Majiji madogo yanayo zidi kukuwa, yametambulika kuwa tisho ya moja kwa moja kwa upatikanaji wa maji, usafi wa mazingira, na uendelevu wa afya.
Siku ya maji inavyoadhimishwa siku ya leo, takwimu zaonyesha upungufu mkubwa wa maji kwa kila Mkenya.
Usitawi wa kiholela huzorotesha pakubwa raslimali ya maji; maji yamepungua kwa kiasi cha asilimia 80 kwa kipindi cha miaka 45 imepita.
Wakihotubia waandishi wa habari, maafisa wa shirika la kibinadamu la Water Aid East Africa, walidokeza kuwa majiji madogo husitawi pasipo mpangilio maalum, hivyo kusababisha changamoto ya maji.