Mabadiliko ya Msimu; Mvua zisizotabiriwa zathiri jamii wenye kuhamahama na mifugo kanda ndogo la Karamoja

Mabadiliko ya Msimu; Mvua zisizotabiriwa zathiri jamii wenye kuhamahama na mifugo kanda ndogo la Karamoja

Kijijini Ariamaoi, wilaya ya Nabilatuk, jamii ya wazee wa Karamojong wanarudi nyumbani baada ya kuzindikisha wafugaji na kuwaelezea njia zenye usalama kwa mifugo kutumia. Iriama Anthony,34, anawaongoza akiwa mbele yao ambaye pia ni mkuu wa kaya ya Manyatta (Nyumba ndogo za Karamoja) kwa kijiji. Yeye ni mtu muhimu sana kwa kupasaha habari kuhusu wingi wa maji, malisho na idadi ya mifugo kwa eneo. Kutembea kwa mustari moja hivi ni utaratibu wa usalama kwao hasa wakati huu  wa uvamizi wa mifugo na migogoro imezidi kwa mkoa.

Na Stuart Tibaweswa

Kanda ndogo la Karamoja, eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda, inafahamika kwa hali mbaya ya  anga  kwanzia hali ya ukame wa mara kwa mara pamoja na  joto ya hali  ya juu  halikadhalika upepo zilizokauka na zenye joto kwa mwaka mfululizo. Kwanzia October 2021, eneo hili limekuwa na mabadiliko ya hali ya anga pamoja na mvua nyingi zaidi usio wa kawaida kunakiliwa kwa wailaya zote tisa; Abim, Amudat, Kaabong, Karenga, Kotido, Moroto, Nabilatuk, Nakapiripirit na Napak.

Hali hii ya anga zinakithiri mtindo wa maisha wakawaidi kwa wafugaji, haswa kwa jamii wakuhamahama waliowengi, ambao kwa miaka nyingi wanategemea mifugo kwa hali yao ya Maisha. Mvua kubwa za hapa na pale pia zinasababisha mmomonyoka wa udongo na uharibifu wa ardhi, ambazo zimechangia  kwa mazao nduni na ukosefu wa chakula Karamoja. (food insecurity in Karamoja)

“Badiliko la Misimu”yaadhirisha jinsi Uganda jamii ya kuhamahama na mifugo waliosalia wanaangaika kutafuta maji  huku mabadiliko ya tabianchi yakizidi kuathiri hali yao ya kawaida maishani kwa ukanda mifugo. Mnamo Oktoba 2021, nilifunga safari ya masaa nane kwelekea mji wa Moroto, kwa siku nane niliwafuata kikundi cha wafugaji wakiendelea na shughuli yao ya kila siku.

Nilifunguka macho kwa sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kwa Kanda hilo. Maisha ya Karamojong ni tofauti sana na vile mimi au wengi wetu wamezoea.

Wanaishi kwa nyumba ndogo-ndogo “kraals” au boma ndogo iliyozingirwa kwa ua yenye miiba na mbao kuwalinda kwa uvamizi na wanyamapori wanaoweza kuvamia mifugo yao.

Asubuhi na mapema saa kumi na moja (saa 11), nililazimishwa kuamka sababu ya sauti kubwa ya milio ya mifugo. Vijana wa kiume kati ya miaka 6 hadi 10 ndio wanakama ngombe, na inastaajabisha vile wanavyofanya kwa haraka mno.

oLcD1H3GVqKHdv206GSFMKqLtSbF6Gs 01i1Hf0CKjk6pIda8oyjbdKKVM GEx2N35nhvHuGrLDHKdtJaZFnRpNMOhAizbT igNsELtd0XRCid4iJ9TKtxseNFGtGe6uB6wWx Uh
Peter Lemukul, 5, anakama ngombe mmoja wa babake hapa kijijij cha Ariamao, wilayani Nabilatuk. Ni desturi yake kafanya hivyo kila siku asubuhi na jioni pamoja na ndugu na binamu wake.

AjsC7ZCG 7y2ACvWIBibfD1K1Z1ZkX3Ng2PnO6zdKhUH6mnU6PTf1Er 1JqpYiI06MaNPT9vRf31h

Saa moja asubuhi, kwa Kijiji cha Ariamaoi, wilaya ya Nabilatuk, Angelle Peter na wenzake huketi pamoja kuota jua huku wakisugua meno kwa vijijiti wakiwa na mazungumzo. Wakati mwingine  moja, walikuwa wakijadiliana kuhusu njia mbadala wakaotumia na mifugo yao baada ya kupashwa habari ya uvamizi na kikundi cha wavamizi eneo hilo. Nilistuka na kutishika nilipotafsiriwa mazungumzo yao, hii ni kulingana na ukosefu wa usalama wakati huo.

cY1PLSFVsUCpU1pS QXOpW2tdmcXTWCzKBtrmyOEbBgAzagyAZJvHyceOVeoKHMOXTitAsJZNE8kHnamjq5ETVmfQaA9uqScldLgGmS3xBRle Drg4WY3F1NvVtZLy clr2gR5E1

Wakati wa saa nne za asubuhi hivi, na umande umekauka, wafugaji walianza safari pamoja na mifugo yao, wakibeba vibuyu vya maji ya kunywa kwa safari ndefu. Yakustaajabisha, vile msimu ulikuwa ni wa kiangazi, wafugaji wa Amudat walikuwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi siku chache zilizopita. Hivyo basi njia ngingi za kuelekea malishoni hayakupitika.

Msimu wa Kiangaza na Mvua

Mnamo Oktoba 2021, ubashiri wa kiangazi, Amudat, Nakapiripit na Nabilatuk waligundua mapema  mvua ngingi, ijapo wilaya za Kotido na Kaabong walipokea  mvua kighafla. Mimea ndogo ndogo yaliota wakati wa mafuriko ya kighfla yalishuhudiwa wilaya za Kotido, Amudat, na Nabilatuk.

b6BgFeSRREyOBGPHwUjVlUmEuCt0Vwa4q3GolSpf0Qo 9TSxjYNjhYQFYGkltc4ROyl2SUj8RSon3c VNuTQVxn c3hKdq940qDsf3

Baada ya mvua nyingi kunyesha usiku uliopita,wafugaji wa Amudat huondoka na mifugo yao kupitia barabara lenye tope kutafuta nyasi. Kwa sababu ya mvua nyingi, barabara nyingi za kuelekea malishoni huwa hazipitiki. Mvua nyingi pamoja na mafuriko huharibu mimea.

QnwbfB6 zfj5xrMmvEaBLHYoS9rgexcgAGwhrpc2uNexI6tH LNmOoU7OSLAiF

 Kwa sababu ya mvua za kighafla, mito mingi hasa ya wilaya ya Amudat, ilionekana ikiwa na maji upande moja ilhali upande mwingine ikiwa imekauka.

6R VgUVZl1zl23NXUS4gJWfUSX2rXF1Z9eZCW cgmdMitny6I4B5VtUptU1m1iYyVPrHt9mdUNMSUKjvtlQWuXIxMtkPmfoDIjzCQdMYHkCQae3RuG3zkUyFR LPGtX26FsMRGE2

Mito mingi wilayani Amudat ilikuwa na maji mengi sana.

2brbfrlT GTAogTcF80pA4faWynm 4dejqi0 hS0Nu6 tHsEHSsz7AaQlSJHTEolQ5kgH dlH 8cirucyPzA8GDDRQR1IbPFSa9z2IeHzyUliZJkqj7Dg2rNmfW6W2r1mNge4OtF

Mfugaji mmoja wa kuhamahama wa Karamojong ajiituliza mwili wake na maji ya mvua iliyonyesha usiku uliopita wilayani Amudat. Wakati wa kiangazi, hali ya joto (temperatures)  hupanda hadi kiwango cha 40°C, lakini kwa wastani ni karibu 29°C wakati wa mchana.

2xVx5 vsWvLmVV3kYVkLBFw1g9o2oIB5UahtvW7zhipLStTF1GB8oNY8I5 yHIGlo08hFR2dicMK8Fblbknnd6aednPYh82bV7PfL9Ec27gXgZKT0q WDiZ YKuUpxeYm 8TUs7G

Sio maneo yote ya Karamoja hupokea mvua aina hii. Mto Omaniman, mojawepo wa mito ndefu sana na uliyokuwa na maji ya mwendo kasi kupitia wilaya Kotido, uliachwa bila maji wakati wa msimu wa kiangazi mwezi wa Oktoba. Mismu wa mvua au wakati eneo la Kotido hupokea mvua, mito hufurika kwa mengi ambapo sazingine yasababisha maafa ya watu na mifugo.

 ‘Wafugaji waliojiondoa’

Mnamo 2014, Karamoja iligaramia takriban asilimia 20 (about 20 percent) ya mifugo wote wa Uganda. Hali ya hewa usiotarajiwa pamoja na mvua ya mara kwa mara imechangia kwa wafugaji wengi kujiondoa, hayo ni kulingana Mathew Lumwinyi, mzee wa wilaya ya Moroto. Wafugaji wa hapo kitambo walianzisha ukulima wa mimea au biashara ndogo-ndogo, lakini walikuwa na changamoto wa ujuzi kwa kilimo. 

Wengi hawakutarajia kulima mwezi wa Oktoba 2021 wakitarajia kiangazi, hivo basi  kuongezea hali duni ya chakula (food insecurity in the region). Kulingana na mzee Mathew,  Lumwinyi, wilaya ya Kotido pekee, Wakaramojong waliokuwa wakiwauza mifugo wao waliongezeka hali usiokuwa wa kawaida hapo awali,hii ni kutokana na hisia yao na mifugo hata kufanya uuzaji wa mifugo kama mwiko.

AEbVqpVI rii25nbbuGSy3n JfHm6RD

Umati wa wauzaji na wanunuzi katika eneo la mbuzi na kondoo kwa soko ya mifugo ya Kanawat, wilayani Kotido. Zaidi ya mifugo 200 wanauzwa kwa siku moja hapa sokoni. Wafugaji hutumia pesa hizo kununua chakula wakati wa kingazi kirefu.

“Wakati huo, ningeuza ngombe moja kati ya 600,000 UGX ($171) and 1,200,000 UGX ($341). Wakati wa mvua, bei ingeongezeka hadi hata mara mbili kwa ngombe mkubwa,” James Okono, mfugaji wa kuhamahama  wilayani Kotido.

iL y6wlyFgLXqe1Uu7R8NM22HMHuLa3UTthfbLeqZvRqPcZRfiXDuC1zrAMQW9ERR6M507GAuRDYi6oigqxUL89ISQQI0ftnXYj EERJRHtXOu2yCpiiFGFp011Oq

Wafugaji hukaridia na kutadhmini hali ya mbuzi kabla ya kuuza kwa soko la mifugo ya Kotido. Baadhi ya mifugo wanaouzwa that (livestock sales in Karamoja)Karamoja bei hutegemea  msimu.Wakati wa mvua nyingi, wanunuzi hukubali kununua mifugo kwa  bei ya wauzaji. Kinyume na wakati wa kiangazi ambayo wananunua kwa bei ya chini au nafuu kwa maana mwili wa ngombe huwa umepungikiwa kwa sababu  ya ukosefu wa lishe bora.

Mvua nyingi za rasharasha, lakini uchache wa maji?

Wafugaji wakuhamahama wa kanda ndogo ya Karamoja hutegemea maji sana. Kwao maji ni rasilimali mojawepo muhimu kwa kuendeleza maisha ya mifugo yao; lakini bado hayatoshelezi mahitaji yao ( insufficient supply )hasa wilaya za Amudat na Kaabong.

Hali mbaya ya udongo umechangia kwa ukosefu wa maji. Hii Kanda ndogo udongo wake unauchache wa kaboni kwa mchanga, ambayo husaidia kushikilia udongo na Kuhifadhi unyevu. 

Ingawaje kuna mvua nyingi isiyo ya kawaida, bado kuna ukosefu wa rasilima ya maji kwa matumizi ya nyumbani. Mifugo wanaweza wakakunywa maji ya juu ya udongo, sio kama bidadamu wanaoweza adhirika kwa magonjwa.

vwQQu4jGKRZr4yvHm8D6e6isI4pp5xSizPCrl207VZX2RlGrvmypOapt DthQfWau3vlsik7POuiKbLCSTx1TS89C f6gjowW 47j5cty9CSYNaCUTj2 FiTwAs

Katika wilaya ya Kotido, mifugo wamevuka kwa ukingo wa mto uliokauka. Baadhi ya mito wilayani Kotido imekauka licha ya mvua nyingi za zilizotawanyika. Siku hizi, wafugaji wanalazimika kutembea kilomita 30 zaidi ili wapate maji ya kutosha  kwa mifugo, hasa kwa wilaya ya Kotido.

Shifting Seasons 13

 Wilaya ya Kotido, mvulana wa Karamojong anachunga mifugo wake. Mto huu ndio wa kwanza kwa mifugo hawa kupata maji siku hii baada ya kutembea kwa masaa manne. Siku hizi ni desturi kuwaona vijana wa Karamoja kati ya umri wa mwaka 6-15 wakiwa malishoni hasa kwenye maeneo ya malisho karibu na Moroto na Amudat. 

1s7grDu06M7lwdXykiSx8j

Wilayani Amudat, kisima cha jamii kimeadhirika na mafuriko ya maji ya chini.  Visima na mabwawa ndogo-ndogo yanatumika sana na mifugo wadogo kama mbuzi na kondoo halikadhalika kwa maji ya nyumbani. Wafugaji wengi huteka maji ya kunywa kwa visima kama vivyo vilivyo kwa hali duni na  vimeadhirika kwa maji chafu ya mvua, ambayo husababisha magonjwa kama kipindupindu (cholera)na homa ya matumbo. Maji yaliyotuama, ambayo ni mazingira nzuri kwa mbu,yamechangia kwa kusababisha ugonjwa wa malaria, hasa kwa watoto(malaria, especially among children).

KOfUoDZuMqJ0bhPmbnSwgZuJvKaXIFsuM4wSV4JM2g4e2EuLV fWcvBuxCKbQrL7U mPAQAcqSjsDPqBKvR2JG9x1y69 qJCxfHA bnz1640oT9o0O F vt2IqTfvDjuZgwBHOnn

Mvulana wa Karamojong achimba shimo la maji safi kwa ufuo wa Mto Loidiri. Mvulana huyu pamoja na rafiki wake walikuwa malishoni na mifugo lakini  wakatulia kwa mto kutafuta maji. Baada ya kufikia maji kule chini, walimwaga maji ya juu, huku wakiacha maji safi yatulie kwa sekunde kadhaa badaye .Binu hii imewasaidia wafugaji wengi kupata maji safi ya kunywa isio chafuka.

fPBkDGzDEixrpRbF6JKMTIYy0vQs3 22 VJ1ahSyd3hiGjdy2Vt4R8HhVn89r EpEdoNsnFtAs4JgXU nievGILvpRhY8LP2Bj0szJ sVWotKhvBhpvpmRkgqEuvl6JAg3lVNvCG

Mwanamke huyu anafua nguo zake mto Ajijim wilayani Nabilatuk. Kwa sababu ni msimu wa kiangazi, misingi ya vyanzo vingi vya maji kwa eneo hili vimekauka kama visima na vingine vingi. Watu wamehamia karibu na pahali pana maji mengi  na wanaweza wakapata ya matumizi ya nyumbani. Kwa mfano, kwa Nabilatuk mtu binafsi anaweza akahifadhi maji aliyeteka kwa kisima au ya mvua yawe ya kunywa na kupika, kisha atumie maji ya mito kwa kuwapa mifugo na matumizi nyinginezo nyumbani.

Dalili ya hali mbaya ya njaa

Baada ya siku refu ya matembezi, tulipiga kambi usiku kwa kijiji cha Ariamaoi, wilaya ya Nabilatuk.  Kikundi cha Karamojong wanajiushisha kwa mazungumuzo za usiku  huku wakikunywa pombe ya kienyeji. Vile niliandamana nao mcha kutwa na pamoja na mifugo wao, kutazama kwa makini sana hawakula chakula chochote mbali na matunda mwitu na maji- maghala yao hayakuwa na kitu.  Usiku wanakunywa maziwa huku wakitafuna mbegu za alizeti.

LKQPSVp1Uj8Wd4 OGbFVjU8V 04pR8fxTE6Ov5hZhmupMRMbrX222UNxpA O3c8w9mx6lEsD0eYMVpHbUKzOSpudvaQZc cx4ARpPU4km0EzKUnXkn8HeEKF8Qz8ngfqe lTbtdF

Ruth Nakwang, mkaazi wa kijijij cha Kakwakou, wilaya ya Kaabong, aonyesha mbegu zilizokauka ambazo huchemshwa kuwa supu kisha kuliwa kwa mahindi. Ruth na jamii yake huzitafuna kando kwa ajili mahindi yao yameisha.

Kulingana na utafiti wa 2014 (2014 study) na Dk. Antony Egeru, mwanaikolojia wa kibinadamu and mtafiti wa shehemu zolizokauka, kunayo uwezekano wa asilimia 70 ya mimea iliopandwa Kata ndogo ya Karamoja hayatafanya vizuri kwa sababu ya mvua usioweza kutabiriwa.

Hii kimsingi ina maana kwamba jumuiya ya jamii wanaishi kwa hali ngumu kwa kuwa mipango yao yote haifui dafu, hivyo basi idadi kubwa sana wanaachwa kwa hatari ya njaa na ukame. 

Julai 2021 uchambuzi wa ripoti na IPC (report analysis by IPC) inaonyesha kwa jumla, idadi kubwa ya watu wanaokosa chakula kwa eneo hili imezidi kuharibika, yameongeza kwanzia asilimia 27 mwezi Juni 2020 hadi asilimia 30 mwezi wa Mach 2021. Hali hii imewaacha watoto wengi kwa familia katika hali ya itapiamlo kwa ukosefu wa chakula cha kutosha hivyo basi husababisha kuongezeka kwa uziwizi wa mifugo na uvamizi.

C7U7XwIIGsGATDtn GlH 5py5EVOff9fGh0e8dBUwTN44nMk287fKvVpTSIwqxF301edqGs1cXbfYZc42uzONEGvIQQJs7NhLlaYIShOC 3WeQSDfpXd5E32O2UWycc6fkykLg5P

Owalinga Lawrence, 16, anakama ngombe mmoja wa jamii baada ya kurejea kwa kraal, Kijiji cha Ariamaoi, wilayani Nabilatuk. Kwa jamii ya kuhamahama, ni vijana wa kiume ndio kukama ng’ombe na kwenda malishoni.

Kuelekea  suluhisho, kwa wakati usio na uhakika

Kati ya changamoto nyingi, rasilimali nyingi za maji and mifumo mingi imetekelezwa kupitia serikali, idara usio wa serikali, na juhudi za jamii kusimamia mgogoro wa kutofautiana kwa hali ya hewa.

Angalau kuna vyanzo sita vya maji kwa eneo hili, ambavyo hutoa maji ya matumizi kwa watu na mifugo: visima, vinu vya upepo, mabwawa,mabwawa ya bonde, kando ya mito, and mito.

Wakati wa kiangazi, watu huchimba mchanga hadi chini ya mto kufikia maji.

Kwa miaka mingi, mfululuzo ya mabwawa ya mabonde (series of valley dams) yamejengwa na serikali ya Uganda ili kuhakikisha maji yanaendelea kutolewa kwa mifugo na matumizi ya nyumbani. Hivi viwango vikubwa kwa mabwawa makubwa ni pamoja na Arecek-Nakicumet kule Napak, Kobebe kule Moroto, na Lomogol kule Kotido, yote yanasaidia sana kwa eneo hilo, hasa Moroto na Napak penye mabwawa muhimu haijawahi kauka tangu ujenzi wao.

JBxrttGbwgM69c7EfzuvB6O88ktT YFXm8EnXbuqgzl4klG9gdVRW3UcJec uoFD Eh4jaGEIdFulXTCDzNJvcsish53nj3YinDkNfypQt2p8dQFAXs pMkOZfyuKH92sc1 VV1j

Bwawa la maji ya Arecek-Nakicumet wilayini Napak, ambalo lilijengwa kati ya 2007 na 2001. Kwa usuli wake ni mlima Napak, ambayo husambaza maji kwa mabwawa enye kina chake ni mita 6 ambayo kwa sasa uhudumia mahitajo mbalimbali yakiwemo unyunyuzi, ufugaji samaki, na husaidia wenye mifugo na mifugo wao hasa wakati wa kiangazi.

Shifting Seasons 21

Katika Nakicumet, wilayani Napak, kikundi cha wakulima wanafanya kazi kwa shamba la kitungu. Pia wanalima pilipili na nyanya, ambayo hutegemea unyunyuzi wa maji kutoka bwawa la Arecek-Nakicumet. Kulingana na wakulima, shamba ndogo limesaidia jamii wengi majirani hasa wakati wasiokuwa na chakula kabisa.

“Wakati wa kiangazi, mfumo wa unyunyuzaji maji kwa matone hayasaidi kwa ukulima wa mimea aina tikitimaji. Mvua isio imara imesababisha tikitimaji kudhofika bila kua,” asema Sire Micheal, anayesimamia vifungua vya shamba.

U4tPWayfTBb1Bbzzd6FuLzg

Msimamizi wa bwawa la maji ya Arecek, ambaye pia ni kaimu mtekelezi wa tangi chini ardhi, anashuka baada ya kufungua mabomba ya maji kuyaruhusu yaingie kwa  mkondo  mkubwa ili wananchi wachote. Wakati wa mvua nyingi, kiwango cha maji huchunguzwa isizidi mita 7. Maji huporomoshwa kwa visima vidogo kutoka kwa mabomba ya tangi chini ardhi kudumisha kiwango cha maji.

Bado, tathmini ya 2021 (assessment) ya mabwawa 26 yaliyoka Karamoja ilipatikana ya kuwa licha ya mabwawa ya Kobebe na Nakicumet-Arecheke, mabwawa yingi yalikuwa yanakauka: Maji kwenye mabwawa mengine hayenge yalikuwa chache sana kutosheleza msimu wa kiangazi, na ubora wa maji ilikuwa duni, halikadhalika na mchanga. Haya yalitokana na watu kunywesha mifugo wa moja kwa moja ndani ya bwawa badala ya kutumia vijaa vya maji vilivyo tengewa mifugo, ambavyo vinakaribia kuharibika, utafiti ilidhibitisha.

YznzfTgnaZmDmQqC2WmLjhkXepW iuOF8W9ow iefyuvv2F7WB5i9 rZuEPZU ChdTseaQpCsON6iKpGYXAWWAMvB4Yo6dfHw

Kijiji cha Ariamaoi, wilayani Nabilatuk, jamii ya Karamajong wamesimama kando ya bwawa lililojengwa na binadamu. Kwa kutumia majembe na vifaa vinge, walichimba bwawa hili kwa kujitairisha kwa kiangazi wa muda mrefu lakini hawajatumia kwa sababu eneo hili linapokea mvua. Kulingana nao, bwawa hili lenye kina cha futi 5 lilijazwa kwa mvua za awali na linaweza kusitiri maji kwa muda wa miezi miwili wakati wa kiangazi kirefu.

 “Wanaume wote eneo hili wanakuja pamoja ili tuchimbe bwawa. Tunatumia maji haswa wakati wa msimu wa kiangazi,” asema Ariama Anthony(kulia), kiongozi wa jamii.

Habari hii imechapishwa kwa usaidizi wa InfoNile na ufadhili kutoka IHE-Delft Water pamoja na Development Partnership Programme. Uhariri na taswira za data imefanywa na Annika McGinnis.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts