Na Aimable Twahirwa
Ni masaa ya asubuhi Jumatatu moja lenye joto jingi huko Nyamagabe, ambayo ni wilaya iliyo na milima mingi Kusini mwa Rwanda, ambako kundi la vijana limekusanyika kwa mkutano, ili kushiriki katika mafunzo muhimu ya kuzuia momonyoko wa udongo wa kila mara hadi mto jirani wa Nyabarongo.
Mkakati huu ni mojawapo ya zoezi la kuhusisha jamii, katika jitihada za kitaifa za kulinda vyanzo vya maji vya mto Nyabarongo, ukilenga wakulima milioni 1.9 waliokandarasiwa ili kumudu manufaa inayoletea jamii asili kupitia mashamba yaliyowekwa matuta, upandaji miti kati ya mazao na upandaji miti kwenye kingo za mto huu, ambayo ni sehemu ya juu ya Mto Nile.
“Kupitia mradi huu, tulipata kujifunza mengi kuhusu mbinu bora za ukulima, zinazozingatia sera kadhaa za uhifadhi,” alisema Alphonsine Mukangarambe, mkuu wa “Abishyizehamwe” shirika enyeji la wakulima vijana.
Abishyizehamwe, linalomaanisha ‘wale wanaokuja pamoja,’ lilianzishwa mwaka wa 2015 kuhamasisha jamii enyeji wilayani Nyamagabe, katika uhifadhi wa udongo na maji inayobebwa kando kando ya mto Nyabarongo.
Ulimaji Mkubwa wa Mashamba ya Matuta
Kufukia Agosti 2019, takriban hektari 138,452 katika chanzo cha juu cha mto Nyabarongo, zilikuwa tayari zimeshadumishwa na wamilki ardhi, kwa mujibu wa makadirio rasmi.
Katika awamu yake ya utekelezaji, mradi huu uliwalenga vijana wanaojihusisha na harakati tofauti za kiuchumi, kama vile ukulima katika wilaya kadhaa, zikiwemo Muhanga (Kati ya Kusini), Ngororero (Magharibi), Ruhango (Kusini), Nyamagabe (Kusini) Gakenke (Kaskazini), kwa madhumuni ya kulinda chanzo cha mto Nyabarongo kupitia upunguzaji wa momonyoko wa udongo, na kulinda na kudumisha ubora wa maji.
Upande wa juu wa chanzo cha Nyabarongo ni sehemu ya bonde la Mto Nile, inayoteremka kutoka kusini hadi kaskazini katika eneo la magharibi nchini Rwanda, ukubwa wake ukiwa ni kilomita mraba 3,348.
Chanzo hiki cha maji, kinafahamika kama mnara wa maji unaozipa nguvu vijito vingi, miongoni mwao na yenye umuhimu mkubwa ni (kutoka kusini hadi kaskazini) Mto Mwogo (kilomita 81.1), Mto Rukarara (kilomita 47.4 zinazozuka kutoka mito ya Rubyiro na Nyarubugoyi), Mto Mbirurume (kilomita 51.6), Mto Mashiga (kilomita 12.2), Mto Kiryango (kilomita 10.4), Mto Munzanga (kilomita 24.4), Mto Miguramo (kilomita 15.0) na Mto Satinsyi (kilomita 59.7).
Kufikia sasa, jamii zinazomiliki ardhi katika chanzo cha mto Nyabarongom tayari zimeshasajiliwa kupokea usaidizi na kushirikishwa katika utekelezaji wa mradi, huku maafisa nchini Rwanda wakitilia mkazo wa utumizi bora wa maji.
Huku juhudi hizi zikiwalenga vijana wa mashambani na wakulima wachanga, kundi hili la wafanyakazi linahimizwa kuzingatia kilimo cha matuta kama njia ya kupunguza upoteaji wa udongo unaosababishwa na msukumo wa maji.
Chini ya miradi tofauti ya kuhifadhi mto huu, hektari 912 kati ya hektari 1,102 inayokalia vyanzo vya Nyabarongo, tayari imesharegeshwa wilayani Muhongo (ya Kati) na Ngororero (Magharibi) kupitia mashamba ya matuta, upanzi wa miti na upanzi miti mashambani pamoja na kuendeleza uchimbaji madini endelevu, kwa mujibu wa ripoti rasmi. Kupitia juhudi hii, baadhi ya wakulima wachanga huko Nyamagabe wamewezeshwa kukuza mazao kama vile muhogo, viazi, viazi vitamu, mahindi na maharagwe.
Mukangarambe sasa asema kuwa juhudi hizi zimebadilisha jinsi ambavyo wakulima wachanga wanavyoendeleza kilimo katika maeneo yenye mwininuko mkubwa, huku wakizuia momonyoko na kutoa chakula pamoja na kuthibiti mapato kwa njia endelevu, kando kando ya mto Nyabarongo.
Mkuu wa idara ya uthibiti maji ya Integrated Rain Water Management katika mamlaka ya raslimali asili ya Rwanda Natural Resources Authority, Francois Xavier Tetero alieleza kwamba, kwa kuweka mipangilio mathubuti inayohusisha vijana katika jamii asili za kilimo, raslimali za maji nchini Rwanda zaweza kutumika kwa njia muafaka.
Hata hivyo, Mukangarambe alalamika kwamba wakulima wachanga kutoka maeneo haya ya mashambani hawapatiwi nafasi muafaka kutoa mchango wao katika utekelezaji wa juhudi kama hizi.
“Wakulima hawa wachanga huathiriwa zaidi ya kundi lingine lolote ila, wakati juhudi kama hizi zinapodumishwa, utapata kwamba idadi chache sana ya vijana kutoka maeneo haya uhusishwa,” alisema.
Pingamizi dhidi ya ukuu ndani ya bonde la mto Nile
Mradi wa chanzo cha mto Nyabarongo uliaanzishwa mnamo mwaka wa 2010 baada ya Rwanda kuidhinisha makubaliano ya Nile Basin Cooperative Framework Agreement, inayohakikisha maji tosha kwa miradi ya umwagiliaji maji, viwanda vya usambasaji maji, miradi ya umememaji na miradi zingine zinazohitaji leseni ya matumizi ya maji.
Sheria iliyoidhinishwa mwaka wa 2010 inaziwezesha kila moja ya nchi kutumia raslimali shirikishi kwa maendeleo yao binafsi, bali na kuhitaji kwamba mradi wowote mpya usije ukasababisha mathara kwa nchi ingine, kulingana na wataalamu.
Mto Nile ulio na urefu wa kilomita 6,853 na unaopitia mataifa kumi na moja, ni tegemeo muhimu ya takriban nusu bilioni ya watu.
Majiji yote kando kando wa mto huu, yamekuwepo kutokana na maji haya. Hii ni dhahiri haswa kwa nchi ya Misri: pasingelikuwepo mto Nile, basi nchi hii ingelikuwa tu sehemu mojawapo ya Jangwa la Sahara.
Nchi ya Misri imejitahidi kudhibiti mto huu kwa karne nyingi zimepita, huku ikiazimia usimamizi wa kipekee wa matumizi yake. Hata hivyo, nchi ambamo vyanzo vya mto huu unapatikana, ikiwemo Rwanda inapinga ubabe wake, ikitaka ugavi mkubwa wa maji ndani ya vyanzo ya mto huu.
Nchi za Misri na Sudan bado zinazingatia maagano mawili ya miaka ya 1929 na 1959, kuwa halali kirasmi, huku mataifa yenye vyanzo vya mto – baada ya kujipatia uhuru – yalianza kupinga makubaliano haya yaliyoafikiwa chini ya utawala wa kikoloni.
Agano la mwaka wa 1959 ilipatia nchi ya Misri asilimia 75 ya maji ya mto huu, huku Sudan ikambulia masalio.
Misri daima imetetea ubabe wake kwa misingi ya hali yake ya kijiografia na maendeleo ya kiuchumi, kwa vile nchi hii ni kame na kuwepo kwake hakuwezekani pasipo maji ya mto Nile, huku nchi zilizoko katika vyanzo vya mto huu hupokea mvua tosha kuendeleza kilimo kisichotegemea umwagiliaji maji.
Jitihada lile la The Nile Basin Initiative (NBI), liloanzishwa mwaka wa 1999 kwa azimio la “ kulinda na kutumia kwa usawa maji na raslimali ambatisho la bonde la Nile”, huenda ukawa mfano muafaka wa kutatua migogoro la eneo hili, hata hivyo hii imesalia tu kuwa maongeo unaohusu udhibiti wa maji.
Kitaasisi, jitihada hili la NBI sio tume. Ila ni “la mpito” tu, huku likisubiri maafikiano kamili ya utumiaji wa maji ya mto Nile, hivyo basi halina nguvu kisheria zaidi ya makubaliano yake ya makao makuu na nchi ya Uganda, kunakokaa ukatibu.
Kutokana na tofauti ambazo hazijatatuliwa, NBI imeangazia tu miradi ya kiufundi, yasiyo ambatana na siasa. Hii inapelekea kuhafifisha asasi kwa vile Misri haioni tofauti kati ya maswala ya kisiasa na kiufundi. Hivyo basi, Cairo ilisitisha kushiriki kwake katika mengi ya maswala ya NBI, hivyo kudhoofisha hali ya asasi kisiasa.
Ukupanuaji wa uwezo
Maafisa nchini Rwanda wanaamini kuwa uhifadhi wa vyanzo vya Nyabarongo huchochea utaratibu ambao hupelekea vitendo ambavyo hulenga kupanua uwezo wa kulinda maji pamoja na kuhimiza matendo mema ya raslimali ya Integrated Water Resource Management nchini.
“Tunarajia kwamba itakapotimia mwaka wa 2024, mikakati hii ya pamoja kutoka kwa wadau wote, wakiwemo vijana, itasaidia kubadilisha maji ya mto Nyabarongo kuwa masafi,” alisema.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na wanahabari jijini Kigali, Ebel Smidt, kiongozi katika shirika la maji la Water for Growth Rwanda alieleza kwamba sehemu ya juu ya chanzo cha Nyabarongo ilikuwa ni mradi wa kwanza wa kuregesha na kuhifadhi hali ya mandhari ya kiwanda cha umememaji kilichozinduliwa nchini Rwanda.
“Tunajitahidi kupanua uwezo na ustadi wa wadau mbalimbali katika taaluma ya kudhibiti raslimali ya maji kando kando ya chanzo cha juu cha mto Nile,” alisema Smidt.
Mradi huu ambao unadhaminiwa kwa pamoja na Serikali ya Rwanda na wadau wengine, unalenga maji ya juu ya ardhi, yanayotokana na mvua ndani ya mipaka hii na ambayo inateremka hadi kipenyo cha kugawizwa.
Hivi leo, maafisa wa serikali za mtaa wanaona uwezekano wa kuwahusisha vijana katika kulinda raslimali asili, kama mojawapo ya njia ya gharama ya chini ya kuhakikisha ugavi wa maji yenye kubebeka.
Katika mipango ya kulinda vyanzo vya maji, kama ile ipatikanayo kando ya mto Nyabarongo, wakulima wachanga hulipwa kutumia mbinu za kuhifadhi udongo na maji – haya ni malipo ambayo hunufaisha jamii, alisema Jean Lambert Kabayiza, makamu wa meya anayesimamia maswala ya kijamii na kiuchumi wilayani Nyamagabe.
Ripoti hii ilichapishwa kutokana na usaidizi wa kifedha wa InfoNile na CIVICUS Goalkeepers Youth Action Accelerator.