Katika kisiwa cha Ghana, wilayani Ukerewe wavuvi wajiandaa tayari kwa shughuli ya uvuvi, majira ya jioni, wakiandamana na watafiti wa taasisi ya utafiti ya uvuvi Tanzania (TAFIRI). Imekamilisha awamu yake ya pili ya utafiti katika ziwa Victoria ili kubaini aina gani ya nyavu zitumike kwa shughuli ya uvuvi kufuatia zoezi la uchomaji nyavu haramu unaoendeshwa nchi nzima.
Marejeo ya wavuvi hawa yanaanza kutupa majibu ya nyavu zipi zifaazo. Tayari, dalili zaonyesha kwamba wavuvi hawaipendi ile nyavu inayopendekezwa na serikali.
“Yani ni kama vile unatega ndege wa angani, bali sio samaki,” asema Mkulasi Petro, mvuvi kisiwa cha Ghana, huku akiitandaza wavu wake ulio tupu ndani ya mashua yake.
Nicolaus Mwere, ambaye vile vile ni mvuvi kisiwani hicho, anakubaliana na maoni haya.
“Sijapata chochote, nimetega jana jioni, nimeshaleta, yani sijapata kitu chochote,” Mwere aeleza kwa masikitiko.
Hata hivyo ufujaji wa mizani ya kupimia samaki unachukua sura mpya kwa kuonekana kuchochea uvuvi haramu
Hivyo basi, inakuwa vigumu kwa wavuvi kama Ally Rajab kujikimu kimaisha. Yeye, kama wenzi wake anatilia shaka kama juhudi za kukabiliana na uvuvi haramu zitafaulu.
“Kulingana ninavyonelea, hii ni kazi ngumu, hata huu uvuvi haramu wanasema ya kwamba utaisha, ni kazi ngumu sana,” adai Rajab.
Kwa upande wake, Bakari Kdabi ambaye ni mjumbe wa muungano wa wavuvi wa TAFU, ahisi kwamba ikiwa upunjaji unaotendeka katika mizani hautaondolewa, basi uvuvi haramu hauna budi kuendelea.
“Mvuvi anapopima samaki wake na kupunjwa kwenye mizani basi anaamua kutafuta njia mbadala ya kupata samaki wengi,” aeleza. Azidi kusema kwamba njia mbadala ya kupata samaki wengi ni ile ya kujihusisha katika shughuli za uvuvi haramu.
Kusanyiko hili la wavuvi na viongozi wao linatoa tumaini jipya wakiamini ripoti itakayokabidhiwa kwa waziri mwenye dhamana itajadiliwa na kuwapa afueni.
Kulingana na watafiti, nia yao kubwa ni kubaini kama mbinu zinazotumika kwa sasa za uvuvi, zitawezesha raslimali zilizoko kuendelea kuwepo siku hizo za usoni.
“Sisi kama watafiti tunaangalia uendelevu wa raslimali tulio nayo kama ikivunwa jinsi inavyovunwa sasa, je tutaendelea kuwa nayo?” aeleza Philemon Nsinda mtafiti pale TAFIRI.
Wavuvi wanayo hamu kutaka kujua matokeo ya utafiti huu, wakitumaini kwamba itashughulikia maswala yao, iwapo serikali itayapa umuhimu mapendekezo yake.
“Tunazamia kwamba majibu ya utafiti huu yatapelekwa wizarani, na wizara itaandika mswada kwa ajili ya kupelekwa bungeni ikiwa kuna mapendekezo tofauti na yale yaliomo na sheria, yani ya single ,” asema Jefta Machandali, Katibu Mkuu wa TAFU.
Ni bayana kwamba wavuvi wengi hawaipendi ile nyavu aina ya single.
“Tunasema kwamba single haifai kwa matumizi ya uvuvi kwa Ziwa Victoria, na kweli inaokena, kwa sababu kila tunakoenda single inakuja bila samaki,” adai Kdabi.
Hivyo basi, wavuvi wanabaki kupata hasara. Aongezea kusema kuwa, hili ni jambo serikali itapata kuona kwenye matokeo ya utafiti.
Shughuli za kiutafiki zimefanyika katika visiwa vya ikuza nkome nkome mchangani na Ghana ikuhusisha nyavu aina ya single.double,double mbili,double nne tano na sita ambapo nyavu aina ya singo ambao zilikuwa zikipendekezwa na serikali kuwa hazifai kwa uvuvi wenye tija katika ziwa Victoria.