- Taita Taveta lina viungo vingi vya maji lakini hayana maji.
- Kilimo kinatetereka licha ya uwepo wa vyanzo vya maji
- Tatizo ni uhaba wa uchumi, sio uhaba wa maji.
- Viwango vya maji vimeshuka kutokana na hali ya hewa.
- Mabwawa kadhaa katika kaunti hiyo yamekauka, huku mengine yakiwa yamepunguza uwezo.
Na Lina Mwamachi
Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME) namba 6 inalenga ulimwengu kufikia upatikanaji wa maji na mahitaji ya usafi wa mazingira kufikia mwaka wa 2030. MME namba 13, Hatua ya Hali ya Hewa, inalingana na lengo la maji. Zote mbili zinalenga kutekelezwa ifikapo mwaka wa 2030. Swali ni je, yatafikiwa?
Kusini-mashariki mwa Kenya, mabadiliko ya tambia nchi inadhuru hali ya maji kwa kaunti yenye inajitahidi kujikimu na maji masafi licha ya kuwa na viungo vingi vya maji.
Kaunti ya Taita Taveta nambari 006, ipo kwenye sehemu ya pwani ya Kenya. Inajivunia rasilimali nyingi kama mabwawa, maziwa, mito, na vijito. Imewekwa kati ya mbuga mbili muhimu za hifadhi za taifa, Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi, ambayo ambayo inakuza uchumi wa kaunti na Kenya kwa ujumla kupitia mapato ya sekta za utalii.
Ziwa Jipe, Ziwa Chala, vijito vya Njoro, vijito vya Mzima, Mto Lumi, na viungo vingine vya maji huipatia kaunti maji mengi, ingawa viwango vya maji vimepungua ‘kidogo’ kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Maeneo haya ya maji, yakitumiwa na kusimamiwa vyema, yanaweza kufanya kaunti hii ikichangia sana kutoka kwa kilimo.
Inashangaza kwamba licha ya rasilimali kuwa nyingi, kaunti hii ina uhaba mkubwa wa maji. Wakulima katika kaunti hiyo wanatatizika kupata maji baada ya bwawa ambalo lilikuwa na msaada kwa kuwasaidia watu 15,000 lilikauka kabisa.

Zaidi ya kilomita 100 kutoka Voi mjini, Kaunti ya Taita Taveta, ninapanda milima ya Taita kuchunguza hali ya maji. Hoja yangu ya kwanza ni Mzazala Werugha, ambapo nakutana na wakulima ambao wamevamia na kulima ndani ya mkondo wa maji wenye yanamwagia maji bwawa la Kishenyi.
Maji ya bwawa la Kishenyi yalikuwa yakihudumia wakazi 15,000 wa sehemu ya chini ya kaunti. Bwawa hilo, ambalo lilijengwa mnamo 1959, limekuwa msaada kwa wakazi katika suala la kilimo kikubwa,mifugo, uvuvi na matumizi ya nyumbani.
Kulingana na Solomon Kilambo, katibu wa Jumuiya ya Watumia Rasilimali za Maji Kishenyi, vijiji vinne vinavyotegemea bwawa kubwa la ekari 30.6 sasa wanatatizika kupata maji huku wakingoja kutolewa tope kwa bwawa hilo, baada ya Chama cha WRUA kupata kibali ya shilingi milioni 11 kama ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Udhamini wa Maji. Pesa hizo pia zinalenga kuharakisha shughuli za upandaji miti, kusaidia kwa kupitisha mabomba ya maji hadi kwa mitaa iliyoadhirika, na kujenga bwawa ili kuhakikisha hakuna maji yanayovuja chini ya ardhi au mmomonyoko wa udongo kando ya bwawa.
Solomon asisitiza ya kwamba shughuli kali za kibinadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa kukauka kwa bwawa la Kishenyi na vyanzo vingine vya maji katika kaunti hiyo.
Kilimo kando ya kingo za mabwawa, kukata chini miti ya kiasili, na uchomaji wa vichaka na mkaa kando ya bwawa kuchangia uharibifu wa ardhi na kukauka kwa bwawa.
Hapo awali, maeneo yanayozunguka bwawa yalikua mianzi ambayo ilisaidia katika kuchuja na kusafisha maji yanayoteremka hadi kwa bwawa, pamoja na kudhibiti udongo usiingie kwenye bwawa. Lakini mara mianzi iliharibiwa, mmomonyoko wa udongo kutoka kwa kilimo kilishamiri. Mvua iliponyesha, udongo ulitiririka ndani ya bwawa, kukaziba kina chake na kushindwa kubeba maji.
Sasa kwa kuwa bwawa ni kavu, baadhi ya wakulima wa Mzazala Werugha wamechimba visima vilivyomo ndani ya bwawa lililokauka ili kupata maji kwa ajili ya kilimo na matumizi ya nyumbani, lakini hawana uwezo wa kubaini usalama wa maji.
Richard Mwangeka, mkulima, asema mabadiliko ya hali ya hewa na na mvua kidogo iliwalazimu kuchimba visima ili kupata maji kwa unyunyuzi na matumizi ya nyumbani.
“Hatuna lingine ila kulima ndani ya bwawa lililokauka. Kulikuwa na miti mingi lakini yote imekatwa ili tuweze kulima hapa,” asema Mwangeka.
Vile vile, katika shamba la Lauren Kambale, hali ni hiyo hiyo. Lauren asema badiliko la hali ya hewa na misimu ya mvua isiyotabirika ilifanya wachukue hatua ambazo polepole zimepunguza rasilimali na uharibifu wa ardhi kwa pamoja.
Mwadime Mwamburi, mkulima wa Kishushe, pia ameachana na kilimo cha kutegemea mvua na kuwekeza maji kwa kutumia vidindwi vya maji, ambayo ni mabwawa ya kina kifupi yaliyo na vifaa na kufunikwa na mifuko nyeusi ya plastiki ili kuzuia maji yasimwagike.
Ukame umemlazimu kuacha ukulima na kujishughulika na mambo mengine mbadala kama ufugaji wa mifugo na kuku.

Chifu Ethel Mwasi wa eneo la Kishushe anawasihi serikali za kaunti na kitaifa kufanya mipango ya kuanzisha vyanzo vingi vya maji ambavyo vinaweza kutumika kwa kilimo, matumizi ya nyumbani na wanyama, wote wa kufugwa na waporini.
Anaiomba serikali kuchimba mabwawa, visima na vidimbwi vya maji na wazingatie mabwawa kando ya mitaro ambayo hutiririsha maji katika Bahari ya Hindi.
Simon Thuo, ni Mshauri katika Muungano kwa Urekebishaji wa Maji Ulimwenguni, Ukanda wa Afrika Mashariki, asema maji yana jukumu muhimu katika mabadiliko ya hali ya hewa na ukame kwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Thuo asema kiwango cha maji kimepungua kutoka mita 60 hadi 300 kwa maneo kama Kaunti ya Nairobi, akihusisha mabadiliko hayo na kuongezeka kwa idadi ya visima inasukumwa na ongezeko la idadi ya watu.
Anaongeza kuwa Kenya inafaa kuiga jinsi Ethiopia ilivyowekeza katika usimamizi wa maji. Mfano huo ni pamoja na kukamata maji yanayotiririka kupitia mabwawa madogo na pia kutumia maji ya chini ya ardhi na kupunguza uharibifu wa ardhi kwa kuongezeka mimea ifunike mchanga.
Gavana wa Taita Taveta, ambaye pia ni mwenyekiti wa Maji, Usimamizi wa Maliasili na Kamati ya Misitu kwa Baraza la Magavana, pamoja na serikali ya kitaifa Katibu Wakudumu Dk. Paul Kiprono, Wizara ya Maji na Usafi wa Mazingira, wameanza kujadili miradi ya maji itakayotekelezwa na serikali ya kitaifa katika kaunti.
Serikali hizo mbili zinalenga kuimarisha ushirikiano wao katika kutekeleza miradi ya maji katika kaunti ya Taita Taveta huku kukiwa na ukame iliyosababishwa na unyogovu wa mvua.
Kwanza, wanapanga kutekeleza miradi ya Njoro Kubwa na Mzima 2 miradi ya maji kama suluhisho la muda mrefu la matatizo ya maji. Miradi hii inalenga kujenga mtambo mkubwa wa maji wa kilomita-50 na mabomba ya kupitisha maji kuanzia Chemchemi ya Mzima na Kitobo Kaunti ya Taita Taveta ili kuwezesha ongezeko la maji kutoka lita milioni 15 hadi 60 kwa siku.
Je, ni uhaba wa maji kweli? Profesa Boubacar Barry, mwanasayansi wa mambo ya maji katika Afrika Mashariki, asema ambapo kuna rasilimali nyingi za maji na ni dhahiri kuna uhaba wa rasilimali, basi sio uhaba wa maji bali uhaba wa kiuchumi.
“Maji yana mwisho; hatuwezi kuiongeza, badala yake tunaweza kufanya matumizi yake endelevu,” Boubacar aongeza.
Upatikanaji wa Maji kwa Kaunti ya Taita Taveta
Kulingana na data ya 2019 kuhusu idadi ya Watu na Makao nchini Kenya kama ilivyokusanywa na InfoNile, takriban asilimia 36 tu ya kaya ya kaunti ya Taita Taveta walikuwa na maji ya mfereji kwa mwaka huo, ilhali takriban asilimia 15 bado walipata maji moja kwa moja kutoka kwa mito na vijito. Takriban asilimia 5 walikuwa wakipata maji kwa visima na asilimia 1 kutoka kwa mabwawa na maziwa.
Nchini Kenya kwa ujumla, takriban asilimia 3 ya kaya ilipata maji kutoka kwa mabwawa au maziwa mnamo 2019, kulingana na sensa. Asilimia hii ilikuwa kubwa zaidi (asilimia 5) katika maeneo ya vijijini.
Sio tu Taita Taveta
Viwango vya maji vinashuka sio tu Taita Taveta lakini pia katika hifadhi zingine kadhaa za maji na mabwawa nchini. Matembezi ya hivi majuzi kule bwabwa laThika-Ndakaini na Sasumua lilioko Kinangop Kusini Kenya, ambayo husambazia maji kaunti ya Nairobi, ilibainika kuwa viwango vya maji vinapungua katika mabwawa haya pia.
Wanasayansi wanahusisha changamoto na hali ya hewa na shughuli nyingi za kibinadamu.
Kulingana na mhandisi Job Kihumba, Mkurungenzi mkurugenzi mtendaj wa bwawa la Thika (Ndakaini), bwawa hilio lina uwezo wa kuhifadhi maji milioni 70 mita za ujazo na kusambaza takribani mita za ujazo 230,000 za maji siku moja kwa Nairobi, ambayo ni asilimia 84 ya maji yanayosambazwa kaunti ya Nairobi. Hata hivyo Thika inaongezewa kutoka mabwawa mengine ya usambazaji ambazo pia ziko katika hali mbaya. Kihumba asema bwawa kwa sasa lina uwezo wa asilimia 56, ambayo ni ya chini kabisa katika suala la uwezo endelevu..
Profesa Boubacar asema kitendawili cha uhaba wa uchumi kinaweza kutatuliwa tu na serikali, kwa kuweka hatua na rasilimali madhubuti ili kuwawezesha wananchi wake wapate maji kwa njia tofauti ili kujiendeleza na rasilimali ya maji iliyopo.
Hadithi hii imeandikwa na Lina Mwamachi kwa usaidizi wa Water Sector na Afrika 21. Imefanyiwa uhariri na kuongezwa taswira ya data na Annika McGinnis, InfoNile.