Na Melanie Aanyu
Sehemu ya wasichana na wanawake katika kata ndogo Mashariki ya Bugisu wamebaini kuwa utafutaji wa maji yaliyokuwa yanahatarisha maisha yao kwa wabakaji, wanajisi, na majambazi mara kwa mara sasa imekuwa historia.
Baadhi ya wasichana na wanawake tuliozungumza nao walisema hii ilitokana na kuwepo kwa visima katika jamii.
Kwa kusaidia jamii kama hizo, Kongamano la Bonde la Nile (NBI) kwa sasa inatekeleza mradi ambao unaolenga kuimarisha ufundi wake, uwezo wake wa kustahimili, na taratibu za kitaasisi za kimipaka kwa matumizi endelevu na usimamizi wa chemichemi yaliyoteuliwa kwa Maziwa ya Ikweta ya Nile (yaani Nile Equatorial Lakes- NEL) na mabonde madogo yaliyo Nile Mashariki. Chemichemi ya Mlima Elgon ni miongoni mwa eneo la NEL.
Mradi huu, haswa unapania kujenga na kustawisha rasilimali za maji chini ya ardhi kupitia tathmini ya kina na ramani kwa mifumo ya chemichemi na miongozo ya maendeleo (kiufundi na sera) kwa utafiti endelevu na matumizi ya maji chini ya ardhi halikadhalika matumizi yake na maji juu ya ardhi.
Sikiliza ripoti kamili na Melanie Aanyu kwa kubofya kanda iyo juu/chini.
Nakali hii ilipeperushwa kwanza kwa Kituo cha Time FM nchini Uganda Mashariki. Iliwezeshwa kwa usaidizi wa InfoNile na udhamini wa Nile Basin Initiative.