Kuna hofu kwamba hali mbaya ya hewa katika Kaunti ya Turkana huenda ikachochea pakubwa ukosefu wa chakula, huku shaka ikitanda kuwa wanafunzi watakatiza masomo yao. Wanafunzi wamekosa chakula baada ya mashirika yaliyosaidia serikali katika mpango wake wakuwalisha wanafunzi kusimamisha usaidizi huo, kufuatia kucheleweshwa kwa msaada kutoka kwa wahisani. Afisa anayesimamia ubora wa elimu katika Kaunti hiyo, Bwana Kavai Kisia, alisema kuwa ukame umathiri vibaya mashule.
