Paneli za nguvu za jua hugeuza nishati inayotokana na jua na kuifanya umeme. Baadaye, umeme huu hupitia katika mdhibiti hadi kwenye betri. Kazi kuu ya kimsingi ya mdhibiti ni kudhibiti upashaji nguvu kwenye betri na kudumisha viwango vipasavyo vya umeme ambao huifadhiwa katika betri.