Na Fredrick Mugira
Halmashauri ya Mji wa Kakukuru-Rwenanura unapatikana Wilayani Ntungamo eneo la Kagera nchini Uganda. Zaidi ya miaka sita iliopita, mabwawa 12 na visima 16 vimekauka, hii ni kulingana na aliyekuwa mwenyekiti wa kata ndogo ya Rwikiniro ambaye ni Meya wa Halmashauri ya mji wa Kakukuru-Rwenanura.
Karibu kila bwawa lenye kina fupi eneo hili limechimbwa kwa mkono na huadhirika zaidi katikati ya mwaka wakati wa msimu wa kiangazi. Tofauti miaka kadhaa iliopita, wachimba visima kwa sasa huchukua siku nyingi sana na kutumia nguvu nyingi kuchimba zaidi ardhini kufikia maji. Wakati mwingine hawapati maji. Na mara kwa mara, hata visima vipya hukauka tu miezi michache baada ya kuchimbwa.
“Tulijaribu kuchimba visima vyenye yenye vina vifupi wakati nilikuwa mwenyekiti wa kata ndogo la Rwikiniro, lakini kina cha chemichemi ya maji iko mbali sana,” asema Kahinda Misach.
Katikati ya changamoto hii ya maji, Kahindi anaamini suluhisho ingali chini zaidi ya ardhi; maji ya chini ya ardhi.
Tumushangye Tom, afisa wa maji wilayani Ntungamo, anakubaliana na Kahinda. Anasema kina cha chemichemi ya maji kiko mbali sana katika eneo hili la wilaya lakini inawezafikiwa baada ya utafiti na kuchibwa chini zaidi. “Hii ndiyo maana tunapendelea visima kwa makata madogo badala ya miradi ya maji ya mtiririko wa mvuto,” asimulia Tumushangye.
Shirika moja iliyoko Entebbe pia inaripoti ongezeko la matumizi ya maji ya chini ya ardhi kwa matumizi mengi ya kiuchumi, yakiwemo kilimo cha unyunyizi, uchimbaji madini, na viwanda.
“Maji chini ya ardhi yanaonesha dalili nzuri ya kupunguza mahitaji na usambazaji wa maji na pia kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi na kutofautiana katika eneo la bonde la mto Nile,” kulingana na ripoti ya NBI.
Wakazi wa bonde la mto Kagera hupata maji yao kwa visima, chemchemi na mifumo iliyoainishwa miongoni mwa njia nyinginezo ambapo maji haya ya chini ya ardhi hutumika kwa madhumuni mbalimbali kuanzia matumizi ya nyumbani hadi kwa mifugo na mimea.
Wilaya ya Ntungamo kusinimagharibi mwa nchi ya Uganda, pamoja na Kabale, Isingiro, na wilaya ya Rakai, yako chini ya chemichemi ya maji ya Kagera. Nchi zingine zinazonufaika na hii chemichemi yenye kilomita mraba 5, 778 ni Tanzania, na Rwanda. Kwa bahati mbaya, wilaya zote za Uganda zenye ziko chini ya chemichemi hii zina ukosefu wa maji, haswa katikati ya mwaka, msimu wa kiangazi.
Tumushangye asema baadhi ya jamii wamepanda miti ya mikaratusi kwenye chemichemi ya maji ambayo hukausha vyanzo vya maji na maeneo ya vyanzo vya maji. Miti mingi ya mikaratusi ina mizizi ambayo imezama ndani ya udongo na hufyoanza maji kutoka kwenye chemchemi.
Halikadhalika, Muchunguzi Sam, mwenyekiti wa wilaya ya Ntungamo, anasema watu wamebadilisha ardhi oevu kuwa ya kilimo na makazi na kuathiri chemichemi ya maji. Ardhi oevu hushikilia maji yanayotiririka, na kuyawezesha kuzama kwa udongo ili yakusanyike kama maji ya ardhini.
Wilaya ya Kabale, Jennifer Twasiima, mkulima kutoka kata ndogo ya Buhara, asema baadhi ya mimea ilifyekwa katika kijiji chake. Hali hii iliacha ardhi tambarare bila ya kizuizi cha mtiririko wa maji, ambayo hupotea kwenye chini ya bonde, maziwa, na vijito. Hivyo basi hali hii hairuhusu chemichemi ya maji ya chini ya ardhi kufurika tena.
Aliwahamasisha jamii ya mitaa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira, akisema jamii nyingi vijijini hawafahamu kuhusu maji chini ya ardhi, akiwaelezea ni kama “rasilimali fiche.”
Soma Pia: Tanzania inataka sheria ziwianishwe ili kulinda mazingira na kulinda maji ya chini ya ardhi
Milton Kwesiga, mwanamazingira wa Kabale na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Disaster Reduction Research Emergency Missions (ADREEM) ambaye pia ni mkazi wa Kabale, asema baadhi ya mabonde ya maji wilayani yameingiliwa na wakulima na ujenzi. Alisema hii ni kutokana na ongezeko kwa idadi ya watu wilayani.
Katika Parokia ya Kamubizi, wilaya ya Isingiro, chanzo cha maji safi na salama kwa jamii ni ya Mto Kagera, ambayo ni maili tisa kutoka kwa makazi ya watu. Kulingana na wanajiji, chaguzi nyingineyo ni bwawa lenye maji chafu ya chumvi isio salama kwa matumizi.
Tweyogyere James, mkazi wa eneo hili na baba wa watoto watano, anadhibitisha ya kuwa aliacha shule kwa sababu ya shida ya maji nyumbani kwa wazazi wake. “ Ilikuwa inanilazimu kuchagua kati ya kwenda shule na kusomba maji ya familia; Niliamua kusomba maji,” Tweyongyere asimulia.
Jeconious Musingwire, mwanasayansi wa mazingira na meneja wa mazingira ya kitaifa anayesimamia NEMA sehemu ya kusinimagharibi, anawashutumu changamoto ya maji ni kutokana na “watu wanaoharibu mazingira.” Asema, “ maji chini ya ardhi yanahusiana moja kwa moja na maji juu udongo na mazingira.”
NBI kwa sasa inatekeleza mradi wa kuimarisha maarifa, uwezo, na kwa maeneo yenye kitaasisi ya mifumo matumizi na usimamizi endelevu kwa chemichemi yaliyochaguliwa katika mpaka wa Nile Equatorial Lakes (NEL) na bonde ndogo Mashariki ya Nile. Chemichemi ya Kagera yako kwenye mkoa wa NEL. Mradi huu umedhaminiwa na Global Environment Facility (GEF) kupitia kwa UNDP.
Mradi huu, hasa utajenga na kupanua ufahamu wa rasilimali ya maji chini ya ardhi kupitia ramani wa kina na kutathmini mfumo wa chemichemi yaliyoteuliwa na maendeleo ya miongozo (kiufundi na sera) juu ya utafutaji endelevu na matumizi ya maji chini ya ardhi halikadhalika kuunganisha matumizi ya maji juu ya udongo.
Ni muhimu pia kujumuisha matumizi ya maji juu ya udongo na chini ya ardhi, kuimarisha uwezo wa maji chini ya ardhi kwa usimamizi katika ngazi ya kitaifa na kikanda na kuongeza ufahamu.
James Byaruhanga, mkazi wa Omundizi, wilaya ya Isingiro, ambayo pia ni sehemu ya bonde la mto Kagera, anakaribisha wazo ya kuongeza ufahamu kuhusu maji ya chini ya ardhi. “Unahitaji kuhamasisha jumuiya za mitaa jinsi ya kulinda na kuzalisha upya maji ya ardhini; hata hivyo, wengi wao hawajui,” asema Byaruhanga.
Habari hii imewezeshwa kuchapishwa na usaidizi wa InfoNile kwa udhamini wa Nile Basin Initiative.