Jinsi familia moja huko Mbale iliokoa jirani wake kwa kutumia maji ya chini ya ardhi

Jinsi familia moja huko Mbale iliokoa jirani wake kwa kutumia maji ya chini ya ardhi

Na Henry Lutaaya

Katika kijiji kidogo cha Namakye katika Parokia ya Buluambu Kaunti Ndogo ya Busiu wilayani Mbale, wanakijiji wamekuwa wakifurahia maji mengi masafi ya kunywa kwa miaka 7 iliyopita bila kulazimika kulipa hata senti moja.

Ni shukrani kwa mchango wa ukarimu wa wana wao wawili ambao walitaka kukomesha kumbukumbu zao wenyewe za kubeba maji kichwani kwa umbali mrefu.

Bw. Nathan Wolakawu Wanda na mdogo wake Bw. Michael Wamateke Wanda walilelewa kati ya miaka ya 1960 na 1970 katika familia isiyojiweza. Kama watoto wengi katika maeneo maskini ya vijijini nchini Uganda, mojawapo ya majukumu yao ya msingi nyumbani ilikuwa kuchota maji. Ilikuwa kazi ngumu hasa kwa vijana kwa sababu ya hali ngumu ya kazi, lakini pia kwa sababu ya hatari waliyokumbana nayo wakichota maji kwenye madimbwi yaliyo wazi.

“Tulikulia kijijini. Mbali na kufanya kazi zingine kama vile kulima, kulikuwa na kazi ya kusomba maji. Na kwa kawaida ni vijana wanaosombea maji watu wazima. Wakati fulani, kaka yangu ndiye aliyekuwa akinichotea maji,” anakumbuka Bw. Wolukawu.

water scarcity Uganda
Watoto wakielekea nyumbani baada ya kuchota maji. Picha na Charles Nambasi kutoka Pixabay

Walibahatika kupata elimu na kazi ambazo ziliwapa maarifa mapya ya matumizi ya maji masafi kutoka kwa vyanzo mbadala kama vile maji chini ya ardhi.

Bw. Wolukawu aliendelea na akawa mwanajiolojia na kufanya kazi na iliyokuwa Kiwanda cha Simiti ya Uganda, kabla ya kubinafsishwa na kubadilishwa jina kuwa Tororo Cement. Ndugu yake mdogo Michael alihamia Ubelgiji ambapo anakaa hadi sasa na hutembelea nyumbani mara kwa mara.

Mojawapo wa kusafiri kwake akirudi nyumbani mwanzoni mwa miaka ya 1980, Michael alikasirishwa kwamba maisha hayakuwa yamebadilika kwa miaka mingi tangu wakiwa watoto; wanawake na watoto bado walilazimika kuchota maji kutoka kwenye madimbwi machafu na kubeba  vichwani vyao kwa masafa marefu.

Alishauriana na kakake Bw. Wamateke kuhusu nini wangefanya kujaribu kusahau mazingaumbwe, angalau kwa kijiji chao. Maswali yao yaliwaongoza kwenye mradi uliodhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa cha Denmark (DANIDA). Nathan anakumbuka kwamba mradi huo ulikuja kuchimba visima kwa jamii, kwa masharti ya kwamba jamii angalau ingechanga fedha ili kukidhi gharama ya kisima. Katika hali nyingi, anakumbuka, hii kwa kawaida ilikusudiwa kuhakikisha kwamba jamii wanashiriki katika mradi huo na kutoutazama kama mradi wa wafadhili.

Nathan alijitolea kutafuta pesa hizo mwenyewe, na ombi lake la kisima hicho likafanikiwa.

Kwa bahati nzuri, wakati wa mchakato wa kuchimba visima, wahandisi walipata  hifadhi kubwa ya maji iliyofukiwa chini ya miamba.

“Ninawafahamu watu waliokuwa wakichimba visima na walinijulisha kuwa walikuwa wamepata chemchemi ya maji – mfumo wa miamba ambayo ina uwezo wa kuhifadhi maji – ambayo yalikuwa na rasilimali nyingi za maji kwamba hata tukitaka kuyatumia kwa unyunyizi mdogo, hatuwezi kuyamaliza kwa urahisi.”

Kisima kilichowekwa na wakazi kiliwapa nafuu, angalau kutokana na kunywa maji machafu kutoka kwenye madimbwi. Lakini wengi bado walilazimika kutoka mbali ili wafikie kisima hicho.

Bw Wamateke aliporejea nchini, alisikitishwa na misururu mirefu ya watu kwenye kisima waliotaka kuchota maji. Aliweza kuongea na kaka yake mwenye wazo nzuri zaidi; kuboresha kisima na kuongeza mifereji zaidi ili watu wasilazimike kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Ushauri wa Bw. Wolukawu ulikuwa kununua tanki kubwa la kuhifadhia maji, kuiweka kwenye jukwaa la urefu wa mita 10 juu ya ardhi kuhakikisha nguvu ya kutosha ya kuvuta maji yatiririke na kuongeza mifereji kadhaa ambayo itarahisisha watu wapate maji. Pia walihitaji jenereta ili iwashe pampu ya kusukuma maji.

Walielewana na kuketi chini ili wakadirie gharama. Nathan anakumbuka kuwa ingawa gharama ilizidi shilingi milioni 20, dhamira ilikuwa ni ya kuvunja dosari ya uhaba wa maji, kwa hivyo aliwaongoza wawili hao kupuuza gharama zinazowakabili.

Bw. Wolukawu anakumbuka  moja ya matatizo waliyokutana nayo, ilikuwa kuiinua tanki ya lita 24,000 hadi kwenye jukwaa lake lililoinuliwa juu.

“Ilitubidi kutumia shilingi za Uganda milioni 2.5 ( Dola za Marekani 695) kukodisha kreni kutoka Kampala ili iweze kuja kufanya kazi ya dakika 10 ya kuinua tanki na kuiweka kwenye jukwaa lilojengewa. Lakini tuliazimia kulifanikisha,” Bw Wolukawu akumbuka. Lakini haya yote hayakuwa muhimu kwa sababu walikuwa wamedhamiria kuwawekea wakazi maji.

Kama juhudi zinginezo hii haikukosa shida. Kwa kuwa Bwana Wolukawu alifanya kazi mbali na kijiji, alikabidhi mradi huo kwa baadhi ya vijana kusimamia shughuli zake. Wale waliokabidhiwa kazi hiyo hawakuwa na nia njema sawa kama ya waanzilishi. Walichota mafuta ya jenereta na kuwauzia waendeshaji pikipiki almaarufu boda boda kijijini. Mifereji ya maji ilianza kukauka kwa ukosefu wa mafuta. Waanzilishi walibuni njia ingine. Walibadilisha matumizi kutoka kwa jenereta hadi kutumia miale ya jua.

water tank elevated
Tangi iliyoinuliwa ya kuhifadhi maji na pampu iliyozama inayoendeshwa na miale ya jua.

Ili kukabiliana na changamoto ya kuhakikisha kwamba wataendelea kulipia gharama za kudumisha kituo hicho, waliamua kufungua biashara nyingine. Walitulia kufungua biashara ya kutengeneza maji ya chupa.

“Nilimwambia kaka yangu kwamba ili tuendelee kutoa maji bure kwa jamii; tuanzishe biashara ya kuuza maji ili gharama ya kusukuma maji iweze kulipwa na biashara. Tulikubaliana juu ya hilo. Kwa hivyo akatafuta pesa za kununua mashine za kuweka maji kwa chupa na yenye mfumo wa kusafisha maji,” anakumbuka Bw. Wolukawu.

Kuweko na malighafi muhimu – maji – iliwasaidia sana Wandas kuanza kuzalisha maji ya Aquaria – mojawapo ya chapa ya kwanza ya maji ya madini kwa chupa iliyozalishwa na kutumika katika mji wa Mbale.

Chapa ya maji ya Aquaria kwa chupa labda ingekuwa kubwa zaidi kama si tamaa ya kupita kiasi kwa upande wa waasisi. Baada ya kipindi cha biashara kuimarika, walielekeza faida kwenye kiwanda cha kusaga mahindi ambayo kando na kuondoa wamiliki mawazo kutoka kwa biashara ya maji, iliwavutia wafanyakazi ambao walipata motisha ya  kwenda nyumbani na chakula kutoka kwa kinu kipya.

Masharti ya kufungwa kwa ajili ya COVID-19 hivi majuzi iliongeza matatizo ya kampuni ya maji na kuifufua tena itabaki kuwa tu mada ya mjadala.

Wakati huo huo, waasisi waliamua kwamba wanapotafuta usimamizi mpya kuendesha biashara ya kutengeneza maji kwa chupa, mtu yeyote kijijini aliye na uwezo wa kuinunua na kuweka mabomba nyumbani kwake, wako huru kufanya hivyo.

“Kwa wakazi wenye hawakubahatika, tulipanua mabomba hadi sehemu tatu zaidi zinafikia eneo la mita 350 hivi. Na pia tulikubaliana kuwa mtu anayepeleka maji nyumbani kwake, wanapaswa kuweka mifereji njiani ambapo watu wanaweza kupata maji bila kulazimika kutembea masafa marefu,” anasema Bw. Wolukawu.

Shukrani nyingi ni kwa uhisani wa mradi, karibu wakazi wote wa Namakye – takriban kaya 300 wameweza kupokea maji masafi na kwa wingi ya kunywa bila malipo kwa miaka 7 iliyopita.

Na wakati wa kiangazi, Nathan anasema, watu zaidi kutoka sehemu za mbali huendesha baiskeli na pikipiki kuelekea Namakye kuchota maji hayo masafi. Hawapigwi marufuku.

Namakye residents fetching water
Wakazi wa Namakye wakichota maji kwenye mabomba ya maji yaliyowekwa na kuunganishwa kwenye tanki kuu la kuhifadhia maji.

Jamii ya kijiji cha Namakye wanafuraha sana na Wandas kwa kujitolea mhanga na nia njema usiopingwa.

Bw. Makuma Franco, mwenyekiti wa kijiji asema tangu jumuiya yake walipoanza kupokea maji ya bomba, hajashuhudia visa vyovyote kwa wakazi wakiugua  magonjwa yanayotokana na maji.

“Hapo awali, watu walikuwa wakichota maji kwenye visima vya wazi  karibu na mto wa Manafwa. Lakini tangu kuweko kwa maji ya bomba, watu wana furaha na wenye  afya njema,” anasema Bw. Makuma.

Maji ya bomba, anaongeza, yamewaokoa kutokana na hofu nyingine. Wakati wa mvua kubwa, Mto Manafwa, moja ya vyanzo vya maji kwa jamii yake wakati huo, ingekuja na majeneza na mabaki ya wanadamu ambayo yalikuwa yameng’olewa na maporomoko ya ardhi ambayo mara nyingi huharibu nyanda za juu.

Kutoweka kwa magonjwa yanayotokana na maji, kulingana na Bw. Wolukawu, kwa kiasi kikubwa inatokana na ukweli kwamba maji chini ya ardhi kwa ujumla hayana uchafu yakilinganishwa na vyanzo vya maji vilivyo juu ya ardhi kwa kawaida mabwawa  au mito.

Upanuzi wa maji chini ya ardhi ili yafikie wakazi wengi wa Namakye kwa kutumia mabomba imeonekana kuwa uvumbuzi muhimu wa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini.

Inazingatiwa na wengi kwamba chaguo bora kwa maji ya kunywa nyumbani, vyanzo vilivyoboreshwa vya maji chini ya ardhi kama vile Namakye vina manufaa zaidi kwa jamii hasa wanawake na watoto ambao kitamaduni huchota maji ya matumizi nyumbani, lakini pia huwa hatarini zaidi mara yanapochafuliwa.

Yakiwa hayajachafuliwa na vyoo, maji ya kisima hupunguza mizigo ya magonjwa na hukuza matokeo bora ya elimu kwani watoto hutumia muda mfupi kuyachota maji kabla ya madarasa.

Kwa Bw. Wolukawu, majaribio ya maji chini ya ardhi ya Namakye yanaonyesha kwamba inawezekana kuwa na maji ya bei nafuu yanayosambazwa kwa jamii hata kufanyia kazi kubwa zaidi kama vile biashara, au hata unyunyizi wa ziada. Kwa sasa, Nathan anatafakari kutumia baadhi ya maji kuanzisha mradi wa kilimo cha matikiti maji.

“Uzoefu wetu unaonyesha kwamba inawezekana kuwapa watu maji masafi kwa jumuiya za mitaa kwa njia ya gharama nafuu zaidi, kuliko pengine kuhamisha maji ya bomba kutoka kwa mtandao mkuu wa gridi ya taifa,” Nathan anaongeza.

“Hatungekuwa hata na uhaba wa chakula kama tulivyo hivi sasa ikiwa watu walikuwa na njia ya kuyachota baadhi ya maji haya ya ardhini kunyunyizia mimea yao.”  

Kuwezeshwa kwa usambazaji wa visima imesaidia jamii kupata maji masafi katika maeneo mengi ya Uganda, inathibitisha kwamba kwa hakika juhudi fulani zimefanywa aidha na serikali kuu au za mitaa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kujaribu kutatua changamoto ya maji nyumbani ambayo imeendelea kutatiza jamii nyingi.

Dk. Michael Kizza, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa NBI, anaona kuwa idadi kubwa ya watu katika maeneo ya vijijini ambao hukaa mbali na gridi kuu ya maji, hutegemea maji chini ya ardhi, ikilinganishwa na wale wanaotegemea maji juu ya ardhi.

 “Maji chini ya ardhi ni chanzo muhimu sana cha maji hasa kwa matumizi ya nyumbani katika sehemu nyingi za Uganda, lakini pia kuongezeka kwa shughuli za viwanda na kwa unyunyizi. Kwa kweli, kwa sababu yanasambazwa zaidi kuliko vyanzo vya maji ya juu, unakuta watu wengi wanayategemea, hasa yale ambayo yako mbali na gridi kuu ya maji,” anasema Dk. Kizza.

Dk. Maha Abdelraheem Ismail, Mkuu wa Maendeleo ya Mradi wa Maji Chini ya Ardhi kwa Mpango wa Bonde la Nile (NBI) anakubali. Anasema kwamba dunia imejaliwa kuwa na maji mengi chini ya ardhi kuliko maji juu ya ardhi.

Katika mahojiano yaliyochapishwa katika jarida la kila robo mwaka la NELSAP-CU, Dk. Maha amenukuliwa akisema: “Maji masafi yanapatikana katika hifadhi nne kubwa; anga (hewa na mawingu), lithosphere (katika miamba), hydrosphere (maziwa na mito) na biosphere (katika mimea na wanyama). Maji huzunguka kila wakati katika hifadhi hizi nne kuu. Mbali na nguzo za dunia, maji mengi masafi yanayopatikana ni ya chini ya ardhi(0.61%) huku mito na maziwa yakishikilia  asilimia ndogo tu (0.009%) hivyo kufanya maji ya ardhini kuwa ya pili kwa umuhimu wa maji ya hifadhi kimkakati.”

Utafiti wa hivi karibuni kati ya Jumuiya ya Jiolojia ya Uingereza na Msaada wa Maji pia ilionyesha kuwa nchi nyingi za Afrika zina maji ya kutosha ambayo yanaweza kuwasaidia kuishi angalau miaka mitano ya ukame, wakati mwingine yanaweza kudumu hadi miaka 50.

“Kila nchi ya Afrika kusini mwa Sahara inaweza kutoa lita 130 za maji ya kunywa kwa kila mtu kwa siku kutoka chini ya ardhi bila kutumia zaidi ya 25% ya wastani ya kutiwa nguvu ya muda mrefu, na nyingi chini ya 10%. Hii inamaanisha maji chini ya ardhi yanaweza kuzuia dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa miaka mingi ijayo, hata katika tukio lisilowezekana kwamba hakuna mvua.

