Swala la mafuta nchini Sudan ni lile la mabishano, vurugu la pesa, mapigano na ubeberu ambalo limepindamana na muongo mzima wa vita. Uchunguzi mpya wa InfoNile unabaini wazi masikitiko kwa wakaazi wa jimbo la West Kordofan, nchini humo, yanayoletwa na sekta ya mafuta: ukame unaongezeka, mifugo kufa hata kutokea kwa hali ya afya isiyoeleweka, ambayo inawakumba watu na mifugo isababishwayo na uchafuzi wa hewa katika mabarabara na vyanzo vya maji.
