Uokoaji Wa Twiga aina ya Rotchild nchini Kenya

Uokoaji Wa Twiga aina ya Rotchild nchini Kenya

Mwandishi: Sharon Atieno

  • Twiga wa Rothschild hupatikana tu nchini Uganda na Kenya
  • Kumekuwa na upungufu wa karibu 40% katika idadi ya twiga nchini kwa zaidi ya miongo mitatu iliyopita.
  • Soma zaidi juu ya hatua za Kituo cha Twiga kuokoa Rothschild kupitia Uhifadhi na Uhamishaji

Kati ya aina tisa za twiga zinazopatikana barani Afrika, tatu mingoni yazo zimo nchini Kenya: aina hizi za twiga ni pamoja na Rothschild, Maasai na Reticulated. Hata hivyo, kumekuwa upungufu wa takriban 40% ya idadi ya twiga kwa miongo mitatu iliyo pita.

Katika mwaka wa 1998, idadi yote ya twiga ilikadiriwa kuwa wanyama takriban 45,000. Mpangilio wa kuokoa twiga nchini Kenya wa miaka kati ya 2018-2022, yadokeza kuwa idadi ya wanyama hawa inepungua kufikia twiga 28,850.

Hali hii ni mbaya zaidi hata ikapelekea Mkurugenzi Mkuu wa Shiraka Za Wanyama Pori nchini Kenya, Brigedia (mstafu) John Waweru kusisitiza umuhimu wa kurekebisha hali hii.

Janga la Covid-19 huenda likaadhiri idadi ya wanyama hawa hata zaidi. Akizungumsa katika kongamano mtandaoni kuhusu adhari ya Covid-19 kwa uhifadhi wa wanyama pori ndani ya jamii ya Afrika Mashariki,  Brig. (mstaafu) Waweru alisema kwamba wakati huu wa janga la Covid-19, visa vya uwindaji haramu wa wanyama pori umeongezeka, na kwamba twiga wamekuwa miongoni wa wanyama pori wanaowindwa kiharamu.

“Kati ya miezi ya Januari na Mei 2019, tani 1.8 za nyama za wanyama pori waliowindwa kiharamu, zilinaswa na wakati huo huo kati ya miezi ya Januri hadi Mei 2020, tunazo tani 2.8, kwa hivyo, tunazungumizia oengezeko la takriban 51.4%,” Mkurugenzi Mkuu wa shirika la KWS alisema.

“Utaharishi wa nyama pori na ulaji wake ni njia mwafaka ambayo chembechembe za maradhi husambaziwa binadamu kutoka kwa wanyama pori.”

Bernard Bett, MWANASAYANSI, SHIRIKA LA ILRI

Katika mwezi wa Juni, jarida moja liliripoti kwamba, jitihada za pamoja zilizo shirikisha maafisa kutoka mashirika la KWS, Northern Rangelands Trust pamoja na shirika la kidadisi zilipata kunasa kilo 150 za nyama za twiga na mizoga minne ya digidigi pamoja na miwili mingine ya tandala katika eneo la Ijara ilioko Jimbo la Garissa.

Kulingana na Bernard Bett, mwanasayansi mkuu, anaye ongoza utafiti wa pamoja kuhusu maradhi ya ukambuzikana katika shirika la kimataifa la utafiti wa mifugo  (ILRI), twiga wamekabiliwa na shindikizo pengine kutokana na njisi wao tunaswa kwa urahisi, ikilinganishwa na wanyama pori wengine, na pia wao huandamwana kwa urahisi katika maeneo lalio wazi.

Mili yao mikubwa huuza kwa bei ya juu katika soko la nyama za wanyama pori ikilinganiswa na wanyama wengine wadogo.

Alisema kwamba, utaharishi wa nyama pori na ulaji wake ni njia mwafaka ambayo chembechembe za maradhi husambaziwa binadamu kutoka kwa wanyama pori.

“Inapaswa kuhimizwa ya kwamba, utafiti umetambua mizoga ya twiga na ya wanyama wengine wakubwa kama vile nyati, pofu, swala, ngiri, punda milia na nungunungu zinazo chembechembe za ushambazaji maradhi, kama vile Bacillus, Brucella na Coxiella spp.,” Bett aliondeza, akisema kwamba chembechembe hizi kusambaziwa binadamu kupitia mgusano, ulaji wa nyama mbichi ama nyama ambayo haijapikika vyema, pia kupitia chembechembe zinazoelea hewani wakati wanyama hawa kuzuiliwa na kuchinjwa ama wakati mizoga inaposafirishwa.

Miongoni mwa aina za twiga nchini, ile ya Rothschild ndio ambayo iko katika hatari kubwa kulingana na orodha ya KWS. Licha ya kwamba, idadi ya twiga nchini Kenya ni takriban wanyama 29,000 (ambayo ni robo ya idadi ya tembo kwa kiafrika), idadi ya aina ya twiga ya Rotchild ni wanyama 765 pekee, kulingana na makadirio ya shirikia la the International Union for the Conservation of Nature (IUCN) ya mwaka wa 2018.

Aina ya twiga huyu, ijulikanao kwa jina la kisayansi kama Giraffa camelopardalis Rothschild, hupatikana katika nchi za Uganda na Kenya pekee. Aina ya twiga huyu anatambulika kwa rangi nyeupe miguuni (inaoanzia magotini hadi kwenye kwato zake na huwa haina madoadoa) twiga huyu hula matawi ya miti aina ya mguga na ile ya mti wa aina ya combretum ambayo hupatikana katika maeneo tambarare ya savana.

Aina ya twiga huyu anatambulika kwa rangi nyeupe miguuni (inaoanzia magotini hadi kwenye kwato zake na huwa haina madoadoa)”

UKWELI HALISI YA MAMBO KUHUSU TWIGA

Kabla ya mwaka wa 2018, aina ya twiga huyu aliodhoreshwa katika orodha ya IUCN Red List kama mnyama aliye hatarini mno na ni hivi karibuni tu, hali yake ilibadilishwa na kuwa mnyama ambaye anakaribia kuwa hatarini kutokana na ongezeko dongo ya idadi ya mnyama huyu katika nchi za Kenya na Uganda, hadi kufikia wanyama 2,098 kwa jumla.

IUCN yadokeza kwamba, idadi ya mnyama huyu nchini Kenya, imedidimia pakubwa kwa kiasi kwamba ameshakoweta kabisa kutoka kwa mazingira yake halisi kufuatia uwindanji haramu, shughuli za kilimo, ardhari za binadamu, uharibifu wa mazingira na uharibifu wa ardhi.

Kituo cha Twiga; tumaini kwa Twiga wa Rothschild

Kupitia jitihada za uhifadhi na uhamashishaji wa twiga huyu, idadi yake nchini Kenya imeokolewa. Kutoka mamia kidogo tu katika miaka ya 1960s hadi kufikia idadi ya hivi sasa ya wanyama 765.

Kituo cha twiga kimekuwa mstari wa mbele katika juhudi ya uhifadhi, ambalo ni shirika la wakfu wa African fund for the endangered wildlife (AFEW) Kenya.

Waanzilishi wa kituo hiki – Jock na Betty Leslie-Melville, katika juhudi za kuokoa twiga huyu baada ya kupoteza makao yake asili maghagiribi mwa Kenya kufuatia maskuota kupewa makao, wakiwaleta twiga wawili katika nyumbani mwao ilioko kiungani Langat’a, kusini magharibi wa Nairobi. Walianza kuwalea ndama na kuanzisha mpango wa kusazisha twiga katika hifadhi hii.

“Wazo lilikuwa kuzazisha twiga aina ya Rothschild katika kituo hiki kisha baadaye kuhamisha baadhi ya twiga wachanga kila baada ya miaka mwili au mitatu kurudi mwituni ili kwamba idadi ya wanyama hawa ipate kunawiri,” alielezea Emmanuel Ngumbi, Meneja wa Mipango ya Uhifadhi , Kituo cha Giraffe Centre.

Kando la ushalishaji ya twiga aina ya Rothschild, kituo hiki pia huendesha elimu ya huifadhi, ambapo Wakenya uhamanyishwa,hususan vijana, jinsi ambavyo, aina tofauti ya twiga wanaweza hatarika.

giraffecentre 20184336 110510359607016 6744825356127043584 n
Watoto wa shule waelimika kuhushu twiga na uhifadhi wake katika kituo cha Giraffe Centre, Nairobi, Kenya

“Makundi ya shule huja hapa bila kulipishwa chochote, mradi tu wawe arifu mapema, kati ya shiku za Jumatatu na Ijumaa. Sisi huwapokea wanafunzi 50,000 kila mwaka, ambao walipishwi chochote. Wao huelimika kuhushu twiga na shughuli za uhifadhi nchini, na wao hupata nafasi ya kuwakaribia twiga hawa na kuwalisha na kutangamana nao na kutizama filamu ya kimazingira,” alisema.

Kituo hiki chenye ekari 120 kinawahifadhi twiga 11: watano miongoni wao wakiwa wale wadogo, watano wengine wakiwa wa kike na wa kiume mmoja.

Kituo hiki kinaendesha mpango ya kuzalisha twiga kikitumia mbinu asilia, pasipo kuhusisha mbinu ya kisasa.

Meneja ya mipango ya uhifadhi anasema kwamba baada ya twiga kujifungua, ndama hukaa katika kituo hiki wa mdua wa miaka miwili au mitatu, kabla cha kuhamishwa mwituni.

“Ili kuzuia uzalishaji wa ndama kutoka kwa twiga zilishokaribiana kijamii, sisi huwaleta twiga mmoja au wawili kutoka nje baada ya kila miaka mitatu au minne, ili kudhibiti kizazi cha twiga, hivyo basi kuhashikisha kwamba ndama wataoshaziwa badaye ni wenye afya bora,” alionyezea kusema.

Tangu uwanzilishaji wake, kituo hiki kimepatia hifadhi twiga 60, huku kikifanyikisha uhamisho wa twiga 25 katika sehemu tofauti mwituni kote nchini, waliko aina sawa ya twiga hawa.

DSCN1638 1
Twiga aina ya Rothschild katika kituo cha Giraffe Centre

“Hatuwezi hamisha twiga hawa hadi sehemu zilizoko twiga aina wale wengine wawili tofauti kwa sababu watazaa nao, hivyo kutapoteza kizazi kake ama kutatokea kizazi mseto,” alieleza Ngumbi.

Baadi ya twiga wamehamishwa hadi sehemu za Soysambu, Mbuga ya Ziwa Nakuru, Samba la Sergoit na hifadhi ya Mbuga ya Mwea.

Ngumbi alamikia mangojwa kuwa changamoto katika mpangilio wa kuzalisha twiga hawa, na kwa vile tafiti chache tu zimechafanyika kuhusu aina ya twiga tofauti, uthibiti wa majongwa umekuwa mgumu.

“Kuna wakati kumepoteza twiga mmoja baada ya mwingine, na hata baada ya kupeleka sampuli katika maabara, hatujafanyikiwa kumapata matokeo kamili,” asema.

Meneja huyu wa hifadhi aongeza kusema kwamba kituo hiki cha twiga hakina muuguzi wake wa wanyama.

“Hivyo basi hatuna budi ila kutengemea shirika la KWS, kwa hivyo iwapo maafisa wake wamesongwa na kazi na wako mbali na makao makuu, basi itawachukuwa mda mrefu kushugurikia kwa upesi visa vya twiga vinavyoripotiwa kwao,” Ngumbi asema.

Akiri pia kwamba, hawana kitendo maalum ya kuwanasa twiga na bado wao kutegemea shirika la KWS, kuwahamisha twiga kutoka kituo cha twiga hali kathalika kuwaleta twiga wengine kutoka sehemu tofauti hadi kituoni ili kuthibiti kizazi chake.

Sekta ya utalii imo hatarini

Utegemeaji kwa utalii umekuwa changamoto kubwa kwa hifadhi hii, hususan wakati huu wa janga la Covid-19, ambapo kuna marafuku wa usafiri. Ngumbi aleleza kwamba, hii imezorotesha kiwango cha mapato lao, na huenda ikatoa changamoto katika siku za usoni kwa mapangilio kwa kuzalisha twiga.

Aongezea kusema kwamba, ikiwa hawataweze kukusana fedha za kutosha, itakua vigumu kwao kushughulikia vilivyo maslahi ya twiga, wafanyakazi wao ambao huwalinda twiga na pia hawatakuwa na uwezo wa kuzisaidia mashirika mengine ya uhifadhi, ambao huendeleza kushughuli za kuhifadhi wanyama aina nyengine wa pori.

Kando na jitihada zao muhimu za kuokoa twiga aina ya Rothschild kuepuka kutoweka kabisa, kituo hiki kinajivunia mchango wake katika ubunifu wa mkakati maalum wa kuhifadhi twiga, ambao utaelekeza shughuli za uhifadhi wa aina zote tatu za twiga nchini.

Kituo hiki kinatumia mbinu za utafiti, zinazo husisha upigaji picha kisha kuziweka picha hizi katika programu ambayo huchanganua vielelezo vilivyoko katika mwili wa twiga, kwa vile vielelezo hivi ni fafanuzi kabisa kama alama za vidole, kimeshirikiana kwa karibu na shirika la KWS kufanyia utafiti idadi ya twiga aina ya Rothschild katika mbuga ya Ruma National Park, Mwea Game Reserve na Lake Nakuru National Park.

“Pamoja na wakfu wa Giraffe Conservation Foundation and Kenya Wildlife Service tulikuwa watu wa kwanza kutumiwa teknologia hii mpya nchini katika kufanya utafiti wa twiga, ambapo hauitaji kutunga wanyama hawa vishale; wala hauitaji mda mwingi kufanya utafiti kwa kimsingi,” alisema.

Ngumbi anahamiza watu kufanya juhudi na kueleza fedha katika shughuli za utafiti wa twiga kama mnyama anayehitaji kuokolewa kwa manufaa za siku za usoni.

“Kila mtu duniani, anazungumzia tembo na faru, linapokuja suala la fedha za uhifadhi na utafiti, zaidi hasa wanasayansi na wahifadhi pia wanajikita zaidi katika tembo na faru, lakini ukifikiria idadi tunayopoteza hasa twiga, ina maana kwamba tunahitaji kujitafakari tena na kuanza kujikita zaidi katika uhifadhi wa twiga, la sivyo watapotea,” alisema

Miongoni wa aina tisa ya twiga ziliyochunguzwa na shirika la IUCN, aina mbili pekee ndizo ambazo zimeweza kuimarisha hali yao kutoka kuwa hatarini (Twiga wa Magharibi wa Afrika na aina ya Rothschild) hadi katika hali ya kuwa rahisi kuduruhiwa na karibu kutishiwa. Aina nyinge za mnyama huyu hazija onyesha mabaliko katika hali yao. Hivyo basi, juhudi ya pamoja zahitajika kati ya serikali za Afrika na mashirika ya uhifadhi, ili kuhakikisha kwamba twiga aina yote wamehifadhiwa hivyo basi kuepuka kutoweka.

Ripoti hii imefanikishwa kupitia ushirikiano wa Code for Africa na usaidizi wa Internews-Earth Journalism Network.

Makala haya yanichapishwa mara ya kwanza katika Science Africa tarehe September, 14 2020

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts