Fred Mwasa na Sylidio Sebuharara
Kwenye mto wenye urefu wa takriban kilometa 297 mabwawa manne ya kuzalisha umeme yameshajengwa huku bwawa lingine la kuzalisha umeme likiendelea kujengwa na ujenzi wa bwawa lingine la sita ukiwa mbioni kuanzishwa siku si nyingi zijazo. Wakati mabwawa haya yanazalisha umeme unaohitajika, kwa maendeleo ya nchi, nyuma yake ujenzi huu kunaacha uharibifu mkubwa wa mazingira, uharibifu ambao kama hautashughulikiwa sasa hivi unaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa kizazi kijacho.
Hebu tujiulize, mto Nile ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa kilometa 6,695 ukiwa na mabwawa ya kufua umeme yapatayo 25 hadi kufikia mwaka 2019 na kaa ukijua kwamba mto Nyabirongo unaingia mara 23 kwenye mto Nile. Kwa muktadha huo mto Nile ungepaswa kuwa na mabwawa 113 ya kufua umeme.
Mto Nyabarongo ni tegemeo kubwa la uzalishaji umeme unaotumika nchini Rwanda na kufikia mwaka 2020 uwezo jumla wa uzalishaji umeme nchini humo ulikuwa ni mega wati 224.4 kutokana vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na gesi ya methane na jua. Umeme unaotokana na maji ni takriban asilimia 46.8 ya umeme wote unaozalishwa nchini humo na asilimia kubwa ya umeme wa maji unatoka kwenye mto Nyabarongo na vijito vyake na asilimia 12.8 inazalishwa na kubwa lijulikanalo kwa jina la Nyabarongo 1.
Wakati uchumi wa Rwanda ukikua kwa kasi miaka ishirini iliyopita, serikali ya nchi hiyo inahitaji umeme ili kuhimili kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi huku ikiweka lengo la kuzalisha mega wati 512 hadi kufikia mwaka 2023 na 24.
Hata hivyo wataalaam wanaainisha ya kwamba lengo hilo bado ni dogo ikilinganishwa kile ambacho nchi inaweza kuzalisha. Wataalamu wanasema Rwanda kwa kutumia umeme wa maji, gesi ya methane na joto ardhi vyanzo vinavyokadiriwa kuwa na megawati 1,613 ingeweza kuzalisha umeme kiuchumi kwa kutumia vyanzo vya ndani na kwa mantiki hiyo nchi hiyo kwa sasa inatumia asilimia 10 tu ya uwezo wake.
Mikondo ya maji yenye uwezo wa kuzalisha umeme nchi Rwanda si mingi na hivyo kuuacha mto Nyabirongo kuwa ndio chanzo kikuu cha maji kwa mabwawa yote ya kuzalisha umeme.
Chanzo cha mto Nyabarongo ni mito miwili mikubwa ya Mwogo na Mbirurume iliyopo Kusini kati nchini Rwanda ambapo mto Rukarara unaochipuka kutoka mto Rubyiro na mto Nyaruguboyi ndio mito inayounda mto Mwogo. Mto Mbirurume kwa upande wake unatiririka kutoka katika milima y Gisovu ukipokea vijito mbalimabali vingine kwenye eneo hilo.
Mito ya Mwogo na Mbirurume inaungana kwenye mpaka unaoziunganisha Wilaya za Nyamagabe, Muhanga na Ruhango na hapa ndipo mto Nyabarongo unapoanzia. Mto huu unapoelekea kaskazini na kasha kusini unaishia kwenye Mto Akanyaru kwenye eneo lingine la makutano kati ya wilaya za Kamonyi Nyarugenge na Bugesera kutoka hapo unaingia kwenye mto Akagera unaelekea ziwa Rweru linalozishirikisha kwa pamoja Rwanda na Burundi.
Kutokana na mito hii serikali tawala mbali mbali zilizotawala nchi Rwanda zilijikita katika kujenga mabwawa hadi kufikia miaka ya 2000, bwawa la kwanza likiwa limejengwa mwaka 1957 na lingine likijengwa miaka miwili ilifuata. Hadi kufikia mwaka mwak 1994 kulikuwa na mabwawa matano tu , makubwa yakiwa ni bwawa la Ruzizi 1 na Makungwa 1 ambapo kila bwawa lilikuwa linazalisha megawati 12 pamoja na bwawa la Ntaruka ambalo lilikuwa linazalisha megawati 11.25.
Hadi kufikia mwaka 2021 mabwawa ishirini na nne mengine ya kuzalisha umeme yameongezeka kati ya hayo manne makubwa zaidi yajengwa kwenye mto Nyabarongo.
Idadi hiyo kubwa ya mabwawa kwenye mto huo imezidisha tatizo kubwa ambalo Rwanda imekuwa ikikabiliana nalo kwa miongo kadhaa la mmonyoko wa udongo na hivyo kupoteza udongo kwa kiasi kikubwa.
Utafiti uliofanywa mwaka 2016 unaonyesha kuwa makadirio ya upotevu wa udongo kwa mwaka ulikuwa tani milioni 409 upotevu ambao ni 490 kwa heka.
Mabwawa na upotevu wa udongo
Uchunguzi huru unaonyesha kuwa mto Nyabarongo unakabiliwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira kutokana na maporomoko ya ardhi, uchimbaji madini, kilimo kisicho kuwa endelevu na takataka za majumbani na viwandani. Sababu hizi zinafanywa kuwa baya zaidi maeneo ya milimani kuliko wekwa alama na miteremko mikali kando ya mito na matokeo yake ni kuwa mto Nyabirongo umekuwa na maji udhurungi kwa miongo kadhaa.
Hata hivyo jambo ambalo hadi sasa halijachunguzwa ni mchango wa mabwawa ya kufua umeme katika kuzidisha kiwango cha upotevu wa udongo katika bonde la mto Nyabarongo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Chronicles unabainisha kuwa mabwawa ya kufua umeme yana mchango mkubwa katika kuzidisha tatizo lililopo kuwa baya zaidi. Wanasema “ Matokeo ya utafiti wetu mabwawa yaliyopo mto Nyabarongo yamesababisha upana wa mto huo kuongezeka maradufu na kumega sehemu kubwa ya ardhi ya kilimo na kukifanya kina cha maji kupungua kutokana na udongo unaochukuliwa hivyo kuzidisha kasi ya mtiririko wa maji”
Timu ya wanahabari ya The Chronicles ilitembelea viunga vya mabwawa yote manne kwenye mto Nyabarongo. Wanasema; “ tulipita pembeni mwa mto, tukisafiri zaidi ya kilometa 300 kupitia wilaya za Karongi, Ngororero, Kamonyi na Bugeserahuku tukiangalia kiwango cha uharibifu kilichoachwa na uharibifu ambao utendelea kutokea na wakati wa safari yetu tulipata wasaa wa kuongea na wakaazi wa eneo hilo kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi”.
Wanaendelea kusema;” Tuliona kwamba mto Nyabirongo hubadilika na kuwa na rangi ya udhurungi kuanzia kwenye vyanzo vyake vikuu viwili yaani mto Mwongo na Mbiruruma na kwenye makutano haya Mto Mwongo unasifa ya kuwa mweusi zaidi kuliko Mbiruruma na timu yetu ilibaini kuwa Mto Mwongo unaotoka Mto Rukarara ambao una mabwawa matatu ya kufua umeme – mabwawa ya Rukarara I, Rukarara II, na Cyimbili/Rukarara V una kina kirefu zaidi kinachofikia mita mbili. Pamoja na kina hiki mto huo una kiasi kikubwa cha matope chini yake ikiwa na maana kwamba mtu anaweza kuzama zaidi.”
Timu ya Chronicles iligundua kuwa Mto Mwongo unatiririsha maji yake kwa utulivu kuliko mbirurume na hii inaweza kuwa ni matokeo ya kutokuwepo miamba isipokuwa matope yaliyotokana na udongo uliosombwa kutoka kwenye vijito. Kwa upande mwingine Mbirurume ulikuwa unasomba mchanga mwingi na ilithibitisha kuwa Mto Mwongo umechafuliwa kutokana na takataka zilizosukumwa kwa nguvu kubwa ya maji ikisaidiwa na na mabwa hayo matatu.
Wakati timu ya Chronicles ikisonga mbele ilipita kwenye mabonde makubwa ambayo yamekuwa yakitumika kwa shugfhuli za kilimo kwa karne kadhaa. Uharibifu uliofanywa na mabwawa haya athari zake zinaonekana kwenye kitongoji cha Mabuga eneo la Murambi ambapo timu hii iliwkuta watu wakiwa wamekaa kwenye kilabu ch pombe za kienyeji huku wakilalama ya kuwa hawana kitu cha kufanya kwa kuwa eneo kubwa la ardhi yao imechukuliwa na na mto Nyabarongo ambao unaendelea kupanuka tangu tangu ujenzi wa Nyabarongo II ambao unatoa megawti 28 ulipo jengwa mnano mwaka 2008.
Wakazi walianza kuona athari za mafuriko kuanzia mwaka 2012 na waliimbia timu ya The Chronicle ya kuwa tangu bwawa hili lijengwe wanalima mazo kwa msimu mmoja tu, hususan mpunga. Kabla walikuwa wakilima na kupanda mazao kwa misimu miwili.” Sasa hivi kama unavyotuona umetukuta hapa tukinywa pombe kwa sababu hatuna cha kufanya na ardhi unayoiona imechanyanyika na mchanga uliosababishwa na mafuriko ya Mto Nyabarongo kwa hiyo hakuna kitu kinachostawi pale” anasema bwana Telesphore Nyandwi mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Pascal Habenimana (49), mkazi mwingine wa hapa anasema; “kila kitu kimebadilika, mto huu ulikuwa ni kijito kidogo tu miaka ishirini iliyopita na sasa ni ni mto mpana ambao umepanuka karibu mita mbili kila upande.
Ifikapo mwezi wanne ambacho ni kipindi cha mvua kubwa bonde linakumbwa na mafuriko yanayo sababishwa na tangi la kuhifadhia maji wakati tangi hilo linaposukuma maji na kusababisha maji zaidi ya mto kumwagikia juu ya mto huku maji mengine yakitokea milimani. Kabla ya bwawa hili halijajengwa, wakulima walikuwa wakiliam migomba kando ya bonde hili na sasa hivi kuna migomba michache na kadiri mambo yanavyokwenda hakutakuwa na migomba miaka ijayo.
Timu hii ya The Chronicle inabainisha kwamba ilikuwa ni vigumu kupata utafiti wa kisayansi juu ya athari zilizosababishwa na ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyabirongo I. Kwa mujibu wa timu walikutana ripoti ya tathmini ya athari zilizoletwa na bwawa hili ya Aprili mwaka 2020 .
Ili kufahamu jinsi mabwawa hya ya kufua umeme yanavyobadili asili yam to Nyabirongo timu ya Chronicle ilizungumza na baadhi ya wanasayansi na watafiti maji na mabwawa ya kufua umeme nchini Rwanda ambao walitaka majina yao yahifadhiwe kutokana na unyeti wa jambo lenyewe.
Kwa nyakati tofauti watafiti wanasema mabwawa yaliyopo Nyabirongo ni tatizo lililo dhairi kama ilivyo kwa mabwawa mengine kokote kule kwa sababu yanasababisha kile walichokiita mzunguko wa mmomonyoko. Wanasema hapa kinachotokea ni kuwa njia ya asili ya kuondoa mchanga kwenye mto ni vijikonakona vilivyopo nje ya mto na kwa asili hapa ndipo panapoanzisha mafuriko kwa kuwa sehemu hii ni asilia ya kuzuia mchanga usiingie ziwani.
Uwepo wa mabwawa unabadilisha uelekeo wa maji kila siku na vizuizi vya bwawa vinafungwa na maji yanakosa pa kupitia. Shughuli hizi za ufuaji umeme zina athari kubwa kwenye kuta za mito na vijito vyake hivyo kusababisa udongo kwenye kingo kuondolewa.
Wakati mzunguko wa mmomonyoko ukiendelea, sehemu ya juu ya kingo za mto inaangukia ziwani na kusukumwa na maji. Hali hii inajirudia miaka nenda rudi na kupelekea mto kupanuaka
Athari za kimazingira na kijamii za bwawa la Nyabirongo I kwa mujibu wa tathmini ya mazingira zilizoainishwa hapo juu zinajumuisha pia usafirishaji wa mchanga na mmomoyoko wa udongo , wakazi kuhamia makazi mengine, athari kwa viumbe ambavyo vipo hatarini kutoweka, kupoteza uhai wa samaki kwenye kinu cha kufulia umeme.
Wakati mto Nyabirongo ukiingia kwenye hifadhi ya maji, timu ya The Chroniles ilishuhudia vipya vikiwa vimechafuliwa kutokana na machimbo yaliyopo milimani na hatimaye kuingia kwenye mto Nyabirongo. Kilometa takriban tano kutoka kwenye hifadhi ya maji linaonekana rundo la mchanga limejikusanya nah ii inatokan na kina kifupi cha hifadhi nah ii inatokana na wa kiangazi uliokuwapo miezi kadhaa iliyopita.
Timu ya The Chronicles iliomba kutembelea mabwawa haya ikiwa ni sehemu ya uchunguzi hata hivyo mashirika yanayo simamia mabwawa haya ikiwa ni pamoja na lile la serikali Energy Utility Corporation Limited linalosimamia bwawa la Nyabirongo I na Prime Energy Ltd shirika la binafsi linalosimamia mabwawa matatu kwenye mto huo hawa kujibu barua za maombi ya kuingia kwenye maeneo yao.
Timu pia ilishuhidia maji ya kimwagika kwenye vizuizi kulia moja ya mwa bwawa la Nyabirongo I na wakazi waliiambia timu hiyo kuwa kizuizi hicho kilifunguliwa na kimekua kikitoa maji kwa takriba miaka miwili.
“Tulisikia ya kuwa vizuizi viliharibika kabla ya janga la korona na mafundi bado hawajarudi na kusababisha ziwa kumwaga maji masaa ishirini na nne na ytunashindwa kuvuka mto.” Anasema Mukandutiye Aniziya mama wa watoto wawili.
Labda hali hii inaweza kuwa ni kielelezo ya kwamba kwa nini kiwango cha maji kimepungua kwenye hifadhi wakati upande moja wa hifadhi ukiwa wazi na maji yakitoka kwa kasi kubwa ya namna hii ni wazi kutakuwa na athari kubwa kwenye mkondo wa maji wa Nyabirongo.
Ushuhuda jambo hili unaonekana kwenye makutano ya mito ya Akanyaru na Nyabarongo sehemu ambayo mto Akagera unaazia sehemu hii inayokutanisha mito hii imepanuka kwa kiasi cha mita hamsini kwa miaka kumi iliyopita nah ii ni kwa mujibu wa wakaazi wa hapa.
Kingo za mto Nyakarongo, kwa kadiri mto unavyo kwenda kupitia kwenye maeneo oevu kuelekea kwenye makutano na mto Akanyaru zimepanuka kwa kiasi cha mita mbili kila upande kwa kipindi hicho cha miaka kumi wanaeleza wakazi wa hapa.
Ziwa Rweru lina rangi ya hudhurungi pia
Ushahidi mwingine wa kiasi cha udongo na mashapo ambayo ambayo mto Nyabarongo unapitisha ni ukweli kwamba kina cha mto ni mita mbili zinazoambatana na matope chini yake. Timu ya Chroniles iliwakuta watu wakivuka mto kwa kutumia mitumbwi kutoka pande mbili za mto wakitumia miti mirefu ya mianzi ambayo ilikuwa ikiwasaidia kuongoza mitumbwi yao na walichukua fursa kuomba moja ya wanaoongoza vyombo hivi kuzamisha miti hii katikati ili waweze kujua urefu wa kina cha mto na baada ya zoezi hilo walibaini kina kilikuwa mita nne zaidi.
Safari ya timu hii ilielekea kwenye eneo la Rweru na kushuhudia kutoka kwenye upeo wa macho ziwa likionekana kuwa na rangi ya udhurungi. Hata hivyo hawakuweza kufika kwenye eneo halisi ambapo mto Akagera unaingiza maji yake kwa sababu eneo hilo lipo ndani ya eneo lenye ardhi oevu.
Kwenye kingo za ziwa maji yana rangi ya udhurungi na magugu maji yametapaka. Mmea huu hatari umeharibu maziwa na mito kwenye eneo la maziwa makuu. Wenyeji na wavuvi waliokuwepo hapo wanasema mmea huu umeletwa kwenye ziwa hili na mto Akagera na wanasema wamekuwa wakiyaondoa magugu maji hayo kwa kutumia mitumbwi yao kila siku.
Kwa mujibu wa taarifa za wenyeji, kwa kipindi cha kati ya miaka mitatu na mine mto umevunja njia yake ya asili na sehemu kubwa ya mto inapita pembeni mwa ziwa Rweru na kuendelea hadi ziwa viktoria na hivi sasa mto unaingiza maji yake ziwani na kuendelea na safari yake na kile kipande cha ardhi kilichokuwa kinatenganisha mto na ziwa kimebomolewa. Kwa minajili hiyo mujibu wa wavuvi sio tu mto umegauka kuwa na rangi udhurungi bali pia umejaa matope.
Ili kuthibisha mabadiliko ya ziwa kama vile kuwa na rangi ya udhurungi kutokana na matope upana wa mto Akanyaru kwenye sehemu unapoingia ziwani na ukubwa wa ziwa timu ili tafuta na kupata picha za setilaiti na kufanya uchunguzi. Kwa kifupi matokeo ya uchunguzi huo yalikuwa ya kushangaza: Mwaka 1984 wakati picha za kwanza za setilaiti zilipoanza kukusanywa takriban asilimia 70 pmka 80 ya ziwa lilikuwa la bluu. Hii inaashiria kwaba hata mito ya Nyabarongo na Akagera pamoja na kuwa na rangi ya udhurungi haikuweza kuyaathiri maji ya ziwa maji ya ziwa Rweru. Inaonekana rangi ya maji imeanza kubadilika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mtazamo wa mwanasayansi
Si kila kitu kinachohusu mabwawa ya kufua umeme kwenye mto Nyabarongo ni cha kuhuzunisha. Mabwawa haya yameleta faida Fulani. Kwa mujibu wa watafiti ikiwa ni pamoja na wale chuo kikuu cha Yale na Chuo kuku cha kimataifa cha Florida vyote vya Marekani ambao walifanya utafiti wa mkusanyiko wa madopo yaliyopo Mto Nyabarongo wanasema “ Athari chanya zilionekana kwenye maji kwani ungavu wa maji kwa wakati fulani uliongezeka kutokana na uepo wa madopo ambayo yakikuwepo kwenye hifadhi za maji” Kwa mujibu wa Dr Amartya Saha, ambaye aliwasiliana kwa njia ya barua pepe na Chronicles.
Dokta Amartya Saha anabainisha ya kuwa madopo yananasa kwenye hifadhi na yanabaki maji yanapoacha kutiririka, hivyo maji yam to yakuwa na mawimbi madogo mno.
Anasema ujenzi wa mabwawa madogo unaweza kuwa mhimu kwa uhifadhi wa maji lakini mabwawa makubwa yanasababisha uharibifu wa mazingira.
Majibu ya Serikali
Taasisi inayohusika moja kwa moja na miundo mbinu ya maji nchini inabainisha ya kuwa serikali inge jenga mabwawa ya kufua umeme kwenye mito kama yangekuwa na athari. “ Upembuzi yakinifu unafanywa kabla ya kujenga bwawa na kwa upande Nyabirongo tatizo ni mmomonyoko wa udongo tatizo ambalo linatafutiwa ufumbuzi”: Anasema bwana Prime Ngabonziza mkurugenzi wa Bodi ya rasilimali za maji nchini(Rwanda Water Resources Board RWB).
Anaongeza kusema “Iwapo itabainika mabwawa yakijengwa mengine zaidi ni jambo zuri basi yatajengwa kwa sababu serikali haiwezi kujenga mabwawa kama tathminiya mazingira inaonyesha vinginevyo.
Serikali inapigia debe uingiliaji kati wa serikali katika kubadili mto wenye rangi udhurungi na kuwa maji safi kwa kuutaja mto Secoko moja ya mito inayotokana na mto Nyabirongo. Mto huu unatoa maji yake kutoka milima ya wilaya ya Ngororero magharibi kati na kupitia Rutsiro mpaka Karongi ambako inakutana na Nyabirongo.
Kwa miaka mungi mto Secoko umekua ukisababisha uharibifu hususa sehemu za Rutsiro. Utafiti wa mwaka 2016 uliogharimiwa na shirika la misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) uligundua kwamba mto Secoko kati ya Januari na Aprili ulikuwa unasomba kiasi kikubwa cha madopo na kuingiza kwenye mto Nyabirongo na kingo zake.
Mnamo mwezi machi 2019 serikali ya Rwanda ilizindua program iliyogharimu faranga za kinyaraunda 16 billion sawa na dola za kimarekani milioni 16 katika kutekeleza miradi mbalimbali itayozuia mmomonyoko kwenye mto Secoko. Miradi hii iliyopo kwenye eneo la hekta 10,000 ilihusisha upandaji miti, kuboresha kilimo n.k
Mpango wa Serikali wa mwaka 2018 hadi 2024 kwa ajili ya urejeshaji wa asili wa sehemu ya juu ya Nyabirongo uliuainisha mto Secoko kuwa ni kitu cha dharura na moja ya shughuli za ukarabati ilikuwa kuzuia uwapo wa makorongo kwenye eneo la hekari 26 kukiwa na kilometa 5.6 za mabwawa ya kuangalia. Mabwawa ya aina hii yapo katika miundo tofauti, yamejengwa kwenye njia yam to ili kupunguza mwendo wa maji kudhibiti udongo.
Hivi sasa mto Secoko umebadilika kwa jumla kwani maji yanayotiririka kwenye mto huu ni maangavu na yana kiasi kidogo cha udongo unaosombwa na maji yam to.
Ili kukabiliana na mmomonyoko wa udongo nchi nzima, hususan kwenye mikoa yenye milima, Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Maji bwana Ngabonziza anasema makadirio gharama ya program hii ni faranga za kinyaruanda 500billion sawa na dola za kimarekani 500 milioni kwa kipindi cha kati ya miaka 15 hadi 30 ijayo.
Matarajio
Kwa mabwawa yaliyopo wanasayansi wanaamini kwamba kwa mabwawa yaliyopo hususan bwawa la Nyabarong I, miuondo mbinu mipya inahitajika ili kuzuia magopo yanayotoka kwenye vijito ili kuruhusu maji yanayotoka kwenye hifadhi ya maji kupita. Ufumbuzi mwingine ulioainishwa ni ni kujenga mifereji ambayo magopo hayatajikusanya kwenye kuta za sehemu ya kufua umeme nah ii itahitaji kuondoa maji mara kwa mara.
Kuhusu mabwawa mapya ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji yaliyopangwa, utafiti ulipendekeza kwamba maeneo ya mabwawa yanapaswa kuchaguliwa katika mikoa yenye mavuno kidogo ya mashapo. Watafiti pia waliweka mbele kile kilichoelezewa kama “hifadhi inayoendeshwa (kupunguza upotezaji)”, ambayo kimsingi inaweka hifadhi kubwa sana ambayo inaweza kushikilia mchanga kwa hadi miaka 50.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stellenbosch cha nchini Afrika ya Kusini ulipendekeza kuwa mabwawa ambayo yapo hivi sasa kwenye mto huu yanahitajika kuchepusha mashapo kwenye njia ya mto na kujenga hifadhi ya maji nje mkondo wa maji.
Na kwa yale mabwawa yalipo mbioni kujengwa, utafiti huo ulipendekeza kuwa maeneo ya ujenzi wa mabwawa yangefanywa kwenye sehemu zinazoonekana kuwa na uzalishaji mdogo wa madopo. Watafiti hao walipendekeza ya kuwa kiwepo kipaumbele cha kuwa na mabwawa yatahifadhi maji ambayo yatapunguza kiasi cha maji kinachomwagika, hii ikiwa na maana kujengwe hifadhi kubwa zaidi ambayo itahimili madopo kwa muda wa miaka hamsini.
Iwapo mabwawa yaliyopo hivi sasa kwenye mto Nyabarongo yanasababisha uharibifu kama huu hivi sasa bado haijafahamika kitakachotokea baada ya kukamilika kwa bwawa la kuzalisha umeme la Nyakabarongo II linalo tazamiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 43.5 mwaka 2025kwa ghrama ya dola za kimarekani 214 milioni huku bwawa la Rukarara VI litakalo kuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati kumi ujenzi wake ukiwa unaendelea.
Makala haya yalitolewa kwa ushirikiano na InfoNile kwa ufadhili wa JRS Biodiversity Foundation.
Hadithi hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye The Chronicles.