Patrick Kossima, Unyanja FM Radio
Hali ya kukimbizana kimbizana kati ya wavuvi na maafisa wa idara ya uvuvi katika kijiji kimoja cha ufukwe wa Ziwa Nyasa, huenda kinachangia kutokuwa kwa vyoo vinavyotosheleza eneo hili.
Kijiji cha Chiulu kiko takriban kilomita 7 kusini mashariki mwa makao makuu ya Wilaya ya Nyasa. Watu hapa wanajihusisha na aina mbali mbali ya shughuli za kujipatia tija, ikiwemo uvuvi ambayo ndiyo inakimu maisha ya wengi hapa. La sivyo, wanavijiji hujishughulisha na aina mbali mbali ya biashara ndogo inayojumuisha pakubwa ile ya uuzaji wa vyakula na vinywaji kadhaa.
Ripoti hii imedhaminiwa na InfoNile na Code for Africa. Ilipeperushwa hewani na Unyanja FM