Mto Athi waanza katika mabonde yanayosifika ya Ngong, yakipaa juu ya jiji la Nairobi. Mkondo wake wapita jiji hili kuu na katikati mwa hifadhi la kitaifa la wanyama la Tsavo East, hadi linapofika Bahari la Hindi. Mto huu, vijito pamoja na kingo zake ni chanzo cha maji ya kunywa na yanayotumika kwa kilimo cha umwagiliaji maji kwa mamilioni ya watu na wanyama pori. Maji na kingo zake ni muhimu kwa viwanda kadhaa katika eneo hili, ikiwamo ile ya uchimbaji migodi na utalii.
