Konjit Teshome
Addis Ababa, Uhabeshi
Awamu ya pili ya majadiliano mjini Addis Ababa, kati ya mawaziri wa maswala ya kigeni na wale wa kilimo cha unyunyuziaji maji wa mataifa matatu ya Uhabeshi, Misri na Sudan yalikamilika kwa mafanikio, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uhabeshi, Workineh Gebeyehu. Baada ya masaa kumi na mbili, majadiliano kuhusu maswala ya GERD, wajumbe wa mataifa haya matatu walitangaza kuwa wameafikiana kusonga mbele.