Ushahidi unaokua juu ya upatikanaji zaidi wa rasilimali za maji chini ya ardhi katika eneo hilo, inaweza kusaidia kurejesha matumaini hasa kwa nci za bonde la Nile ambazo zilizidi kuchoshwa na ripoti za wataalamu kwamba eneo hilo linakabiliwa na uwezekano wa kukosa maji katika miaka thelathini hadi hamsini ijayo. Hii inatokana kwa kiasi kikubwa na shughuli zisizoratibiwa na zenye ushindani wa matumizi ya maji kwa nchi wanachama zinazotokana na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu na upanuzi wa uchumi wa nchi.

Chambuzi tofauti kutoka kwa baadhi ya wanasayansi ziliwasilishwa hivi karibuni wakati wa kongamano ya Maendeleo ya Bonde la Nile, zilionyesha  picha mbaya ya hali ya maji katika eneo hilo. Hii ililazimisha nchi hizi kuelekeza shirika la Bonde la Nile (NBI) kufanya tathmini ili kubaini kiwango cha  tatizo na waje na suluhisho za kutatua changamoto hizo.

Zoezi la udadisi huo lilipewa jina la Uchambuzi Mkakati wa Rasilimali za Maji, na ripoti ya awali ilichapishwa mnamo 2016. Ilionyesha kuwa kweli nchi zingekabiliwa na changamoto kubwa za uhaba wa maji, kwa kiasi fulani kwa sababu ya kutotekelezwa kwa mipango sambamba na maendeleo ya nchi wanachama wa Bonde la Nile, kuchangiwa zaidi na hali ya hewa na kuongezeka kwa haraka ya idadi ya watu na changamoto za ukuaji wa uchumi.

Ripoti ya awali ya kwanza ya Udadisi wa Mkakati wa Rasilimali za Maji ambapo wataalam walidadisi usambazaji wa maji unaopatikana dhidi ya ongezeko linalotarajiwa kwa mahitaji ya maji kulingana na  mipango ya nchi  kwa maendeleo ya taifa inayosema hivi:

“Kulingana na mipango ya kitaifa, jumla ya ongezeko la maeneo ya unyunyizi inakadiriwa kuwa hekta milioni 3.7 ifikapo mwaka 2050, takriban hekta milioni 8.7 za ardhi zinakadiriwa ziwe kwa unyunyizi. Ikiwa unyunyizi  utategemea maji  juu ya ardhi na ufanisi wa sasa wa unyunyizi maji unabakie vile vilivyo, jinsi mipango mingi iko chini, kuna uwezekano kwa bonde kukabiliwa na upungufu wa maji takriban 40 – 45 BCM kwa mwaka. Upungufu huu unatarajiwa kujotokeza hatua kwa hatua katika kipindi cha miongo 3 hadi 4 na, kwa hivyo, hatua zinahitajika kuchukuliwa ili kukabiliana na uhaba huo kabla haujakuwa  dharura,” inasema ripoti hiyo.

Ripoti ilipendekeza haja ya kuendeleza rasilimali za maji chini ya ardhi kama moja ya pendekezo kuu kwa ajili ya kukabiliana na makadirio ya uhaba wa maji katika miongo ijayo.

Licha ya njia mbadala ya kuahidi kukabiliana na mishtuko inayotokana na kupugnua kwa maji katika maziwa na mito, wataalam kwa jumla wanakubaliana kwamba ni machache sana ambayo yanajulikana kuhusu tukio hilo halikadhalika madhara ambayo huja kwa utegemezi mkubwa wa maji chini ya ardhi.

Kujaza pengo hili la ujuzi kwa suala la ramani ya vyanzo vya maji ya ardhi na kufanya uwekezaji muhimu pamoja na kuweka sera na miongozo ya matumizi endelevu katika nchi mbalimbali bado ni jukumu la kimsingi kwa serikali za kitaifa husika.

Changamoto kuu ni ule uliyoshirikiwa au chemchemi ya kuvuka mipaka. Sio tu kwamba nchi na jumuiya zinapaswa kuzingatia usawa wa upatikanaji wa rasilimali, pia wanapaswa kuhakikisha kwamba yanatumika kwa uendelevu na sio kuyapunguza au kuyachafua yasababishe madhara kwa jamii walio  upande wa pili wa mpaka.

Kwa mfano, ikiwa chemchemi inayosambaza maji kwa mradi wa Namakye imeunganishwa na chemchemi ya Mlima Elgon, matumizi zaidi ya rasilimali za maji nchini Kenya itaathiri upatikanaji wa maji kwa maskini wakaazi wa Namakye.

Kwa bahati nzuri, labda, kwa sababu ya mamlaka yake ya kukuza ushirikiano kati ya nchi 10 wanachama kupitia uundaji wa maarifa,  kutekeleza mazungumzo na kusaidia miradi ya pamoja ya uwekezaji, NBI imeanza kujivutia zaidi sio tu kutoa maarifa kuhusu vyanzo vya maji vilivyoshirikiwa, lakini pia katika kujaribu kuunga mkono mazungumzo kwa nchi wanachama husika kuweka miongozo ya namna ya kutumia  rasilimali kwa njia endelevu zaidi. 

Shirika la kikanda kinatekeleza mradi wa miaka mitano wa dola za Marekani milioni 5.3 inayolenga kutoa habari zaidi juu ya vyanzo vitatu vilivyoshirikiwa; chemchemi ya Mlima Elgon inayoshirikiwa na Uganda na Kenya, chemchemi ya Kagera inayoshirikiwa kati ya Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania na  chemchemi ya Gedaref-Adigrat inayoshirikiwa kati ya Uhabeshi na Sudan.

Kama Dk. Michael Kizza, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa NBI aonelea, vyanzo vya maji vilivyoshirikiwa vinakabiliwa na shinikizo zaidi kwa sababu ya ukosefu wa mifumo ya usimamizi kwa pande zote za mipaka.

“Unapata shughuli mbalimbali zinafanyika bila uratibu. Kwa hivyo, kando na kukusanya habari juu ya vyanzo hivi vyote vya maji, pia tunaweka mipango ya kazi na kuanzisha miradi ya majaribio jinsi tunavyoweza kukabiliana na baadhi ya changamoto kama vile upungufu wa maji, uchafuzi wa mazingira na ukataji miti katika baadhi ya maeneo ya vyanzo vya maji ambayo husababisha upungufu kwa upatikanaji wa maji kwenye chemchemi za maji,” anasema Dk Kizza.

Mfumo wa ikolojia dhaifu wa Mlima Elgon huathiri vyanzo vyake vya maji.

Mlima Elgon ni sifa ya kipekee ya kijiografia ambayo ni muhimu kwa nchi za Uganda na Kenya – nchi mbili ambazo zinashirikiana kwa uzuri zao na kwa maji mengi, rasilimali za mimea na wanyama. Pia ni ya umuhimu mkubwa kwa Bonde la Nile kwa sababu ndilo chanzo kubwa cha maji kinachoshuka chini kupitia mito mingi na husaidia  maisha vilevile kwa pamoja na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Kaldera kubwa- au ziwa linaloundwa  kutokana na volkano iliyozimika- na msitu unaozingira eneo zaidi ya kilomita 2000 mraba juu ya mlima, ndio chanzo cha mito  kama vile mto Sipi, ambayo inatiririka kwa kiwango kikubwa kuelekea chini.

Kwa kubarikiwa  na zaidi ya mito 12 na vijito vya msimu kadhaa, wilaya ya Bududa Mashariki mwa Uganda inaonyesha umuhimu wa kanda kama moja yenye kulainika zaidi  lakini pia minara ya maji tete kwa bonde la Nile.

Zaidi ya maji mengi juu ya ardhi ambayo yanapitia kati ya mito kutoka mlimani, kuna ushahidi wa kisayansi kuonyesha kwamba mamia ya maelfu ya watu wanaoishi katika wilaya na mikoa inayozunguka Mlima Elgon pande zote mbili za mpaka wa Kenya na Uganda, wamebarikiwa zaidi na rasilimali nyingine – maji chini ya ardhi.

Uchunguzi wa kijiolojia umethibitisha kwamba Uganda inashirikiana kwa chemchemi ya maji karibu na Mlima Elgon pamoja na Kenya.

Makala rasimu ya utafiti moja wa kisayansi ulioagizwa na NBI unaonyesha kuwa chemchemi ya Mlima Elgon, kiasi kikubwa cha maji na kueneza kwa  umbali unaofikia kilomita 37,486 katika nchi hizo mbili.

Nchini Uganda, inaaminika chemchemi ya Mlima Elgon hujumuisha angalau wilaya 9 nazo ni Kapchorwa, Kween, Amudat, Bududa, Bukwo, Bulambuli, Nakapiripirit, Namisindwa na Sironko. Uwezekano kwamba wilaya jirani au hata Mbale ambayo iko chini ya mlima  huo unaodhihirika waziwazi, ziko juu sana. Kwa upande wa Kenya, chemchemi hiyo inaenea katika kaunti nne, ya Pokot Magharibi, Busia, Trans-Nzoia na Bungoma.

Chemichemi ya Mlima Elgon, wataalam wanasema hustawi kwa usawa wa mara kwa mara na kulingana na maji kutiliwa nguvu na isipotiliwa nguvu, kwa hivyo ni dhana ya matumizi ya pamoja.

Vile Dk. Maha Ismail anaelezea, maji chini ya ardhi yanatiliwa nguvu wakati maji juu ya ardhi yanachuja kupitia tabaka za juu za udongo kupitia miamba na mashapo yaliyo chini ya mito mpaka yafikie mifumo ya miamba ambayo ina uwezo wa kuyahifadhi kwa muda fulani. Kwa upande mwingine, baadhi ya maji hutolewa kupitia visima, vilevile kupitia vijito na vidimbwi. 

Kuenea kwa mito mingi, ikisaidiwa na mvua kubwa na mfumo wa miamba unaoweza kupenyeza maji, inaaminika kuwa na jukumu muhimu kwa afya ya chemchemi ya Mlima Elgon.

Shughuli za kibinadamu kama vile makazi na kilimo katika mfumo wa ikolojia dhaifu wa Bududa, pamoja na ukataji miti, ni baadhi ya vitisho vinavyoweza kukwamisha mchakato wa kutilia nguvu tena sio tu kwa chemchemi kubwa lakini pia kwa chemchemi ndogo karibu kwa sababu ya athari mbaya ambazo zinaweza kuwa nazo kwenye mvua.

Kwa bahati nzuri, viongozi wa jamii ya Bududa, kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali, yamekuwa yakihamasisha wakulima kuhifadhi mazingira kama njia ya kupunguza athari na kasi ya maporomoko ya ardhi.

Katika Kaunti Ndogo ya Bukalasi, ambayo iko kwenye mipaka ya mbuga ya taifa ya Mlima Elgon, viongozi wa jamii mara kwa mara hushirikisha wakaazi kuchimba mitaro na kudumisha makorongo ambayo husaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo.

Sam Wakibi, Afisa wa Maendeleo ya Jamii ya Kaunti Ndogo ya Bukalasi, katika wilaya ya Bududa alieleza hayo kwa msaada kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile Africa 2000 Network, wamefundisha wakaazi namna ya kukuza vitalu vya miti kwa kuzingatia aina ya asilia.

“Tunawahimiza watu kupanda miti ya kiasili kwa sababu haibadilishwi haraka kuwa mbao kama mikaratusi ambayo ni ya kawaida katika ukanda huu,” anasema Wakibi.

Wanapofanya kazi ya kuzuia maporomoko ya ardhi, inaaminika kuwa maji huzama kwenye tabaka za vina vya miamba ambayo huongeza nguvu zaidi ya mchakato.

Kwa wakaazi wa Bukalasi, uhusiano kati ya wanaofanya kazi juu ya mto na jinsi  wanavyoathiri jamaa zao wa karibu wa Namakye, haijathaminiwa sana. Mtu anatumaini, hiyo inawezakana ikiwa maarifa haya yangepatikana kwa urahisi zaidi, basi kutegemeana kungehimizwa sana.

Hadithi hii ilichapishwa mwezi wa Juni 2022, kwa usaidizi wa InfoNile na media in Cooperation and Transition (MiCT) kwa ushirikiano na Nile Basin Initiative (NBI) na usaidizi wa Deutche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH, ikaidhinishwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts