Wafugaji nchini Kenya wageukia programu ya simu ya rununu ili kupunguza hatari zinazoletwa na ukame

Na Anthony Langat

ARKAMANA, Kenya, Mei 7 (Thomson Reuters Foundation) –  Wakati wa ukame, mfugaji Buchu Boru hulazimika kutembea kilomita nyingi, kutafutia mifugo wake lisho, pasipo hakikisho kwamba atafanikiwa.

“Utaelezwa kuwepo kwa lisho, ila tu utaporejea hupati lolote,” alisema Boru, mzee wa miaka sitini, ambaye hulazimika kutembea kutoka nyumbani kwake hadi kupita mpaka wa Ethiopia kutafuta nyasi.

Lakini, wakati mwingine mvua zikitakapopotea – tatizo ambalo ni la mara kwa mara kaskazini mwa Kenya – anatumaini kuwa programu mpya ya simu ya rununu mpya, itamsaidia kuelekeza mifugo kwenye lisho, pasipo kufuja hela au kupoteza wakati mwingi.

Share the Post:

Related Posts