Utililishaji wa maji taka na uchafu katika mazingira hususani ya Milimani,umetajwa kuwa chanzo kikuu cha uchafuzi wa maji ndani ya ziwa Victoria.
Kutokana na hali hiyo mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) imelazimika kuanzisha mradi wa ujenzi wa bomba za kusafirisha maji taka kwa maeneo ya milimani hadi katika mabwawa ya kutibu maji ili kutunza ubora wa maji hayo ndani ya ziwa kabla ya matumizi ya kibinadamu .
Star tv kwa kushirikiana na InfoNile na code for Africa Wanadhuru eneo la kilimahewa mojawapo ya wanufaika wa mradi huu.
Hii ndo maana halisi ya Rock city , kutokana na maeneo mengi ya jiji hili la Mwanza kuzungukwa na milima.
Inaelezwa kuwa hapo nyuma wakazi wa eneo hili la mlima wa Kilimahewa kuona maji taka yatokanayo na vyoo ilikuwa ni jambo la kawaida hasa nyakati hizi za Mvua.
“Kabla ya mabomba kuwekwa, tulikuwa tunasumbuka, kwa vile mashimo tunayoyachimba yanakuwa mafupi kwa sababu eneo hili limejaa mawe, na ambayo hufukuliwa wakati wa mvua,” Kasema Fransis Sumuni, balozi mtaa wa Kilimahewa.
Restuta Vicent, mkaazi wa Kilimahewa, anashiriki maoni haya na ambaye anaongezea kusema kuwa hali hii inachangia kuenea kwa magonjwa.
“Mashimo mafupi hufukuliwa kwa urahisi wakati mvua inaponyesha, na kwa sababu ilitubidi kuchimba mashimo mengi, basi magonjwa yalienea kwa upesi,” kasema Vicent.
Mabomba ya mradi huu wa simplified sewerage unaonekana kuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hili la mlima wa kilimahewa kwani licha ya uwekaji wa bomba pia njia zimerahisishwa
Kwa sasa hali inaonekana tofauti kwa kaya zaidi ya 100 ambazo tayari zimekwisha nufaika na mradi huu wa kwa ujenzi wa mabomba ya kusafirisha maji taka kwa maeneo haya.
“Wapo wanaokaa sehemu sehemu walikuwa wanawinda wakati wa usiku utashtukia hali ya hewa imeharibika kabisa,” asema Joel Ifrahimu, mkaazi Kilimahewa.
Hali imeimarika pakubwa, kufuatia kutekelezwa kwa mradi huu, kulingana na Jovita Deogratiua mkaazi Kilimahewa.
Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha ubora na utuzanji wa maji na usafi wa mazingira kwa jiji la Mwanza Lakini JE ! kwa nini mradi huu uitwe simpilified sewerage na si jina lingine?
“Tunauita simplified sewerage kwa maana ya kwamba, tunalegeza vigezo halisi vya muundo kwa lengo tu la kuondoa maji taka kutoka kwa maeneo ya wakaazi,” aeleza mhandisi Antony Sanga, mkurugenzi wa Mwauasa.
Tahadhali ya magonjwa yatokanayo na maji taka yatokanayo na vyoo imechukuliw ana mamlaka kabla ya kuingia ziwa Victoria ambapo ndipo chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
“Kutokana na hayo maji yakishachafuliwa, yakiingia kule, lazima yanachafua ubora wa maji wa Ziwa Victoria ambalo ndio chanzo kikubwa ya maji ya wakaazi jijini Mwanza,” aeleza Mhandisi Leonard Msenyele mhandisi katika Mwauwasa.
Mradi huu unajengwa kwa ufadhili wa serikali na utaendelea kujengwa katika kaya zilizosalia kwa wkazi wa Kilimahewa pamoja na maeneo mbalimbali yenye milima jijini Mwanza.