Vijana Wabadilisha Kinyesi Kuwa Nishati Eneo la Sebei

Vijana Wabadilisha Kinyesi Kuwa Nishati Eneo la Sebei

Na Melanie Aayou

Kundi moja la vijana, wengi wao wakiwa wa kike wilayani Kapchorwa, iliyoko eneo ndogo la Sebei, mashariki nchini Uganda, wameanzisha mradi mpya unaotumia nguvu za jua kuibadilisha kinyeshi cha mifugo na binadamu kuzalisha nishati madhubuti ya upishi.

Pick It Clean, aina ya biashara mpya ya kijamii – ni kampuni la kifaida linaloendeleza wema wa kijamii – limeanza kugawa vyoo vya kuchukulika katika maboma yasiyo na mazingira bora ya usafi. Kampuni hii pia inagawa mifuko ya taka kwa wakaazi walio na mifugo, kwa matumizi ya kukusanya samadi.

Mwanahabari wetu mkuu wa maswala ya mazingira Malanie Aanyu  anadokezea zaidi kuhusu habari hii ya uvumbuzi.

Ikiwemo katika jiji la Kapchorwa, iliyo takriban kilomita 225, sawa na maili 148, kaskazini mashariki mwa jiji la Kampala, kampuni ya Pick It Clean, linadhaminiwa pakubwa na jamii hususan wakulima. Hali ya joto jingi pamoja na mvua nyingi, imesababisha kuchelewa kwa shughuli za upanzi katika eneo ndogo la Sebei ingawaje msimu huu mpya tayari inashuhudia mvua kubwa inayonyesha.

Katika miaka 30 ya kuendesha ukulima, William Chelengat asema kwamba hajawahi chelewa kupanda mahindi kama miaka mitatu iliyopita.

“Wakulima hawana chakula cha kutosha tena ikilinganishwa na miaka 15 iliyopita: wakati mwingine inaponyesha siku hizi mvua huja kwa  kishindo hivyo kuharibu mazao shambani,” asema Chelangat aliye na miaka 75.

“Hata hivyo, jua huwaka kwa muda mrefu wakati mwingine hivyo kupelekea mazao kunyauka,” asema Yusuf Muhamud Mudundo aliyevunjika moyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu katika shirika la Kaserem Area – KACE.

Wakulima wa shirika hili, asema Mudondo, walimudu kuzalisha tani metriki 500 ya mahindi pekee katika msimu wa kwanza kiwango ambacho ni cha chini ikilinganishwa na tarajio la metriki tani 700, huku waliokuza maharagwe waliweza kuzalisha metriki tani 140 badala ya tani metriki 200 kama ilivyokuwa mwaka jana.

Taswira hii yaonyesha kwamba madiliko ya hali ya hewa inawafadhaisha wakulima hivyo kuhujumu uzalishaji wa mazao na kupelekea kutokea kwa njaa.

Mtazamo huu umepelekea vijana wa kiume na wale wa kike kujitokeza na uvumbuzi ambayo wanaamini kwamba itatoa majibu ya baadhi ya maswali ya mabadiliko ya hali ya hewa inayokumba jamii.

Copy of Story 3 viz 1

Kikundi hiki kinasema kwamba juhudi hizi zitazuia ama kuepusha jamii kudhuru mazingira unaosababishwa na ukataji miti, jambo ambalo wanasema linaongeza viwango vya tabia nchi.

Joan Chusto, ambaye ni kiongozi wa kikundi hiki, anaamini kwamba Sebei Youth Biogas Project linalojulikana pia kama Pick It Clean itakabiliana na ukataji mkubwa wa miti kwa minajili ya kuchoma makaa.

Wanaonelea pia kwamba juhudi hii ni mkakati madhubuti kuboresha hali ya usafi katika jamii, ambayo watu wake wengi hawana vyoo manyumbani mwao na pamoja na kutengeneza mbolea itakayotumika katika shamba zao.

Kikundi hiki kimeweza kuwavutia washirika zaidi ya 350 ambao tayari wanatumia uvumbuzi huu muhimu.

Uvumbuzi huu ni wa kwanza aina yake katika eneo hili ndogo la Sebei, mashariki nchini Uganda, ulioanzishwa miaka miwili iliyopita na ambao uhitaji wake uko juu – huenda basi hii inaashiria kuwa watu wa kawaida katika eneo hili la nchi wameanza kuthamini na kuelewa mchakato wa tabia ya nchi.

“Ni wazi kwamba siku zetu za usoni zitaamuliwa na hali halisi mashinani. Idadi enyeji sasa inathamini uvumbuzi wetu na sasa wameumiliki,” alisema William Chepteok, mkuu wa harakati katika kikundi cha Sebei Youth Biogas Power Plant Project.

Kulingana na Chepteok, daima imekuwa madhumuni yao kuhakikisha kwamba hawajiweki hadharani ili kuepuka kujiweka katika hali ngumu ya kuchunguliwa.

“Kila wakati sisi uhakikisha tunajifunza kutoka kwa makosa tunayofanya na kuyarekebisha pasi na watu kutoka nje kutufanya tufe moyo, sisi kama kikundi. Tunajivunia bila shaka kuwa hatimaye tumefika mahali tupo sas, ila bado yako mengi tunahitaji kugundua na kufanya,” Chepteok aliongeza kusema.

Kundi hili lina wanachama kumi; saba kati yao wakiwa wakike na wakiume watatu, wengi wao wakiwa wahitumu wa vyuo vikuu ambao hawana kazi. Saba ya wanachama hawa walisomea taaluma ya kilimo ama uhandisi wa kemikali katika chuo kikuu.

Kulingana na Joan Chemusto, ambaye ni kiongozi wao, walilazimika kuingilia kati kwa vile jamii ilikumbana na adhairi za tabia nchi. Walianza kwa kuwazua mikakati muafaka dhidi ya tabia nchi kabla ya kuafikiana kuhusu pendekezo la kiwanda cha kuzalisha nishati itokanayo na samadi.

Vyoo vilivyoundwa na wenyeji vijulikanavyo kama “Blue Boxes”, hubebeka na havihitaji usakinishaji.

Baadaye, kinyeshi kilichokusanywa na kikundi kutoka kwa vyoo hivi hutiwa ndani ya mtambo, kama malighafi. Ili kupata kutumia choo hiki, itakulazimu kujisajilisha kama mtumizi wa kila mwezi ama hata bora zaidi, kujisajilisha kama mtumizi wa kila mwaka kwa gharama ya UGX 10,800 (shilingi elfu kumi na mia nane), sawa na $3, pesa za Marekani.

Huku UGX 129,600 (shilingi elfu mia moja ishirini na tisa na mia sita), sawa na $36 pesa za Marekani ndio gharama ambayo mtumizi anapaswa kulipa kwa mwaka.

Waliojisajilisha huruhusiwa kukatiza uchango wao watakavyo, ila tu hutozwa gharama iliyo ya juu kidogo wanapobadili nia na kurejelea kupokea huduma hii tena, hii kulingana na masharti na taratibu za mradi.

Madhara kwa jamii yatokanayo na ukosefu wa hali bora ya vyoo vya kisasa ni kubwa, alisema Dkt. Beatrice Aguti wa hosipitali ya rufaa ya Mbale mkoani.

Sababu kubwa ya vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano nchini Kenya ni kuharisha, shida ambayo inachochewa zaidi na ukosefu wa hali bora ya vyoo, alisema. Maboma mengi katika maeneo yaliyo kando na miji hayana usakilishaji wa mabomba ya ndani kwa ndani majumbani, hivyo kupelekea wakaazi kuenda haja kubwa nje, alisema.

“Uondoaji kinyesi ulio salama ni njia bora zaidi ya kuepusha uharishaji. Hii ni changamoto kubwa kwa wengi wa wakaazi katika maeneo yaliyo kando ya miji, ambao kwa kawaida huwa wa mapato ya chini,” Aguti alisema.

Chemusto asema kwamba ilichukuwa muda wa miezi sita kukusanya hela na kushawishi wanavijiji kujiunga na harakati hii.

Patrick Chemonges one of the team members feeds empty plastic water bottles into the chrushing machine

Alipoulizwa ni hali gani ya kifedha iliwawezesha kuzindua mradi huu, Chemusto alisema kwamba iliwagharimu kitita kilichozidi UGX milioni 15, ambayo ni sawa na $4,166.6 pesa za Marekani. Hela hizi ziliwasaidia kununua mitambo kadhaa, kukodisha nafasi ya kufanyia kazi, kununua mifuko halisi ya taka na kugharamia ajara.

Takriban vyoo 60 tayari vimeshatolewa kuhudumia watu 300. Hata hivyo kinachofanyiwa kinyesi baada ya kukusanywa kutoka vyoo hivi ndicho kitu kinachofanya mradi huu kuwa na umuhimu mkubwa zaidi ya juhudi ya kawaida ya kuboresha hali ya usafi.

CHANGANYA, PIKA NA CHOMA

Kinyesi huchanganywa na vumbi wa makaa na mabaki ya mimea iliyotolewa kutoka kwa mashamba ya maua jirani, ambayo huwa tayari ishachomwa na kupondwa hadi kuwa poda nyepesi. Pick It Clean hutumia teknologia ya nguvu za jua inayoelekeza miale ya jua, hivyo kuipasha moto kinyeshi hiki hadi kufikia hali ya joto ya juu zaidi inayouwa viini vilivyomo, na kuifanya salama kutumika tena.

Mchanganyiko huu hufinyangwa na kuwa matofali yasiofuka moshi ambayo watu hununua ili kupikia nyumbani. Chemusto asema kwamba, mradi huu wao ni mojawapo wa miradi ya aina ya kipekee unaotumia mfumo wa kubadilisha kinyesi kutumika kama makaa.

Norah Chelengat, mama wa watoto tano kutoka Manispaa ya Kapchorwa amekuwa akitumia choo cha Blue Box nyumbani, huku akipikia matofali ya Pick It Clean kwa mwaka mmoja.

“Kwa vile choo hiki hubebeka, inamaanisha ya kwamba kinaweza kutumika katika chumba chochote cha nyumba. Hivyo basi, hupaswi kutatizika kuenda nje ili kukitumia,” alisema.

Chelengat hutumia nusu kilo ya matofali haya kupikia. Ingawaje humgharimu shilingi 900 ($0.25) kwa kilo moja, gharama iliyo juu kidogo ya pesa angehitajika kulipia makaa ya kawaida, asema kwamba matofali haya hudumu kwa muda mrefu – hadi masaa manne.

“Hauhitajiki kuongeza makaa kila mara unapopika, kwa vile yanadumu kwa muda mrefu,” Chelengat alisema. Faida yake ingine ni kwamba matofali haya hayafuki moshi wala kutoa harufu, alisema.

“Wateja wanapotumia matofali haya, yaliyonunuliwa kwa bei ya juu kuliko makaa, inamaanisha kuwa, ufanisi wake wa huduma ya muda mrefu, kwa hakika huwaokolea asilimia 10 hadi 15 ya gharama wanaotumia kununua makaa kila mwezi,” Chemusto alikadiri.

Anaamini kwamba, watu wanapendelea huduma hii kwa vile huwapa nafasi ya kutumia choo kisafi katika manyumbani mwao.

DOSARI

Ingawaje jamii nyingi nchini zahitaji huduma hii, hata hivyo kikundi hiki kinasema kuwa,hakina uwezo wa kupanua uvumbuzi wao.

Hawana hela za kutosha kuendeleza mradi huu hadi kupanda katika jukwa lililo kubwa zaidi, hii ni kando na kuwa bado hawajajisajili na mamlaka ya umeme ya Electricity Regulatory Authority – ERA.

Isaac Kiprotich, ambaye ni mkuu wa mipango anasema kwamba wao wanahitajika pia kupata elimu kuhusu uzalishaji na usimamizi wa nishati mbadala ya hali ya juu, jambo ambalo anasema limekwama kutokana na ukosefu wa fikra mpya.

“Changamoto kuu tuliyokumbana nayo tangu uanzilishi wa mradi huu hapo mwaka wa 2017 imekuwa ni gharama ya kupanua ujuzi tulionao kuhusu nishati mbadala kwa vile hatunazo hela kufanikisha lengo hili,” alisema.

Licha ya changamoto hizi, kikundi kimejizatiti na kukodisha mtambo wa kusaga chupa za plastiki, katika jitihada za kulinda mazingara.

“Chupa za plastiki ambazo zimekwisha kazi, huchukuwa nafasi kubwa pasi na kusagwa, na kama hazitatumika tena, huenda zikasababisha madhara makubwa katika mazingira,” Bw. Kiprotich alisema.

Akiendelea kusema kwamba, “kuzisaga halafu kuzikusanya katika vijalala huokoa nafasi hivyo basi kuwezesha nchi yetu kuzitumia tena chupa hizi kwa wingi.”

Wao huajiri vibarua ambao husaidia katika ukusanyaji wa chupa za plastiki zisizo na kazi kutoka mkoa mdogo wa Sipi ikiwemo Bukwo, Kween na Kapchorwa. Wao pia hupata chupa hizi kwa kiwango fulani kutoka mji wa Mbale.

Chupa hizi husagwa kutumia nishati ambayo wao wenyewe wamezalisha.

Chembechembe hizi za chupa zilizosagwa hupimwa kwa kilo ambazo huuziwa makampuni ya chupa mjini Kampala kila wiki.

“Sababu kuu ya kuzisaga ni kwamba chupa hizi huchukuwa nafasi kubwa na muda mrefu zaidi wa kuzisafirisha hadi kwa wanunuzi mkoani Sipi ambao huzifanya zitumike tena,” Kiprotich alihoji.

Baada ya haya yote, kikundi kinasema kwamba hawawezi fanikisha mawazo yao ya kufana pasi na usaidizi kutoka kwa serikali, wafadhili na umma.

Irene Muloni, waziri wa nishati apongeza juhudi ya mradi wa Sebei Youth Biogas Power Plant.

Hata hivyo, Muloni alihimiza kikundi hiki kulifanya ombi lao la kutaka usaidizi wa serikali kuwa rasmi, ili kupelekea kutueuliwa kwa kundi maalum litakalosimamia harakati zao, pamoja na kufahamisha wizara na mashirika husika kuhusu hatua wanazozipiga.

“Serikali iliyoko mamalakani imejitolea kuwapa moyo na kutoa usaidizi kwa vumbuzi kama hizi zinazoendeshwa na jamii, na ningependa kuwaahidi kwamba afisi yangu itafuatilia mradi huu ulioko Kapchorwa kuhakikisha kwamba unasaidika punde tu tutaamua hivyo,” Muloni ambaye ni waziri wa Nishati alisema.

Copy of Story 3 viz 3

Sawa na Muloni, waziri mwenzake, Sam Cheptoris katika Wizara ya Maji na Mazingira alivutiwa na juhudi hii ya kupambana na tabia nchi inayoendeshwa na jamii na vijana. Cheptoris, ambaye pia anatoka mkoa mdogo wa sebei ambamo mradi huu unaendeshwa, alisema kuwa afisi yake itatilia maanani usaidizi wowote muhimu utakaohitajika na kikundi hiki, ili kuinua mradi huu wao.

Kulingana na mamlaka wa kitaifa wa misitu – NFA, ni kwamba mkoa wa Sebei ni ya pili tu nyuma ya Teso mashariki nchini Uganda kwa ukataji miti. Rekodi za mwaka wa 2017 zaonyesha kwamba mkoa huu hukata 38% ya miti kila mwezi. Lawama imeelekezwa kwa ukusanyaji kuni na kufyeka ardhi kwa minajili ya shughuli za kilimo.

Washirika wa kundi la Sebei Youth Biogas Project wanaisisitiza ya kwamba, jambo hili libakia kuwa kumbukumbu tu, hata hivyo watahitaji usaidizi mkubwa wa kiufundi, kifedha na usaidizi mwingine wowote ili kufanikisha jitihada hizi.

Makala haya yameandaliwa na Time FM pamoja na Elgon Daily kwa hisani ya InfoNile, shirika lisilo la kifaida.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts