Sharon Kiburi & Caroline Njoroge
Wakazi wa Baringo Kaunti iliyoko bonde la ufa nchini Kenya sasa wanapata ahueni baada ya mradi wa maji wa bwawa la Chemususu kukamilika. Ukiwa unakaribia Counti hii ukitokea mjini Nakuru, unakaribishwa na uwanda wa kijani na pembeni mwa barabara kuna bango linalosomeka “SASA UNAINGIA KASKAZINI MWA DUNIA” na eneo hili limeainishwa kuwa eneo kame lenye vichaka na magugu yenye miiba mikali ambayo wakazi wanaviita Mathenge au kwa lugha ya kitaalamu Prosopis juliflora.
Ukiwa Baringo unaweza kujihisi kama upo nchi nyingine kwani wakazi wa hapa ni wepesi kufahamu wageni wanaohitaji maelekezo.
Bonde la Eldamani ni moja ya maeneo ambayo yana utulivu wa kutosha na tunaarifiwa ya kuwa wakazi wa mji huu wanafurahia kujinasibu kuwa eneo hili ni nyumbani kwa mabingwa na Kenya inapofanya vizuri kwenye uwanja wa riadha kimataifa wakazi wa hapa humwaga sifa zote hizo kwa eneo lao ambalo ni kitovu cha wanariadha wengi. Eneo hili pia ni maarufu kwa kilimo na biashara ya maua ya kimataifa.
Ukiwa unaelekea katikati bonde la Eldama ambapo kuna mji wa Eldama unakutana na ofisi za kampuni ya maji cha Chamsusu inayosimamia mradi huu wa maji.
Tukiwa kwenye ofisi za Kampuni ya maji ya Chamsusu tunakutana na bwana Samuel Koech ambaye ni mkurugenzi mtendaji na anatathmini ya mradi kufikia lengo la kuwapatia huduma ya maji ya kuaminika wakazi wa hapa. Anasema “ Mradi wa maji wa Chamsusu una thamani ya shilingi za Kenye Bilioni tano na umegharimiwa na serikali na unakaribia kukamilika ukiwa na hifadhi za maji 30 kwenye bonde la Elma na wilaya za Mogotio, Baringo, na Rongai na mradi huu umekamilika kwa asilia 70%.”
Maji haya yanapatika kutoka kwenye bwawa la kina cha mita 45 likiwa na mita za ujazo 11.2 million na mradi huu ulizinduliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta mnamo mwaka 2017 na unatazamiwa kukamilika ifikapo mwezi wanne mwaka 2020. Hata hivyo janga la korona lilifanya mradi huu kususua.
Kwa mujibu wa bwana Koech, mradi huu utakapokamilika, wakazi wa Baringo na Nakuru wanatazamia kupata maji safi na salama ya kutosha licha ya misimu ya hali ya hewa tatanishi iliyopo kwenye eneo hili .Kwa sasa kampuni hii inatoa huduma kwenye robo ya eneo linalotazamia kupata huduma kuzunguka eneo la bonde la Eldama.
Licha ya usumbufu uliotokea kutokana na janga la korona, ujenzi wa bwawa unaendelea kama ilivyopangwa na awamu ya kwanza ikiwa imekamilika na kufanya kazi . Awamu hii inasambaza maji kwenye bonde la Eldama na lengo ikiwa ni kuhudumia pia eneo la Mogotio.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa TALAFRICA, taasisi huru ya waandishi wa habari nchini kenya imeonyesha kwamba kazi usambazaji kwenye barabara inayoziunganisha Nakuru na Bonde la Eldama inaendelea kwa kasi na karibu hifadhi 30 za maji zimeshakamilika.
Tukiwa kwenye eneo la bonde hili , Bwana Koech anatutembeza kwenye maeneo muhimu ya mradi ikiwemo eneo la kusafishia maji na maeneo ya kuhifadhia maji.
Eneo la kusafishia maji linajikita katika kupunguza magonjwa yatokanayo na maji yasiyo salama ambayo yamekuwa yakiwaathiri wakazi wa maeneo haya kwa kipindi kirefu kutokana na matumizi ya maji kutoka vyanzo ambavyo si salama na sense ya mwaka 2017 iliainisha vyanzo vya maji kwa ajili ya familia 150,174 waliopo Kaunti ya Baringo kwa mujibu wa kanza data ya Idara fedha na mipango ya kaunti hiyo.
Bwawa linatazamiwa kumaliza kabisa tatizo la misimu ya upungufu wa maji na kubadili muundo wa hali ya hewa na kuchechemua uchumi wa wakazi kwenye kaunti zote mbili kwani wakati wa masika na mvua kubwa watapata maji ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kilimo.
“ Mradi ukikamilika tutakuwa na uwezo wa kusambaza maji kwa ajili ya matumizi ndani kwa wingi na tunatarajia magonjwa yanayotokana na maji yasio salama ambayo ni ya kawaida katika eneo hili yapungua , magojwa ambayo ni ya kawida kila msimu wa mvua unapowadia” anasema bwana Koech.
Zaidi ya hayo bwana Koech anatuhakikishia ya kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza majanga yote yametiliwa maanani na wa wakandarasi na wasanifu wa mradi huu. Wamefikiria makadirio ya hali ya hewa ya kaunti hizi mbili kwa siku za usoni.
Bwawawa hili ni mradi mkuu ulioibuliwa na serikali ya Kenya katika mpango wake wa maendeleo wa hadi mwaka 2030 lengo ikiwa ni kusambaza maji kwa wananchi ili kubuni ajira.
Mmiliki wa taksi wa eneo hili bwana Clapton Sichel anasema “ Mradi huu umeniwezesha kutitumia taksi yangu kusafirisha vifaa vya ujenzi na wafanyakazi hadi kwenye eneo la ujenzi . Fursa hii ilikuja mara tu niliporudi Eldama eneo ambalo ndipo nilipokulia na niliondoka mara baada ya kumaliza shule na kwenda kutafuta riziki sehemu nyingine”
Bwana Sichel anabainisha kwamba wakazi wengi wa eneo hili wamefaidika kwa kufanya kazi ndogo ndogo zinazousaidia mradi na pia bwawa limesababisha maji ya kutosha kupatikana muda wote. Kwenye eneo hili na uwekezaji huu umechechemua shughuli za kiuchumi hususan kwenye sekta ya ujenzi ambayo ilijihusiha moja kwa moja kwenye usanifu, uhandisi, na ujenzi wa miundombinu ya ujenzi wa vyanzo vya maji.
“Pia kulikuwa na fursa za ajira ambazo zimetengenezwa kwa wafanya kazi wasio na ujuzi zilizotolewa na watu binafsi ndani na nje ya jamii, jambo ambalo liliwawesha wakazi hao kupatia ujuzi kwa njia mafunzo kazini chini ya uangalizi na pia kufanyiwa majaribio” anasisitiza bwana Koech
Bwawa hilo limeleta manufaa kadhaa ikiwepo uwepo wa ujenzi wa barabara zinazotumiwa kupitishia vifaa vya ujenzi wa kituo hicho. Tunakutana na mkazi wa wa hapa Sebi Abudala ambaye anatuelezea madiliko na manufaa yaliyopatikana kutokana na mradi huu.
“Maji yamekuwa na manufaa kwetu licha ya tofauti iliyopo wakati mvua zinakipungua. Kabla ya mradi huu tulilazimika kutembea mwendo mrefu hadi maeneo ambayo yana visima vilivyo chimbwa atu binafsi na kununua maji kwa wamiliki wa visima hivi kwa bei ya juu sana”
Wanawake nao hawajaachwa nyuma, kwani na wao wanapata manufaa yanayotokana na mradi.
Janet mama wa watoto wa nne mwenye umri wa miaka ishirini mfanyabiashara ya hoteli anaelezea utofauti wa kuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya matumizi yake ya nyumbani
“muda wa saa nzima ambao tumekuwa tukiutumua kutafuta maji sasa muda huo tunautumia kwa kupika na pia usafi umeokeongezeka kutokana na uwepo wa maji”
Wakulima kwenye ukanda huu wamekuwa wakitegemea misimu miwili ya mvua kila mwaka na hakuna njia nyingine ya kupata maji isipokuwa kutegemea misimu hii ya mvua. Hata hivyo maji yanayotiririka kutoka bwawa la Chamsusu yamekuwa muhimu na baadhi ya wakulima wanaoshi maeneao yenye ukame wamefaidika na kwa mashamba yao kupata maji yanayomwagika kutoka kwenye bwawa hilo
Inafaa kukumbuka kuwa matumizi ya maji kwenye bwawa hili yatawafanya wakulima kutotegemea tena mvua za msimu kwa shughuli zao za kilimo na kujikita kwenye kilimo cha umwagiliaji na pia kuongezeka kwa usambazaji wa maji, uhifadhi wake na uvunaji hivyo kusaidia lengo la lililopendekezwa kitaifa la uvunaji na usambazaji wa maji la mwaka 2019, pia uwezo wa kukabiliana na misimu ya mvua isiyo na mpangilio unaoeleweka.
Zaidi ya hayo uwekezaji kwenye uhifadhi wa maji, kama ilivyo ainishwa kwenye sheria zilizopendekezwa utaongeza ustahmilivu wa wakulima katika kukabiliana na misimu ya mvua isiyo ya uhakika.
Bwawa hili linakamilisha mipango iliyopo ya serikali ya kuongeza uzalishaji kwenye sekya ya kilimo. Mfano ni ule wa sekta ya utafiti katika kilimo iliyotengewa kiasi kikubwa cha rasilimali ikilinganishwa na sekta ya maendeleo ya mifugo na uvuvi kati ya mwaka 2017 mpaka 2021, ambapo kiasi cha juu kilichotolewqa kilikuwa dola za kimarekani bilioni nne zaidi.
Bwana Koech anaendelea kutanabaisha ya kuwa maji ni bidhaa adimu na nyeti kwenye maeneo yenye ukame na bidhaa hii inaweza kuhatarisha usalam wa Taifa na kuzua wasi wasi wakati jamii za wakulima zikikabiliana na mgogoro mkubwa unaotokana na bidhaa hii kutokana tishio la ukame la mara kwa mara. Kwa hiyo ni ukweli usiopingika ya kuwa unapotokea mradi mkubwa wa miuondo mbinu ya maji kwenye eneo lolote lile kunaambatana na tishio la usalama na kuzua migogoro kwenye jamii.
Lakini ni muhimu kujua ya kwamba kumekuwa na ushirikiano wa kutosha kati ya Taifa kwa ujumla wake na wakazi wakati wa ujenzi wa Bwawa la maji la Chemususu ikiwa ni pamoja na kuangalia mahitaji ya jamii inayofaidika na mradi pamoja faida za kiuchumi zitazotokana na bwawa hili.
Kwa mujibu wa Laura Muniafu ambaye ni muhandisi wa miundo mbinu anayeishi jijini Nairobi yeye anasema “ Ujenzi wa bwawa unategemea sana upatikanaji wa maji kwa mwaka mzima na wingi wa maji wakati wa masika, hivyo basi kufanya upembuzi yakinifu ni muhimu kabla ya ujenzi bwawa haujafanyika na vipaumbele vyote kupangwa.”
Anabainisha kuwa kufanya uchanganuzi wa rasilimali za pamoja ule uchanganuzi wa kihadrolojia, muundo wa ardhi, mmonyoko wa udongo na eneo la mavuno na hifadhi linalopendekezwa na anasisitiza kuwa ni muhimu kusababisha vichocheo vya uhifadhi kwa kila eneo la bwawa ili kuhakikisha matumizi ya aina mbalimbali ya maji yanawezekana na kufikia lengo bora la utendeji kazi wa hifadhi zenyewe unakuwa bora.
Inatarajiwa kuwa ujenzi wa bwawa hili la maji utakidhi mipango ya kimataifa kama vile mpango wa ushirikiano wa matumizi ya mto nile mpango ambao ulianzishwa mwaka 1997 ambao unaziruhusu nchi zinatumia mto huu kujenga mabwawa na kuanzisha miradi inayohusika. Mhandisi Laura anasema ili bwawa hili liweze kudumu na kugharimiwa katika ngazi ya kitaifa inapaswa kuzingatia sheria zilizoainishwa n Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira kufanyia tathmini kila sheria.
Anaendelea kusema” Ujenzi unapaswa kufuata sera za ulinzi wa mazingira za Benki ya Dunia zinazotaka taarifa ya ushiriki wa umma, matukio na utekelezaji wa usimamizi mipango wakati wa uhamishaji watu wakati wa uhamishaji makazi ya watu hao”
Makala haya yametolewa kwa usaidizi kutoka kwa InfoNile na JRS Biodiversity Foundation