Wakimbizi Wageuza Kinyesi Cha Binadamu Kuwa Kuni Mbadala Ya Kupikia Kwa Madhumuni Ya Kuhifadhi Miti Na Kukabiliana Na Tabia Nchi

Wakimbizi Wageuza Kinyesi Cha Binadamu Kuwa Kuni Mbadala Ya Kupikia Kwa Madhumuni Ya Kuhifadhi Miti Na Kukabiliana Na Tabia Nchi

Na Robert Ariaka

Kundi la wanawake wakimbizi wa Sudan Kusini wilayani Arua, wanatengeneza matofali kutokana na kinyesi cha binadamu ili kutumika badala ya kuni na makaa.

“Matofali yatokanayo na kinyesi cha binadamu hutumika kwa muda mrefu wa masaa manane, hivyo kurahisisha shughuli ya upishi ikilinganishwa na kuni za kawaida,” asimulia Roda Selwa, kijana ambaye ni mwanachama wa kikundi cha wanawake cha Loketa kinachobadilisha kinyesi cha binadamu kutumika kama kuni mbadala.

Tabu Regina the secretary Loketa women group in Ariwa village in Rhino Camp explains how they make briquettes using crop residues and human waste Photo By Robert Ariaka

Kikundi cha wanawake cha Loketa ni miongoni mwa makundi matano mengine katika makao ya Rhino-Camp, Imvepi, Omugo na Bidibidi ambayo yalinufaika na elimu ya kuunda matofali ya makaa kupitia shirika la Oxfam.

Kusudio la awali lililenga kuunda matofali ya makaa kutokana na mabaki ya mazao. Hata hivyo, wanawake hawa waliiga mbinu mpya ya kubadilisha kinyesi cha binadamu kuwa matofali makaa, baada ya kupokea elimu mjini Nakuru, Kenya.

Tabu Regina, ambay ni katibu wa kundi hili katika kijiji cha Ariwa kilichoko makao ya Rhino Camp alisema kuwa walipokea usaidizi kutoka shirika la Oxfam uliowawezesha kutengeneza matofali haya kutumia mabaki ya mazao na kinyesi cha binadamu.

Matofali haya hutengezwa kutokana na bua la mtama na wa simsim, shina la maharagwe pamoja na matawi ya ndizi. “Sisi huyachoma mabaki haya, na punde tu yanageuka rangi kuwa nyeusi; huyaponda kutumia mtambo kisha huyachanganya na uji utokanao na unga wa muhogo kuunda matofali,” Regina alisema.

Rashid Mawejje, mratibu wa afya ya umma anayefanya kazi na shirika la Oxfam alisema kwamba walitumia Sh373.3m katika uelimishaji, ununuzi wa vifaa na kutoa usaidizi ufaao kwa wanawake wakimbizi.

Wawejje alisema kuwa shirika la Oxfam unasaidia makundi matano katika mradi wa utengenezaji matofali makaa. “Utumizi wa mara tena wa taka ngumu ndio ilikuwa mwanzo tu, lakini wanawake sasa wameingilia usindikaji wa kinyesi cha binadamu hadi kuwa matofali makaa,” Mawejje alisema.

Regina yuko na matumaini kwamba punde utengenezaji wa matofali haya utapanuka, basi utachangia pakubwa kupunguza ukataji miti.

Mary Ajonye the chairperson of Loketa women group explains how the Charcoal Briquettes are made in different sizes ranging from the smollest to the biggest Photo By Robert Ariaka

Anahimiza serikali kuyapa nguvu makundi ambayo tayari yanatengeneza matofali haya na kwamba ishirikiane na washirika wengine katika kambi za wakimbizi ili kuongeza elemu miongoni mwa vijana na wanawake katika kukabiliana na tabia nchi.

Wanawake wachanga, waliokomaa na ambao ni wazee katika makundi haya, hutumia mikono yao kuifinyanga mchanganyiko hadi kuwa mfinyazo. Punde unakuwa tayari, wanawake hawa huifanya mchanganyiko huu kuwa matofali makaa ya ukubwa tofauti tofauti, kuanzia ndogo hadi iliyo kubwa.

Kando na matofali haya, kikundi hiki sasa kimeanza kutengeneza matofali makaa kikitumia majivu ya kinyesi yaliyotibiwa. Shirika la Oxfam hutoa majivu haya ya kinyesi yaliyotibiwa kutoka eneo la Lira.

Hata hivyo, wanachama wanaliomba shirika hili kuanzisha kiwanda cha usindikaji kinyesi cha binadamu katika makambi ya wakimbizi ili kurahisisha upatikanaji wa majivu haya.

Bohari tayari limeshatengenezwa na Oxfam litakalowawezesha wanawake hawa kuhifadhi matofali makaa, huku wakiyatafutia soko.

Alidhibitisha kwamba wanawake hawa walianza kutengeneza matofali mwaka wa 2018. Sasa wameborehsa hali yao ya kiuchumi huku wakiweka pesa katika akiba katika SACCO, shirika la akiba na mkopo.

Kikundi hiki huchukuwa nafasi ya kutafutia matofali yake soko wakati wageni huja kutembelea makao yao na wakati ambapo shughuli ya kugawiwa chakula hufanyika.

“Hatulazimiki tena kutafuta kuni vichakani, shughuli ambayo ni hatari. Baadhi ya wanawake hubakwa kule kichakani wanapotafuta kuni,” Regina alisema.

Neima Gaba resident of Ariwa village in Rhinocamp refugee settlement now uses uses Charcoal Briquettes for cooking Photo By Robert Ariaka

Ukulima kama njia ya maishilio ya ziada

Kwa vile simsim ni zao muhimu linaloleta pato katika eneo hili, kikundi hiki kiliingilia ukuzaji wa mmea huu. Mabaki yanayopatikana baada ya kuvuna zao hili hutumika katika utengenezaji wa matofali.

Regina alisema kwamba matofali makaa husaidia kuhifadhi mazingira, sababu ambayo imewafanya kutoa elimu ya utumiaji wa matofali haya kwa jamii na kusitisha ukataji miti.

Alitoa ombi kwa washirika wanaofanya kazi katika makao ya wakimbizi kuongeza usaidizi wao na kusambazia wakimbizi miche ili waipande kwa lengo la kurejesha mazingira katika hali yake ya kawaida.

Kulingana na Regina, matofali makaa huwa ni ya bei nafuu, hudumu kwa muda mrefu na huzalisha joto jingi la kupikia. Na pia huiwacha sufuria ikiwa safi, wakati wa kupika.

Alisema ukataji miti kwa shughuli ya utengenezaji makaa huchosha. “Tumeshuhudia jinsi ambavyo watengenezaji makaa huteseka ila utengenezaji matofali huwa ni rahisi na inahitaji bidii kidogo tu,” Regina alieleza.

Alizidi kusema ya kwamba, utengenezaji matofali makaa hutoa nafasi za kazi kwa wanawake na vijana katika makao ya wakimbizi. Kikundi cha Loketa kina wanachama 40 ambao wamejiajiri kupitia utengenezaji matofali.

Wanawake hawa hutengeneza matofali 300 kwa siku na huzitafutia soko ndani ya makao yao na sehemu zingine za maeneo ya magharibi ya Nile.

Copy of Story 4 viz 2

Akiba katika shirika la VSLA

Regina anasema kwamba  faida wanayoipata husaidia wanachama wa kikundi kumudu mahitaji yao ya kinyumbani kama vile ulipaji karo ya shule na masalio yake huwekwa katika shirika la akiba la wanavijiji la VSLA.

Kikundi hiki hukodi ardhi kwa upanzi wa simsim kisha hutumia faida wanayoipita kupanua akiba yao na hutumia masalio ya mazao katika utengenezaji wa matofali zaidi. Wanachama hawa wanao uwezo wa kukopa fedha kutoka kwa akiba hii na kuilipia riba rmkopo huo riba hivyo basi kuinua kiwango cha akiba yao.

Baadhi ya wanachama wamepata kuanzisha biashara baada ya kukopa fedha kutoka kwa kikundi. Akiba ya kikundi hiki kimeboresha hali ya maisha ya kina mama wasio na waume, walemavu, wajane pamoja na walioolewa.

“Sisi husaidiana kifedha na kisaikolojia kama kikundi jambo ambalo ni sababu tosha linalotufanya kuhitaji usaidizi zaidi wa kifedha kutoka kwa mashirika mbali mbali utakaotuwezesha kuinua kiwango cha akiba pamoja na uwezo wa kukopa,” alisihi Regina.

Regina anaeleza kwamba pesa huwa haitoshi wakati wanachama wote wanapohitaji mkopo, jambo ambalo anadhani serikali na mashirika tofauti yanaweza kusaidia ili kuinua kiwango cha akiba kupitia msaada wa kifedha.

Kwa wakati huu, Regina anamudu biashara ya saluni pale Ariwa, ambayo alianzisha baada ya kupokea mkopo wa shilingi 300,000 kutoka kwa akiba ya kikundi.

Vile vile, Regina pia hufanya kazi kama mtetezi wa hali bora ya usafi katika kijiji chake na ambaye anawatunza watu 9. Shughuli zingine zinazoendeshwa na kikundi ni pamoja ushonaji fulana, kuoka mikate na utengenezaji shanga zilizorembeshwa. Bidhaa hizi huuziwa wafanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali, ambao hufanya kazi katika makao ya wakimbizi.

Mary Ajonje ambaye ni mwenyekiti wa kikundi hiki alisema kwamba matofali makaa husaidia kuzuia ukataji miti. Alielezea kuwa, kutumika kwa matofali makaa yaliyotengenezwa kutoka kwa kinyesi cha binadamu katika kupika kimepunguza gharama ya kununua kuni na makaa.

Ajonye alisema kwamba wanawake walioipanga utaratibu wa upishi wao vyema huweza kuandaa kiamsha kinywa, chakula cha mchana na hata kile cha jioni wakitumia matofali yaliyotengenezwa na kinyesi cha binadamu bila haja ya kuongeza matofali mengine.

Wamama hawa huyauza matofali kwa Sh. 1,000 hadi 3,000. Biashara hii ya matofali imewaepusha kuumwa na nyoka na kubakwa vichakani.

Jenifer Cana P6 Pupil of Ariwa Primary school in Ariwa village Rhinocamp Refugee settlement says she sells food ration to buy firewood Photo By Robert Ariaka

Ajonye ambaye pia hufanya kazi kama mwalimu anasomesha motto wake katika shule ya msingi ya Sir Andrews iliyo mjini Arua. Hali kadhalika, anamudu duka ndogo ambalo linampa pesa zaidi.

Ajonye, mama wa watoto tatu na ambaye anaishi na wengine watatu anasema kwamba mumewe hana kazi, hivyo yeye ndiye anayesimamia nyumba. Mumewe husaidia katika shughuli zingine nyumbani pamoja na kumudu shamba ndogo walio nayo.

Jenifer Cana, mwanafunzi wa darasa la P.6 katika shule ya msingi ya Ariwa aliambia gazeti la New Vision kwamba, huuza chakula kidogo kidogo ili apate hela za kununua kuni za kupikia.

Tita la kuni hugharimu Sh. 3500, sababu ambayo anasema matofali makaa ni bora zaidi.

Naye Neima Gaba mama mkimbizi wa mtoto mmoja aeleza kwamba, kabla aanze kutumia matofali makaa, yeye alitegemea kuni na makaa yaliotokana na miti.

“Wakati Oxfam ilileta mitambo ya kutengeneza matofali, niliwachana na kuni, sasa mimi natumia matofali makaa yanayodumu kwa muda mrefu kuliko kuni,” alisema Gaba.

Anazidi kusema kwamba matofali makaa umefanya wamama kutulia hivyo kuwapa nafasi ya kushughulikia kazi zingine huku wakiendelea kupika chakula.

Makundi mawili yamenufaika na mradi huu katika kambi ya Rhino, kikundi kimoja kikiwa sehemu ya Imvepi na mawili mengine yakiwa sehemu ya Bidibidi.

Utengenezaji wa matofali kutumia kinyesi cha binadamu ulianzishwa baada ya kikundi kuzuru mji wa Nakuru nchini kenya na kuelimika kuhusu mbinu zaidi.

Shirika la Oxfam limepata sehemu katika kambi ya Yoro kwa madhumuni ya kujenga kiwanda kitakachotumia kinyesi cha binadamu kutoa mali ghafi itakayotumika na wanawake kujenga matofali mengi zaidi. Kando na kiwanda hiki, kidimbwi kitajengwa cha kuzoa kinyesi kutoka mashirika tofauti. Huduma ya usafirishaji wa kinyesi kilichotibiwa utatolewa kuwezesha usambazishaji wa mali ghafi hii kwa vikundi hivyo kurahisisha utengenezaji matofali.

Hali kadhalika, baisikeli ya magurudumu matatu yatakuwa sehemu muhimu ya kiwanda hiki, ambazo zitakazotumika kusaidia wamama wakimbizi kupata soko na kuuza bidhaa yao ndani ya makao. Upanuaji wa uwezo, kuweka mikakati maalum ya soko, kuhusisha jamii na kutambua washika dau muhimu itazidisha jitihada za kulinda mazingira pamoja na kutoa njia mbadala za nishati huku ikiinua sekta ya kilimo.

Mawejje alisema kwamba mabadiliko makubwa yameshuhudiwa katika maisha ya wanachama ambao hupata tija yao kwa kuuza bidhaa hizi, hivyo kumudu maboma yao.

Utengenezaji matofali makaa hupunguza pakubwa ukataji miti hivyo kusaidia mazingira katika vita dhidi ya tabia nchi.

Mawejje alieleza kwamba tabia nchi ni jambo linalokumba ulimwengu mzima, ambalo husababisha mabadiliko ya misimu ya mvua, kitu ambacho kinahitaji washika dau wote kutilia maanani ulindaji wa mazingira na kuto njia mbadala wa nishati.

“Tukushinda kuzungumzia swala la mazingira na ukataji miti bila kutoa aina mbadala ya nishati, haiongezi manufaa,” Mawejje alisema.

Shirika la Oxfam huhakikisha kwamba sheria za mazingira pamoja na maswala yanayohusu maji yamehusishwa katika miradi yake. Katika kambi ya Rhino, wanachama 65 tayari wamenufaika, Imvepi wanachama 25 na wanachama wengine 50 katika makundi mawili tofauti yamenufaika kule Bidibidi, kila kikundi kikiwa na wanachama 25.

Copy of Story 4 viz 1

Biomass ya juu kwa juu AGB

Katika mwaka wa 2018, utafiti wa Woody Biomass Survey and Mapping uliendeshwa na shirika la World Agroforestry Center (ICRAF) katika kambi ya Rhino na makao ya wakimbizi ya Imvepi wilayani Arua.

Utafiti huu ulifanyika eneo la hektari 138,615.96 na biomasi la juu kwa juu, yaani Above Ground Biomass AGB wa mwaka wa 2018 ulitolewa katika takwimu zilizokusanywa mnamo Machi, 2018. Uzito wa wastani ulihesabiwa kwa uzani wa tani kwa kila hektari.

Bayomasi iliyopatikana ilikuwa ni tani 1,678,748.46 katika eneo zima ikiwemo ile ya kilomita 5 ya ziada. Biomasi ya miti ilikuwa tani 1,397,046.39 na tani 281,702.07 ya miti midogo midogo.

Kwa upande mwingine, bayomasi iliyopatiakana katika kambi ya Rhino ilikuwa tani 501,972.95, na tani 701,028.14 ilipatikana kule Imvepi katika kilomita 5 ya ziada.

Kati ya mwaka wa 2015 na 2018, palitokea mabadiliko ya aina ya mimea yanayokuwa katika eneo hili. Aina ya mimea ya LULC yalipungua huku aina nyingine ikinawiri. Mabadiliko haya yalisababisha mabadiliko makubwa ya bayomasi inayopatikana katika eneo la makao.

Kati ya mwaka wa 2010 and 2015, AGB iliongezeka kwa kiasi cha tani 96,680.10 huenda kwa sababu ya ile sehemu ya miti iliyotengwa kufuatia awamu iliyopita ya kuwakaribisha wakimbizi na kati ya mwaka wa 2015 na 2018, ilitokea hasara ya tani 522,255.76. katika miaka mitatu iliyopita hasara ya AGB ilikuwa tani 522,255.76.

Uharibifu mkubwa wa bayomasi ya miti unaonekana katika makao. Kati ya mwaka wa 2010 na 2015, bayomasi ya miti iliongezwa kupitia kutengwa kwa sehemu ya miti, hivyo kuongezeka kwa kiasi cha tani 96,680.10.

Hata hivyo, kati ya mwaka wa 2015 na 2018 hali ya bayomasi ya miti ilihatarika pakubwa, kufuatia ongezeko kubwa la matumizi ya kuni, vigingi ya ujenzi, utengenezaji wa matofali na makaa pamoja na uzalishaji mbao.

Hii ilisababisha hasara ya tani 522,255.76 ndani ya muda wa miaka mitatu. Hii inamaanisha ya kwamba hasara ya bayomasi kwa mwaka ni tani 174,085.25. ikizingatiwa ya kwamba kiasi cha bayomasi kwa jumla katika maeneo ya makazi ni tani 696,018.26, itachukuwa muda wa miaka takriban minne pekee, ikiwa wakimbizi watategemea bayomasi hii peke yake katika makao.

Njia mojawapo ya kuongeza kiwango cha bayomasi katika maeneo ya makao ili kukidhi mahitaji ya raslimali ya miti huenda ikawa ni kama ifuatavyo: kuirekebisha maeneo yaliyoadhirika kupitia upanzi wa miti, kumudu ustawishaji asilia wa mazingira, kuthibiti uvunaji haramu wa miti mikubwa kama ile ya Afzelia, Mahogany na aine ingine ya miti kwa madhumuni ya kutengeneza mbao.

Hitaji la kuthibiti moto msituni unaozuia ustawi asili wa maeneo ya miti ni muhimu katika kulinda miti na mimea asili katika makao ya wakimbizi.

Kurejesha hali ya kimazingira yafanikiwa

Jackson Olema, mkurugenzi wa mipango wa Rural Initiative for Community Empowerment RICE West Nile alisema kwamba katika mwaka wa 2018 juhudi za kurejesha miti iliyoharibiwa pamoja na mimea asili katika makao ya wakimbizi RICE ilipanda miti 317,000 katika eneo la hektari 288.18.

Hii imefanikiswa kwa upanzi wa miti zaidi katika mwaka wa 2019, wakati RICE West Nile ilipanda miti 1,041,729 katika eneo la hektari 890.75.

Upanzi huu unafuatia uharibifu wa miti katika makao ya wakimbizi iliyofanyika kurejesha hali kawaida ya mazingira.

Habari hii ilichapishwa kwa usaidizi wa kifedha wa InfoNile na CIVICUS Goalkeepers Youth Action Accelerator.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts