Ukosefu wa Maji Wasababisha Kipindupindu

Ukosefu wa Maji Wasababisha Kipindupindu

Kwa ufupi

Mlipuko wa kipindupindu Mkoani Songwe, Wilaya ya Songwe ilikuwa ni changamoto kuu mwishoni wa mwaka uliopita hadi mapema mwaka wa 2018. Sababu ya mlipuko huu ilikuwa ukosefu wa maji. Hata hivyo, wanavijiji hawa walihamasishwa jinsi ya kuzingatia kanuni za usafi ili kuepuka na maradhi haya siku za usoni. Waliona kuwa jambo njema.

Raymond Mkala wa kituo cha radio cha Bomba FM alizuru eneo hili. Makala yake huangazia maswala ya maji, mazingira na usafi binafsi.

Ripoti zinaonyesha kwamba jamii iliathirika kutokana na maradhi ya kipindupindu kufuatia ukosefu wa maji safi na salama. Aidha, jamii kutozoea kutibu maji ulichangia kuenea kwa maradhi.

Ripoti zinaonyesha ndani ya kipindi cha miezi tisa kati ya mwezi Septemba 2017 na Mei 2018 vimeripotiwa visa vya ugonjwa wa kipindupindu ndani ya kata tisa za wilaya ya hiyo, ambapo wagonjwa 852 waliugua na kutibiwa na vifo vya watu wawili vilitokea.

Kijiji cham Mbuyuni kata ya Mbuyuni ni miongoni ya maeneo ambako wakaazi wake walikumbwa na maradhi haya mlipuko. Nimefika kijijini hapa na kuwauliza ni nini chanzo cha wao kukumbwa na maradhi haya. Wanasema ukosefu ya maji ya uhakika yenye usalama, ndio chanzo.

“Mazingira ya kwetu kinachotusumbua zaidi ni maji. Maji tunachota sehemu ambazo hazieleweki. Maji yanatoka sehemu mbali mbali. Vijana wachungaji wanatupa vinyesi vyao ovyo. Nzi akitoka pale anaenda kutua kwenya maji. Kwa hiyo zaidi zaidi, kipindupindu tunapata mlipuko kwa ajili ya maji”

“Maji yenyewe tunakunywa sio masafi. Mara ingine wanaweka vinywele wanaenda kutupa kisimani. Ikifika usiku tunachota tunaenda kuweka kwenye chungu.”

“Hatuna visima bora, hata visima vipo lakini utaratibu ambao uko pale sio mzuri. Kwa sababu watoto wanaotoka kuchunga hawana utaratibu mzuri. Atafika pale kwa uharibifu tu. Hata kisimani tu anaweza ingiza chombo chochote ambacho hakistahili kuingia pale”

“Huku mashambani tunatumia maji ya mito, tunachimbua visima pembeni mwa mito. Tunakunywa tu ovyo ovyo maji.”

“Lakini hata hivyo, tuliambiwa tuna maji aina mbili. Kuna visima viko mitaani venye tunatumia kwa ajili ya shughuli za kawaida hizi za kuoga na kupikia. Lakini visima hivyo, inasemekana viko karibu na vyoo. Changamoto kama hizo pengine zilipelekea ugonjwa kudumu zaidi kijijini kwetu”

Wananchi hawa wanabainisha kuwa vyanzo vinavyotumika kupata maji si salama, sababu kuna shughuli za kibinadamu zinafanyika humo na kuchafua maji.

“Huko Mto Songwe yaani ni msimu mzima kuna kilimo cha kiangazi. Watu wanaishi huko kuanzia asubuhi mpaka hadi jioni. Na pia hata wakati wa kifuku hiki, watu wanalima mbali kidogo pembezoni na mto Songwe. Kwa hiyo tunayatumia yale maji na hatuelewi yanatoka wapi. Ndivyo ilivyo wanaoga, wanafua, tunachota hadi maji ya mapombe haya, mpaka maji ya kiangazi tunachota huko Mto Songwe. Hata tunachota yanayotembea.”

“Ukiangalia pambalizi kwenye eneo ya machinjio, kile kimto kinapita pale. Sasa Machinjio yote ya wanyama wanatumbukiza ndani ya maji yale. Kwa hivyo inapofika kwetu sisi, ndio tunayoitumia wakidhani kwamba yamejichuja. Tunatumia kwenya visima vya maji yale ya chini, ndio tunatumia ya kunywa. Kwa hivyo maji hakuna safi na salama.”

Lakini jamii hii pia tangu kale haina mazoea ya kutibu maji ya kunywa. Pia wanasema kuna baadhi ya mazingira wakiwa na kiu, hawawezi kupata maji yaliyo tibiwa kwa kunywa.

“Kabla ya elimu hii kuna watu wanapochota maji kutoka Songwe yaani hakuna ile haja ya kuchemsha wala kuweka water guard. Walikuwa wanachukuwa tu kwa kuona maji ni mazuri, wanakunywa. Kumbe maji hayo si salama. Kwa hivyo hilo ni tatizo kwa wale wanaochota maji Mto Songwe”

“Kwa mfano kama kipindi cha nyuma ambapo bado elimu haijapita ya uchemshaji wa maji, ukichemsha maji, unakuta mototo au mtu tu mkubwa anasema hayo maji, mbona sio mazuri, hayakati kiu, mara haya maji mbona yanaleta kaharufu fulani ka moshi? Lakini kulingana na elimu tuliyoipata, juu ya kuchemsha maji, yanachemka sana pia unaacha yanapoa, unachukuwa kitambara safi, unayachuja yale maji unayaweka maji yako kwenye mtungi, aidha kwenya ndoo. Kwa sasa hivi, tumeona jambo ni jema.”

Ripoti hii imeandaliwa kwa hisani ya InfoNile na Code for Africa, ikishirikiana na Bomba FM.

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts