- Je tunafahamu umuhimu wa ndege katika mazingira yetu?
- Je tunafahamu aina nyingi za ndege wanaopatikana duniani kote?
- Lakini je unafahmu kuwa kuna ndege wanaopatikana kaunti ya taita taveta pekee na hawapatikani kwingineko duniani?
Lina Mwamachi
Ndege aina ya Taita Apalis kwa jina la kisayansi Apalis Fuscigularis, ni ndege anayepatikana Kaunti ya Taita Taveta nchini Kenya pekee na yuko hatarini kuangamizwa.
Jambo hili limesababisha kutengwa kwa shamba la ekari 15, sehemu za milimani kaunti ya Taita Taveta kama makaazi ya ndege kuzaana na kuhifadhiwa.
Paul Gacheru ni msimamizi wa maswala ya sayansi na utafiti wa mazingira na ndege katika shirika hilo.
Aidha anasema ndege aina ya Taita Thrush anayefahamika kisayansi kama Turdus Helleri, yuko katika hatari ya kuangamia ikiwa mazingra hayatahifadhiwa wakiwa wamesalia tuu ndege kati ya 1000-1500.
Mwanzoni mwa mwaka huu 2021 katika siku inayofahamika kama Global Big Day, Kenya iliorodheshwa nambari 6 duniani kiashiria kuwa utalii wa kutazama na kuhesabu ndege umeanza kutiliwa maanani hapa nchini.
Kenya ilikuwa ya sita baada ya kurekodi ndege aina mbali mbali 817 nyuma ya taifa la Columbia, lililorekodi ndege 1,289, ikifuatwa na Peru, Ecuador, Brazil and Bolivia.
Kila mwaka tarehe 8 mwezi wa tano na tarehe 9 mwezi wa kumi husherehekewa siku ya uhamaji wa ndege ulimwenguni yaani World Migratory Bird Day, pale kila mmoja hupata fursa ya kutazama ndege kuwahesabu na kunakili majina na sauti zao, mahali popote alipo, zoezi linalofanyika tarehe 9 mwezi huu wa oktoba mwaka huu 2021, kauli mbiu ikiwa Imba, puruka, Paa kama ndege.
Kulingan na Nature kenya, siku hii ni muhimu kwa wanamazingira kubaini afya na mazingira yalivyo kwa ndege, kulingana na jinsi wanavyotapakaa na kupatikana.
Hayo yakifanyika himizo linatolewa kwetu sote kushirikiana kuwahifadhi viumbe hai kwa kuyahifadhi mazingira yao, kwa kupanda miti kwa wingi na kuwacha shughuli zinazoharibu mazingira, haswa ndege hawa Taita Apalis na Taita Thrush ili kuwavutia watalii zaidi kuzuru sehemu zetu za milimani tukiikuza hadhi na maadhari mazuri ya Kaunti ya Taita Taveta.
Hadithi hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye Sifa FM, Voi Kenya