Addis Ababa COVID-19 ni changamoto na pia fursa

Addis Ababa COVID-19 ni changamoto na pia fursa

Mekonnen Teshome na Tesfaye Abate

Ethiopia imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji safi kwa kipindi kirefu sasa. Lakini mwamko ambao umeoneshwa kwenye sekta ya usafimjini Addis Ababa, ambao ni mji mkuu mkongwe wenye miaka 133, baada ya kuibuka kwa maradhi ya COVID-19, umekuwa kichocheo cha kuifanya sekta ya usafi kuwa ni kipaumbele katika mikakati ya kulinda afya za watu.

Bekele Balcha, mlinzi anayehudumia hospitali ya Eka Kotebe, ambayo ni kituo kikuu cha kuhifadhi wagonjwa wa COVID-19 mjini Addis Ababa, anasema kuwa tangu janga hilo lilipotokea, usambazaji wa maji katika hospitali hiyo na maeneo yanayoizungukaumeimarika sana.

“Kama maji ya bomba hayatoki, Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka ya Addis Ababa inasambaza maji kwa jamii kwa kutumia na magari yake maalum na wanafanya hivyo kila wakati tunapowaaarifu kuhusu

kukosekana kwa huduma ya maji,” alisema.

“Ikiwa utapatwa na shida yoyote inayohusiana na maji, kuna utaratibuwa  kupiga simu ya bure kupitia nambari 804 na utawapata watu wa kitengo husika unaoweza kuwaarifu kuhusu shida hiyo.  Ninaona hatua zinazotia moyo sana katika huduma za usambazaji maji wakati huu wa COVID-19.”

Licha ya changamoto za muda mrefu, vita dhidi ya janga la COVID-19 vinawezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma za usafi kwa bei nafuu na kuimarisha utamaduni wa usafi miongoni mwa jamii za Waethiopia. Na halihii inaweza kujenga ulinzizaidi dhidi ya magonjwa yatokanayo na mazingira yasiyo safi katika siku za baadaZe.

4

Mahitaji ya maji ambayo bado hayajafikiwa

Maji safi ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linapendekeza kuwa majengo yote ya biashara ya umma na ya binafsi yawekewe vifaa vya kusafisha mikono katika milango ya kuingilia ili watu waweze kuosha mikono yao mara kwa mara kama njia ya  kupunguza kuenea kwa maambukizo.

Hata hivyo, upatikanaji wa maji safi unabaki kuwa moja ya changamoto katika mapambano dhidi ya janga la Corona na mahitaji ya maji bado hayakidhi viwango katika nchi nyingi ulimwenguni. Hali hiyo pia inaukumba mji waAddis Ababa, ambako wakaazi wake wanakabiliwa na upungufu wa maji safi na salama.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, ni asilimia 63 tu ya idadi ya watu 108,113,150 nchini Ethiopia na asilimia 4 tu ya wakazi wake wa mijini, ambao ni sawa na asilimia 21.3 ya watu  wote, ndio wapatao maji salama kwa matumizi ya binaadamu na  yasiyo na vijidudu.  Takwimu hizo ni kwa mujibu wa makadirio ya mwezi Julai.

Ukame wa mara kwa mara, mafuriko, na kuongezeka kwa joto vinafanya iwe ngumu zaidi kusimamia vizuri rasilimali za maji na kuhakikisha mwendelezo wa kudumu katika utoaji wa huduma hiyo.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka ya Addis Ababa (AAWSA), ambalo ni shirika la umma linalosimamia usambazaji wa mifumo ya maji ya bomba katika mji huo,

ina uwezo tu wa kusambaza maji salama kwa theluthi mbili ya idadi ya watu wa jijini humo kwa kutoa  mita za ujazo 575,000 za maji ya kunywa kwa wakazi wake kila siku. Mahitaji ya maji salama kwatheluthi moja iliyobaki ya wakaazi wa mji huo hayajafikiwa. Njia pekee waliyonayo ni kutembea umbali wa hadi kilometa 2kutoka katika makaazi yao kwenda katika maeneo yenye vyanzo vya maji ambavyo baadhi yake vinatoa maji yasiyo salama.

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha AAWSA katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia watoto UNICEF nchini Ethiopia,Serkalem Getachew,alisema, “Pengo kati ya mahitaji ya maji yaliyopo na kiwango kinachopatikana  sasa Addis Ababa linaathiri juhudi zinazofanywa katika mji mzima kuzuia kuenea kwa maradhi ya COVID-19.”

Naye Mkuu wa Kitengo cha Usafishaji Maji dhidi ya Vijidudu na Usafi wa Mwili (WASH) katika UNICEF nchini Ethiopia,  Kitka Goyol, anabainisha kuwa ukosefu wa upatikanaji wa vifaa vya msingi vya kunawa mikono upo si kwenye nyumba tu bali pia shule, sehemu za kazi na vituo vya huduma za afya.

“Upatikanaji wa maji pia ni tatizo katika maeneo mengine ya umma ambapo watu hukusanyika kama vile masoko na vituo vya usafirishaji. Katika maeneo  hayo, usafi wa mikono ni muhimu katika kuwalinda watoto, walimu, madaktari, wauguzi, na wafanyikazi wengine dhidi  ya maambukizo ya COVID-19,”alisisitiza na kuongeza  kuwa“Nchini Ethiopia karibu nusu ya idadi ya watu (watu milioni 45) hawana mahali pa kunawa mikono kwa sabuni majumbani mwao. ”

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Zinabu Assefa Alemu na Michael O. Dioha  uliopewa jina la ‘Uundaji matukio ya upatikanaji endelevu wa maji na mahitaji yake katika jiji la Addis Ababa, Ethiopia’ unathibitisha changamoto hiyo hiyo ya uhaba wa maji katika mji wa Addis Ababa.  “Mji wa Addis Ababa una rasilimali chache sana za vyanzo vya  maji vya chini na juu ya ardhi ambavyo vina mchango mkubwa katika kusaidia kukidhi mahitaji ya maji majumbani hasa katika majumba yanayokaliwa na watu wengi”. Kwa hakika hasa si maji tu ndiyo yanakosekana bali na sabuni pia. 

Mwezi Mei mwaka 2020, UNUN ilichapisha ripoti baada ya kufanya tathmini ya athari za kijamii na kiuchumi za COVID-19 nchini Ethiopia iliyoonesha kuwa watu wanashindwa kusafisha miili yao mara kwa mara kwa sababu hakuna maji na sabuni au kama vipo, basi kuvipata kwake kuna gharama kubwa sana ambao wananchi wengi wananshindwa kuimudu.

Addis Ababa River Map 1

Gharama ya ukosefu wa usafi

Kwa mujibu wa Mkakati wa Kitaifa wa Usafi wa Mwili na Afya ya Mazingira, ukosefu wa usafi wa mazingira huigharimu Ethiopia asilimia 2.1 ya pato la taifa. Ili kuondoa mazoea mabaya ya uchafu katika jamii, serikali inahitaji kujenga vyoo imara milioni 6 na watu wavitumie. 

Shirika la UNICEF nchini Ethiopia inaonesha kuwa asilimia 60 hadi 80 ya magonjwa ya kuambikiza nchini humo yanatokana naukosefu wa maji safi na salama pamoja na huduma hafifu za usafi wa mwili na mazingira. Shirika hilo linaongeza kuwa kuna uhusiano mkubwa sana baina ya usafi wa mazingira na udumavu na kwamba tabia ya kujisaidia ovyo ovyo inaweza kusababisha magonjwa yanayotokana na kinyesi kama vile tumbo la kuharisha, jamb oambalo litazidisha zaidi utapiamlo.

“Kuharishani sababu inayoongoza ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Ethiopia, ikichangia asilimia 23 ya vifo, idadi ambayo ni zaidi ya watoto 70,000 kwa mwaka,” ilidokeza UNICEF.

Naye Abireham Misganaw, ambaye ni mtaalam wa afya ya umma na mjumbe wa timu ya usimamizi wa takataka katika wizara ya afya ya Ethiopia, anathibitisha kwamba kuenea kwa trakoma katika kundi la watoto wenye umri wa miaka 1-9 kwa asilimia 40 kunatokana na ukosefu wa upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na uchafu wa mazingira.

Na wakati huu, maji yamekuwa ni mojawapo ya mahitaji ya msingi katika mapambano dhidi ya COVID-19 pamoja na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu na kwa kweli ni muhimu sana pia katika vita dhidi ya magonjwa ya mripuko hata hapo baadaye sio tu kwa mji wa Addis Ababa lakini pia mahali kwengine ambapo nishati hiyo ni adimu.

Poster

Kubadilisha changamoto za COVID-19 kuwa fursa za WASH

Mara tu baada ya mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 kuthibitishwa nchini Ethiopia mnamo Machi 2020, serikali ya nchi hiyo na washirika wake wa maendeleo walifanyia tathmini ya upatikanaji wa maji kwa watu, usafi wa mazingira na usafi wa mwili (WASH), kati ya mahitaji mengi muhimu, kwa kupitia awamu ya sasa ya Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya uliofanyika hivi karibuni nchini humo. 

Matokeo ya uchambuzi wa utafiti huo yanaonesha kuwa viwango vya sasa vya upatikanaji wa maji na sabuni ni muhimu katika kupitisha mapendekezo ya kunawa mikono.

Licha ya changamoto kubwa za uhaba wa maji salama mjini Addis Ababa, juhudi zinafanywa kuhakikisha maji yanapatikana katika mji huo ili kuzuia kuenea kwa COVID-19. Serikali za mitaa mbalimbali pamoja na Taasisi Zisizo za Kiserikali na watu binafsi pia wanashirikishwa katika mipango ya kuhakikisha maji hayakosekani hasa kwa matumizi  ya usafi wa mikono.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma cha Mamlaka ya Maji safi na Maji taka ya Addis Ababa, Serkalem Getachew, amesema kuwa tangu kuthibitika kwa mgonjwa wa kwanza wa COVID-19, serikali ya mji inafanya juhudi za hali ya juu kuzalisha maji kwa kadri ya uwezo wake na kuhakikisha hayakatiki. 

Getachew amesema kuwa hadi sasa upatikanaji wa maji ni wa uhakika katika wadi nyingi za mji huo ambako ndiko kuna kambi za wagonjwa wa COVID-19, huku wadi zingine 104 kati ya 116 zinapata  maji katika mzunguko mfupi kwa kadri iwezekanavyo.

Serkalem amesema kuwa serikali imeanzisha mpango maalumu wa usambazaji maji, huduma za majitaka, taarifa na mawasiliano pamoja na kuunda kamati ya masuala ya ugavi ili kuratibu huduma za maji na usafi wa mazingira kwenye mji huo.   

Anasema kuwa umakini wa pekee umeelekezwa katika usambazaji wa maji kwenye vituo vyote vya mabasi vya wilaya, hospitali, vituo vya karantini, na maeneo mengine ya umma kwa kutumia malori 28 ya matanki la maji na mengine yaliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed pamoja na Wizara ya Maji.

“Pamoja na kuufanyia marekebisho mpango uliopo wa usambazaji wa maji kwa jamii ili kuongeza huduma kwa umma, serikali ya jiji inaboresha vyanzo vya maji chini ya ardhi katika maeneo zaidi ya saba mjini Addis Ababa,” ameongeza.

Serkalem anasema kuwa mamlaka hiyo pia inahakikisha kuna usimamizi mzuri wa majitaka akibainisha kuwa uzalishaji wake umeongezeka jijini humo kwa sababu ya kuimarika maji kwa  ajiliya kunawa mikono na usafi  wa mazingira ili kudhibiti COVID-19.

7 1

Shirika la UNICEF ni miongoni mwa washirika kadhaa ambao wanachangia kikamilifu katika mapambano dhidi ya janga hilo.Moja ya mipango yao”ilisababisha maendeleo ya kupatikana kwa ujumbe unaotoa tahadhari kuhusu COVID-19 ambao unatumika kwa sasa. Kwa msaada wa serikali, kampuni ya taifa ya simu ilitumia ujumbe huo wa COVID-19 uliotengenezwa kama mliowa sauti katika huduma zake za simu na kuwafikia  wateja wote wa kampuni hiyo nchini humo,” alisema mkuu wa Kitengo cha Utunzaji na Usafi wa mwili (WASH) katika ofisi za UNICEFEthiopia, Kitka Goyol. 

Goyol alionyesha kuwa UNICEF inafanya kazi kuhakikisha hata watu maskini zaidi wanaendelea kupata huduma za kunawa mikono wakati wote wa janga la COVID-9.

Goyol amesema kuwa UNICEF inafanya kazi kuhakikisha kuwa watu masikini zaidi katika taifa hilo masikini wanaendelea kupata huduma ya kunawa mikono wakati wote wa janga la COVID-19. “Mara nyingi jamii hizi ndizo zilizokuwa na uhaba wa vitu muhimu inavohitajika kwa usafi wa mwili na mazingira yao kabla ya mripuko wa virusi vya Corona,” aliongeza.

Anasema kuwa UNICEF tayari imeshatoa na kufunga matanki sita aina ya ROTO ambayo kila moja lina uwezo wa kubeba lita 10,000 kwa ajili ya kuhifadhi maji jijini Addis Ababa. Shirika hilo limeweka pia mabomba ya kuvuta maji ardhini yanayotumia umeme ili kuimarisha upatikanaji wa maji kwenye vituo mbalimbali vya afya pamoja na kutoa mahitaji mengine kwa watumishi wa afya zikiwemo sabuni 13,050, chupa 250 za dawa za kuua vijidudu mikononi yenye ujazo wa mililita 150 kila moja.

Vifaa vingine vilivyotolewa ni pamoja na ndoo za plastiki 250, ndoo ndogo 95, masinki 95 ya kuoshea mikono yaliyofungwa na mabomba yake, dawa za kuua wadudu za kupuliza kwenye mazingira 12, na mitungi 30 ya kemikali ya klorini (HTH 70%) ambayo hutumika kuuwa vijidudu kwenye maji iliyotolewa kwa ajili ya kusafisha maeneo. 

construc

UNICEF kwa kushirikiana na Mtandao wa Programu za Usalama katika Maeneo ya Mjini (uPSNP) ulizisaidia familia zote masikini katika vitongoji vya mji wa Addi Ababa kwa kuwapa sabuni 210,000 pamoja na ujumbeunaohamaisha watu kuhusu umuhimu wa kunawa mikono. 

Kupitia “Mradi wa Pili wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira nchini Ethiopia” Benki ya Dunia inafanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Addi Ababa (AAWSA) kuungeza zaidi upatikanaji wa mji jijini humo. 

“Miongoni mwa kazi zinazofanywa sasa ni pamoja na ukarabati wa visima kwa ajili ya kuimarisha vyanzo vya maji vya ardhini vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali mjini humo na ubadilishaji wa pampu za maji 20 ili kuweyesha patikanaji wa kudumu wa maji safi na salama katika maeneo yenye watu wengi,” ilisema ripoti ya Benki ya Dunia.

Mradi huu unasaidia huduma muhimu za maji na usafi wa mazingira kwa zaidi ya Waethiopia milioni 3 na kuwawezesha zaidi ya watu 623,000 katika maeneo ya miji kupata vyanzo vya maji vilivyoboreshwa. Imesaidia pia kuunganisha mtandao mpya wa maji ya bomba katika kaya 61,000, kuimarisha uhifadhi bora na salama kinyesi kwa watu milioni 2.7 katika maeneo ya mijini,kugharamia uunganishaji wa mifumo ya majitaka ipatayo 50,000 huko Addis Ababa pamoja na ujenzi wa vyoo vya umma 1,000.

Mkuu wa Kitengo cha kusimamia Maji safi na Usafi wa Mazingira (WASH) katika shirika la UNICEF Ethiopia, Kitka Goyol, anasema UNICEF imeunda na kukubaliana juu ya mipango ya kazi na Wizara za maji, afya, na elimu na ofisi za mkoa nchini Ethiopia kutekeleza shughuli mbali mbali za WASH kote nchini katika wa mwaka ujao wa Fedha.

Hata hivyo, baadhi ya wenyeji wa mji huo walibaini kuwa baada ya juhudi hizo za pamoja kufanyika kwa miezi kadhaa, huduma za usambazaji maji jijini Addis Ababa zimepungua katika siku za hivi karibuni.

Worke Debebe, mfanyabiashara ndogondogo katika mji mdogo wa Arada uliomo katika mamlaka ya jiji la Addis Ababa, anasema kuwa motisha ya watu katika kupambana na virusi hivi sasa imepungua na usambazaji wa maji na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka ya Addis Ababa umeonekana kufuata mwelekeo huo.

River

“Usambazaji na upatikanaji wa maji katika matangi ndogo ya maji yaliyowekwa kwa ajili ya kunawa mikono katika mitaa ya Addis Ababa sio endelevu. Tulikuwa tunapata maji kila kona ya jiji kwani magari ya kubeba maji yalikuwa yakileta na kujaza maji kwenye matangi huku mitaani kila siku, lakini sasa hii imedorora zaidi,” alisema Worke.

Hata hivyo, bado wenyeji wengi wanatoa sifa stahiki kwa juhudi jumuishi zilizofanywa na washirika wa maendeleo pamoja na uongozi wa jiji kutoa maji kufuatia kuzuka kwa virusi hivyo, wakiwataka viongozi wasiache shughuli hiyo.

Lakech Zeleke ambaye ni mjasiriamali mdogo katika jiji la Yeka, alisema usambazaji wa maji umeboresha haswa katika maeneo yaliyochaguliwa kama hospitali, vituo vya treni na maeneo ya soko. “Ninafurahiyasana juhudi za usambazaji wa maji za serikali ya jiji na taasisi mbali mbali katika jiji letu,” anasema.

“Kwa maoni yangu, utamaduni wa kunawa mikono na usafi wa mazingira ambao unastawi sana Addis Ababa na juhudi zote za usambazaji wa maji za uongozi wa jiji vinahitaji kuwa utamaduni pia katika siku zijazo hata wakati wa baada ya COVID-19. Ni muhimu kwa afya yetu na za watoto wetu. ”

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts