Nini Kinachofanya MV Leimba Kupoteza Nafasi Yake ya Uegeshi Ndani ya Ziwa Tanganyika?

Nini Kinachofanya MV Leimba Kupoteza Nafasi Yake ya Uegeshi Ndani ya Ziwa Tanganyika?

Makala Asili ya InfoNile

Na Prosper Kwigize

Kwa miaka 100 iliyopita, uegeshi salama katika bandari ya Kigoma Harbor ndani ya Ziwa Tanganyika, ilikuwa shughuli ya kawaida kwa MV Leimba, mojawapo ya meli zee duniani, iliyoundwa takriban miaka 100 iliyopita nchini Ujerumani.

Lakini sasa mambo yamebadilika. Uegeshi salama hauwezekani kamwe! Ziwa linapungua. Upwa nao umeharibika. Na kuelea kwa MV Leimba ni kwa bahati tu majini.

“Kupungua kwa kiwango cha maji kinaathiri shughuli za bandari,” asema Moris Mchindiuza, meneja wa bandari ya Kigoma.

“Kushuka kwa kiwango cha maji upwani na kando kando mwa bandari ya Kigoma zinaathiri uegeshaji laini la MV Liemba na meli zingine.”

Anaamini kwamba meli hili liko kwenya hatari ya kuzama, hivyo basi kuharibika.

Kigoma Marine Parking area in Kigoma Port
Kigoma marine parking area in Kigoma Port

Bandari ya Kigoma linawapa huduma za kibahari wakaazi millioni 30 wa eneo la bonde la Ziwa Tanganyika nchini Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia.

Ziwa Tanganyika ni la pili kwa kiwango cha maji na la pili kwa kina kikubwa ulimwenguni. Ndilo ziwa ndefu duniani la maji matamu lenye urefu wa kilomita 650 na upana wa kilomita 50. Eneo la bonde lake lina ukubwa wa takriban kilomita 250,000 mraba.

Kando na usambazaji maji manispaa na viwandani, Ziwa Tanganyika ni chanzo cha maji kwa ukulima wa umwagiliaji maji, uvuvi na usafiri, miongoni mwa matumizi mengine.

Ziwa hili hupokea maji yake kutokana na usimbishaji wa moja kwa moja, mito kadhaa, 20 miongoni mwao iko katika maeneo sita nchini Tanzania: Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Shinyanga na Songwe.

Hata hivyo, kuwepo kwa vyanzo hivi vyote, hakujazuia ubadilikaji mkubwa wa kina, kwa mujibu wa takwimu za idara ya ukulima ya Marekani, yaani United States Department of Agriculture, hivyo kuashiria mwelekeo mkuu wa upunguaji mkubwa wa maji kwa miongo miwili imepita.

Upunguaji wa Ziwa Tanganyika, hauathiri tu MV Liemba, bali linaathiri pia maelfu ya wavuvi wanaotegemea raslimali hii ya maji  kujikimu kimaisha.

Abdalla Sendwe, ambaye ni mvuvi, anasema kwamba idadi ya samaki aliyokuwa anavua imepungua kwa miaka imepita.

Ameshuhudia kushuka kwa kiwango cha maji kwa miongo ya hivi karibuni, na anadhani kwamba hii ndio sababu ya kupotea kwa nafasi ya uegeshaji ya MV Liemba.

Pia, “samaki na viumbe vingine majini havina makao salama sasa,” alalamika Sendwe.

lake tanganyika

Vile vile, Alhaji Amir Hamim wa miaka 68, ambaye ni mkaazi wa Kigoma aliyetegemea uvuvi wa kibiashara kutoka Ziwa Tanganyika, asema kuwa alilazimika kuingilia kilimo baada ya uvuvi kushindwa kumletea pato lingesaidia jamii yake kujikimu.

“Wengi ya wavuvi mamegeukia shughuli mbadala za kiuchumi ili kujikimu, kufuatia kupungua kwa samaki,” aeleza.

“Walioendelea na shughuli za uvuvi sasa wanaishi katika umaskini mkubwa.”

Mnamo mwaka wa 2016, utafiti uliochapishwa na chapisho la Proceedings of the National Academy of Sciences, toleo la Agosti 8, na watafiti wa Marekani, ambao ulichunguza mashapo yaliochimbwa kutoka Ziwa Tanganyika miaka 1,500 iliyopita,  ulionyesha kupungua kwa samaki ulitokana na mabadiliko ya tabia nchi, bali sio uvuvi wa kupita kiasi kama ilvyodhaniwa.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kiwango cha joto ziwani lilikuwa likipanda kutoka karne ya 19. Hii, kulingana na utafiti, ilipelekea kupungua kwa chakula cha samaki, na hatimaye kupungua kwa idadi ya samaki.

Hivi karibuni, serikali ya Tanzania imeripoti kwamba Ziwa Tanganyika limepoteza mita 1.5 ya ujazo ya maji yake, na pwani lake limepoteza takriban mita 500 ambayo ni sawa na kilomita 0.5 eneo la Ujiji.

Inalaumu nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kuondoa vizuizi vya maji vilivyojengwa kati ya Mto Lukuga na Ziwa Tanganyika. Hivyo basi, imepelekea maji kutoka Ziwa Tanganyika kutiririka ndani ya mito ya Lukuga na Congo.

Sababu zingine inazotaja ni pamoja na uchafuzi wa viwanda, mabadiliko ya tabia nchi, ukulima wa umwagiliaji maji, makao holela na mpangilio duni wa mji karibu na maziwa ya Kigoma, Rukwa na Katavi nchini Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Zambia.

Samson Anga, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, anatambua athari za ukuwaji wa miji kando ya ziwa.

Aeleza kwamba uingiliaji ya maeneo kando ya ziwa imeathiri kutiririka kwa maji kutoka na kuelekea ziwani, hivyo kupelekea kuongezeka kwa mchanga na uchafuzi wa ziwa. Hii inapelekea kupungua kwa kina cha ziwa, kwa mujibu wa Anga.

“Haieleweki jinsi ambavyo waweza jenga sehemu za hifadhi ama maeneo za milima, huku ukitambua ni hatari kwa mazingira,” Anga asisitiza.

Anaongeza kusema kuwa jukumu la kulinda na kudumisha ziwa halitegemei serikali tu, ila ni jukumu la wananchi wote. Awataka wote wanaotumia Ziwa Tanganyika waliwajibikie siku zake za usoni.

Mahmod Mgimwa ni mwenyekiti wa kamati la kudumu la bunge la Tanzania linalowajibikia maswala ya maji, ukulima na mifugo. Yeye pamoja na wanachama wa kamati walizuru eneo la Kigoma. Walikagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji kando wa Mto Luiche, mojawapo ya kijito kiingiacho Ziwa Tanganyika pamoja na mradi wa maji ndani ya Manispaa ya Kigoma miongoni mwa miradi mingine.

Kwa mujibu wa Mgimwa, serikali ya Tanzania yatambua athari ya miradi ya maendeleo kama ile ya ukulima wa umwagiliaji maji, utekaji maji kiholela kutoka ziwani, lakini hatua kadhaa zinachukuliwa ili kunusuru hali ilivyo na kuhifadhi ziwa.

Anataka mradi wa kuvuna maji ya Tanganyika kubuni mbinu za kuwezesha utumiaji maji mara tena baada ya matumizi yake nyumbani, ndani ya manispaa ya Kigoma, ili kuwezesha maji hayo kurudi hadi chanzo chake baada ya kutumika.

Katika mpangilio wake wa miaka ya 2006-2025 yaani ile ya Water Sector Development Program, eneo la Kigoma lanuia kubuni mpango ya raslimali yote ya maji inayohusisha bonde zima la Ziwa Tanganyika yaani Integrated Water Resources Management and Development (IWRMD).

Mpangilio wa IWRMD utalinda raslimali ya maji ndani ya bonde, na kuunda mfumo utakaoboresha maishilio ya watu wanaoishi ndani ya bonde. Mpango huu utasitawisha usawa, ufanisi, ulindaji mazingira na maendeleo ya raslimali ya maji ambayo ni endelevu.

 

Ripoti hii imewezeshwa kwa hisani ya InfoNile na Code for Africa

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts