Tunaandamana na mkulima Mkenya kwa zaidi ya miaka minne ili kuonyesha jinsi ambavyo mabadiliko ya tabia nchi yanamuathiri mwanadamu. Mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maeneo yote ulimwenguni, lakini maeneo mengine yako mashakani zaidi.
Maeneo kadhaa ya Afrika Mashariki tayari yanashuhudia msukosuko wa athari za hali ya hewa, zikiwemo zile zinazotegemea kilimo kwa maishilio kuwa katika mstari wa mbele kuathirika pakubwa.