Kamati la Uridhi wa Dunia, lilokutana kuanzia Juni 24, liliamua leo kusajili Hifadhi ya Kitaifa ya Ziwa Turkana katika orodha ya Uridhi wa Dunia Mashakani, kwa kasababu ya athari za bwawa liliko eneo hilo.
Kamati lilitaja wasiwasi wake kuhusu athari haribifu za bwawa la Gibe III nchini Uhabeshi katika mtiririko na mazingira ya Ziwa Turkana na mradi wa sukari wa Kuraz, ambazo zinahatarisha zaidi eneo hilo.