Jinsi mradi mdogo wa unyunyizi unabadilisha maisha ya watu kwa magatuzi 11 nchini Kenya

Jinsi mradi mdogo wa unyunyizi unabadilisha maisha ya watu kwa magatuzi 11 nchini Kenya

Henry Neondo, Gitonga Njeru na Joseph Abuje

Mipango ya African Development Bank- kuunga mkono mradi wa Unyunyizi Mdogo na Kuongeza Thamani (Yaani Small Irrigation and Value Addition Project – SIVAP) kwa kubadilisha maisha ya wakazi wa magatuzi 11 yaliyoko mashambani nchini Kenya imepata changamoto nyingi sana zikiwemo Covid-19 iliozuka mnamo mwaka wa 2020.

Walakini, mradi uliopangiwa kunufaisha utendaji wa kilimo umefanikiwa kukabiliana na changamoto hizo kwa kunufaisha watu 520,000 kwa kaya 104,000, wanawake na vijana walio wengi, wakiwasaidia wakulima wa vijijini na kutoa ajira kwa vijana wengi.

Imetekelezwa kwa magatuzi ya Bomet, Kajiado, Nyeri, Tharaka Nithi, Meru, Muranga, Nyandarua, Machakos, Kitui, Makueni na Mto Tana, ambapo kwa sasa SIVAP  inajihusisha kwa ujenzi wa miradi tisa ya unyunyizi pamoja na ukarabati wa nyingine tatu. Hii inafanywa kwa njia ya kuchimba ardhi, kuweka chini mabomba ya maji, kufungua mitandao ya usambazaji maji kwa mashamba ya kibinafsi ambapo wakulima wanaishi ndani ya maeneo ya awamu iliyokamilishwa yanaweza kuunganisha vinyunyizio vyao vya maji. Zaidi ya hayo, SIVAP pia inakuza juhudi za uhifadhi wa udongo na maji kupitia ujenzi wa kuvuna maji na miundo ya kuhifadhi.

SIVAP 1
Mradi wa umwagiliaji na SIVAP

Wizara ya Kilimo pia imeongeza sana huduma za kilimo ugani. Wakulima wanapata pesa nzuri kwa ongezeko la thamani. Wakulima kama Godhana Ali Omar asema kwa sasa hawana haraka tena kuuza  mazao yao ya shamba. Godhana ana uwezo wa kuchukua muda wake na kutafuta njia ya kuongeza thamani kwa mazao yake ili ayauze kwa bei ya juu.

“Tangu kuanzishwa kwake mnamo 2013, tumekuwa na huduma bora za kilimo ugani kupitia ziara za mara kwa mara za wafanyakazi wa ugani wa kilimo,” alisema Lydia Kiprop,  mkazi wa Chepalungu, Gatuzi la Bomet.

Matatizo makubwa yanayowakabili wakulima wa Mto Tana na magatuzi 11 ni ukosefu wa pembejeo za kilimo, gharama kubwa ya mafuta kwa kilimo cha mashine na masoko yaliyodorora kwa ukosefu wa uwezo wa wateja kununua.

Kulingana na Profesa Hamad Boga, aliyekua Katibu Mkuu katika Idara ya Jimbo la Maendeleo ya Mazao na Utafiti wa Kilimo, mradi wenye dola za Marekani milioni 28 ulikaribia kuzuiliwa na Covid-19. Ugonjwa huo, alisema, uliathiri sekta ya kilimo kwa kuzuia huduma za ugani na kupunguza ufikiaji wa masoko.

Kwa sasa, ingawa hali ya Covid imeimarika, ukame, mbolea isiyoweza kufikiwa na gharama kubwa ya mafuta bado ni pigo kubwa sana kwa wakulima. Ongezeko la bei na changamoto za ugavi zimeharibiwa zaidi na mzozo wa Urusi na Ukraine.

Walakini, kulingana na Harry Kimtai, aliyekua katibu mkuu katika Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Unyunyizi nchini Kenya, mradi huo sio tu unashughulikia mapungufu yenye yamekuwa kwa sekta ya kilimo, lakini pia hivi vikwazo vingine.

Kwa Gatuzi ya Mto Tana, SIVAP inatekeleza barabara unganishi, mifereji ya maji, masoko na kilimo cha mashine. Hii imesababisha mamia ya vijana kupata ajira.

Mradi huu unatafuta kutoa aina mbadala wa kilimo cha kutegemea mvua na kuongeza uzalishaji wa chakula, hasa katika mazingira ya mabadiliko ya tabianchi.

Kati ya Julai- Septemba 2022 makadirio ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu, zinaonyesha kuwa takriban asilimia 24 ya idadi ya Wakenya wanaoishi katika maeneo kame na nusu kame kama Magatuzi ya Mto Tana, Kajiado, na Tharaka Nithi hawana chakula cha kutosha.

Kwa hivyo, uzalishaji salama wa chakula, kunatakikana kupunguza kutegemea kilimo chakutegea mvua kwa kutumia rasilimali za maji kwa unyunyizi  chini ya usimamizi endelevu wa mazingira

Inaaminika kuongeza thamani itasaidia Kenya kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Madhara ya unyunyizi mdogo na mradi wa kuongeza thamani kwa Mto Tana

Tangu kuanzishwa kwake, mradi huu umewapa serikali za gatuzi changamoto kuendeleza miundombinu ili isaidie kilimo ndogo-ndogo. Kulingana na Kimtai, SIVAP tayari ilitengeneza pedi za maji kumwagilia mazao kwa Mto Tana pamoja na magatuzi mengine 10 yanayopokea huduma.

“Magatuzi kwa sasa yanajenga mabwawa ya maji na visima ya jumuiya kutoka kwa mvua au maji ya chini ya ardhi kwa maeneo ya makazi jamii wanaweza kufikia kwa urahisi,” aliongezea.

Kwa kuongezea, Kimtai alisema, mradi huo umesaidia barabara za unganishi nyingi kwa kuhakikisha mazao ya shamba yanafika masoko. Tangu 2019, kaunti zimejenga zaidi ya kilomita 69 za barabara za mashambani.

Kimtai asema ya kwamba maji ya chini ya ardhi hutolewa kupitia chemichemi iliyochimbwa vizuri. Kisha kisima hujazwa kupitia bomba ili kufikia maji ya chini ya ardhi. Anaongeza kusema kuwa pampu ya maji hutumiwa kuleta maji juu ya ardhi, ambayo hutumika kwa uendelevu  kuruhusu chemichemi ya maji chini ya ardhi kuchaji tena.

Mradi huu pia una sehemu ambapo wakulima hupewa uwezo wa kuhifadhi maji ya mvua, kuwahakikishia riziki ya mwaka mzima ya bidhaa hiyo ya thamani.

SIVAP6 1
Tangi la uashi kuhifadhia maji kaunti ya Nyeri

 “Kama mkulima, kwa sasa nina furaha vile nimehakikishiwa kupatikana kwa mfufulizo wa maji thabiti. Haijakuwa rahisi, haswa hapa Chepalungu tulipo upande huu wa ukavu na mvua sio nyingi kama upande wa Kericho. Sasa tunategemea kidogo kilimo cha kutegemea mvua,” alisema Kiprop. Aliongeza kuwa mradi huo umesaidia wakazi kuongeza uzalishaji wa chakula kwa muda wa miezi michache kuzinduliwa.

Pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa usambazaji wa maji thabiti, jumuiya zingine kwa Gatuzi la Mto Tana wameanza kupanda miti. Upanzi wa miti pia umepata umaarufu huku maafisa wa kaunti walivyohimiza wakulima wapande miti kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Baadhi ya wakulima katika kata ya Bura, kwa mfano, wameanzisha vitalu vya miti. Wakulima wanachanganya upanzi wa miti kama vile Malakote (pia unajulikana kama llwana). Hii hupendwa sana na wakulima kwa wingi wa faida yake kama vile lishe ya wanyama, matunda na thamani yake kidawa,” alisema Kimtai.

Kulingana na Bola Mlae, mkulima wa Bura, mradi wa SIVAP pia umechangia ongezeko la maafisa wa huduma ugani.

“Hivi sasa, tuna maafisa wa ugani wanaofikika kwa urahisi ambao ni wa maana sana wanapohitajika. Hii pia imetusaidia kuongeza uzalishaji wetu wa chakula, uhifadhi na usindikaji wa mazao,” alisema Mlae.

Kwa mfano, Mlae alisema wakulima walinufaika na mafunzo jinsi ya kuhifadhi mazao yao kwa usalama kulingana na aina ya mimea.

Madhara ya Covid-19 kwa kilimo nchini Kenya

Mnamo Machi 2020, serikali ilitangaza janga la Covid-19 kama jambo la dharura. 

Kwa sekta ya kilimo, Covid-19 iliathiri masoko na kuzorotesha usafiri wa umma na huduma za ugani baada ya serikali kutangaza hatua za kukabiliana nayo na kuzuia kusambaa kwake.

 “Wakati wa Covid, familia yangu iliathirika kwa ukosefu wa pesa. Tulipata mavuno mengi lakini hapakuwa na soko la kuuza mazao yetu. Watu walikwepa kwenda sokoni. Hata kama tulithubutu kutembea umbali wa kilomita 12 kutoka kijijini kwetu kufika sokoni, tungekaa huko siku nzima bila kuuza kitu. Ilikuwa ngumu sana,” Grano Nduru wa kijiji cha Gamba alisema.

Kwa kwendeshwa na mafuta na bidhaa zingine za petroli, ambazo karibu zote zinaagizwa kutoka nje, na kushuka kwa thamani ya ubadilishaji wa pesa (Benki Kuu ya Kenya), Wakenya walishuhudia kupanda kwa bei vya vyakula na bidhaa nyinginezo .Kupanda kwa viwango vya mfumuko wa bei vinavyotarajiwa kuwa asilimia 8.3 kufikia Julai 2022 haikusaidia chochote.

Leo, ingawa nchi imeshinda dhidi ya Covid-19, madhara ya muda mrefu wa ugonjwa huo bado yanaonekana, sio tu kwa Gatuzi la Mto Tana lakini kote nchini.

Mapema 2021, Kenya ilitambuliwa rasmi kama nchi katika mdororo wa uchumi, jambao ambalo lilipunguza kasi ya uzalishaji kutokana na gharamu kubwa ya pembejeo za kilimo. Ingawa hofu juu ya athari za mfumuko wa bei umepungua, uzalishaji wa chakula bado unateseka na unazoroteshwa na ukame mbaya zaidi katika Pembe ya Afrika kwa miaka 70, kulingana na Kituo cha Utafiti cha Pamoja cha EU.

Bei za vyakula viko kwenye mkondo wa gharama ya juu kihistoria na vimekuwa mbaya zaidi kwa kurejea polepole kutoka na janga hili, ukame na mfumuko wa bei. Miezi michache majuzi imekuwa ngumu kwa Wakenya katikati ya kupanda kwa gharama ya mafuta ya kilimo cha mashine.

Musina Ngatana, mkulima kutoka kijiji cha Mikameni, alisema kupata usafiri wa kwenda kwa masoko ya mijini leo ni rahisi. Hata hivyo, tatizo ni kwamba hakuna wanunuzi katika masoko, labda kwa kiasi fulani ni kutokana na uchumi duni uliopo na unaosuasua. Wakati wa Covid-19, aliongeza, hakukuwa na magari na wala hakuweza kuruhusiwa kusafiri kwa sababu ya umri wake. Wazee hawakuruhusiwa kutangamana na umma kwani ilisemekana kuambukizwa kwao ni rahisi.

 “Nilipatwa na msongo wa mawazo kuona kabichi yangu inaharibika kwani sikupata wanunuzi wala sikuweza kupata usafiri wa kwenda masokoni. Kwa kawaida, wasafirishaji wangekuja kununua mazao hapa kwenye shamba langu. Sio tangu 2020. Serikali ilikuwa imetufungia ndani na watu hawakuwa tayari kutangamana. Ilibidi nijadiliane na sacco ya kijiji changu ili kupanga upya ratiba ya mikopo nilichukua kuwekeza shambani,” alisema Ngatana.

Hata hivyo, leo “gharama ya usafiri iko juu kwa sababu ya kupanda kwa gharama za petroli na dizeli,” anaongeza.

Gatuzi la Mto Tana

Gatuzi la Mto Tana, limetambuliwa kwa muda mrefu na migogoro, ukosefu wa usalama na vurugu za kisiasa, imekuwa ikirekodi vibaya kwa viashiria vingi vya kijamii na kiuchumi na mara nyingi imerodheshwa miongoni mwa magatuzi maskini zaidi kati ya magatuzi 47 ya Kenya.

Gatuzi hilo pia limekuwa likikabiliwa na ukame. Eneo hilo hupokea mvua yenye wastani chini au karibu milimita 60 kila mwaka

Leo, gatuzi hili ni miongoni mwa 23 ambayo yameathirika zaidi na ukame, kuwaathiri vibaya wafugaji na wakulima ambao walikuwa na matumaini ya kuibuka na nguvu kutoka kwa athari ya Covid-19.

Tana basin 1
Bonde la Mto Tana

Mohamed Hussein, mkazi, alisema gatuzi hilo pia lilikumbwa na uvamizi wa nzige katika msimu wa 2019-2020 ambao waliacha mashamba yakiwa yameharibiwa. Lakini juhudi zake na za majirani zake kuanzisha mashamba ya umwagiliaji maji baada ya uvamizi mkubwa wa nzige bado hazijazaa matunda.

Hussein, ambaye ndiye mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha Abafodho kwa Gatuzi la Mto Tana, alisema nzige hao walikula mazao yao na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

“Ili kuzidisha mambo kuwa mabaya zaidi, serikali haijawahi kuwa na dhamira ya kuwafidia,” alisema.

Baada ya Covid, Prof Boga alisema wakulima wanakabiliwa na changamoto ya kuongezea uzalishaji wa chakula kwa sababu mbolea inayopatikana ni ghali na gharama ya mafuta imepanda kutokana na serikali kuondoa ruzuku kwenye bidhaa.

Khadija Guyo, mkazi, alibainisha kuwa wengi wa wakulima katika eneo hilo wanakabiliwa na matatizo ya kifedha na hawezi kumudu gharama ya pembejeo za kilimo pamoja na kuajiri wakulima wa mikono.

 “Tumepata nafuu kiasi kutokana na athari za Covid-19. Halafu kulikuwa na uchaguzi mkuu na sasa, serikali mpya na sera yake ni kinyume na ruzuku ya mafuta. Mambo si mazuri kwa sasa,” Guyo alisema.

Mradi mdogo wa unyunyizi 

Profesa Boga alisema mradi wa SIVAP una sehemu kuu nne: umwagiliaji ulioimarishwa miundombinu na maendeleo ya rasilimali za maji; kuboresha upatikanaji wa masoko na kuimarisha mfumo na thamani yake; uimarishaji wa taasisi na ukuzaji wa uwezo; na kushirikisha na usimamizi wa mradi.

Wanaofaidika moja kwa moja na wasio wa moja kwa moja ni pamoja na kaya za wakulima 104,000 (54,000 wafaidi  moja kwa moja na zaidi ya 50,000 wasio wa moja kwa moja) kufikisha watu  520,000 – asilimia 58 ya ambao ni wanawake na vijana.

Zaidi ya asimia 60 ya wakulima wa Gatuzi la Mto Tana ni wanawake, wengi ni wenye umri wa miaka 60 lakini mara nyingi wanasaidiwa na vijana kulingana na takwimu kutoka serikali ya gatuzi la Mto Tana. Hata hivyo, jamii ya mfumo dume inawanyima haki ya ardhi na huamua jinsi ya matumizi ya ardhi.

Mto Tana una urefu wa kilomita 1000 hivyo basi ni mto mrefu zaidi nchini Kenya. Mfereji wake wa maji unashughulikia zaidi ya kilomita 100,000 mraba, takribani asilimia 20 ya ardhi ya nchi.

ewaso nyiro 1
Mto Tana uliofurika

Ushirikiano wa Arid Lands Development Focus (ALDEF) na serikali ya Gatuzi la Mto Tana umewezesha wakulima 25 sehemu za Gatuzi la Mto Tana kila mmoja kupokea shilingi 38,400 kuwasaidia kupona kutoka kwa majanga ambayo yaliwaangukia miezi michache iliyopita.

Kulingana na mmoja wa wasimamizi wa mradi kwa Baraza la Unyunyizi wa Taifa, Johnson Muko, serikali ilikuja na mipango ya kuboresha usalama wa chakula nchini na ilitazamia eneo kubwa la chini la Bonde la Tana Delta na magatuzi mengine 10 yenye sifa yanayofanana na maeneo yanayowezekana.

Katibu wa zamani wa baraza la mawaziri wa kilimo, Peter Munya, alisema serikali itazingatia magatuzi maskini na yenye hukabiliwa na ukame mara kwa mara.

Serikali ya Rais William Ruto imeimarisha juhudi hizi zaidi kwa kuhama kutoka kusaidia watumiaji hadi upande wa uzalishaji. Gatuzi la Mto Tana, kwa mfano, lilipewa bajeti ya shilingi milioni 949 (USD $7.9 million) ya kilimo na maendeleo ya miundombinu kwa kipindi cha 2018 hadi 2022. Fedha hizo zimetolewa kwa awamu.

Hadithi hii imewezeshwa kuchapishwa kwa usaidizi wa InfoNile na ufadhili kutoka IHE-Delft Water and Development Partnership Programme.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts