Maji Chini ya Ardhi yanabadili vijiji vya Kenya, lakini ukataji miti unatishia kugeuza hili

Maji Chini ya Ardhi yanabadili vijiji vya Kenya, lakini ukataji miti unatishia kugeuza hili

Na Tony Wafula

Upatikanaji bora wa maji kwa vyanzo vya maji vya chini ya ardhi nchini Kenya eneo la Mlima Elgon inahuisha vijiji kutokana na changamoto kubwa la ukataji miti.

Harrison Naibei, mkulima kutoka Kaunti Ndogo ya Kopsiro, aliyechimba maji chini ya ardhi kwake nyumbani kutokana na upungufu wa maji juu ya ardhi, asema chanzo cha maji sasa kinahudumia jamii nzima na shule.

Naibei ansema katika siku za hivi karibuni; mkoa huo umekabiliwa na uhaba wa maji unaohusishwa na kukata miti mara kwa mara kutoka Msitu wa Mlima Elgon na kijijini.

Harisson Naibei 2 1
Harrison Naibei katika shamba lake la vitunguu katika kijiji cha Chemwenda huko Kopsiro, Mlima Elgon

“Mlima Elgon unajulikana kwa kuwa na minara ya maji lakini, kwa bahati mbaya, sisi ndio tunalalamikia uhaba wa maji,” Naibei asema.

Naibei alifichua kuwa alichimba kisima chake cha maji mnamo 2021 baada ya mkoa wake kukumbwa na ukame iliyoathiri shamba lake la vitunguu na kupelekea upotevu wa fedha kati ya shilingi 30,000 (Dola za Marekani 245)- 40,000 (Dola za Marekani 327). Kando na vitunguu, Naibei hukuza mahindi, viazi vya kizungu, dania, na nyanya kwenye ekari zake tatu.

 “Shamba langu liko karibu na chemchemi ya maji, lakini kuna uhaba wa maji wakati wa kiangazi. Hii ndiyo sababu niliamua kuchimba maji ya chini ya ardhi, Ilinibidi kutambua njia mbadala ya kupata maji ya kumwagilia mazao yangu” alisema.

Naibei baadaye alijihusisha na kampuni ya maji ambayo iliwezesha kusukuma maji kuhudumia jamii nzima ikijumuisha shule iliyo karibu- shule ya msingi ya Kamachei. Hii imewaokoa wanafunzi kutoka kwa kutembea umbali mrefu  kuchota maji, ambayo asema huwaelekeza wasichana wadogo kwa mimba za utotoni.

Naibei asema ukame unaooneka kuja, ako na wasiwasi kuhusu mgogoro wa uhaba wa maji.

Anaitaka serikali na mashirika mengine yanayohusiana na mazingira kufanya kazi pamoja na jamii ya Mlima Elgon kwa kupanda miti zaidi katika msitu na ndani ya jamii kuonya kuwa iwapo hali itaendelea, minara ya maji katika mkoa  iko kwa hatari ya kukauka na hii itaathiri mtiririko wa mito. Ardhi oevu na misitu hutega maji yanayotiririka, kuiwezesha kuzama katika tabaka za udongo ili kuunda maji ya chini ya ardhi. Uharibifu wa ardhi oev na athari za kukata miti huathiri vibaya maji ya chini ya ardhi.

Mt. Elgon deforested 2 1
Muonekano wa angani wa eneo la Mlima Elgon, ambao umekatwa miti kwa kiasi kikubwa

George Wara, ni MhifadhI wa Mazingira wa  Wahifadhi Msitu nchini Kenya (KFS) Kaunti ya Bungoma, alalamika kasi ya ukataji miti eneo la Mlima Elgon na alisema kwamba Walinda Msitu nchini Kenya (KFS) wanafanya kazi na wadau wengine kwa kuhakikisha msitu umerejeshwa.

“Tuko na mipango ya kurejesha Msitu wa Mlima Elgon, hatuwataki wakazi waendele kukata miti kwa sababu tayari tunahisi athari zake” Wara alibainisha. Maji ya chini ya ardhi ndiyo chanzo muhimu zaidi ya maji ya kunywa kwa watu, pamoja na mifugo na umwagiliaji wa wanyamapori katika nchi 11 yalioko Nile Basin. Kulingana na Nile Basin Initiative (NBI), ushirikiano baina ya serikali za nchi 10 za  Nile Basin, zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wa vijijini kwa mkoa huu hutegemea maji ya chini ya ardhini.

Vincent Mahiva, Mamlaka ya Kitaifa kwa Usimamizi ya Mazingira (NEMA), Kaunti ya Bungoma alisema ya kwamba Mlima Elgon ni ikolojia muhimu katika mkoa kwa vile hutoa vyanzo vya maji kwa ajili ya mito ya Kenya na Uganda. Alielezea ya kwamba kando na kusaidia kupunguza uvukizi wa mimea, miti inaunda zulia laini linaloruhusu maji kuloweka mvua inaponyesha.

Moses Wambusi, Afisa wa Afya ya Umma Kaunti ya Bungoma, alilamika ya kwamba ni vigumu kwa wakazi wa Mlima Elgon kuchimba vyoo virefu kwa sababu ya mwamba mgumu katika eneo hilo, na husababisha hali mbaya ya afya na usafi wa mazingira.

Kwa kuwasaidia jamii ya Mlima Elgon kwa juhudi zao ya matumizi na usimamizi endelevu wa vyanzo vya maji Mlima Elgon, NBI kwa sasa inatekeleza mradi wa kuimarisha msingi wa ubunifu, uwezo, na taratibu za taasisi kimipaka. Mradi huu pia unalenga vyanzo viwili vya maji: Chanzo cha maji cha Kagera basin, kinachotumika kwa pamoja na Burundi, Rwanda, Tanzania, na Uganda, na Chanzo cha Gedaref-Adigrat, kinachotumika kwa pamoja kati ya Uhabeshi na Sudan. 

Mradi wa miaka mitano (2020-2025) kwa Dola za Marekani milioni 5.3 umedhaminiwa na Global Environment Facility (GEF) kupitia Program ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP).

Nakala hii ilisaidiwa na InfoNile kwa udhamini kutoka kwa Nile Basin Initiative.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts