Na Lina Mwamachi, Sifa Radio, Taita Taveta Kenya
Ozi ni lokesheni inayopatikana Sub county ya Tana Delta, divisheni ya Tarasaa kaunti nambari nne Tanariver, ikiwa ni kati ya kaunti sita zilizoko mkoa wa pwani.
Idadi ya watu wa ozi inakadiriwa kuwa watu 4,500 ikiwa ni sawia na nyumba kati ya 1000 na 1500.
Wakaazi wa Ozi ni wakulima wa mpunga, uvuvi, na utalii., ila ukulima wa mpunga unachukua asilimia kubwa eneo hili. Wakulima wa Ozi walifanikiwa kuvuna mpunga kwa wingi kutokana na uwagiliaji asili au natural irrigation.
Ungana nami lina mwamachi katika Makala maalum Umwagiliaji wa asili au Natural irrigation, ulivyoongeza zao la mpunga licha ya ujio wa gonjwa la Covid-19 Ozi,Tanariver. Makala haya yamewezeshwa kwa ufadhili wa shirika la Info Nile pamoja na JRS Biodiversity.
Wakulima zaidi ya 1000 wa Ozi, walipata mavuno maradufu licha ya changamoto zilizoletwa na ujio wa gonjwa la Covid-19. Said Nyara ni mkulima wa mpunga Ozi.
Afisa wa kilimo kaunti ndogo ya Tana River Zilambe Kombo anasema wakulima wa OZI wanategemea unyunyizaji wa asili yani natural irrigation, kwa mwaka mara mbili na mavuno mazuri.
Mabadiliko ya hali ya hewa ni Dhahiri shahiri kuwa yatakuwepo nasi kwa mda mrefu, Je mpunga usipofanya vizuri wakulima wafenyeje?
Huyo ni msimamizi wa miradi za shirika la Nature Kenya Tana Delta Odera George. Akielezea jinsi wakulima wa ozi walivyofanikiwa kuvuna mpunga kwa wingi, wakati wa covid-19, ikilinganishwa na misimu ilyopita.
Msimamizi huyo anahoji kuwa wakulima Zaidi ya 180 walikuwa wameomba mbegu mwaka 2019, ila wakati wa covid-19 idadi ya wakulima iliongezeka hadi wakulima 247.
:Anasema wakulima Ozi walifanikiwa kuvuna mpunga kwa wingi ikilinganishwa na miaka mingine, sababu kuu ikiwa wakaazi wengi wa Ozi waliokuwa mijini walirejea nyumbani kwa ukosefu wa kazi uliosababishwa na janga la Covid-19.
Odera anashikilia kuwa wakulima Zaidi ya 120, walichukua mbegu ya mpunga mwaka 2019, na idadi hiyo ikongezeka hadi wakulima 240, wakati wa Covid-19.
Odera anasema mwaka 2019, wakulima 126 walijotosa kwa ukulima, lakini chagamoto za muingiliano wa maji yam to nay a baharini, wakulima 91, pekee walifanikiwa kuvuna kwa ujumla mpunga kilo 78,897, ambao ulitoa kilo 51,284 za mchele baada ya kuukoboa, ikiwa ni kima cha shilingi, 3, 076,983.
Aidha mwaka 2020, wakulima waliongezeka na kufikia 245, waliofanikiwa kuvuna mpunga kilo 122,500, ambao baada ya kuukoboa ulitoa kilo 79,625 za mchele, uliowapa shilingi 4,777,500.
Wakulima hao walipata mafanikio hayo licha ya kuathiriwa na muingiliano wa maji ya bahari na ya mto tana ambayo ni changamoto kubwa Ozi.
Anavyoelezea Odera, unyunyizaji asili au Natural irrigation umekuwa wa faida na wa kipekee kurahisishia kazi ya wakulima.
Anavyoelezea msimamizi huyo ni kuwa Ili kujikwamua katika shida ya maji chumvi kuingia katika mashamba ya mpunga na kuharibu mazao, shirika la Nature kenya likishirikiana na shirika La KALRO wameanzisha mikakati ya utafiti wa mbegu spesheli itakayostahimili maji chumvi na maji tamu ili kuimarisha na kudumisha zao la mpunga sehemu hiyo ya Ozi. John Kimani ni mtafiti kutoka shirika la KALRO Mtwapa.
Kimani anasema wataanza kupeana mbegu ya mpunga itakayovumilia mchanganyiko wa maji tamu na maji ya chumvi kutoka baharini, sehemu ya Ozi.
Aidha anasema mbegu inayotumika sasa ya EATER 310 pamoja na pishori 217 au basmati 370 ni mbegu nzuri na inazaa haraka na kwa wingi, na, imewezesha wakulima kuvuna kwa wingi.
Mtafiti huyu anashawishi wakulima wa mpunga sehemu za pwani kukumbatia mbegu mpya ya KOMBOKA inayotoa mazao kwa wingi, msimu unaokuja.
Kulingana na mtafiti huyo wanashirikiana na mashirika ya kibinafsi, serikali na wadau wengine ili taifa la kenya liweze kuzalisha mpunga kwa wingi kwa manufaa ya kuuza na kupata pesa na chakula.
Halmashauri ya kitaifa ya takwimu za kiuchumi (Kenya national Bureau of Statistics on 2021 Economic Survey), inaonyesha kuwa kenya imekuwa ikiagiza mchele kutoka mataifa ya nje kama Pakistan, India, Tanzania, Thailand and Myanmar.
Mwaka uliopita shirika la KALRO lilishirikiana na Korea-Africa Food and Agriculture Cooperation Initiative, liliboresha uzalishaji mpunga mwambao wa pwani, kwa kuwapa mbegu zilizopasishwa kwa upanzi pamoja na kuwashauri kupelekea mbegu kwa idara ya ukaguzi wa mbegu KEPHIS. Kenya Plant Health Inspectorate Service (KEPHIS) for certification.
Kimani anasema hatua hiyo imewezesha uzalishaji wa mbegu zilizothibitishwa ukanda wa pwani kwa mara ya kwanza.
Anasisitiza kuwa taifa la Kenya lina uwezo wa kuzalisha mpunga wake kutoka sehemu za Taita Taveta, Ozi na sehemu za juu kama vile Mwea, bila kuagiza kutoka mataifa ya nje, ili fedha hizo ziweze kutumiwa katika shughuli nyingine za kuinua sekta nyingine, kiunua viwango vya elimu pamoja na miundo misingi nchini.
Makala haya kuhusu umwagiliaji asili ulivyoongeza zao la mpunga Ozi, Tana Delta licha ya Covid-19, yameandaliwa nami lina mwamachi sifa fm Voi na yamewezeshwa kwa ufadhili wa shirika la Info Nile pamoja na JRS Biodiversity.