Miti ya Matunda Inavyoanguka, Ndivyo Njaa Inavyotishia Kenya

Miti ya Matunda Inavyoanguka, Ndivyo Njaa Inavyotishia Kenya

KAJUKI, Kenya, Aprili 20 (Thomson Reuters Foundation) – Wakati Leah Mutembei alipokua kijiji cha Kajuki, kilichoko Kenya ya Kati, miti ya avokado ilizagaa mashamba mengi kule.

“Lakini sasa, hayapo tena,” kaeleza Mutembei, mkulima wa mahindi mwenye umri wa miaka thelathini na miwili, huku akinyosha kidole chake kuonyesha shamba lilivyobaki kavu.

“Ilitubidi kukata miti ndiposa tupate kuni na makaa,” kasema Mutembei.

Eneo hili ambalo hutegema kilimo pakubwa na ambalo limeadhirika kutokana na hali ya anga isiyotabirika, pamoja na mvua isiyotosheleza, hivyo kusababisha mavuno finyu, sasa imepelekea wakulima kukata miti na kuuza mbao na makaa.

Lakini sasa, uharibifu wa miti ya matunda haswa, inanyima wanavijiji chakula na lishe muhimu, wasema wataalamu – ambayo wangetegemea wakati mavuno ni mabovu.

“Maembe, avokado na ndizi yana vitamini muhimu kwa ukuwaji wa watoto,” alisema David Mugambi, mhadhiri wa maswala ya usimamizi wa rasilimali asili, Chuo Kikuu cha Chuka.

“Ukataji kiholela wa miti ya matunda, inawanyima watu kiwango kikubwa cha mlo,” aliambia Thomson Reuters Foundation.

Print Friendly, PDF & Email

Like this article?

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Linkedin
Share on Pinterest
Share on Telegram
Share on WhatsApp

Leave a comment

Related Posts