CAIRO – Mei 22, 2018: Misri itawakaribisha wataalamu wa maji kutoka nchi 53 kushiriki katika kongamano la “Wiki ya Maji Cairo”, ambalo litafanyika Oktoba 14-18 kujadili maswala ya maji.
Iman Sayed Ahmed, mkurugenzi mkuu wa sekta ya mipango katika Wizara ya Raslimali ya Maji na Kilimo cha Umwagiliaji Maji, alisema kuwa Rais Abdel Fatah al-Sisi atafadhili kongamano hilo ambalo linaonyesha dhamira ya Misri kukabiliana na changamoto za maswala ya maji, kama vile kuenea kwa jangwa, ukosefu wa maji na mabadiliko ya tabia nchi.