Ujangili Baada ya Kusitishwa Shughuli za kawaida:Tishio kwa Uhifadhi katika Lulu Iliyojaliwa ya Afrika

Ujangili Baada ya Kusitishwa Shughuli za kawaida:Tishio kwa Uhifadhi katika Lulu Iliyojaliwa ya Afrika

Na Cliff Abenaitwe

Stanley Turyakira mkazi wa Wilaya ya Kanungu, Kusini Magharibi mwa Uganda anakabiliwa na kifungo cha miaka miwili hadi mitano jela au faini ya mamilioni ya shilingi ya Uganda au zote mbili kwa sababu ya ujangili.

Turyakira ni miongoni mwa mamia ya washukiwa ambao wanahukumiwa na Standards, Utilities & Wildlife Court (SUW). Alikamatwa mwaka wa 2021 akiwa na meno manne ya simba, vipande viwili vya ngozi ya simba, Miiba ya nungu, manyoya ya Tembo, mafuta ya Simba, na kinyesi cha tembo.

Anashukiwa kufanya uhalifu huu katika Mbuga ya Kitaifa ya Malkia Elizabeth – Uhifadhi wa pili kwa ukubwa kwa eneo nchini Uganda, iliyoko magharibi mwa Uganda kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

national parks in Uganda 1
Ramani ya Uganda inaonyesha hifadhi za Taifa na maeneo ya uhifadhi

Ripoti ya 2018 kuhusu Tathmini ya Usafirishaji Haramu ya Wanyamapori toleo ya TRAFFIC ilibainisha Uganda kama mojawapo ya vituo vya kawaida vya usafiri wa wanyamapori na bidhaa za wanyamapori katika Kanda ya Afrika ya Kati na Mashariki yenye mashirika ya uhalifu hasa yanayohusishwa na ulanguzi wa pembe za ndovu, lakini katika miaka ya hivi karibuni pia wamekuwa sana wamehushishwa na usafirishaji wa pangolini.

Kulingana na ripoti hii, na hivi karibuni ongezeko wa uhalifu kwa wanyamapori, zaidi ya nusu ya sokwe wa milimani waliobaki duniani, 50% ya aina ya ndege wa Afrika, karibu 40% ya aina mbalimbali za wanyama wa Afrika na 19% ya aina ya amfibia barani Afrika – walio Uganda- wako hatarini.

Kulingana na Hangi Bashir, Mamlaka ya Wanyamapori Uganda (UWA) mtangazaji, “ uhalifu wa wanyamapori haswa ujangili na usafirishaji, bado ni kikwazo kikubwa kwa uhifadhi nchini Uganda.” UWA ni wakala wa serikali ya Uganda enye mamlaka juu ya Hifadhi za Taifa na mapori ya akiba zote (maeneo ya uhifadhi kisheria la serikali nchini Uganda).

Uganda Wildlife Authority Publicist Bashir Hangi 1
Bashir Hangi, Mamlaka ya Wanyamapori Uganda (UWA)

Wakati wa Covid-19 iliyosababisha kusitishwa maisha ya kawaida( mwaka wa fedha 2020/21), UWA ilisajili ongezeko la ujangili. Hali mbaya zaidi kulitokea wakati simba sita waliuawa kwa Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth mwaka wa 2020.

Takwimu za UWA zinaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, washukiwa 2,310 wa uhalifu wa wanyamapori walikamatwa na zana 22,449 tofauti tofauti za ujangili zikiwemo bunduki 10. Hili ni zaidi ya ongezeko la asilimia 16 kwanzia mwaka wa fedha 2019/2020 wakati washukiwa 1,987 walikamatwa, na zana 13,645 za ujangili pamoja na bunduki 23.

Hangi anaeleza kuwa hali hii ilitokana na hali ngumu ya uchumi watu wengi wenye walipitia wakati huo.

Soko la faida kubwa la nyama pori, pamoja na soko linaloshamiri la kimataifa la bidhaa kama vile pembe za ndovu, ngozi za wanyama, uume wa tembo, na magamba ya pangolini, huchochea ujangili.

Hangi halikadhalika anasema viwango vya kukamatwa ni kutokana kwa kuongezeka kwa juhudi za nchi kupambana na uhalifu wa wanyamapori.

Kwa mujibu wa Hangi, mamlaka ya uhifadhi na usalama pia wameongeza ushirikiano wa mashirika na nchi sasa ina Kikosi Kazi cha Pamoja cha Kuratibu Wanyamapori. Kikosi kazi hiki kinajumuisha wakala kama UWA, maafisa wa forodha, polisi wa Uganda, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), na Mamlaka ya Ujasusi wa Fedha miongoni mwa vyombo vingine. Inalenga kuimarisha uratibu kati ya mashirika mbalimbali kupambana na uhalifu wa wanyamapori.

“Tunajua uhalifu wa wanyamapori hutokea kwa njia ya kuunganishwa, na wakati vitu ni moto, lazima zisafirishwe ndani na kuvuka mpaka,” Hangi alisema, akiongezea kwamba “kwa kufanya kazi pamoja, kikosi kazi kimepata mafanikio zaidi lakini pia kinatazamia kupata mengi zaidi katika mapambano dhidi ya uhalifu wa wanyamapori hasa biashara ya wanyamapori.”

Mbarara News iliweza kutazama timu katika sare tofauti za wakala kwa mpakani Mpondwe kivuko kwenye mpaka wa Uganda na DRC wilayani Kasese. Pia timu za usalama zinazojumuisha polisi, jeshi la taifa (UPDF), na walinzi wa UWA ni kawaida kuonekana hasa kwenye njia kuu katika maeneo ya uhifadhi kama Katwe na Kikorongo makutano katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth.

Juhudi hizi zote zinalenga kulinda wanyamapori wa Uganda ambayo ni msingi wa sekta ya utalii – mtaji mkubwa wa fedha za kigeni kwa nchi.

Wakati unakuwa mgumu?

Mamlaka ya uhifadhi nchini Uganda inaonekana wameelewa maana ya msemo wa zamani: ‘hali inapokuwa ngumu, wagumu wanazidikwenda,’ sasa wale wawindaji haramu wanaonekana kuwa mahiri zaidi katika shughuli zao.

“Ni kweli majangili wanazidi kuwa wajanja na wakati mwingine hutumia binu ya kisasa katika shughuli zao, lakini kama UWA, daima tuko mbele na werevu zaidi,” Hangi alisema.

Alielezea kwamba UWA imeongeza uwezo na idadi ya walinzi kwa hifadhi za taifa, na kuimarisha doria katika maeneo yote ya uhifadhi kulinda wanyamapori na kuwazuia uhalifu kama ujangili.

“Sasa tuna akili kamili, vitengo vya uchunguzi, kukusanya ushahidi na uendeshaji wa mashtaka kukabiliana na uhalifu wa wanyamapori. Lengo letu ni kupunguza uhalifu wa wanyamapori hasa ujangili lakini pia kukomesha nchi yetu kuwa pahali pa njia nzuri ya kupita kwa wafanyabiashara
wa wanyamapori,” mhifadhi anaeleza.

Elephants in Ugandas National Parks are a major target for poachers because of ivory 1
Tembo katika Mbuga za Kitaifa za Uganda wanalengwa zaidi na wawindaji haramu kwa sababu ya pembe za ndovu

Mbinu Zinazotokana na Jamii dhidi ya Ujangili

UWA imekubali kutegemea mbinu zinazotokana na jamii kukuza uhifadhi. Mbinu hizi zinalenga kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa uhifadhi miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo yanayopakana na hifadhi ya taifa, kwa mujibu wa Hangi.

Anaeleza kuwa jamii zinaungwa mkono kutekeleza miradi ya kuongeza kipato na rafiki kwa uhifadhi kama eneo la nyuki kwenye mipaka ya maeneo ya uhifadhi. Baadhi ya miradi hii iko katika maeneo kama Muhoma (Msitu wa Bwindi usioweza kupenyeka), Kanyaryeru ( karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Mburo), Bweyare na Karuma (pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Murchison Falls).

Mbali na miradi ya kuongeza mapato, jamii jirani na hifadhi ya taifa pia kufaidika na ugavi wa mapato. Ilianzishwa na serikali mwaka 1995, mpango wa kugawana mapato unalenga kusawazisha hasara ambazo watu hukutana nazo kwa kuishi karibu na maeneo yaliyohifadhiwa huku ikikuza tabia bora ya uhifadhi.

Chini ya utaratibu huu, UWA inashiriki asilimia 20 ya ada ya kiingilio katika eneo lililohifadhiwa na serikali za mitaa ili kunufaisha jamii karibu na hifadhi za taifa. Kwa jamii jirani na Hifadhi ya Kitaifa ya Misitu isiyoweza kupenyeka, mapato yanaongezwa na 5 USD kwa kibali cha kufuatilia kila sokwe.

“Tumeweza kujenga mabwawa ya maji kwa ajili ya jamii ya tarafa ya Biharwe inayopakana na Hifadhi ya taifa ya Ziwa Mburo kwa kutumia rasilimali za kugawana mapato. Hii imepunguza uhaba wa maji na wakulima hawatembelei mara kwa mara katika hifadhi ya taifa kwa ajili ya maji,”asema Robert Kakyebezi, Meya wa Jiji la Mbarara, kusini magharibi mwa Uganda.

Apollo Mwesigye, afisa maendeleo ya jamii wa kata ndogo wa Katunguru wilayani Rubirizi (wilaya mojawepo karibu na Hifadhi Taifa ya Malkia Elizabeth) asema uhamasishaji ya jamii a matumizi endelevu ya fedha zilizopokelewa chini ya mpango wa kugawana mapato imesaidia watu kufahamu thamani ya wanyamapori na kukuzwa kwa hifadhi.

“Sasa tunawatazama wanyamapori kama hazina tunapaswa kulinda kwa sababu ya faida zinazoonekana na tunafurahia,” anaona Tweteise Mwinemugisha, mwenyekiti wa kijijij cha Kyambura wilayani Rubirizi.

Mbinu Kali dhidi ya Uhalifu wa Wanyamapori

Kwa mujibu wa Hangi, UWA inatoa mafunzo kwa walinzi katika kugundua uhalifu wa mtandao na usimamizi, kuanzisha mbinu zaidi zinazohusiana na teknolojia. Pia anasema wameweka kamera za kunasa katika Uhifadhi Taifa ya Malkia Elizabeth. Ziko na uwezo wa kunasa picha na kutoa muda halisi kuhusu shughuli yoyote katika eneo la uhifadhi.

“Pia tunafanya majaribio ya matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) mara kwa mara kwa kugundua uhalifu wa wanyamapori,” anafafanua, akiongeza kuwa haya yote inalenga kuhakikisha kuwa Uganda haiwi kimbilio salama ya usafirishaji wa wanyamapori duniani kote.

A heard of buffaloes in Queen Elizabeth National Park. These are commonly poached for meat. 1 1
Kundi la Nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth. Hizi kawaida huwindwa kwa ajili ya nyama

Kwa miaka mingi, Uganda imeongeza kitengo chake cha mbwa katika njia kuu za kimataifa za usafiri, hasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kukatiza biashara haramu ya wanyamapori kinyume cha sheria. Vitengo hivi vimepanuliwa hadi maeneo mengine pia, na moja huko Karuma, iko katika sehemu ya Kaskazini Magharibi mwa nchi, kwenye barabara kuu ya Kampala – Sudan Kusini, katika pana ya Hifadhi Taifa ya Murchison Falls.

Mnamo 2020, Naibu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shughuli za UWA, Charles Tumwesigye alinukuliwa na Mfuko wa Wanyamapori wa Afrika (Africa Wildlife Fund) akisema; “eneo la kaskazini-magharibi huhifadhi njia za usafirishaji magendo ya wanyamapori kuvuka mpaka wa DRC na kuongezeka kutoka Sudan Kusini huku sehemu ya kukutanisha ikiwa ni Kurama.” Hata hivyo, mamlaka katika UWA wanaamini kwamba kitengo hiki cha mbwa ni ufanisi katika kugundua shughuli hizo haramu katika eneo hili la usafirishaji.

Kushughulikia Kesi za Wanyamapori: Mahakama ya Huduma nchini Uganda

Mnamo 2017, Uganda ilianzisha Mahakama ya Viwango, Huduma na Wanyamapori (SUW). Katika uzinduzi wake, Jaji Mkuu wa wakati huo, Bart Katureebe, alikumbuka (noted that) “somo la viwango, huduma na wanyamapori muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa nchi. Kwa vile upatikanaji wa haki katika eneo hili una uwezo kukuza uwekezaji katika maeneo muhimu ya uchumi, ulinzi wa mazingira, afya ya umma na mazoea ya kimaadili ya biashara.”

Pamoja na kuanzishwa kwa mahakama ya SUW, utunzaji wa uhalifu wa wanyamapori nchini Uganda imeimarika.

Kati ya Julai 2020 na Juni 2021, mahakama ilishughulikia kesi 468 za uhalifu wa wanyamapori. Kwa mujibu wa taarifa kutoka idara ya sheria na masuala ya ushirika wa UWA, kesi 230 zilikamilishwa na 207 kupatikana na hatia, 20 kutupuliwa mbali, moja kuachiliwa, na mbili ilitolewa kwa dhamana ya polisi.

Hata hivyo, 238 zilibakia zikisubiri, huku 179 zikitakiwa kusikilizwa zaidi.

Kwa mfano, katika kipindi hicho, mahakama ilimfunga Anguyo Yusuf kwa miezi 17 gerezani kwa kumiliki vipande 13 vya pembe za ndovu. Mahakama hiyo tu ikamfunga Aribo Jennifer miaka mitatu gerezani au alipe faini ya shilingi milioni tatu kwa kumiliki vipande 83 vya meno ya kiboko.

Mahakama ilishughulikia kesi ya hali ya juu kati ya Julai 2020 na Juni 2021iliyohusisha You Jing Dao na wengine sita. Walikamatwa na vipande kumi za uume wa ndovu, kilo moja ya magamba ya pangolini na kobe sita hai. Walitozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 15 pamoja na amri ya kulipa UWA faini ya USD 1500.

Uandishi wa Habari za Uchunguzi wa Mazingira ya Oxpeckers, kampuni isiyo ya kiserikali inayotumia uchambuzi wa data ya kijiografia kufuatilia na kufichua makundi ya wahalifu inayowahusisha viongozi na mashirika wala rushwa na yanayopora maliasili za Afrika, inaorodhesha zaidi ya kesi 100 za wahalifu wa wanyamapori, wanaolaumiwa, kesi mahakamani na kukamatwa kwa watu nchini Uganda.

Ramani ya data ya kijiografia (geo-data map) zinazozalishwa na Oxpeckers kwa ushirikiano na InfoNile inaonyesha kuwa kesi 48 za uhalifu wanyamapori zilirekodiwa kutoka sehemu ya magharibi ya Uganda, tano katika sehemu ya kusini magharibi, Kesi 12 katikati mwa Uganda, tisa kaskazini mwa Uganda na sita katika mikoa ya kaskazini na mashariki mwa Uganda katika miaka ya hivi karibuni.

Data hii bado inasasishwa, lakini inatoa muhtasari wa kiwango cha uhalifu wa wanyamapori nchini Uganda.

Kwa mfano, #WildEye data zinaonyesha kwamba Benson Bob Bwango, alikamatwa kutoka Waseko –moja ya maeneo ya kutua kwa Ziwa Albert. Alikamatwa mnamo Julai 2019 na kilo 60.54 za pembe za ndovu. Alihukumiwa na mahakama ya SUW na kutozwa faini ya shilingi milioni tano (USD 14,000).

Kulingana na data sawia, Kawunde Gyavira mwenye umri wa miaka 34 pia alikamatwa mwaka wa 2019 jijini Kampala akiwa na kilo 61.4 za pembe za ndovu. Alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa au faini.

Maendeleo, Lakini Lazima Tuimarishe Vita – Wataalam Wazingatia

“Ni lazima tuhifadhi kwa ajili ya leo na siku zijazo,” asema Grahams Tumwekwase, msomi wa uhifadhi. “Ujangili unatishia mamilioni ya wanyamapori wa thamani. Baadhi ya wanyama aina kama pangolini hatari ya kutoweka kama viwango vya ujangili havitapunguzwa. Ningependa kuona uratibu zaidi kutoka nchi za kikanda hasa katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori ambayo yanaonekana kupangwa zaidi kila siku,” alitoa mtazamo.

Dk. James Musinguzi, mtaalamu wa utalii na uhifadhi kutoka kwa Kituo cha Elimu na Uhifadhi wa Wanyamapori nchini Uganda anapania kukuza uhamasishaji zaidi wa jamii.

“Maeneo ya hifadhi inakaribiana na jamii. Hawa ndio watu wanaonufaika moja kwa moja na rasilimali hizi, lakini pia wao ni kawaida maeneo ya mawasiliano katika ujangili na biashara haramu,” alitoa mtazamo.

Kulingana na Musinguzi, kuna haja ya kuendelea kuhamasisha watu kutambua na kufahamu umuhimu wa uhifadhi, lakini pia kuweka timu za kutekeleza sheria ya wanyamapori na fununu ya watu wa katikati wanaofika katika maeneo yao ili kuwezesha ujangili.”

“Tumepiga hatua, lakini lazima tuendeleze na mapambano,” asisitiza.

Dr. James Musinguzi a conservation specialist 1 3 scaled
Dkt. James Msanguzi, Mtaalamu wa Uhifadhi

Yayeri Kabugho, mwendeshaji wa utalii na usafiri mwenye makao wilayani Kasese – Uganda Magharibi- ako na hofu kwamba ujangili utaathiri sekta ya utalii katika miaka ijayo, ikiwa mwenendo unaendelea. Kulingana na Kabugho, Uganda imejaliwa kuwa na wanyamapori wa kipekee kutoka simba anayepanda, sokwe wa milima, miongoni mwa wengine, yote ambayo yanapaswa kulindwa.

“Bila aina hizi za kipekee, hatutakuwa na kitu cha kipekee cha kuwapa watalii. Hii inamaanisha kupungua kwa mapato ya watu halikadhalika nchi. Lazima tuwe wagumu kwa uhalifu wa wanyamapori kupitia kupitia adhabu kali na faini, ongeza idadi ya walinda usalama ili wakomeshe kuingia kinyume cha sheria katika hifadhi za taifa, na kuongeza akili ili kugundua mipango ya uhalifu mbele ya wapangaji,” Kabugho asema.

Maoni ya Mbarara News

Kusimamia wanyamapori kwa mafanikio uhifadhi sio msingi tu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu bali ni jukumu la pamoja la kizazi cha sasa kwa vizazi vijavyo.

Ni wajibu wa kila Mganda, kila kiongozi, kila kitengo cha kitaifa, wilaya, kata na kijiji, kulinda wanyamapori, kutoa taarifa za vikundi vya ujangili na kuchangia katika uhifadhi wa wanyamapori. Ni rahisi zaidi na kwa bei nafuu kulinda wanyama wetu, kuliko kuzibadilisha zikiisha.

Usaidizi wa  ukuzaji na utengenezaji wa hadithi hii ulitoka kwa InfoNile, kwa ushirikiano na Oxpeckers Investigative Environmental Journalism, kwa ufadhili wa Earth Journalism Network. Vielelezo vya data na Ruth Mwizeere na Annika McGinnis / InfoNile.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts