Pamoja na Kuzidisha Visa vya Unyakuwaji Ardhi: Mabwawa na Matanaki Yazidisha Ukosefu wa Maji

Pamoja na Kuzidisha Visa vya Unyakuwaji Ardhi: Mabwawa na Matanaki Yazidisha Ukosefu wa Maji

Kaswa ni kijiji kidogo kando ya mto Muzizi, kilomita 285 magharibi ya Kampala, katika mpaka wa wilaya za Kagadi na Kyenjojo. Hekta 17 ya kijiji hiki kimekalia eneo ambalo, kwa muda wa miaka mitatu ijayo, litageuka kuwa bwawa la uzalishaji umeme.

Wanavijiji katika eneo hili ni miongoni ya watu 829 watakaohamishwa kwa madhumuni ya ujenzi wa bwawa la umeme la Muzizi, utakaozalisha megawati 45 wa umeme, ambao ni mradi wa serikali ya Uganda.

“Kwa ujumla, mradi utahitaji hekta 473,” asema Vincent Kisembo, mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini katika kampuni ya uzalishaji umeme ya Uganda Electricity Generation Company Limited. Na wale watakaohamishwa, “watafidiwa vyema,” adumisha Kisembo.

Hata hivyo, Jennifer Mbabazi, mmbunge wa wilaya ya Kagadi asema kwamba walioadhirika kutokana na mali yao kuthaminiwa hapo awali, “wamekumbana na shida zisizotajika.”

“Walilazimishwa kutia sahihi kwenye hati za ukadiriaji. Mali yao ilidhaminiwa kwa kiwango cha chini na sasa hawawezi kupata ardhi kwa makaazi mapya,” asema Mbabazi.

Mgogoro wa upatikanaji ardhi kwa madhumuni ya ujenzi wa bwawa sio kisa geni. Imebakia kuwa swala shindani ulimwenguni mzima. Kwa mfano, bwawa maarufu la Grand Ethiopian Renaissance Dam katika Mto Nile nchini Uhabeshi, ilipelekea watu 20,000 kuhamishiwa; lile la Upper Atbara na Setit Dam Complex katika Mto Atbara uliozinduliwa na serikali ya Sudan katika mwaka wa 2017, iliwalazimu watu 30,000 kuhama. Na hapa nchini Uganda, takriban watu 300 walioishi vijiji vile vya Akurudia, Karuma, Awoo na Nora walihamishwa ili kufanikisha ujenzi wa bwawa la uzalishaji umeme katika Mto Nile.

Upatikanaji na matumizi ya maji katika mabonde ya mito yanawiiana kwa undani na maswala ya ardhi. Mabwawa na matanaki makubwa hupunguza kiasi cha ardhi asili, hivyo kuzidisha ongezeko la wakimbiaji wanaotoroka migogoro na kuongeza shindikizo la ardhi katika jamii zinazowapokea.

Mabwawa na matanaki yanavyozalisha nishati mbadala ambayo inahitajika kwa kiasi kikubwa; pia hutoa maji ya kilimo; matumizi ya viwanda; uthibiti wa mtiririko wa mto na mafuriko. Hata hivyo, utafiti mpya ya wanasayansi yaonyesha kwamba mabwawa na matanaki yanaweza kurembua athari mbaya zitokanazo na ukame na ukosefu wa maji.

Utafiti huu uliochapishwa katika jarida la Nature Sustainability mwisho wa mwaka uliopita, ni juhudi ya miaka tatu ya ushirikiano kati ya wanasayansi kumi wanaotafiti maswala ya ukame kutoka mataifa manane tofauti, na ambayo iliratibiwa na Profesa Giuliano Di Baldassare katika idara ile ya Sayansi za Dunia katika chuo kikuu cha Uppsala kilichoko Uswidi.

Katika makala haya ya maswali na majibu, Fredrick Mugira ambaye, mnamo mwaka wa 2017, alishirikiana na Benedict Moran mwandishi kutoka Uingereza kunakili kikamilifu katika New Vision Online jinsi ambavyo ujenzi wa bwawa la Gibe III kando ya Mto Omo nchini Uhabeshi umeathiri ziwa, na jamii ya El Molo – kabila ndogo yenye idadi ya watu chini ya 2,000 nchini Kenya. Tegemeo pekee la jamii hii likiwa samaki kutoka Ziwa Tana,. Mugira alimuhoji Profesa Giuliano kuhusu utafiti huu mpya ambao aliuratibu.

Fredrick: Itakuwaje mabwawa na matanaki yaliyojengwa kukabiliana na ukame na upungufu wa maji kuzorotesha hali hii?

Profesa Giuliano: Tunahoji kwamba kuna dhana mbili zisizowiana na ambazo zahitaji kuzingatiwa katika upanuzi wa matanaki: Duru ya ugavi-hitaji ya maji na athari za matanaki. Duru hizi zaelezea jinsi ambavyo kuongezeka kwa ugavi wa maji hupelekea mahitaji yake kupanda, hadi kufutilia mbali manufaa ya hapo awali yatokanayo na matanaki. Athari hutokana na kuzitegemea matanaki kwa kisasi kikubwa hivyo kuzidisha hatari na kupelekea uwezekano wa mathara yasababishwayo na ukame. Twamaanisha kwamba, kusudi lile la matanaki la kukabiliana na athari za ukame na upungufu wa maji, huzorotesha zaidi hali hii kwa uhakika. Hii ni kinyume na ufahamu na mara nyingi huwa haitarajiwi.

Fredrick: Ni mabwawa na matanaki kama yapi Afrika yaliochochea hamu yako ya utafiti?

Profesa Giuliano: Bwawa lile la Grand Ethiopian Renaissance Dam limetajwa wazi katika utafiti. Bwawa hili ni miongoni mwa mabwawa na matanaki mapya yanayopangiwa kujengwa katika nchi za kanda ya kusini ulimwenguni.

Fredrick: Kuna mipango ya miradi mikubwa ya mabwawa na mengine yanaendelea katika bonde la Mto Nile, ambamo asilimia 90 ya uzalishaji umeme hutokana na umememaji, je yawezekanaje kupendekeza kutotegemea pakubwa miundo msingi mikubwa ya maji, kama vile mabwawa na matanaki katika eneo hili?

Profesa Giuliano: Hatuwezi jumulisha visa vyote kwa pamoja, kwa kuwa kila kisa ni tofauti. Je, matanaki huwa mabaya kila mara? La, si mabaya. Swali letu ni, wakati njia mbadala za kukabiliana na ukame na upungufu wa maji zinapotathminiwa, inafaa tumakinike kwa uwezekano wa kutokea kwa athari zisizo tarajiwa ambazo uhusishwa na kuongezeka kwa upungufu wa maji. Kila mbinu badala hupelekea kutokea kwa athari za kijamii, kimazingira na zile za kiuchumi, ambazo vile vile huandamana na manufaa za kijamii, kimazingira na za kiuchumi kwa makundi tofauti ya jamii. Kwa kawaida, maswala yote yahitaji kuangaliwa kikamilifu, kwa njia ya uwazi na ya kidemokrasia ambamo wadau pamoja na wataalamu kutoka nyanja tofauti wahusishwe kikamilifu.

Fredrick: Utafiti wako watumia mifano ya kule Marekani, je inawiana vipi na hali halisi iliyoko Afrika?

Profesa Giuliano: Tunachanganua kumbukumbu ya data ya ulimwengu nzima pamoja na ya eneo hili na kufafanua maelekeo ya kijumla. Kwa kweli, utafiti wetu ulichochewa na mapendekezo ya ujenzi wa mabwawa na matanaki zaidi katika mataifa mengi barani. Hii inatokana na dhana asilia kwamba “inatubidi kuongeza upatikanaji wa maji kukithi mahitaji”. Naonelea kwamba, fikira hii imebakia kudumu pia kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa maarifa ya athari za siku za usoni (miongoni mwao ikiwa mathara yasiyo tarajiwa) inayohusisha maeneo na muda unaohitajika kwa ugavi, upatikanaji na hitaji ya maji. Kwa hio, tunapendekeza ajenda ya utafiti inayohusisha nyanja tofauti kwa menajili ya kuelezea uhusiano kati ya masuala ya maji, jamii na miundo misingi ya maji.

Fredrick: Wamaanisha vipi unaposema ugavi wa eneo na muda?

Profesa Giuliano: Namaanisha, jinsi ambavyo upatikanaji na mahitaji ya maji yanavyobadilika kulingana na eneo ambapo makundi fulani hunufaika zaidi ya mengine kwa muda, huku hali ya hewa na ile ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi ikichangia pia.

Fredrick: Kulingana na matokeo ya utafiti wenyu, ni mikakati ipi inafaa kuzingatiwa na serikali za nchi zilizoko katika bonde la Nile, ambazo hukumbana na mafuriko na upungufu mkubwa wa maji, ili kuhakikisha kwamba mabwawa na matanaki yanayojengwa hayarembui mikasa hii?

Profesa Giuliano: Kando na iliyotajwa hapo mbele kuhusu umuhimu wa uhusikaji katika maamuzi ya masuala ya maji, ni muhimu kutotegemea pakubwa miundo misingi, ila kusisitiza mikakati mingine. Miongoni ya mikakati hii ni kwa mfano, mifumo ya tahadhari ya mapema na kuweka misimbo ya mafuriko pamoja na kuzingatia kilimo kisichotumia maji mengi.

Makala haya yamewezekana kwa hisani kubwa ya Pulitzer Center on Crisis Reporting

Print Friendly, PDF & Email

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts