Migogoro ya binadamu na wanyamapori Hifadhini yaibua ubunifu

Migogoro ya binadamu na wanyamapori Hifadhini yaibua ubunifu

Na Linah Mwamachi

Katika kaunti ya Taveta nchini Kenya, mitafaruku katika ya wanyamapori na binadamu imekuwa ikijitokeza kwa miaka mingi mtafaruku mkubwa ni wa kugombania bidhaa adimu ambayo ni maji.

Mabadiliko mabaya  ya hali ya hewa  yameathiri kwa kiasi kikubwa tabia na taratibu  za wanadamu za kila siku katika eneo hili hasa pale wanadamu wapolazimika kuvamia misitu kwa ajili ya nishati ya kuni, mkaa na pia mbao.

 Huku mabadiliko ya hali ya hewa yakiendelea kuzifanya jamii hizi kuwa fukara, wanajamii hawa baadhi wanajiingiza kwenye ujangili wa wanyamapori na kusababisha vita kubwa kati ya wanyamapori na wanadamu kwenye mbuga za wanyama nchini Kenya .

Wataalamu wanasema mabadiliko haya mabaya ya hali ya hewa ndiyo sababu kuu ya ujangili na mtafaruku uliopo kati ya binadamu na wanyapori.

 

 

Copy of Elephants and Hippos Lake Jipe National Park Taveta
TEMBO NA VIBOKO HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA JIPE

Wanyama hawa  wanashindwa kupata malisho na maji kwenye hifadhi hasa kipindi cha kiangazi  kinapowadia na hivyo kuwafanya wavamie mimea ya mashambani .

Mfano mmoja  ni katika kaunti ya Taveta ambako wakulima kadhaa wamelalamikia  uharibifu unaofanywa na wanyamapori ambao wanaharibu vyakula na mazao mbalimbali.

Katika Makala hii ambayo inaripotiwa na Linah Mwambachi, inaelezwa kuwa jamii zinzoizunguka Hifadhi ya Tsavo nchini Kenya wamebuni njia nyingine ya kumaliza migogoro hii kati ya wanadamu na wanyama pori kwa kuanzisha miradi ya upandaji miti.

Miti hii inapokuwa na kukomaa inasababisha kuwapo na hali ya hewa inayo sababisha mvua na kuziwezesha jamii hizi kupata maji kipindi cha kiangazi kuepuka kuingia kwenye mbuga kutafuta bidhaa hii muhimu na kwa wanyamapori wanapata ahueni kwa kupata maji mbugani na wanaepuka kutafuta maji kwenye jamii zinazozunguka mbuga.

 

 

Mvua hizi pia zinasababisha ukuaji wa majani na miti kwa ajili ya malisho ya wanyam pori, na kuzuia uvamizi wa wanyama  kwenye mashamba na miti hiyo hiyo inasaidia upatikanaji wa kuni kwa wenyeji.

Wataalamu wa hali ya hewa wameupa kongole za dhati ubunifu huu na wanatoa wito wa kutolewa kwa elimu kwa jamii zinazozunguka hifadhi za nchini Kenya kutokana na ubunifu huu.
Mtaalamu wa hali ya hewa Collison Lorez na mwanasayansi wa wa hali ya hewa Oliver Kikogey kutoka ICPAC( Igad Climate Prediction and Application Centre) Afrika mashariki wanasema elimu ya umma kuhusu madiliko ya hali ya hewa na ubunifu kama huu ni muhimu katika kupunguza hali hii.

Sikiza ripoti kamili ya Linah Mwamachi kwa kubofya kwenye kicheza sauti hapo juu.

Hadithi hii ilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye Sifa 107.7 FM Voi, Kenya tarehe 27 Agosti 2020.

Hadithi hii ilitengenezwa kwa kushirikiana na InfoNile kwa msaada kutoka kwa Kanuni ya Afrika na ufadhili kutoka kwa Mtandao wa Uandishi wa Habari wa Internews na Earth.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts