Na Jesse Chenge
Mlima Elgon ni mojawapo ya milima ya minara kuu ya maji nchini Kenya. Uko kaskazini mwa Ziwa Victoria katika Bonde la Nile na unafikia mwinuko wa mita 4,321 juu ya usawa wa bahari. Mlima huu huunda eneo la juu la vyanzo vya maji kwa mito miwili mikubwa: Nzoia na Turkwel na hutoa maji kwa Mto Malakisi.
Hata hivyo kuongezeka kwa ukataji miti, maeneo yanayozingira Mlima Elgon yamekuwa yakikabiliwa na ongezeko la joto na kupungua kwa mvua, na kusababisha tishio kubwa kwa upatikanaji wa maji ya chini ya ardhi na, kwa upande wake, kwa shughuli za kijamii na kiuchumi katika eneo la Magharibi mwa Kenya.
Jamii, hasa wakulima ambao huteka maji ya ardhini kumwagilia mimea yao, wanaogopa pigo kali la kupoteza riziki yao huku visima vikikauka.
Harrison Naibei ni mkulima katika kijiji cha Chemwenda huko Kopsiro, Mlima Elgon. Anasema alipata hasara kubwa wakati mradi wake wa kitunguu ekari 2 ilishindikana kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa mifumo ya mvua, ilimlazimisha kuwekeza katika mradi wa kisima cha maji kilichomgharimu takriban KSh 25,000 (Dola za Marekani 204). Yeye hutumia mfumo wa jua kusukuma maji kwa mimea.
“Baada ya kuwa na changamoto la kiangazi mwaka jana, niliamua kuchimba kisima chenye kina cha futi 32,” alisema Naibei.
Naibei aliongeza kuwa maji ya chini ya ardhi ni chanzo kizuri cha maji kwa umwagiliaji na matumizi ya nyumbani. Anasisitiza kuwa kuwa kiwango cha maji sharti kidumishwe.
Richard Walukano, mtaalam wa maji katika mkoa huo anasema minara ya maji nchini Kenya inakauka sana. Walukano aongoza Shirika la Kenya-Finland (KEFINCO), mradi uliochimba visima zaidi ya 100 kwa wakazi ili wapate maji safi na salama ya kunywa.
Walukano, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la wazee la Bukusu, anaonya kuwa suala la maji lisichukuliwe kirahisi
Jane Towett Naibei kutoka Mlima Elgon anasema jumuiya yao imekuwa ikitumia maji kutoka kwa chemchemi ya asili zaidi ya miaka lakini kiwango cha maji kimepungua kwa kiasi kikubwa, hasa wakati wa kiangazi
“Nilizaliwa hapa katika eneo hili; babu yetu alichota maji kwenye chemchemi hii ya asili ambayo yamekuwa hapa kwa miongo kadhaa, lakini maji yanapungua kila siku,” alisema Naibei.
Fred Ndiwa kutoka Kijiji cha Kopsiro atoa wito kwa serikali ya Kenya kuja na mpango wa kichocheo cha kutoa mafunzo na kuhamasisha jamii zinazoishi katika mkoa wa Mlima Elgon umuhimu wa kupanda miti na kulinda mito na vyanzo vya asili kudumisha viwango vya maji na hivyo kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani na madhumuni mengine.
Alisema baadhi ya mito inakauka, akibainisha kuwa changamoto hiyo ilianza mwaka 2016 wakati wa kukata miti kinyume cha sheria kwa ajili ya makaa na kuni zilikithiri katika eneo la chemichemi ya Mlima Elgon. “Tulikuwa na maji ya kutosha hapa, lakini kwa sababu ya kukata miti, maji katika mito yetu yameanza kupungua huku vijito vya maji vimekauka,” anasema Ndiwa.
Alionya kuhusu hatari ya eneo la vyanzo vya maji Mlima Elgon kuwa jangwa ikiwa msitu haitatunzwa.
Judith Chebet kutoka kijiji cha Korong'otuny, Cheptais anasema kijiji chake kinategemea maji ya kisima ambayo hutumika kwa umwagiliaji wa mimea na kwa matumizi ya nyumbani.
"Sikuizi nafua nguo zangu nyumbani kutumia maji ya kisima changu, ukilinganisha na kitambo nilipohitajika kutembea mda mrefu kuteka maji kutoka kwa Mto Ndakuru," anaeleza Chebet.
Anasema idara yake imerudisha hekta 7000 za ardhi ya misitu, ambayo ilikuwa imevamiwa.
George Wara afisa wa anayesimamia msitu wa Kaunti ya Bungoma, anakubali kwamba Msitu wa Mlima Elgon ni eneo muhimu la chanzo cha maji. Alifichua kuwa idara yake inafanya kazi na wadau wengine kutatua tatizo la ukataji miti na uvamizi.
Kulingana na Mpango wa Bonde la Mto Nile (NBI), mifumo ya maji ya juu ya ardhi, hasa misitu na maeneo oevu, inajukumu muhimu katika kudumisha maji chini ya ardhi ubora na wingi, kutoa chombo cha kuhifadhia maji, na kusaidia mfumo tata wa ikolojia maeneo yenye umuhimu wa kiuchumi na kimazingira.
NBI kwa sasa inatekeleza mradi yenye lengo la kuimarisha msingi wa maarifa, uwezo, na taasisi zinazovuka mpaka taratibu za Mlima Elgon chemichemi inayoshirikisha kati ya Kenya na Uganda na vyanzo vingine viwili vya maji ya Gedaref-Adigrat, chemichemi kati ya Ethiopia na Sudan na chemichemi ya Kagera inayoshirikisha Burundi, Rwanda, Tanzania, na Uganda.
Kwa miaka mitano (2020-2025) mradi wa dola milioni 5.3 unafadhiliwa na Kituo cha Mazingira cha Ulimwenguni (GEF) kupitia Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Hadithi hii ilichapishwa kwa usaidizi wa InfoNile kwa ufadhili kutoka Nile Basin Initiative.