Wahifadhi Kenya washindwa kulipa ardhi waliyokodisha kutokana na janga la COVID-19 linalohusishwa na kushuka kwa mapato ya utalii

Wahifadhi Kenya washindwa kulipa ardhi waliyokodisha kutokana na janga la COVID-19 linalohusishwa na kushuka kwa mapato ya utalii

Na Lenah Bosibori 

Janga la korona limeziathiri kwa   kiasi kikubwa  hifadhi za nchini Kenya.  Shughuli za kitalii kwenye mbuga ya wanyama ya Maasai Mara ambayo ni maarufu Duniani zimeshuka sana na kupelekea miradi ya uhifadhi kuwa hatarini kutokana na ukosefu wa fedha.

Hadi sasa Kenya imepoteza takriban asilimia themanini ya mapato yake yatokanayo na utalii, huku asilimia 90 ya mapato yatokanayo  na watalii kutoka nje ya nchi hiyo yakishuka tangu Machi wakati janga la kwanza la Korona liliporipotiwa nchini humo.

Shirika la Huduma za wanyama pori la Kenya (Kenya Wildlife Services) linasema kati ya mwezi Februari na Juni  mwaka huu, sekta ya Utalii ilipoteza takriban shilingi za Kenya bilioni 80 kutokana na kufutwa kwa safari za ndege kunakohusishwa na janga la korona.

Takwimu kutoka kitengo cha takwimu cha serikali ya nchi hiyo (Kenya National Bureau of Statistics) zinonyesha kwamba kiasi cha shilingi bilioni 167 kilikusanywa kupitia sekta ya utalii  mnamo mwaka 2019 ikiwa ni sekta iliyokuwa kabla ya janga hili kuibuka na ilikisiwa kwamba kiasi  cha shilingi bilioni 189 kingeweza kukusanywa  kufikia mwaka 2020 na mwaka 2021.

Wakati hifadhi nyingi zilizopo Mara zikijitahidi kuendeleza mikataba ya uhifadhi iliyosainiwa miaka 25 iliyopita, hifadhi zinatoa msaada wa kulinda wanyama na maisha  na tamaduni za wamasai zina changamoto kubwa inazozikabili katika siku za usoni.

Mtendaji Mkuu wa chama cha hifadhi za wanyama Pori nchini Kenya Bwana Dickson Kaelo anasema Kenya imepiga hatua kubwa ingawa changamoto zilizopo  ni nyingi. “Tuna changamato kubwa; kambi zetu nyingi zimefungwa na hifadhi zimeathirika wakati utalii ndio chanzo chetu pekee cha mapato kwa hifadhi zetu” anasema muhifadhi huyo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa njia ya mtandao ikiratibiwa na Wizara ya Utalii  na Wanyamapori.

Ingawa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya uhifahi ni kubwa, janga la Korona linatishia jitihada za miongo mitatu za kulinda urithi wa wanyama pori uliopo nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Chama cha Hifadhi za Wanyama Pori nchini Kenya, nchi hiyo imepoteza takriban asilimia 70 ya wanyama pori kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita. Chama hicho kinasema  hali hii inatokana na ukosefu wa nafasi na muunganiko, shughuli za kimaendeleo, matokeo ya   mabadiliko ya tabia nchi na muingiliano wa binadamu na wanyama pori.

Sekta hii ya mabilioni ya fedha ndio inayochangia kukuza pato la Kenya na inaendelea kukumbwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi, ukosefu wa nafasi na hivi sasa janga la korona.

Image by Kenya Wildlife Conservancies Association
Picha kutoka Kenya Wildlife Conservancies Association

Uhifadhi, tehemeo pekee la ulinzi wa wanyamapori

Hifadhi zinabakia kuwa tumaini pekee kwa kuwa hifadhi ni eneo linaloweza  kusimamiwa na mmiliki wa ardhi binafsi, kikundi cha wamiliki wa ardhi, mashirika au makampuni au jamii kwa minajili ya uhifadhi na matumizi mengine ya ardhi yatakayo  boresha maisha.

Muhifadhi wa kutoka Uingereza awali alihamasisha ulinzi wa wanyamapori kwa kuanzisha hifadhi kadhaa za Taifa akianza na Hifadhi ya Taifa ya Wanyama Pori ya Nairobi mnamo mwaka 1946. Hifadhi hii ipo kilometa saba kusini mwa jiji la Nairobi na hadi sasa kuna Hifadhi za Taifa za wanyama pori zipatazo 25 zinazosimamiwa na Shirika la Huduma la wanyama Pori (Kenya Wildlife Services)

Hata hivyo ujangili hasa wa faru kutokana pembe zake unazidi kuongezeka na hivyo kupelekea kutenga maeneo ya ardhi ya hifadhi zilizowapa uwezo jamii kuzisimamia na kufadika nazo. Mandhari ya hifadhi unawezesha muunganiko  unaosaidia kutoa mwanya kwa hifadhi za akiba na hifadhi za Taifa za wanyama pori kuwa na faida kwa jamii na jamii kufaidika nazo kwa kuzisimamia na kuwa wadau wakuu katika jitihada uhifadhi.

Kenya ina hifadhi zipatazo 160 ambazo zimegawanyika katika makundi ya aina tatu: Hifadhi zizomilikiwa na wanajamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinapatikana Maasai Mara, Hifadhi zinazomilikiwa na vikundi vya watu and Hifadhi za watu binafsi ambazo zinapatikana kwenye makazi wanyama pori yaliyopo kwenye maeneo ya malisho ya wanyama pori yaliyopo kaskazini na kusini mwa Kenya.

Utafiti uliofanywa na kikundi cha wanasayansi kinachojulika kwa jina la Living With Lions Organization kilitoa ushahidi unaoonesha kwamba hifadhi hizi zimekuwa na jukumu kubwa katika ongezeko la idadi ya wanyamapori kwenye maeneo yasiyo na uzio. Utafiti wao ulibaini ongezeeko mara dufu la idadi ya Simba kwenye hifadhi takriban nne zilizopo Kaskazini Hifadhi ya Mara   katika kipindi cha miaka mitano ongezeko lililotokana na uhifadhi wa kijamii wa kulinda wanyama pori.

Mawakala wa Kabila la Kimasai

Shirika lisilo la kiserikali la Maa Trust limekuwa kwenye mstari wa mbele katika kukuza faida za  wanyamapori na ulinzi wake kupitia mpango wake endelevu wa maendeleo tangu mwaka 2006.  Mpango huu ulifanikishwa kupitia ushirikiano baina yake na hifadhi ambazo zilikuwa zikikodisha ardhi kutoka kwa familia za kimaasai na kufanya malipo moja kwa moja kwenye akaunti za benki za familia hizo kila mwezi kutokana na mapato yaliyotokana na shughuli za utalii.

Maa Trust inaziwezesha  jamii hizi kuanzisha biashara ndogo ndogo na asasi ndogo ndogo za kifedha ili kuziwezesha jamii hizi kujitegemea kifedha na kuwekeza kwenye maendeleo ya familia zao.

Miradi tekelezwa kupitia mpango huu ni pamoja na miradi ya shanga na  asali  ya Maa. Shirika halipimi kiasi cha fedha iliyopatikana pekee yake bali fedha hizo ni kwa namna gani zimebadilisha hali zao za maisha  ya kila siku.

Kutokana na janga hili la dunia miradi yao yote ilikosa usimamizi kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais ya kutaka serikali zote na biashara kuanza kufanya kazi wakiwa nyumbani. “ Tuna kazi chache sana tunazofanya na wanawake watunga shanga, hii inatokana kufungwa kwa shughuli za utalii na utalii ndio soko letu kuu” anabainisha DK. Crystal Mongesen Mtendaji Mkuu wa Taaasisi ya Maa.

Kutokana na kufungwa kwa hifadhi wito wa msaada wa chakula ilibidi utolewe kwa vile jamii hiii ilikuwa imejikita kwenye biashara ya shanga na Asali hivyo kusababisha upungufu wa Chakula . Msaada wa dharura wa chakula ulihitajika Maasai Mara kwa vile shughuli za utalii zilisimama na kupelekea kuwepo kwa ukosefu wa kazi:” anabainisha Daktari Crystal Mongesen”

Taasisi ya Side Kick Foundation iliitikia wito huo kwa kutoa msaada wa dola za kimarekani 17,500 na msaada ulitolewa moja kwa moja kwa familia zipatazo 677 ambazo ziliathirika kwa kiasi kikubwa tatizo hili. Hata wakati wa zoezi la ugawaji misaada barabara nyingi zilikumbwa na mafuriko na kusababisha ugumu wa kuzifikia familia nyingi na changamoto hii ilipelekea kupata nguvu ya ziada kutoka kwa mradi wa Tembo wa Motorogi, Hifadhi ya Motorogi na Asilia Kenya.

Uhifadhi ndio msingi wa kulinda wanyamapori

Kenya kuna umoja wa hifadhi na umoja huu una jumuisha hifadhi 160 ambazo ndani yake zinaishi familia zaidi ya 930,000 ambazo zinafaidika na uwepo wa hifadhi hizi. Hii ina maana kwamba karibu asilimia 22 ya wanyamapori kenya wanaishi kwenye hifadhi hizi.

Kupitia umoja huu wa hifadhi, ujangili wa wanyama umepungua kwa kiasi kikubwa nchini Kenya na hivyo kuifanya Idara ya Huduma ya Wanyama Pori (Kenya Wildlife Service) kuwa nguvu zaidi.

“Kampeni yetu ya kuzuia ujangili imekuwa na mafanikio makubwa; hadi kufikia mwanzoni mwa Aprili 2020 ni tembo watano tu waliuawa na majangili ikilinganishwa na tembo 80 na vifaru 9 waliouwawa mwaka 2017 nchini Kenya”
Balala Najib New
Bw. Najib Balala
Waziri wa Utalii na Maliasili ,Kenya

Tangu Bwana Najib Balala ateuliwe kwenye nafasi hii mwaka 2018, serikali ya Kenya imeweka sharia kali za kuzuia ujangili katika kampeni yake ya kuzui ujangili na kulinda rasilimali hii ambayo ni urithi wa Taifa la Kenya. Sheria hizo ni pamoja na adhabu kali ikiwamo kifungo jela cha miaka 15 faini ya hadi dola za Marekani 120,000 kwa anayepatikana na hatia ya kufanya makossa ya ujangili.

Balala abanainisha kuwa maeneo ambayo ni sugu kwa ujangili yanawekewa doria wakati na baada ya hifadhi kufungwa na uchunguzi na upelelezi unafanywa kujua nani ameua wanyama iwapo wanyama  wamekutwa wameuawa wakati huu wa janga la korona.

Waziri huyo anasema ni Tembo 18 na vifaru 4 waliuwawa na majangili mnamo mwaka 2018 na mwaka 2019 ni Tembo 30 na vifaru 4 waliuwawa.

Kwa mujibu wa Takwimu za Idara ya Huduma za wanyama pori Kenya na tovuti TRAFFIC.org jumla ya tembo 2140 waliuwawa na majagili kati yam waka 2008 na mwaka 2017.

Kampuni za kijamii zapambana na kupunguzwa kwa mishahara, walilia msaada wa njia ya mtandao

Shughuli za Utalii na usafirishaji zimeathirika kwa kiasi kikubwa na kadhia hii na ni shughuli hizi ndizo kwa kiasi kikubwa zinagharimia shughuli za hifadhi hizi. Asilimia 25 ya wageni ambao wanatembelea hifadhi wanatoka nje ya nchi kwa mujibu wa Waziri Balala.

Resian Letoluo Meneja wa Mradi wa shanga wa Taasisi ya Maa anasema Korona imeathiri mishahara ya wafanyakazi wote taasisi Maa kwani kwa sasa mishahara ya imepunguzwa kwa asilimia 25.  

“ Siwezi kuwasemea wafanyakazi wengine kuhusu suala la mishahara , lakini kwa upande wangu nimepunguza matumizi na akiba yangu imepungua pia nakabili hali hii kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.” anasisitiza Bwana Letoluo

Mradi  wa shanga wa Maa ni mradi wa kijamii uliowezeshwa na Taasisi ya Maa yenye  makao yake Maasai Mara nchini Kenya. Mradi huu unajuisha wanawake wapatao 576 kutoka familia tofauti kwenye vijiji 17 kwenye jimbo la Narok.

Mradi huu umewasaidia zaidi watu 11000 kwenye kwenye jamii hii ya Kimaasai kupitia mauzo ya bidhaa za shanga zinazouzwa kwa watalii na pia dola 5 zinazotolewa kwa kila mgeni anayefika kwenye kambi zilizopo hifadhi ya Olare. Pia kuna msaada wa kila mwaka unaotolewa na Taasisi ya Asilia Africa iliyopo Hifadhi ya Naboisho.

Tangu janga la mlipuko wa Covid -19 lilipoingia pwani ya Kenya, mradi huo ulisimama kutokana na kufungwa kwa hifadhi.

“Mradi wa Maa Beadwork, umeathiriwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu, tunafanya mauzo yetu kwa watalii wanaotembelea pwani hii na kuuza shanga zetu. Imebidi tupunguze uzalishaji; Hii imesababisha wanawake wanaotengeneza shanga, kukosa mapato,” alisema Letoluo.

Letoluo kwa sasa anawahimiza wageni kutumia mitandao yao ya kijamii kununua bidhaa za shanga na kutangaza kazi zao na hii itawasaidia kuongeza kipato kitakachowasaidia kutunza familia zao katika kipindi hiki kigumu.

Simaloi Saitoto, Ofisa Operesheni wa Maa Beadwork, anaamini kwamba mshahara wake utarejea kama kawaida na anawaasa watalii kuisaidia Maa Trust na kuchangia  kwa kununua bidhaa hizo kwa njia ya mtandao na kwa kutembelea maduka yao wanapofika Mara.

beadwork women
Mradi wa Maa Trust Beadwork unawawezesha wanawake kupata pesa zao na kuwekeza katika maendeleo ya familia zao.

Kwa upande wake, Mdua Kirokor, mnufaika wa bidhaa za shanga anasema amefanikiwa kuongeza kipato chake kupitia bidhaa za shanga akiwa kama mwanachama wa Kundi la watengeneza shanga la Olitiamdoki.

Kipato anachokipata kimesaidia kuwasomesha watoto wake na kununua bidhaa za nyumbani kama tanki la maji na jiko la gesi. 

Kirokor, alijiunga na Maa Trust, mwaka 2017 na ana kila sababu ya kutabasamu kuendelea kufanya kazi na Maa Trust. Anasema maisha yake yamebadilishwa kwa sababu ana kipato cha uhakika.

Mpaka sasa ametumia kipato chake kununua mifugo ambayo inaweza kutumika pia kama ada na mirathi. Pia ana mipango ya kununua ardhi lakini  mlipuko huu umezuia mipango hiyo, hata hivyo anaamini kuwa hali itarudi kama zamani. 

Kirokor pia amekuza ujuzi wake wa kiufundi tangu alipojiunga taasisi hii ya Maa na anatumaini kujifunza zaidi, shughuli zitakaporejea kama kawaida.

Rose Sairowua, Kiongozi wa Operesheni katika eneo la utengenezaji wa shanga, aliwashukuru watalii wanaotangaza kazi zao na wanawatia moyo kuendelea kununua bidhaa hizo kwa njia ya mtandao, kama sehemu ya kuwasaidia. 

Noosokon Lepore, mwanachama wa taasisi hiyo, alisema hajawahi kujuta tangu alipoingia Maa Trust mwaka 2016, kwani kipato anachopata kinamsaidia kukuwasomesha watoto na kutatua matatizo mengine ya nyumbani.

Wanawake hao wamejipanga kurudi katika mradi wao baada ya taasisi hiyo kufunguliwa tena, wiki moja baada ya habari hii kukamilika.

Wakenya wanaotangaza utalii wa ndani

Wakati wa kufunguliwa tena Jumamosi, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Utalii na Wanyamapori, Najib Balala alimteua mmiliki wa rekodi za mbio za ulimwengu za mbio za dunia. Eliud Kipchoge kama balozi wa utalii wa Kenya kwa miezi sita ili kukuza sekta hiyo na kuharakisha ufufuaji wake.

Balala alikiri kwamba sekta ya utalii lilikuwa limeathirika sana, kukaribia kufungwa lakini alibaini kuwa kufunguliwa tena kwa nchi mnamo Julai 15 kumesababisha kurudi polepole kwa maisha katika mbuga za kitaifa, mapori ya akiba kati ya vivutio vingine nchini Kenya.
“Kwa sasa tunajaribu kufufua sekta kupitia mkakati wa ndani; Ndio maana tunawauliza Wakenya kuunga mkono utalii ili uchumi uboreshwe na ajira zipatikane, ”alisema Balala.
Aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa hoteli za Mara zimehifadhiwa kikamilifu na watalii wa ndani ambao wana hamu ya kushuhudia maajabu ya nane ya ulimwengu, uhamiaji wa nyumbu.

Hadithi hii ilitengenezwa kwa kushirikiana na InfoNile kwa msaada kutoka Mtandao wa Uandishi wa Habari wa Internews

Kufuatia kuchapishwa kwa hadithi hii, Benki ya I&M ilitoa KSH milioni moja kusaidia Wanawake wa MAA Beadwork huko Masaai Mara.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts