, ila ana matumaini.

Deogratias Kabebasiza of kigongi Kabale Municpality . he is a member of Upper Maziba Water and Environment Cooperative 1
Deogratias Kabebasiza wa Kigongi, Manispaa ya Kabale. Ni mwanachama wa Upper Maziba Water and Environment Cooperative.

Mkulima huyu mzoefu, hulima mharage, mahindi na viazi ulaya na pia yeye yupo katika ufugaji wa nguruwe. Anasema ardhi katika maeneo oevu inatoa mavuno bora kuliko kwenye miteremko.  

Shamba la Kabebasiza linachukua sehemu mipaka ya ardhioevu iliyo karibu na shamba la mikaratusi, ambalo linamilikiwa na NFA. Wizara ya maji tangu wakati huo pia imeweka vigingi katika sehemu ya ardhi ya Kabebasiza ili kuweka mipaka ya ardhi oevu.

“Ninajua kazi ya ardhi oevu, anasema kiongozi wa zamani wa eneo hilo. Nimejifunza mengi kuhusu mazingira kutoka kwenye redio.  Niko tayari kuondoka kama wataweza kunilipa fidiaa, alisema.

Jolly Takacungurwa kutoka kata ya Mwanjari, Tarafa ya Kusini na wanachama wengine saba wa kikundi chake wako kwenye hifadhi ya nyuki. Walichukua mkopo wa UGX 8 milioni, takriban dola 2,000 mwezi Aprili 2023, ili kuwekeza katika maisha mbadala. Mkopo wao hulipwa ndani ya miezi 18 kwa riba ya asilimia moja. 

“Tuna mizinga 160, ambayo mtu anaweza kuvuna kilo 10 kwa msimu kwa mzinga wa nyuki (ndani ya miezi mitatu). Kwa kilo moja ya asali kwa UGX 10,000 (USD 4) tunaweza kulipa mkopo huo katika miezi sita tu baada ya mavuno yetu ya kwanza na kisha tunafanya biashara,” alisema.

Naibu mratibu wizara ya maji, Annet Nantongo, ambaye ndiye mfadhili wa vyama vya ushirika aliiambia ScienceNowMag kwamba wizara ilifadhili vyama vya ushirika katika maeneo matatu ya vyanzo vya maji. Maeneo hayo ni Maziba Kusini Magharibi, Aswa kaskazini na Awoja mashariki.

Eneo la Maziba ni pamoja na Kabale, Rubanda, Rukiga na Ntungamo. Eneo la Aswa ni pamoja na Kitgum, Lira Otuke huku eneo la Awoja ni pamoja na Serere, Soroto, Kumi, Kapchorwa.

Nantongo anasema kuwa lengo lilikuwa ni kuwaongezea uwezo wavamizi hao kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwapatia njia mbadala za kujikimu zinazowapatia kipato bora kuliko kile ambacho wamekuwa wakikipata kutoka kwenye mabwawa.  

Jamii huchagua shughuli zao wenyewe ambazo wana utaalamu nazo. Ufugaji wa nguruwe, kuku, na ufugaji wa wanyama ndizo shughuli kubwa zinazoanyika Maziba, Siagi na usindikaji wa Alizeti hufanyika huko Aswa, na kwa upande wa Owajo wao hujishughulisha na ufugaji wa mbuzi na kondoo.

Patrick Byakagaba, mhadhiri wa masuala ya maliasili kutoka Chuo Kikuu cha Makerere anaamini kuwa njia mbadala za kujipatia riziki zinatoa chaguo bora kuliko kusema utekelezaji na sheria nyingi.

“Maliasili ni muhimu kwa maisha yao, kwani inaonekana hakuna chanzo kingine cha maisha yao,” anakisia kwa nini wanakwepa ardhi oevu.

Anapendekeza kuwaunganisha wanachama na hoteli na biashara ambazo ni endelevu kama vile hoteli ya Sheraton. “Hii itaboresha kipato chao,” anasema

Mchumi na Mkurugenzi wa Jukwaa la Kiuchumi katika Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala, Fred Muhumuza, alikiita chama hicho cha ushirika wa mazingira kuwa ni mwanzo mzuri lakini alipendekeza kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara kilabaada ya miaka mitatu ya kwanza chini ya kile kinachojulikana kama modeli ya kuhitimu. Hii itasaidia kufanya masahihisho na uboreshaji ili watu wasirudi tena kwenye uharibifu wa vyanzo vya maji n mazingira. 

“Angalia ni nani anayepata tabu,” akimshauri mtekelezaji wa mpango huo. “Fanya nao kazi hadi uhakikishe kuwa wapo. Endelea kuwaangalia. Ni eneo jipya. Ikiwa nina shida, nina mtu wa kushauriana naye, kushindwa. Ikifanikiwa, wizara inaweza kuwa mfano.”

Sawa na Byakagaba, pia alisisitiza umuhimu wa kuwasaidia wavamizi wa zamani wa maliasili kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Henry Tumwesigye, afisa maliasili wilaya ya Kabale, anauchukulia mtindo huo kama njia ya maisha kwani unawapatia wakazi wa eneo hilo mapato mbadala baada ya agizo la Rais Yoweri Museveni la 2022 kuhusu mazingira alilowataka wavamizi wote wa ardhioevu kuondoka kwenye mabwawa.

Anaamini kuwa mradi huo una athari kubwa katika mageuzi ya maendeleo ya kijamii, kwa kuzingatia kiwango cha chini riba cha asilimia moja ambacho walengwa hulipa kama sehemu ya uwekezaji wao.

“Tunahitaji tu watungezee mtaji wa mbegu,” alisihi.

Wanasayansi wanaotafiti uhifadhi wanakubaliana na wenzao katika uchumi na maliasili. 

Utafiti wa Daniel Abowe, “Uhifadhi wa nyani na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa uliotumika katika misitu binafsi ya Budongo-Bugoma,” ulifichua nia ya jamii jirani kushiriki katika shughuli mbadala kama vile upandaji miti na upandaji miti ikiwa watapatiwa mtaji.

Msitu wa Hifadhi ya Budongo umepoteza asilimia 40 ya eneo lake kutokana na wavamizi.

“Njia mbadala za kuishi zitaokoa makazi hayo ya sokwe," anataja katika mapendekezo yake.

Robert E. Katikiro, katika utafiti wake wa 2016 nchini Tanzania, wa“ Afua mbadala za kuboresha maisha katika maeneo ya hifadhi baharini,” ulichapishwa katika Sera ya Bahari, pia anatoa mtazamo wake juu ya kusimamia afua hii ya mradi wa mafanikio wa maisha mbadala.  

Utafiti wake ulijikita katika miradi mbadala ya kuendesha maisha inayofanywa na vikundi vilivyochaguliwa vya watu binafsi katika vijiji sita, vilivyoko katika Hifadhi ya Bahari ya Mnazi Bay-Ruvuma Estuary Marine Park (MBREMP), wilaya ya Mtwara, kusini mwa Tanzania.

Lengo lilikuwa ni kuchunguza jinsi michakato iliyohusika katika utekelezaji wa shughuli hizi mpya za kujitafutia riziki zilivyochangia kuleta faida na kupunguza utegemezi wa jamii kwenye bahari na kuboresha uhifadhi.

Alipendekeza uteuzi sahihi na ushirikishwaji wa walengwa, ikiwa ni pamoja na kutathmini motisha na nia zao. Alitoa wito wa kubuni mbinu za kujikimu ambazo zinaweza kufikia malengo ya kutoa njia mbadala kwa ajili ya shughuli kuu za kiuchumi za walengwa, kuongeza ustawi na kuboresha uhifadhi wa viumbe hai.

Pendekezo lake lilitokana na nadharia iliyoonyesha mafanikio katika baadhi ya nchi na kushindwa katika nchi nyingine. Afua zilizofanikiwa kwa kawaida zilihusisha serikali kusaidia kwa njia ya kutoa mtaji au vifaa.

Suala la urejeshaji na ulinzi wa ardhioevu ni mojawapo ya vipaumbele vya Uganda. Rais Yoweri Museveni ameendelea kutoa wito wa kufukuzwa kwa wavamizi wa ardhioevu akisisitiza umuhimu wake katika usimamizi wa mfumo mzima wa ikolojia tunamoishi, hata kupendekeza fidia kwa wenye viwanda katika maeneo oevu.

Hivi karibuni, Mamlaka ya Kitaifa ya usimamizi wa Mazingira (NEMA) imewakamata na kuwafunga wavamizi.

Hata hivyo, wanamazingira wanakosoa kuendelea kutokujali, hasa miongoni mwa wamiliki wa viwanda wa China na wasomi wa ndani ambao wanaendelea kuharibu ardhi oevu hata kama NEMA inawakamata wenyeji. 

Vinginevyo, viongozi wa vyama vya ushirika wana matumaini hadi sasa kuhusu mafanikio ya ushirikiano na wizara ya maji.

“Tuko katika hatua ya awali lakini uwezo wetu wa kukua na kuwa hai ni zaidi ya 80%” Zaribugire alisema kwa kujigamba.

Taarifa hii imefnywa kwa ushirikiano na InfoNile na kwa ufadhili wa JRS Biodiversity Foundation na Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Maji wa IHE-Delft. Ni juhudi za ushirikiano kati ya mwanahabari na mwanasayansi, haswa Christopher Bendana na Daniel Abowe.

Daniel Abowe ni Afisa Mradi katika Baraza la Kitaifa la Sayansi na Teknolojia, Uganda.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts