Uchunguzi unaonyesha viashiria vya awali vya athari mbaya zinazotishia mazingira zitokanazo na mradi mkubwa wa umeme wa maji wa Julius Nyerere nchini Tanzania.
Na Alexandre Brutelle, Christina Oriesching na Osama Al-Sayyad.
“Mradi huu tayari ni janga la kweli la ikolojia,” anasema Darweshi*, mwanamazingira wa eneo hilo ambaye hataki jina lake litajwe. Anaeleza kuwa “Wanyama wamechanganyikiwa kabisa – na hata ni wakali”. Anatamani kutupeleka kwenye eneo la ujenzi unaoendelea wa Julius Nyerere.
Ni rahisi sana kuelewa wasiwasi wa kijana huyo kutotaka kujulikana- kwani waziri wa zamani wa Mazingira nchini Tanzania, mwaka 2018 alionya kwamba: “Mtu yeyote anayepinga mradi huo atafungwa jela”. Gereza sio mahali pazuri kwa mhitimu mpya kuanzia kazi.
Akiwa amesimama kwenye lango la mashariki la Hifadhi ya Nyerere, eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, akitazama Msururu usio wa kawaida kabisa wa magari yanayoingia, ukiwa na malori makubwa ya ujenzi na kufuatiwa na magari madogo machache ya land cruiser zilizosheheni baadhi ya wageni – wenye wasiwasi.
Kwa mtalii wa kawaida asingetarajia kuwa sehemu ya picha kama hiyo, lakini mbuga hiyo imesalia wazi licha ya ujenzi wa moja kati ya mabwawa makubwa zaidi Afrika Mashariki, kupitia katika mto mrefu zaidi nchini Tanzania, Mto Rufiji.
Ili kufika katika hifadhi hiyo – kubwa zaidi nchini Tanzania – sasa inambidi kukatiza katika wingu la vumbi linaloendelea kunyanyuliwa na lori hizi za usafirishaji ambazo kwa kiasi kikubwa zimejazwa saruji na mabomba makubwa.
Milipuko, Wingu la Vumbi na Msongamano usioisha kwenye eneo la “Urithi wa Dunia”.
Mradi huu mkubwa wenye utata wa kufua umeme wa maji ulizua “wasiwasi mkubwa” na Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO, ambayo hatimaye iliitaka serikali ya Tanzania kuachana nayo mwaka 2020, kulingana na Wakala wa Uchunguzi wa Mazingira (Environmental Investigation Agency -EIA). Sababu kuu ilitaja kuwa ni ukosefu wa utafiti wa kutosha juu ya athari za kijamii na za kimazingira zinazohusiana na bwawa hilo.
Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) uliweza hata kuutangaza mradi huo wa bwawa kuwa “hauendani” na hadhi ya hifadhi hiyo ya Urithi wa Dunia wa UNESCO, kulingana na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira, ambapo tathmini iligundua kuwa “haufai kabisa.”
“Takwimu anga iliyopo ya bayoanuai iliyosambazwa inaonyesha kuwa viumbe kumi na mbili vilivyo hatarini kutoweka vinapatikana katika maeneo ya karibu ya hifadhi. Miongoni mwao ni Tembo wa Msituni wa Kiafrika, Twiga Masai na Tai mwenye kofia, kulingana na Christina Orieschnig, mtafiti wa masuala ya maji wa Jukwaa la Uchunguzi wa Mazingira.
Darweshi tayari ameshuhudia matokeo ya awali kabisa na ya haraka ya mradi huu mkubwa wa nishati. Aliwahi kuwa mlinzi pekee kijana wa hifadhi ya Nyerere mnamo mwaka 2021, kama sehemu ya kazi zake za masomo ya uhifadhi. Kulingana na yeye,anasema athari mbaya za ujenzi unaoendelea kwa viumbe hawa tayari zinaweza kuonekana ardhini.
“Malori 50 hadi 60 yanapita kwenye malango haya kila siku. Vumbi na kelele zinazoendelea husababisha usumbufu mkubwa kwa viumbe ambao ni nembo hapa. Anaeleza kuwa “Usisahau tuko kwenye Big 5”. “Big 5” ni msemo unaotumika kuhimiza kukuza safari/ utalii kutazama twiga, nyati, simba, tembo na faru.
Lakini idadi halisi ya viumbe walioathiriwa inaweza kuwa kubwa zaidi pindi eneo lililokadiriwa la kizuizi (takribani 964 km2) litajazwa maji. “Kundi kubwa linalojumuisha viumbe walioainishwa kuwa wako hatarini kuna uwezekano wa kuathirika”, kulingana na utafiti wa Orieschig.
Anahitimisha kuwa “Maeneo makubwa ya makazi ya viumbe walio katika hatari ya kutoweka kama vile tembo na nyumbu yatapotezwa na kuzuiliwa”. Leo aina hii ya viumbe tayari inaonekana kusumbuliwa.
“Ujenzi unaoendelea tayari unasababisha tembo na wanyama wengine kukimbia hifadhi kutokana na kuchanganyikiwa – au hata kushambulia baadhi ya magari. Na hii haiathiri tu eneo la ujenzi, bali hifadhi nzima. Matatizo mengi yamerekodiwa na hifadhi, ikiwa ni pamoja na ajali za barabarani zinazohusisha Swala mara kwa mara”, Anatushirikisha Darweshi.
Hali hii husababisha matukio ya ajabu ambayo wafanyakazi wa ujenzi wenyewe wamechapisha hadharani kwenye Google Reviews.
Hakuna faini iliyotolewa na mamlaka ya Hifadhi kwa makampuni ya ujenzi kuhusu matukio haya ya kujirudia, kijana huyo anaongeza. Hizi ni pamoja na waendelezaji wa ndani ambao ni TANESCO, makampuni mawili ya serikali ya Misri (Arab Contractors na El-Sewedy), pamoja na kampuni ya serikali ya China ya Sinohydro.
Katika mahojiano ya hivi karibuni, mwakilishi wa Arab Constructors alikiri baadhi ya “Matukio ya Kipekee” wakati wa ujenzi unaendelea, lakini akikwepa vipengele vya msingi vyenye madhara (Vipengele hasi) vinavyoweza kutokea kwa muda mrefu.
Anaendelea kusema “Walinzi wanasaidia kikamilifu makampuni haya na kuhakikisha hakuna mtu anayefikia eneo la ujenzi au kuandika kinachoendelea hapa”. Hakika, baada ya muda mrefu tukiwa kwenye barabara zenye matuta kupitia hifadhini zinazotupeleka kwenye eneo la ujenzi, Ghafla, tunasimamishwa na wasimamizi wa Hifadhi na kurudishwa kwenye lango. “Mbali zaidi barabarani, ni jeshi ambalo utalazimika kukabiliana nalo”, wanaonya.
Licha ya hatua hizi za ufuatiliaji mkali, kampuni inayoungwa mkono na Misri ya Arab Constructors haioni haya linapokuja suala la picha zinazozungumza(Communicating images) kutoka ardhini na wakati mwingine hufanya hivyo kwa mtindo wa Ki- Hollywood, kama inavyoonekana katika picha zifuatazo za ndege zisizo na rubani (Drone) zinazoonyesha milipuko mbalimbali iliyotokea ndani ya eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO:
Picha za Wajenzi wa Kiarabu wanaomilikiwa na serikali kuhusu Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius, 2020] Kwa hisani ya Wajenzi Waarabu.
Uchambuzi wa picha za satelaiti uliotolewa na Orieschnig pia unaonyesha kuwa Km² 7.4 ya mabadiliko ya eneo la ardhi inaweza kurekodiwa tangu mwaka 2016 kwenye eneo la mimea – ikijumuisha 87% ya upotevu wa misitu na 12% ya ukataji miti wa vichaka.
Hii ni takwimu ndogo tu ya ukataji miti ikilinganishwa na kilomita 1000 iliyotabiriwa na UNESCO na IUCN. Sababu kuu ni kwamba bwawa bado halifanyi kazi, na utabiri huu unatarajiwa kutokea kwa muda mrefu zaidi.
“Kitovu kikuu cha Mikoko” Afrika Mashariki kiko hatarini dhidi ya kiwanda cha Umeme cha Julius Nyerere.
Ingawa upotevu huu wa msitu wa kilomita 1000 ndani ya hifadhi ungekuwa janga peke yake kwa makazi ya wanyamapori wa ndani, lakini bado tishio jingine kwa bayoanuwai liko umbali wa kilomita mia na hamsini kutoka kwenye mradi wenyewe, pwani ya Tanzania.
Ni hapo, katika sehemu ya chini ya mto, ambayo Delta ya Rufiji inahudumu takriban hekta 55,000 (ekari 135,900) za msitu wa mikoko, aina ya misitu ya kandokando mwa ziwa/bahari iliyo chini ya tropiki ambayo imethibitisha kuwa sababu kuu ya unyakuzi wa hewa ya ukaa (CO2) duniani kote, NASA iliiunda kama “mizizi ya kaboni” halisi. Delta yenyewe ni sehemu ya eneo kubwa la Rufiji-Mafia-Kilwa RAMSAR, Eneo la ardhi oevu yenye umuhimu kimataifa.
Huku ukataji miti ukiwa umesababisha kupotea kwa asilimia 30-50% ya misitu ya mikoko duniani, katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, hii inatafsiri kuwa wastani wa tani milioni 317 za hewa chafu ya ukaa (CO2) huzalishwa kwa mwaka, mapambano ya uhifadhi wa mikoko yanaaminika kuwa muhimu katika mapambano hayo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Katika Delta ya Rufiji, machifu wengi wa vijiji, wakulima na wavuvi wanafahamu vyema umuhimu wa kuhifadhi misitu hii ya mvua ya kitropiki – ingawa shinikizo la kilimo bado linazuia juhudi za hivi karibuni za uhifadhi, hasa kupitia kilimo cha mpunga.
Lakini juhudi za serikali ya Tanzania katika utoaji wa elimu tangu mwishoni mwa miaka ya 90 zinaanza taratibu kuleta alama kwa wakazi wa eneo hilo, ambao wanaonekana kutofahamu maendeleo ya bwawa la Julius Nyerere na athari zake kwenye mikoko.
Mtunda, Kikale, Nyambati, Mchungu – katika vijiji hivi vilivyotengwa vya Delta ya Rufiji hakuweza kupatikana mtu hata mmoja ambaye anafahamu mradi huu unaoendelea ambao unaweza kusababisha ukataji miti kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko walivyozoea.
Katika kurekebisha viwango vya maji ya mto na kurejesha mtiririko wake wa asili, bwawa la Julius Nyerere linaweza kuzuia misitu hii ya mikoko, iliyotajwa kuwa mikubwa zaidi Afrika Mashariki. Lakini kulingana na Oriesching anasema, ni vigumu kuanzisha makadirio yoyote juu ya suala hilo, kwasababu ya kukosekana kwa takwimu muhimu ili kujenga mifano madhubuti kuhusu uharibifu huo.
Ingawa hawakutoa taarifa hii, Wajenzi wa Kiarabu walikiri kwamba matukio mawili ya mtiririko wa maji tayari yametokea wakati wa maendeleo ya mradi, na kuharibu sehemu ya eneo la ujenzi na maeneo jirani lakini bila kuleta athari yoyote mbaya kwenye mazingira”.
Je, athari hii inayokuja kwenye mikoko inaweza kuwa kali, wastani – au ndogo tu? Ukosefu wa taarifa zinazopatikana hadharani juu ya suala hili hufanya kuwa vigumu kujibu maswali haya. Hii ndiyo sababu kuu kwa nini UNESCO, IUCN na EIA ziliibua wasiwasi mkubwa, zikitoa maoni juu ya tathmini ya kimkakati ya mazingira ambayo haikukamilika kutoka kwenye muunganiko wa makampuni yanayohusika katika utekelezaji mradi huo.
Je, hii ndiyo gharama ya kulipa kwa uhuru wa Tanzaia wenye nguvu? Kinyume na matamshi yanayotumiwa na mamlaka za Tanzania kuhalalisha mradi, kunaweza kusiwe na manufaa yoyote ya wazi ya kijamii na kiuchumi kwake. Kwa hakika, gharama zake halisi zinaweza kufikia dola za Marekani milioni 9.852, takriban mara 2.7 zaidi kuliko ilivyokadiriwa hapo awali, kulingana na mtafiti huru Joerg Hartmann.
Kampuni ya umeme ya El-Sewedy electrics haukujibu maombi yetu ya kupata maoni kutoka kwao. Wala mmiliki wake, serikali ya Misri, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa COP27 hivi majuzi tu. Wenzao wa China pia walikataa kutoa maoni yao, licha ya China kuwa imeongoza kile kinachoitwa makubaliano ya “kihistoria” ya COP15 juu ya bioanuwai, ambayo iliahidi kulinda 30% ya uso wa dunia ifikapo 2030.
Zilipoulizwa iwapo nchi hizo mbili pia zitajitolea kujitenga na miradi ya kutisha iliyopo ndani ya maeneo ambayo yanalindwa kwa sasa, kama vile eneo la Urithi wa Dunia la Nyerere, wizara za mazingira za China na Misri zilishindwa kujibu wala kutoa maoni.
Kulingana na vyanzo vya habari vya ndani, sehemu kuu ya mtambo huo ilikamilishwa mwishoni mwa Oktoba 2022. Lakini bado, hakuna muundo wa mtiririko ambao umefichuliwa hadharani kuhusu shughuli za baadaye za umeme wa maji wa bwawa.
Tangu wakati huo UNESCO imeainisha hifadhi ya Nyerere kama “Sehemu ya Urithi wa Dunia Hatarini” kutokana na mamlaka ya Tanzania kuendelea na bwawa hilo, wakati IUCN imesema kuwa athari za chini ya mto zinaweza kuathiri vibaya maisha ya zaidi ya watu 200,000.